Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, August 31, 2009

TUWAPIGIE KURA AY & SHAA

Msanii Abwene Yessayah 'Ay' akiimba wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari Dar es salaam kuhusu kuuchaguliwa kuwania tuzo za wasanii ya My video ambayo yameandaliwa na MTV na zain kama sehemu ya Tuzo za Muziki Afrika (kulia) ni msanii Sarah Kais 'SHAA'ambap yeye na AY wamechaguLiwa kushiriki katika tuzo hiyo.(Picha na Rajabu Mhamila)

MSONDO KAZINI!!!

Waimbaji wa bendi ya Msondo ngoma music, kushoto ni Rashidi Mwezingo 'Silver Boy' na Isihaka Katima 'Dj Papa upanga', wakiwajibika wakati wa onesho lao lililofanyika wiki iliyopita katika ukumbi wa Afri center.(Picha na Rajabu Mhamila)

Sunday, August 30, 2009

SIMBA YAJIFICHA IRINGA KABLA YA KUIKABILI TOTO AFRICA

Ikiwa ni siku moja baada ya kujikusanyia pointi tatu na kufikisha jumla ya pointi sita katika michezo miwili ya kwanza ya ligi kuu mnyama Simba sasa anataraji kuweka kambi mkoani Iringa kabla ya kukutana na wanakisha mapande Toto Afrika katika uwanja wa Uhuru.
Meneja wa timu ya Simba Innocent Njovu amesema wamefikia maamuzi hayo ya kuweka kambi mkoani Iringa ili kuwapa maandalizi mazuri wachezaji wake ili kuhakikisha wanaendelea kushinda.
Kuhusu Mchezaji Uhuru Suleimani ambaye ajana wametangaza rasmi kukamilisha taratibu za kumsajili, Njovu amesema kocha anamuangalia katika mazoezi.

MATOKEO YA LIGI KUU TANZANIA BARA 29, AGOSTI 2009


Mchezaji wa Bernad Nguya wa Manyema United akimtoka Athumani Idd wakati wa mchezo wa ligi ya vodacom mchezo uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jana,Yanga ilishinda bao3-0.Amir Maftah wa Yanga (kulia) akimtoka mchezaji wa timu ya Manyema United Sixbart Mohamed kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mchezo uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jana ,Yanga ilishinda bao 3-0.
Yanga 3 - 0 Manyema Rangers

Jery Tegete dk 24, 83
Mike Barasa dk 45 (pt)

Tanzania Prison 0 - 1 Tanzania Prison

David Naftali dk 72

Maji Maji 0 - 1 JKT Ruvu

Hussein Bunu

UHURU SELEMANI RUKSA KUCHEZA SIMBA "NI BAADA YA MTIBWA KUPEWA MILIONI NANE"

Wekundu wa msimbazi Simba tayari wameshamalizana na klabu ya Mtibwa Sugar juu ya mchezaji Uhuru Selemani baada ya kutakiwa kutoa kitita cha shilingi milioni 8 katika mtafaruku uliodumu kwa wiki kadhaa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Simba Msemaji wa Timu hiyo Cliford Ndimbo amesema suala hilo walimalizana siku ya jumamosi katika ofisi za Tff na viongozi wa Mtibwa na tayari wameshatoa kiasi cha shilingi milioni 4 na kiasi kingine kilichobaki watalipa kwa awamu.
Ndimbo amesema Simba imefurahishwa na kitendo cha Mtibwa kuonyesha uungwana kwa kuweza kufikia muafaka na kuwakubalia mchezaji huyo lakini anawaomba busara zilizotumika na wao basi zitumike kwa kumalizana na Coastal Union.

SERENGETI BOYS JUMATATU KUSAKA NAFASI YA TATU SUDAN

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys Jumatatu 31, Agosti 2009 watacheza na timu ya taifa ya vijana ya Sudan kuwania nafasi ya tatu ya michuano ya Chalenji.

Serengeti Boys imefikia hatua hiyo baada ya kufungwa katika mchezo wa nusu fainali na Uganda siku ya Ijumaa kwa kufungwa jumla ya magoli 5-3 kwa mikwaju ya Penati baada ya kumaliza dakika 120 huku wakiwa wamefungana 1-1.

