Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, October 31, 2009

SIMBA YAIRARUA YANGA

Kikosi kamili cha timu ya Soka ya Simba, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom na Yanga, Dar es Salaam.
Klabu ya Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1 - 0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa ligi kuu TAnzania bara uliyochezwa leo katika uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam.
Kocha Patrick Phiri akishangilia (kushoto) Mwina Seif Kaduguda katibu mkuu wa Simba (katikati) na Mwenyekiti wa klabu ya Simba Hassan Dalali (kulia)
Goli la dhahabu lilifungwa na mchezo Mussa Hassan Mgosi katika dakika ya 26 kipindi cha kwanza akiunganisha mpira wa krosi uliyopigwa na Dani Mrwanda.Ambani Mshambuliaji wa Yanga Boniface Ambani akichuana na na Joseph Owino, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Simba ilishinda 1-0.Mwenyekiti wa Yanga Iman Madega, akipita mbele ya mashabiki wa timu yake kuhamasisha ushindi, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya timu yake na Simba, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Simba ilishinda 1-0.Mshambuliaji wa Yanga Jerison Tegete akiwa ameketi chini ya Uwanja wa Taifa Dar es Salaam baada ya timu yake kufungwa bao 1-0 na Simba wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya VodacomKikosi kamili cha timu ya Soka ya Yanga kilichofungwa bao 1-0 na Simba Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Friday, October 30, 2009

TAKWIMU MUHIMU - SIMBA NA YANGA

TAKWIMU MUHIMU
Hadi Simba na Yanga zinapambana hapo kesho Takwimu zinaonesha kuwa lango la Timu ya Simba limeguswa mara 3 tu katika mechi walizoshinda.
Waliifunga Toto African 3-1, 2-1 dhidi ya Moro United na 4-1 kwa JKT Ruvu huku Simba ikiwa imefunga mabao 18 hadi sasa.
Kwa upande wa Yanga Nyavu zake zimeguswa mara 7 huku imefunga magoli 13 katika kuchomoza kwao mara 5, Sanjari 3 na kuzabwa mara moja.
Matokeo ya Jumla yanatanabaisha kuwa Yanga na Simba zimekutana mara 82 huku Simba ikishinda mara 30, Yanga mara 24 zilizobaki ni Suluhu.Mchezaji atakayekuwa na mvuto kwa mashabiki wengi ni kipa Juma Kaseja kutokana na Wana Yanga kutarajiwa kuangalia atafanya nini atakavyosimama langoni mwa Simba kumbuka Kaseja alikuwa Jangwani msimu uliopita kabla ya kurejea Msimbazi msimu huu.
Wachezaji wa Simba wanaotakiwa kuchungwa kwa hali ya juu ni Danny Mrwanda , Emmanuel Okwi, Viungo Hillary Echesa na Mussa Hassan ‘Mgosi’ wakali hao wakiwa sanjari na wenzao Kelvin Yondani, Joseph Owino, Nico Nyagawa, Mohamed Banka, Mohamed Kijuso na Ramadhan Redondo wanaweza kupeleka Simanzi Jangwani.
Mnyama atawakosa mchezo huu ni pamoja na Emeh Izechukwu na Henry Joseph waliouzwa katika klabu ya Kongsvinga ya Norway huku pia wakimkosa Haruna Moshi “Boban” aliyekwenda Sweden kwa majaribio ya kucheza soka la kimataifa.
Kwa upande wa Yanga wachezaji wanaotakiwa kulindwa kwa umakini ni Mike Barasa, Jerson Tegete, Mrisho Ngassa, Athuman Iddi’Chuji’ , Kabonge Honore na Nurdin Bakari.
Wachezaji ambao wamewahi kucheza katika klabu ya Simba na Yanga na wanatarajiwa kuteremka Dimbani hapo kesho ni pamoja na Juma Kaseja, Athumani Iddi “chuji’, Nurdin Bakari na George Owino.
Kwa upande wa Yanga watawakosa Nadir Haroub ‘Cannavaro” na Ben Mwalala, Nadir “Canavaro’ anasukuma soka la kulipwa katika klabu ya Vancouver Whitecaps ya CANADA.
Mwamuzi wa Mtanange huo anataraji kuwa Oden Mbaga ambaye katika mchezo uliyopita alikuwa mwamuzi wa mezani hivyo anauzoefu wa presha za mchezo wa Simba na Yanga.