Wednesday, August 26, 2009

TIMU YA VIJANA YA TAIFA YA MPIRA WA MIKONO YAENDA BURUNDI


Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya mikono wakiwa na bendera yao baada ya kukabidhiwa Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la michezo Tanzania Mohamed Kiganja kwa ajili ya kwenda kushiriki mashindano ya Chalenge kwa vijana wa chini ya miaka 20 Bujumbura Burundi.(Picha na Rajabu Mhamila)

Sunday, August 23, 2009

KLABU ZA LIGI KUU HIZI HAPA!!!

Yanga iliyo chini ya udhamini mnono wa mfadhili wao, Yusuph Manji wamesajili kikosi cha wachezaji 30 huku wengi wao wakiwa walioipa ubingwa timu hiyo katika msimu uliopita.
Ndani ya kikosi hicho kuna sura mpya za wachezaji wanane ambao sita kati yao ni wachezaji wa kigeni ambao pia wametoka katika timu kongwe Afrika Mashariki.
Wachezaji hao wapya waliomwaga wino Jangwani ni kipa Nelson Kimati aliyetokea Prisons ya Mbega na beki Bakari Mbegu aliliyesajiliwa kutoka katika timu ya Sifa Politan SC inayoshiriki ligi ngazi ya Wilaya ya Temeke.
Yanga iliyochini ya uongozi wa Mwenyekiti Iman Madega ilifanikiwa kunasa saini za wachezaji wa kulipwa Moses Odhiambo kutoka APR ya Rwanda, Kabongo Honore wa DR Kongo, Steven Bengo kutoka SC Villa ya Uganda na Jama Robert Mba kutoka Canon Sportif Yound ya Cameroon.
Pia Yanga walimaliza utata wa wachezaji wake waliowasajili katika dirisha dogo la msimu uliopita lakini wakakosa nafasi ya kuitumikia klabu hiyo John Njoroge na Joseph Shikokoti kutoka Tusker ya Kenya.
Mbali na vifaa hivyo vilivyoongezwa katika kikosi hicho cha Kondic akisaidiwa na Spaso Sokolovics lakini Yanga wamebakisha vifaa vyake muhimu ambavyo vilipeleka shangwe Jangwani kwa misimu miwili iliyopita.
Vifaa hivyo ni Steven Marash, Wisdom Ndhlovu, Athumani Idd 'Chuji', Nurdin Bakari, Nadir Haroub 'Cannavaro', Michael Barasa, Boniface Ambani, Fred Mbuna, Godfrey Boniface, Mrisho Ngassa, Amir Maftah, Obren Curkovic, Shadrack Nsajigwa, Abdi Kassim, Kigi Makasi, Shamte Ali, Vicent Barnabas, Hamis Yusuph na Jerson Tegete.
Wapinzani wa Yanga katika mbio za ubingwa msimu huu wa 2009/10 ni Simba, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Majimaji, Manyema, JKT Ruvu, Prisons, Moro United, Toto African, Azam FC na African Lyon.
Miaka ambayo Yanga imetwaa ubingwa tangu ligi hiyo ianzishwe ni 1965, 1968, 1969, 1970, 1971, 1974, 1981, 1983, 1987, 1991, 1996, 1997, 2000,2003, 2005, 2006, 2008 na 2009.
Katika usajili wa Simba msimu huu wamefanikiwa kubakisha wachezaji wake wote wa kutumainiwa huku wakiongeza nguvu kwa kusajili wachezaji wapya tisa wakiwemo wa kigeni watatu.
Simba iliwatema wachezaji wake Moses Godwin, Ramadhani Wasso, Nasor Said, Amani Simba na Orji Obinna kutokana na sababu mbalimbali.
Katika kuziba mapengo ya wachezaji waliowaacha na kuongeza nguvu klabu hiyo iliwarudisha wachezaji wake Juma Kaseja aliyesajiliwa Yanga msimu uliopita, Danny Mrwanda aliyekuwa anacheza soka Kuwait.
Mbali na kuwarudisha wachezaji hao walisajili wachezaji wa kigeni, Hilary Echessa wa Kenya, Emmanuel Okwi wa SC Villa ya Uganda na Mganda Joseph Owino kutoka URA ya Rwanda.
Pia waliowaongeza wachezaji Salim Aziz wa Polisi Dodoma,
Amri Kiemba wa Moro United, Uhuru Seleman wa Mtibwa Sugar na Haruna Ramadhani kutoka Toto African.
Vifaa vya Simba vilivyobaki msimu uliopita ambao watakuwa na jukumu la kuwaonesha njia wachezaji wapya ni Haruna Moshi 'Boban', Salumu Kanoni, Kelvin Yondani, Nicco Nyagawa, Adam Kingwande na Musa Hassan 'Mgosi'.
Wengine ni George Nyanda, Ulimboka Mwakingwe, Antony Matangalu, Mohamed Banka, Ramadhani Chombo, Ali Mustapha 'Barthez', Meshack Abel, Jabir Aziz, Deo Munishi, Juma Jabu, Juma Nyoso, Mohamed Kijuso na David Naftar.Wachezaji wapya waliosajiliwa kwa msimu wa 2009/10 ni Shaaban Aboma kutoka Toto ya Mwanza, Faustine Lukoo kutoka Miembeni, Pius Kisambale kutoka Moro United, Erick Majaliwa na Monja Liseki kutoka Shaab Hadhramout ya Yemen, Steven Mazanda kutoka FC Lupopo ya Jamhuri ya Congo na Said Rashid ambaye ni mchezaji huru.
Wachezaji wa zamani wa Mtibwa waliosajiliwa ni Shaaban Kado, Soud Slim, Omar Ally, Obadia Mungusa, Idrissa Rajab, Geoffrey Magori, Chacha Marwa, Shaaban Nditi, Abdulhalim Humoud, Zuberi Katwila, Zahoro Pazi, Saidi Mkopi, Akilimali Yahaya, Yussuf Mgwao, Uhuru Selemani, David Mwantobe, Omar Matuta, Mwamba Mkumbwa na Soud Abdallah.Kikosi kamili cha African Lyon msimu huu kitaundwa na wachezaji Noel Lucas, Stephano Mkomola, Hamad Waziri, Idrissa Abdallah, Abdallah Mpandachi, Victor Tumbanga, Abdul Mwalami, Yahya Abdallah, Hamis Shengo, Sultan Ali, Mbwana Samata, Mohamed Salehe na Yusuph Soka.
Wengine ni Aziz Issa, Godfrey Komba, Mohamed Samata, Rashid Gumbo, Said Kassimu, Zuber Ubwa, Bakari Omary, Karume Songoro, Castory Mumbala, John Mbugua na Robert Ssentongo.
Wachezaji waliongezwa katika kikosi cha Azam na kufanya kuwa na kikosi cha wachezaji 23 katika msimu huu ni Agrey Morrice kutoka Mafunzo ya Zanzibar na Salum Swedi wa Mtibwa Sugar.
Wachezaji waliotemwa Azam ni Salvatory Ntebe, Shekhan Rashid, James Victor, James Adriano, Malegesi Mwangwa, Paul Nyangwe, Ali Alawi, John Mabula, Kassimu Alimbe Kilungo, Adam Shomari, Yusuph Gogo, Musa Kipao, Zuberi Ubwa, Said Nachikongo na Abdul Hamza.
Pamoja na kuwa na idadi ndogo ya wachezaji katika kikosi hicho lakini timu hiyo imesheheni wachezaji wengi wenye uzoefu wa michuano mbalimbali.
Wachezaji ambao walikuwa na kikosi hicho katika msimu uliopita ambao tayari watakuwa wameshaelewana vya kutosha ambao watakuwa ni chachu ya kufanya vizuri kwa timu hiyo katika msimu huu ni Crinsine Odula, Danny Wagaluka, Erasto Nyoni, Habibu Muhina, Ibrahimu Mwaipopo, Ibrahimu Shikanda, Jamal Mnyate, John Bocco, Luckson Kakolaki, Malika Ndeule, Maridadi Haule, Nsa Job, Osborn Monday, Philip Arando, Said Swed, Salumu Aboubakary, Salumu Machaku, Shabani Kisiga, Yahya Tumbo, Vladimir Niyonkuru na Ben Karama.Kikosi kamili cha maafande wa Prison kwa msimu huu ni Exavery Mapunda, Henry Mwalugala, Laurian Mpalile, Aloyce Adam, Mbega Daffa, Patson Chawinga, Fred Chudu, Ismail Suleiman, John Matei, Shaaban Mtupa, Said Mtupa, Said Mtupa, Misango Magai, Lugano
Mwangama,Sudi Ahadi, Roy Shamba, Ramadhani Katamba, Hashimu Kaongo, David Mwantika,Thomas Baragula na Sylvester Kamtande.JKT Ruvu msimu uliyopita walimaliza ligi wakiwa nafasi ya nne kwa kujivunia pointi 33 na Prisons walimaliza ligi wakiwa katika nafasi ya sita.
JKT Ruvu inaongozwa na Kocha Charles Kilinda ambaye kwa kiasi kikubwa ameifanya timu hiyo kuwa tishio katika ligi ya msimu uliopita na msimu huu imesajili wachezaji 26.
Wachezaji walioachwa ni Enock Mkama, Jumanne Ally, George Osei, Buji Selemani, Munubi Mrisho, Mashaka Maliwa, Gerald Crisant na Lucas Simon.
Wachezaji 26 waliosajiliwa ni Abdallah Ngachimwa, Kessy Mwapande, Rashid Matambo, Shaibu Nayopa, Hassan Kikutwa, Boniface Mwakamele, Sostenes Manyasi, Furaha Tembo, Haruna John, Gryson Kundakila, Amos Mgisa, Bakari Kondo na Abdallah Bunu.