MCHEZO WA SIMBA NA YANGA ULINZI WA KISAYANSI

Shirikisho la soka nchini TFF limewahakikishia Watanzania katika mchezo wa kesho wa watani wa jadi wa Simba na Yanga kuwa utakuwa na Ulinzi na Usalama kwa muda wote kabla na baada ya mchezo huo .
Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa TFF Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Fredrick Mwakalebela amesema utaratibu mzima umeshakamilika ikiwa ni pamoja na kuwa na Askari wa kutosha watakaokuwepo Uwanja mzima kwa ajili ya kuangalia usalama na shughuli zingine.
Mwakalebela ameongeza kuwa siku ya kesho hakutakuwa na uegeshaji wa magari ndani ya Uwanja huo hivyo wanatakiwa kuegesha magari hayo katika uwanja wa Uhuru na katika viwanja vya nje vya Balaza la Michezo la Taifa BMT.
Wakati huo huo Mwakalebela amesema katika kuhakikisha soka la Tanzania linakuwa wao kama Shirikisho wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuongea stesheni ya Super Sports kwa ajili ya kuonyesha mpira huo kwa kuurekodi ili uweze kuonyesha na Stesheni zingine za Afrika.
Mwakalebela amesema siku ya leo wamekutana na Timu zote mbili pamoja na Waamuzi na Makamisaa mapema na kuzungumzia kuhus mchezo wa kesho ili kuwapa nafasi Timu hizo kupata muda wa kutosha kujiandaa na mchezo huo mgumu iliojaa ushindani.
Wakati huo huo JESHI la polisi la mkoa wa Dar es Salaam, limejipanga kuweka kamera ili kubaini waanzilishi wa vurugu katika mpambano wa mpira wa miguu kati ya watani wa jadi Simba na Yanga.
Akizungumza Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema, sambamba na kamera hizo pia kutakuwa na namba ya simu ambayo itawaruhusu mashabiki watakao kuwa uwanjani hapo kutuma ujumbe mfupi ili kuwavumbua wahalifu hao.
Kamanda Kova amezitaja namba hizo kuwa ni 0783 034224 ambapo ujumbe utakaotumwa utakuwa ukipita katika kompyuta maalum ambapo utafanyiwa kazi wakati huohuo na maaskari watakao kuwa maeneo hayo.
Amesema, ulinzi umeongezwa mara mbili ili kudhibiti hali yeyote ya utovu wa nidhamu kujitokeza na atakaebainika kufanya uhalifu tachukuliwa hatua hapo hapo ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Amesema, hakutaruhusiwa kila mtu kufanya biashara isipo kuwa kutakuwa na watu maalum kwa ajili ya kufanya biashara ili kuepusha purukushani zisizo za lazima ambazo ndizo chanzo cha vurugu.
Hata hivyo, kamanda kova ametahadharisha mashabiki wa Simba kutokuja na jeneza uwanjani kwa hali hiyo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara na ni kitendo kinachochochea vurugu kwa timu hizo hasa ipatapo ushindi.
Vile vile Kamnda Kova amesema, hakutaruhusiwa uuzwaji wa kilevi cha aina yeyote uwanjani ikiwa ni pamoja na watu kuzingatia gharama za tiketi walizo kata ambapo kila mtu anastahili kukaa sehemu husika.

MWANA FA, BLACK RHINO WAANGUKA TUZO ZA CHANEL O

Wanamuziki wa Tanzania wamemwagwa katika tuzo za Video zinazotolewa na Channel O katika tamasha lililofanyika hapo jana Carnival City nchini Afrika Kusini.
Wanamuziki wa Tanzania ambao waliingia katika kinyang`anyiro cha kuwani tuzo za Video ni pamoja na MwanaFA aliyekuwa akiwaniwa tuzo ya Most Gifted East Afrca Video akichuana na Amani, Xod, Mwana Fa, Wahu, Cannibal na Black Rhino.
Black Rhino aliyekuwa akiwania tuzo mbili, moja ya Most Gifted East Afrca Video akichuana na Amani, Xod, Mwana Fa, Wahu, na Cannibal, pamoja na kuwania tuzo ya Most Gifted Hip Hop Video ambapo alikuwa akichuana na Okyeame Kwame, HHP, Zeus, Jay Ru na Pro.Wanamuziki watatu wametwaa tuzo mbili katika tuzo za Video mwaka 2009 zinazotolewa na kituo cha Televesheni cha Chennel O (2009 Channel O Music Video Awards) katika tamasha lililofanyika nchini Afrika Kusini usiku wa kuamkia leo.
Wanamuziki hao ni kutoka Nigeria, Zimbabwe na Namibia.
Darey Art Alade (Nigeria), Gal Level (Namibia) na Buffalo Souljah (Zimbabwe) ambapo kila mmoja ameondoka na tuzo mbili, na kudhihirisha umahiri wa kazi zao kwa mashabiki wa muziki barani Afrika pamoja na watazamaji wa Channel O ambao wamewachagua washindi katika sifa 14 tofauti (categoies).
Darey ametangazwa kuwa mwanamuziki bora wa kiume katika tamasha hilo lililofanyika katika ukumbi wa Carnival City Alhamisi 29 October, na kuhudhuriwa na watangazaji mashuhuri wa Afrika ambao pia walikuwa ma MC`s watatu Vuzu VJ Nonhle na Lungile na KB.
Wanamuziki ambao walitoa burudani ni 2Face Idibia, Sound Sultan, HHP (Jabba), Nneka pamoja na Bongani Fassie (Jozi) & the Umoja Choir.
Nigeria imepata tuzo tano na wanamuziki wa Afrika Kusini wamepoteza tena huku Khuli pekee akitwaa tuzo ya mwanaziki chipukizi (Best Newcomer award).

Washindi wa tuzo zote hawa hapa:

1. BEST MALE VIDEO
Darey for Not The Girl

2. BEST FEMALE VIDEO
Sasha for Only One

3. BEST NEWCOMER
Khuli for Tswak Stik'em

4. BEST DUO OR GROUP
Buffalo Souljah/Taygrin/Gal level for My Type Of Girl

5. BEST DANCE VIDEO
Lady May for Ndota

6. BEST RAGGA DANCEHALL VIDEO
Buffalo Souljah for Judgment

7. BEST AFRO POP
Gal Level for Touch Me

8. BEST KWAITO
Gazza feat. Bleksem for Passop

9. BEST R&B VIDEO
Darey for Not The Girl

10. BEST HIP HOP VIDEO
Zeus for Gijima

11. BEST AFRICAN SOUTHERN
Lizha James for Estilo Xakhale

12. BEST AFRICAN WEST
Ikechukwu for Shoobeedoo

13. BEST AFRICAN EAST
Xod for I Want You Back

14. VIDEO OF THE YEAR
Naeto C for Ki Ni Big Deal

Tuzo ya heshima imepopkelewa na - Bongani Fassie kwa niaba ya mama yake Brenda Fassie.