Wengine ni Hussein Bunu, Fullu Masanga, Oscar Gasupina, Shaibu Ally, Charles Thadei, Kisimba Luambano, Simon Shadrack, Mayuki Rajabu, George Minja, Shaaban Dihile, Mwinyi Kazimoto, Damas Makwaya na Stanley Nkomola.Wachezaji waliyosajiliwa na Klabu ya Kagera Suger ni Victor kutoka Uganda na Said Biyunga na Msafiri Juma wote kutoka timu ya Toto African ya Mwanza, Godfrey Taita na Geore Kavira kutoka Villa Squard.
Wengine ni Azoro Ndege kutoka katika timu ya mtaani ya Tumbi ya Kigamboni, Dar es Salaam ambaye uongozi wa timu ya Kagera Sugar ulimwona akiwa anacheza katika Kombe la Taifa katika mkoa wa Temeke na hivyo kuvutiwa naye.
Wengine kuwa ni Sayuni Japhet na Aswele Asukile wakitokea timu ya Yono wilayani Njombe, Iringa ambao walikuwa wakicheza mchuano wa Kombe la Taifa katika timu ya mkoa wa Iringa uliofanyika katika kituo cha Mbeya na walivutiwa na uongozi wa timu hiyo, waliotumwa kwenda mkoani Mbeya kuangalia mchuano hiyo ili kuweza kuwapata wachezaji wapya wachanga wa kuweza kuwasajili.
Makipa Rucheke Musa kutoka timu ya Reli Kigoma na Divito Thomas kutoka katika timu ya Victor nchini Uganda ambayo iko Ligi Kuu nchini humo na ndiye golikipa namba moja wa timu hiyo, ambapo Asukile naye ni golikipa kwa hiyo msimu huu wameamua kusajili makipa watatu wachanga.Kikosi cha Manyema kitakachopambana katika msimu huu ni pamoja na kipa mzoefu Oddo Nombo, Amouh Zulu, Yusuph Silas, Adam Matunga, Mussa Kipao, Patrick Mrope,
Mernard Mgaya, Buju Suleiman, Victory Mwambo, Khalid Sabebe na Boniface Bwilu.
Wengine ni Hamad Mumbi, Mzee Mayala, Ali Suleiman, Shabani Ramadhani, Daudi Maganga, Sandey Juma, Yusuph Nguya, Sixbert Mohamed, Thimos Paul, Musa Omary, Mohamed Khatibu, Julius Mrope, Waziri Khatibu, Benedick Ngassa, Khalfan Omary, Humund Juma na Ali Mohamed.Picha ya timu ya Maji Maji miaka ya Nyuma.
Timu ya Majimaji iliundwa mwaka 1978 mkoani Ruvuma ikitekeleza agizo la Mlale la Siasa ni kilimo ikiambatishwa pamoja na masuala ya kukuza na kuendeleza mkoa katika nyanja za michezo.
Hatua hiyo ilibuniwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa wakati huo, Dkt, Lawrent Mtazama Gama kutokana na mkoa huo kuwa nyuma kisoka, hali ambayo ilikuwa ikisababisha timu kutoka katika mkoa huo kujikuta zikifungwa mabao mengi zaidi ya 10 pale zinapopata nafasi ya kuwakilisha katika mashindano mbalimbali ya kitaifa.
Je baada ya kufanikiwa kurejea katika ligi kuu TAnzania Bara msimu huu, itaweza kuhimili mikiki kama ilivyohistoria ya klabu hiyo toka Mkoa wa Ruvuma?TOTO African imechukua hadhi ya Pamba ambayo iliufanya mkoa wa Mwanza kutamba katika medani ya soka kwa muda mrefu huko nyuma.
Ikiwa imeanzishwa mwishoni mwa miaka ya 1960, timu hiyo yenye uhusiano wa kidugu na timu ya soka ya Yanga ya Dar es Salaam ina wanachama wasiozidi 50, iliwahi kucheza katika Ligi Kuu mwishoni mwa miaka ya 90 na mwanzoni mwa mwaka 2000 kabla ya kushuka daraja.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro amewataka wananchi wa Mwanza kuwa kitu kimoja katika kuisaidia Toto na kuitaka timu hiyo ijiepushe na kujihusisha na timu moja kubwa kwani hali hiyo inagawa nguvu za wananchi.
Katibu Mkuu wa kwanza kuajiriwa na TFF, Asheri Gasabile, anasema kuwa, ni faraja kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza, kutokana na timu hiyo kubaki Ligi Kuu.
Kocha Choke Abeid anasema uongozi wa Toto African unatakiwa kuboresha dawati la ufundi la timu ya hiyo, baada ya uboreshaji kazi kubwa itakuwa ni kutengeneza timu ya ushindi, kama mwalimu atahakikisha timu inafanya vizuri, ingawa ni kazi ngumu ,
kwa sababu wapenzi wa soka wa Mwanza wangali na hofu na timu yao.