Tuzo za 2009 Channel O Music Video Awards itarushwa siku ya Jumapili tarehe 8 Novemba kuanzia saa 21:00, ikiambatana na bonge la show ambalo litaanza kuonyeshwa 20:30.

WASHINDI WA BSS WAKABIDHIWA ZAWADI

Mkurugenzi Mtendaji wa Benchmark Production, Rita Paulsen (kulia)akimkabidhi hundi ya shilingi milion 25 kwa mshindi wa mashindano ya Bongo Star Search (BSS), Paschal Cassan wakati wa hafla fupi ya makabidhiano yaliyofanyika Dar es salaam jana anaeshudia katikati ni Ofisa mwandamizi Mkuu kutoka Balaza la sanaa la Taifa (BASATA) na mlatibu wa BSS, Victoria Temu.(Picha na Rajabu Mhamila)

Na Rajabu Mhamila
KAMPUNI ya Bench Mark Productio , imewakabidhi zawadi zao washindi wa mashindano ya kusaka vipaji vya uimbaji vya Bongo Star Seach BSS 2009.
Zawadi hizo za pesa taslim zilikuwa ni sh. milioni milioni 35.5 zilitolewa kwa washindi watano wa mashindano hayo yaliyomalizika 0ktoba 13 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam.

Washindi waliokabidhiwa zawadi hizo ni nyota wa mashindano hayo ya BSS kwa mwaka 2009 Pascal Cassian aliyekabidhiwa sh. milioni 25, Peter Msechu aliyekabidhiwa sh. milioni tano, Kelvin Mbati aliyepata sh. milioni tatu, Jakson George aliyepata sh. milioni 1.5 na Beatrice William aliyepata sh.milioni moja.

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo nyota wa mashindano hayo Cassian amesema kwa kuwa kwake ni mara ya kwanza kushika pesa nyingi kama hizo, atajadiliana na wazazi wake kabla ya yeye kuchukua maamuzi yoyote juu ya kuzitumia pesa hizo.
Mshindi wa tatu wa BSS Kevin Mbati akikabidhiwa milion 3
"Naweza kusema hii ni mara yangu ya kwanza kushika pesa nyingi kama hizi, hivyo kwa kuwa nina wakubwa zangu kama wazazi nitasikiliza kwanza ushauri wao kabla ya kuzitumia,"alisema Cassian.
Amesema kwa sasa anajipanga kutoa nyimbo zake yeye mwenyewe na kwamba yupo katika maandalizi ya mwisho ili kuzikamilisha nyimbo hizo na kuzirusha hewani.
Jackson George mshindi wa nne wa BSS akikabidhiwa kiasi cha Tsh milion 1.5
Naye Mkurugenzi wa Bench Mark Production ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo, Ritta Poulsen amesema Bench Mark ipo katika maandalizi ya awali ya kuandaa mashindano ya BSS 2010.
"Tunawaomba vijana ambao wapo na vipaji vya uimbaji wakae tayari kwani tunatarajia kuanza mchakato wa kusaka vipaji hivi mapema ili kuhakikisha mikoa yote ya Tanzania tunavisaka vipaji hivyo,"amesema Ritta.
Beatrice William mshindi wa tano wa BSS akikabidhiwa fedha taslim Tsh Milioni moja.
Amesema mchakato wa kusaka vipaji hivyo hautakuwa tofauti na miaka iliyopita na kwamba Bench Mark itaboresha zaidi mashindano hayo mwaka hadi mwaka.

Thursday, October 29, 2009

FIFA KUSAIDIA MPANGO WA KUKUZA SOKA TANZANIA

Raisi wa TFF Leodga Chilla Tenga(Kushoto)na Ashford Mamelod mjumbe wa FIFA.
Shirikisho la kandanda Duniani FIFA limeandaa mpango wa kukuza na kuendeleza soka kwa vijana wadogo hapa Nchini Tanzania utakaoanza mwezi March Mwakani ikiwa ni mikakati waliyonayo ya kuhakikisha mchezo huo unaendelea kukua Duniani kote.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Mjumbe kutoka Fifa Ashford Mamelod amesema mpango huo utaanza Mashuleni kwa kuanza na vijana wakike na wakiume wa umri mdogo ambao ni muafaka kwa kuanza kufundishwa mpira.
Ashford ameongeza kuwa anahitaji ushirikiano mkubwa hasa kutoka TFF na Serikali na Wadhamini katika kuhakikisha mpango huu unafanikiwa kwa asilimia kubwa ili baadae waje kupata wachezaji wazuri wa Kimataifa.
Kwa upande wake Raisi wa Shirikisho la soka Nchini TFF Leodga Chilla Tenga amesema amefurahishwa na mpango huo ijapokuwa inahitajika nguvu za ziada katika kusimamia ikiwa ni pamoja na ushirikiano.

GOFU - JOSEPH TINGO ASHINDA FIDDLE

Mcheza gofu Joseph Tango ameibuka kinara wa mashindano ya wiki hii ya Fiddle yaliyofanyika katika viwanja vya klabu ya Gymkhana jijini hapa
Tango ameibuka kinara kwa kupiga mikwaju pointi 38 katika mtindo wa Stable Ford katika mashimo kumi na nane.
Katika kundi A nafasi imekwanda kwa Idan Mziku mikwaju pointi 33, akifuatiwa na Laulence Pangani kutoka katika kundi B aliyepiga mikwaju pointi 37 huku Kei Mwakawago mikwaju point 36 kutoka kundi C akifuatiwa na mwadada Maniwe Pangani mikwaju pointi 37.
Mashindano hayo yenye lengo la kukuza nba kuendeleza mchezo huo hapa nchini yalikuwa na jumla ya washiriki 27 waliogawanyika katika makundi mbalimbali.
Wakatihuohuo, mashindano ya wazi ya Safari maarufu kama Safari Open yataanza kuvurumishwa jumamosi ya wiki viwanjani hapo.
Mashindano hayo ya siku mbili yatachezwa katika mtindo wa Stroken Play katika viwanja 18 na yatashirikisha wachezaji wote wanaoshiriki mchezo huo hapa nchini.
Hadi sasa washiriki zaidi ya 100 wamejiandikisha kushiriki mashindano hayo akiwemo Hamis Ally Idan Mziku na Jane Molell.

MTAMBO WA GONGO AMTAKA MAUGO - BOXING

Bondia Mkongwe wa ngumi za kulipwa Maneno Osward Mtambo wa gongo amewaomba waandaji wa mchezo wa ngumi kuandaa pambano dhidi yake na Bondia Mada Maugo maarufu kama Maugo Junior ili akate mdomo wa bondia huyo.
Akizungumza na kipindi cha michezo na Osward amesema Maugo bado hajui mchezo ila kazi yake ni kuongea tu na vyombo vya habari hivyo yeye ni mwalim wa kurekebisha tabia yake ya kutamba kila kukicha.
Amesema Bondia Maugo anajiona anaweza kumbe awezi na anapopigwa anadai apigwi kwa kuwa wanamaliza naye mchezo na kama atakutana naye atamsambaratisha mapema katika raundi za mwanzo za mchezo.
Hadi hii leo mabondia zaidi ya watatu wanamtaka Bondia Mada Maugo ili wamuonyeshe mchezo katika mabondia hao ni pamoja na Franciss Cheka, Karama Nyarawila na Maneno Osward.

MPIGIE KURA SASA BLACK RHINO KWANI MWISHO LEO

MPIGIE KURA SASA, KURA YAKO NDIYO SIFA KWA TAIFA LA TANZANIAMsanii Black Rhino amechaguliwa kuwa mmoja wa wasanii wanaoshindania tuzo za Afrika za Chanell O Music Awards 2009 akiwa ametajwa kwenye kategori mbili yaani MOST GIFTED EAST AFRICA VIDEO na MOST GIFTED HIP HOP VIDEO.Uongozo wa Chanel O ulitangaza majina ya wasanii wanaowania tuzo hizo kwa mwaka huu kwenye kikao cha wandishi wa jijini Johansburg Afrika Kusini ambapo msanii Black Rhino toka Tanzania alitajwa kuwa tuzo hizo mbili.
Black Rhino anawahimiza sana wa Tanzania waliyo ndani na nje ya nchi kumpigia kura nyingi ili aweze kuibuka mshindi, kwani kushinda kwake katika tuzo hizi kutailetea heshima kubwa Tanzania.

JINSI YA KUPIGA KURAMOST GIFTED EAST AFRICA VIDEO
tuma Nambari 13 E kwenda +27 83 92 0 84 00

MOST GIFTED HIP HOP VIDEO
Tuma Nambari 10F kwenda +27 83 92 0 84 00

Au unaweza pia kumpigia kura kwa kupitia www.channelo.tv au www.channelo.co.za au www.oboma.net

Tuzo za Channel O Music Video Awards 2009 zitafanyika Alhamisi Oktoba 29, 2009 Carnival City, Johanesburg Afrika Kusini.

Albamu ya Black Rhino inaitwa Usipipme inajumla ya nyimbo kumi na iliingia sokoni Februari 2008 na inasambazwa na GMC Mwananchi.

USIKU WA HIP HOP JUMAMOSI MPOTO KUWAKILISHA

Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) kushoto akiimba wakati wa utambulisho wa onesho la HIP HOP litakalofanyika jumamosi hii katika ukumbi wa Diamond Jublie (kulia) ni Msanii Ismail Shabani, wasanii wengine watakao pafom ni pamoja na TMK Wanaume Halisi, Prof Jay, Fid Q, Best Friends Dance Show.(Picha na Rajabu Mhamila)

SHIMUTA KUUNGURUMA NOVEMBA 6

Meneja wa huduma wa Mikopo Midogomidogo, Mashaga Changarawe (kushoto) akimkabidhi fulana Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMUTA) Sadiq Sagawe Dar es salaam vifaa hivyo vitakavyotumika katika mashindano ya SHIMUTA yatakayoanza mwanzoni mwa mwezi ujao anaeshuhudia katikati ni Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Award Safari.(Picha na Rajabu Mhamila)
Na Rajabu Mhamila

BENKI ya NMB imejitosa kudhamini mashindano ya Shirikisho la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMUTA) yanayotarajia kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam, Meneja Mikopo Midogomidogo wa benki hiyo,Mashaga Changarawe amesema wameamua kudhamini mashindano hayo baada ya kuombwa na viongozi wa shirikisho hilo ambapo kwa kuzingatia kuwa na wao ni wanamichezo na muda mrefu ndio maana wakaamua kudhamini.''Sisi siku zote huwa tunapenda kuona nchi yetu inakuwa na maendeleo katika soka ndio maana hata haya mashirika ambayo yanashiriki mashindano hayo ndio maana tukaona si vibaya kama tukawasaidia katika kufanikisha mashindano hayo,'' alisema Changarawe.
Amesema kutokana na wao kuwa wadau wakubwa wa michezo nchini hawakuwa na budi kuwafadhili wenzao kwa namna moja ama nyingine ambapo wametoa fulana 114 zitakazotumika katika mashindano hayo.
Naye Makamu Mwenyekiti wa shirikisho hilo, Sadiq Sangawe amesema wamefurahi kupata hizo fulana, hivyo watazitumia kama inavyotakikana ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Novemba 6 mpaka Novemba 17, mwaka huu
mgeni rasmi katika ufunguzi huo atakuwa mkuu wa Mkoa wa Tanga, Saidi Kalembo.