Saturday, August 22, 2009

RATIBA YA LIGI KUU TANZANIA AGOSTI 23

23. Aug. 2009. 1 YANGA AFRICAN LYON UHURU DAR ES SALAAM
23. Aug. 2009. 2 MAJIMAJI SIMBA MAJIMAJI RUVUMA
23. Aug. 2009. 3 MTIBWA SUGAR MANYEMA RANGERS MANUNGU TURIANI
23. Aug. 2009. 4 TANZANIA PRISONS JKT RUVU SOKOINE MBEYA
23. Aug. 2009. 5 KAGERA SUGAR AZAM KAITABA KAGERA
23. Aug. 2009. 6 TOTO AFRICAN MORO UTD KIRUMBA MWANZA

ILALA YATAMBA MBEYA - POOLTABLE


ILALA oyeeeeeeeee....!!!! ndiyvyo wanavyoonekana katika picha wakishangilia baada ya kufanikiwa kutinga fainali.
Wachezaji wa Pool table wa Mkoa wa Ilala wakishangilia baada ya timu yao kutinga fainali ya mashindano hayo jijini Mbeya yanayo dhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania kupitia bia ya Safari Lager ambapo walikuwa wanatarajia kuchuana na timu ya mkoa wa Temeke katika fainali.(Picha na Rajabu Mhamila)

POOLTABLE TANGA YA FANA!!!


Mchezaji wa Pool table wa Mkoa wa Tanga, Zainabu philipo, akijiandaa kupiga mpira wakati wa mashindano ya taifa ya mchezo huo kwa wanawake katika hatua ya kuingia nusu fainal yanayodhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania kupitia bia ya Safari Lager jijini Mbeya jana ...(Picha na Rajabu Mhamila)