FILAMU YA "THE HIT" INA MHUSU MICHAEL JACKSON YAZINDULIWA DAR

Baadhi ya mashabiki wa Michael Jackson wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa cinema ya THE HIT iliyozinduliwa jana na kudhaminiwa na kampuni ya Zain Tanzania Dar es salaam Mlimani City.(Picha na Rajabu Mhamila)

WADAU WA VIWANJANI WAHITIMU ELIMU YA SEKONDARI

Mwanafunzi wa kidato cha nne Jesca Kailembo(kulia) akiwa na wenzake baada ya kumaliza sherehe fupi za mahafari ya kidato cha nne katika shule ya secondari ya kisutu jijini yaliyofanyika leo.Mwanafunzi wa kidato cha nne Jesca Kailembo( wa tatu kutoka kushoto)akiwa na baadhi ya ndugu zake katika sherehe fupi za mahafari ya kidato cha nne katika shule ya secondari ya kisutu jijini yaliyofanyika leo.Maunda (wa kwanza kushoto) akimkabizi wifi yake zawadi baada ya kumaliza sherehe fupi za mahafari ya kidato cha nne katika shule ya secondari ya kisutu jijini yaliyofanyika leo.Wazazi wa wanafunzi wa kisutu wakiwa katika mahafari hayo ya kidato cha nne yaliyofanyika Kisutu leo

Wednesday, October 28, 2009

BFT YAOMBA VIFAA KWA WADAU

Shirikisho la Ngumi Nchini BFT linaendelea kutoa wito kwa wadau na Wafadhili mbalimbali Nchini kulisaidia Shirikisho hilo kwa Vifaa vya michezo kwaTimu ya Taifa ambalo ni tatizo kubwa linalowakabili.
Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Makore Mashaga amesema kwa muda wa Mwezi Mmoja na nusu sasa Wachezaji wa Timu ya Taifa wanafanya mazoezi bila ya kutumia vifaa vya michezo ikiwermo Glovs na vinginevyo.
Wakati huo huo, Mashaga amesema kufuatia maagizo ya Kocha Mkuu wa mchezo huo wa Ngumi, wameamua kuzigawa timu katika makundi mawili ya A na B ili waweze kufanya mazoezi kwa nafasi.

HASHEEM THABEET LEO KUTUPA KARATA YAKE YA KWANZA NBA

Msimu wa 2009/10 wa ligi maarufu ya mpira wa kikapu ya nchini Marekani(NBA) umeanza rasmi hapo jana. Ni mwanzo wa mikikimikiki ya ushindani mkali ambao hutawala ligi hiyo.
Kwa watanzania wengi, macho na masikio yao,watayaelekeza kwa Hasheem Thabeet ambaye kwa mapana na marefu atakuwa siyo tu anaitafutia timu yake ya Memphis Grizzlies ushindi,bali pia atakuwa akiipeperusha bendera ya nchi yake ya Tanzania kwa njia moja au nyingine.
Habari za Hasheem zitakuwa sio tu za uchezaji bali pia jinsi ambavyo ni “ndoto iliyotimia” kwa kijana kutoka nchi ya “ulimwengu wa tatu” kama ya Tanzania kufikia kiwango cha kucheza katika ligi ya NBA ambayo hata huko Marekani kwenyewe,vijana wengi hutamani sana kufanya hivyo.
Bila shaka jina la Tanzania litatajwa mara nyingi kuliko kawaida katika matangazo ya ligi hiyo.Ni kwa sababu ya Hasheem Thabeet,mtanzania wa kwanza kuchezea katika ligi hiyo.Haishangazi kuona kwamba watu wengi,wakiwemo viongozi wetu,wanajitahidi kuwa karibu zaidi na Hasheem Thabeet.Jina lake ni ishara ya ushindi.Ni lulu.
Ingawa Hasheem hayupo bado katika “First Five” ya timu yake ya Grizzlies Memphis,bila shaka atacheza leo wakati timu yake itakapowakaribisha, Detroit Pistons (kutoka jijini Detroit,Michigan) mjini Memphis,Tennesse yalipo makao makuu ya Grizzlies Memphis.Watabiri wa mambo wanasema Hasheem tayari ameonyesha uwezo mkubwa wa kuzuia mirusho ya timu pinzani lakini wanashauri azidishe juhudi katika rebound.Bila shaka anasikia na atazingatia ushauri huo na pia wa makocha wake.
Viwanjani inaungana na wote wanaomtakia kheri Hasheem.Tunaelewa kwamba mafanikio ya Hasheem ndio mwanzo wa mafanikio ya vijana wengine wengi wa kitanzania ambao naamini kabisa,endapo watapewa nafasi,wanaweza pia kufikia kiwango cha Hasheem.Kila la kheri HT.

MDAU WA VIWANJANI AIBUKA MSHINDI M-MPESA

Meneja Matukio wa Kampuni ya Vodacom, Rukia Mtigwa (kulia) akizungumza na simu Dar es salaam wakati wa kutafuta washindi waliochangia timu za Yanga na Simba kupitia M-PESA ambao watapata tiketi za VIP pamoja na maradhi popote walipo na kuja kuangalia mpambano wa watani wa jadi utakaopigwa jumamosi hii kushoto ni Msimamizi kutoka bodi ya Michezo ya Kubahatisha,Chiku Saleh.(Picha na Rajabu Mhamila)

KAMPUNI ya simu za mkononi Vodacom imeendesha bahati nasibu ya Vodafone M- PESA kwa ajili ya kuwapa fursa wapenzi na mashabiki wa Klabu ya Simba na Yanga kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara ya watani wa jadi itakayofanyika Oktoba 31 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Jumla ya washindi 10 walipatikana katika bahati nasibu hiyo ambapo kila mshindi atakabidhiwa tiketi mbili pamoja na jezi mbili ambapo washindi watano ni wa Klabu ya simba huku watano wakiwa ni wa klabu ya Yanga.
Washindi hao kwa upande wa Simba ni mdau wa viwanjani Rajabu Mhamila 'Super D', Adam Chonya, Husein Lingu, Marry Kaduguda na Thabit Kaisari huku washabiki wa Yanga wakiwa ni Issa Kasim, Ramadhan Fulle, Muhidini Omari, Idrisa Mohamed na Mambo Mkediyo.Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa kuwataja washindi hao Meneja Matukio wa Vodacom Rukia Mtingwa alisema jumla yamashabiki 240 waliweza kuzichangia timu hizo za Simba na Yanga kupitia huduma hiyo ya M-PESA .
Alisema kati ya mashabiki 240 ni mashabiki 52 walifanikiwa kuingia katika bahati nasibu hiyo kwa upande wa Simba huku Yanga ikiwa na mashabiki 57 ambapo kati yao ni mashabiki 10 ndio waliofanikiwa kupata nafasi hiyo ya kushuhudia mechi ya watani wa jadi hao.
Alisema mpango huo wa kuzichangia timu za Simba na Yanga utakuwa ni endelevu na kwamba wapenzi na mashabiki wa timu hizo wanatakiwa kujiunga na huduma hiyo ili kuziwezesha timu hizo kupata fedha zitakazosaidia kuendesha klabu hizo.
Rukia alisema wapenzi na mashabiki wanatakiwa kuzichangia timu hizo kuanzia kiasi cha sh 2,000 ambapo wapenzi wa Yanga watatuma ujumbe huo kwenda namba 200200 huku mashabiki wa Simba wakituma kwenda namba 500500.

MAKAI MORINGA YADHAMINI MISS UTALII ILALA

Mkurugenzi Mtendaji Makai Enterprises Eileen Kasubi ( kushoto) akiwakabidhi zawadi washiriki wa kinyang`anyiro cha Miss Utalii Ilala.

Na Rajabu Mhamila "Super D"

MAKAI Moringa Enterprises, jana imejitokeza kudhamini mashindano ya kumsaka malkia wa Utalii kanda ya Ilala 'Miss Utalii Ilala 2009', yatakayofanyika November 6 katika Ukumbi wa Da West Inn Park uliopo Tabata Dar es Salaam.
Udhamini wa kampuni hiyo utaigharimu sh. 750,000, ikiwa ni gharama za bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Eileen Kabusi, alisema wameamua kutoa zawadi hizo za asili ili kulinda afya za warembo hao pamoja na kuvutwa kwao na mashindano hayo ya Utalii.
Mashindano hayo yatawashirikisha warembo 15, wanaoendelea na mazoezi katika ukumbi wa Dar west Park, Tabata jijini Dar es Salaam.Aliwataja warembo watakaopanda jukwaani ni Flora Nicholaus (22), Edna Endrew (20),Janneth Samson (19), Sheila Said Baamary (23), Sauda Ramadhani (22), Ratifa Iddy (20), Rechal Isaya(19) na Jamida Abdu (21).
Warembo wengine ni Tickey Lighton (21), Agenss Deogratius(20), Grace Msuka(20), Glory Joseph(21), Violeth Mganga (21), Neema Mashala (21) na Rose Luner(21).
Wadhamini wengine katika mashindano hayo ni Chiken Hut Tanzania Limited, Savannah Lounge Paradise City Hotel, Kelken Fitness Center, Dage Saloon, Kiwanga Store & C0, Aucland Tours & Safari, The Grand Villa Hotel, Mashujaa Pub na Sayona Drinks Water.
Wengine ni Moringa Oleifera, Image Smart, Valey Spring, Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan Zungu, VAM General Supply, Victor na Kariakoo, Mama Vanessa, Tigo, Babu Kubwa Magazine & OK News Week, Kiu, Sun, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azan.

Tuesday, October 27, 2009

TUMPIGIE KURA BLACK RHINO - BADO SIKU MBILI

Msanii Black Rhino amechaguliwa kuwa mmoja wa wasanii wanaoshindania tuzo za Afrika za Chanell O (Music Awards 2009) akiwa ametajwa kwenye kategori mbili yaani MOST GIFTED EAST AFRICA VIDEO na MOST GIFTED HIP HOP VIDEO.Uongozo wa Chanel O ulitangaza majina ya wasanii wanaowania tuzo hizo kwa mwaka huu kwenye kikao cha wandishi wa jijini Johansburg Afrika Kusini ambapo msanii Black Rhino toka Tanzania alitajwa kuwa tuzo hizo mbili.
Black Rhino anawahimiza sana wa Tanzania waliyo ndani na nje ya nchi kumpigia kura nyingi ili aweze kuibuka mshindi, kwani kushinda kwake katika tuzo hizi kutailetea heshima kubwa Tanzania.JINSI YA KUPIGA KURA

MOST GIFTED EAST AFRICA VIDEO
tuma Nambari 13 E kwenda +27 83 92 0 84 00

MOST GIFTED HIP HOP VIDEO
Tuma Nambari 10F kwenda +27 83 92 0 84 00

Au unaweza pia kumpigia kura kwa kupitia www.channelo.tv au www.channelo.co.za au www.oboma.net

Tuzo za Channel O Music Video Awards 2009 zitafanyika Alhamisi Oktoba 29, 2009 Carnival City, Johanesburg Afrika Kusini.

Albamu ya Black Rhino inaitwa Usipipme inajumla ya nyimbo kumi na iliingia sokoni Februari 2008 na inasambazwa na GMC Mwananchi.

TIKETI ZA MCHEZO WA SIMBA NA YANGA KUANZA KUUZWA JUMATANO

Shirikisho la kandanda la Tanzania limetangaza vituo na viingilio katika Mchezo wa Dar es Salaam Young Afrikan dhidi ya watani wao wa Jadi wekundu wa msimbazi Simba mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara utakaochezwa Oktoba 31 katika Dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela amefahamisha kuwa Matayarisho yote ya mchezo huo yanakwenda vizuri na Tayari TFF imefanya vikao mbalimbali.
Amesema tiketi zinapatika katika vituo 15, vituo hivyo ni Shule ya Benjamini Mkapa,Big Bon Kariakoo, Big Bon Mbagala, Stears zote, Oil Com Veta, Uwanja wa Uhuru, Sabco Mwembe Chai, Kobil Buguruni, Njia panda ya Tabata, Sheli Ofisi ya Miundo Mbinu, Mtoni Mtongani, na vituo vyote vya plisi Tandika.
Tiketi zitaanza kuuzwa Jumatano Asubuhi katika vituo vyote ambavyo vimetajwa na tiketi hizo zitauzwa kwa siku tatu na siku ya Jumamosi hakuna tiketi itakayouzwa uwanjani siku ya mchezo wa Yanga na Simba.
Naye Katibu Mkuu wa Dar es Salaam Young Afrikan Laurence Mwalusako amesema kwamba timu yake imejiandaa vizuri katika mchezo dhidi ya Simba na amewaomba mashabiki wa Yanga wawe na nidhamu katika mchezo huo.
Akielezea kibali cha Kocha Kostadin Papic Mwalusako amesema anakifuatilia ili katika mechi ijayo awepo katika benchi
Katibu wa wekundu wa Msimbazi Simba Mwina Kaduguda alipotakiwa aelezee maandalizi ya timu yake alikuwa na haya ya kusema.Wakati huo huo wachezaji wa Dar es Salaam Young Afrikan Moses Odhiambo na Amir Maftah walioadhibiwa na kamati ya mashindano kutocheza michezo mitatu baada ya ukosefu wa nidhamu kumtukana mwamuzi katika mchezo wa Yanga dhidi ya Azam FC Oktoba 17 mwaka huu wameachiwa huru baada ya ushahidi kutokamilika.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Shirikisho la Kandanda Tanzania TFF, Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu na usuluhuishi Kamanda Alfred Tibaigana amesema jana walikutana kujadili masuala hayo na walipoangalia makosa waliyoadhibiwa hayakuwa na ushahidi wa maandishi

TAIFA STARS YATANGAZWA, TAYARI KUIVAA MISRI

Kikosi cha wachezaji 31 kinachounda timua Taifa ya Tanzania Taifa Stars kimetangwazwa rasmi hii leo katika ukumbi wa Tff watakaokwenda Nchini Misri kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki Novemba Tano mwaka huu nchini humo.
Akizungumzia utaratibu mzima wa utakaokuwepo mara baada ya kutangazwa majina ya wachezaji hao Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Nchini Tff Fredrick Mwakalebela amesema kambi ya timu hiyo itaingia rasmi Novemba moja mwaka huu.
Mwakalebela ameongeza kuwa TFF litaendelea kutafufa michezo mingi ya kirafiki ya kimataifa ili iweze kufanya vizuri ikiwa pamoja na kujiandaa na michuano ya Four National Tournament na kombe la Challenge.
Majina yaliyotangazwa ni pamoja na: -
Magolikipa
Ally Mustafa - Simba
Shabani DIhile - JKT Ruvu
Shabani Kado - Mtibwa
Mohammed Mwarami - Ferroviaro Maputo

Deffenders
Aggrey Morris - Azam
Shadrack Nsajigwa - Yanga
Erasto Nyoni - Azam
David Naftari - SImba
Nadir Haroub - Vancouver, Canada
Kevin Yondani - SImba
Salum Swedi - Azam
Juma Jabu - Simba
Steven Mwasika - Moro United

Midfielders
Nurdin Bakari - Yanga
Ibrahimu Mwaipopo - Azam
Juma Nyoso - SImba
Shamabi NDiti - Mtibwa Suger
Abdurahim Amour - Mtibwa
Henry Joseph - Kongsvinger, Norway
Rashid Gumbo - African Lyon
Mwinyi Kazimoto - JKT Tuvu
Kigi Makasi - Yanga
Nizar Khalfani - Vancouver,Canada
Saidi Mohammed - Moro United

Forwards
Mrisho Khalfani Ngasa - Yanga
Mbwana Samata - African Lyon
Mussa Hassan Mgosi - Simba
Dani Mrwanda - Simba
John Bocco - Azam
Jerson Tegete - Yanga
Zahoro Pazi - Mtibwa Suger

wachezaji waliyoitwa timu ya taifa toka timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 na 17
Amani Kiata - Moro United U-20
Thabit - African Lyon U-17
Himid Mao - Azam FC U-20
Thomas Emmanuel - TSA U-20
Yusuf Abbas Soka - African Lyon U-20

JOHN BOCCO "ADEBAYOR" MCHEZAJI BORA SEPTEMBA

Jumla ya kura 209 zimempa nafasi Mshambuliaji wa Timu ya Azzam na timu ya Taifa ya Tanzamnia Taifa Stars John Bocco maarufu Adebayo kuwa mwanamichezo bora kwa mwezi Septemba Mewaka huu.
Akitaja matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari ambao ndio waliopiga kura hizo Katibu Mkuu wa TASWA Kigoba Mgaya amesema John Bocco ameibika kidedea kati ya wagombea watatu waliochaguliwa na Waandishi ambapo ni Kocha Mkuu wa Timu ya Simba Patrick Phiri na Mwanariadha Mary Naali.
Wakati huohuo Mgaya ameongeza kuwa Tamasha la Waandishi wa Habari ambalo lilikuwa lifanyike Novemba moja mwaka kuu kuwa watatangaza utaratibu mzima itakavyokuwa hapo kesho kutwa.

SERENGETI WASEMA TOTO NDIYO ILIYOWATENGA

Waliokuwa wadhaminui wakuu kwa miaka miwili wa timu ya Toto African ya Mwanza, ambao ni watengenezaji wa Bia ya Serengeti wamesema sababu kubwa ya kujitoa kuidhamini timu hiyo ni kutopewa ushirikiano wa kutosha na Viongozi wa klabu hiyo..
Akizungumza na kipindi cha michezo cha Radio Times FM Afisa uhusiano wa Kampuni hiyo Teddy Mapunda ametanabaisha kuwa mbali na kujitoa kwenye Udhamini huo lakini wanaendelea kuisaidia timu kwa kuwapa fedha ambapo wiki iliyopita waliwapa shilingi milioni 5 na wanategemea hivi karibuni kuwapa tena milioni tano.
Timu ya Toto African mpaka sasa inashika nafasi ya mwisho katika msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara ambapo katika michezo kumi iliyokwisha cheza imetoka sare michezo minne na kufungwa michezo yote na kujikusanyia pointi 4.

UMEME WAATHIRI KOMBE LA DUNIA

Wakati Tanzania ikiwa umegubikwa na mgao wa Umeme huko katika Jimbo la Kano mnchini Nigeria kimetokea kituko cha Mwaka wakati umeme ukiwa umekatika uwanjani na hivyo mchezo kuongezwa kwa dakika 14 za ziada .
Kamati ya michuano ya Jimbo hilo la Kano linalosimamia michuano ya Kombe la Dunia la chini ya miaka 17 limesema kuwa tatizo kama hilo halitotokea tena.
Matatizo hayo yalitokea katika mtanange wa kundi E baina ya USA na Hispania ikiwa nyuma kwa bao 1 Hispania ikiifunga USA mabao 2 kwa 1.
Jack McInerney aliiongozea USA kwa bao la Dakika ya 4 huku Borja akiichomolea Hispania kabla ya Pablo Sarabia kushindilia msumari wa mwisho dakika 8 baadaye.
Mtanange mwingine utaendelea kesho baina ya Malawi dhidi ya USA huku UAE wakicheza na Hispania katika kundi E.
ARGENTINA WALIZWA NA UJERUMANI
Katika Michuano ya Kombe la Dunia chini ya umri wa miaka 17 inayoendelea huku Nigeria katika Dimba la Taifa la Abuja Ujerumani imeiliza Argentina bao 1-0 goli la ushindi limesukumizwa wavuni na Mshambulizi Mario Jose katika dakika ya 8 ya mchezo.
Japan imeizima Uswisi 2-0 kwa mabao ya Mshambulizi Takumi Miyayoshi katika dakika ya 9 na 20 katika Dimba la Tesilim blogani huko Lagosi.
Usiku huu Saa tatu usiku Majira ya Afrika Mashariki Wenyewe Nigeria watawakaribisha vilivyo Honduras huko Mji Mkuu wa Abuja wakati Huko Lagos Wana Samba Brazil watachuana na Mexico.

TIGO YA MWAGA VIFAA VYA MICHEZO SHIMIWI

Ofisa Uhusiano na Udhamini wa Kampuni ya Tigo, Jackson Mmbando (kushoto) akimkabidhi vifaa Kamishina wa Uhamiaji anayeshughulikia Sheria katika Wizara ya Mambo ya Ndani, Magrusi Hulungi vifaa hivyo michezo mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milion.6.8 kwa ajili ya mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea mjini morogoro,
anaye shuhudia kulia ni Kamishina anaeshuhulikia vibari. Bariki Shayo.(Picha na Rajabu Mhamila)

MTANGAZAJI WA RADIO TIMES FM AJITOSA UCHAGUZI TBF

Mgombea wa Kamishina wa watoto katika Shirikisho la Mpira wa Kikapu Taifa Selemani Semunyu (kushoto) mtangazaji wa Radio Times FM akirundisha fomu ya kugombea nafasi hiyo Dar es Salaam kwa Ofisa Kumbukumbu Mwandamizi wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Adola Said.(Picha na Rajabu Mhamila)Selemani Semunyu wa pili kushoto, akizungumza neno na mdau mkuu wa viwanjani mwenye tisheti ya njano, pamoja na Adamu huseni mwenye tisheti nyekundu na Hussein Musa Mhassa wote wafanyakazi wa Radio Times FM.