Thursday, August 20, 2009

YANGA - WACHEZAJI WA KIGENI WALIYOGOMA KUTINGA KAMBINI KUKIONA

Wachezaji wakigeni wa Yanga sasa Kuchukuliwa adhabu kali na uongozi wa klabu ili kutoa mfano kwa wachezaji wengine na kuhakikisha nidhamu inajengeka katika klabu hiyo yenye mashabiki nchini Tanzania.
Lukas Antony Kisasa ni katibu mkuu wa klabu ya Yanga amesema wanachosubiri ni ripoti toka kwa kocha mkuu wa klabu hiyo Prof. Dusan Condic.
Amesema wachezaji ni watovu wa nidhamu, amesema inashangaza kuona wachezaji wa nyumbani wakiwa kambini huku wachezaji wakikataa kuungana na wenzao kwa madai Jengo la Yanga hallina hadhi ya kukaa mchezaji wa kulipwa huku nao wakiwa ni wachezaji wa Yanga.
Kisasa amesema hatua hiyo ya wachezaji wa kigeni ni sawa na kuwadharau wa Tanzania wengi ambao ni wapenda soka, na kuahidi kuwachukulia adhabu kali itakayokuwa mfano kwa wachezaji wote wa kigeni waliyopo hapa nchini.

DANI MRWANDA AZICHAPA NA GUMBO WAKIELEKEA SONGEA!!!

Pichani Dani Mrwanda akichuana na Rigobert Song katika mchezo wakati Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ilipochuana na Cameroon mwaka jana katika uwanja mpya wa Taifa.
Mchezaji dani Mrwanda wa wekundu wa Msimbazi wakati wa safari ya klabu hiyo kuelekea Songea tayari kukipiga na Maji Maji katika mchezo wa kwanza wa ligi Kuu Tanzania Bara ambayo itaanza rasmi Agosti 23 ametajwa kuzichapa na makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Omari Gumbo.
Imebainishwa chanzo cha kuzuka ugomvi huo ni kufuatia mchezaji huyo kukaidi agizo la kuvaa jezi ya Simba, kama walivyofanya wachezaji wenzake ikiwa ni sare maalum ya klabu hiyo wakati wa safari.
Simba siku ya Jumapiliitakipiga na Maji maji ya Songea katika uwanja wa Maji maji mjini Songea.

Wednesday, August 19, 2009

AZAM FC NAYO YAIFUATA KAGERA SUGER...!!!


Timu ya Azam FC imeondoka Alhamisi Alfajiri ikiwa na wachezaji 22 na Viongozi 8 kuelekea Kagera kucheza mchezo wake wa kwanza na Kagera sukari katika uwanja wa Kaitaba mechi ambayo ni ya ufunguzi wa ligi kuu ya Tanzania Bara itakayoanza Agasti 23 mwaka huu.
Mwenyekiti Msaidizi wa Klabu ya Azam FC Said Mohammed amesema ligi kuu msimu huu itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zingine kupanda daraja na hata timu ambazo zimebaki zimezidi kujiimarisha zaidi.

SIMBA YAWASILI RUVUMA TAYARI KUKIPIGA NA MAJIMAJI

Vijana wa Mtaa wa msimbazi Simba Sports klabu tayari wamewasili Mkoani Ruvuma kucheza mchezo wake dhidi ya wana lizombe Maji Maji ya Songea ikiwa ni mechi ya ufunguzi ya michuano ya ligi kuu Tanzania Bara msimu huu itakayoanza Agasti 23 mwaka huu.
Afisa habari wa kuajiriwa wa klabu ya Simba Cliford Mario Ndimbo amesema kikosi kimeondoka na wachezaji 23 akiwemo kocha mkuu Patrick Phili,Amri Said kocha msaidizi,meneja Innocent Njovu na mkuu wa msafara, Makamu Mwenyekiti Omary Gumbo.
Ndimbo amesema dhumuni la kwenda mapema Songea ni pamoja na kuzoea uwanja ambao umefanyiwa marekebisho na hali ya hewa ya huko kabla ya kuelekea Mbeya kucheza mchezo mwingine na Tanzania Prison.
Akijibu swali kwa nini wachezaji 5 hawakwenda Songea kujiunga na wenzao Ndimbo amesema wachezaji watatu kati ya hao wana matatizo mbalimbali wakiwemo Ramadhani Chombo,Jabir Aziz ambao ni majeruhi.
Ndimbo ametanabaisha kuwa mchezaji Haruna Moshi Boban ameachwa kwa kuwa amefunga ndoa hivi karibuni lakini kwa wachezaji wawili Olimboka Mwakingwe na George Nyanda wameachwa kwa kosa la utovu wa nidhamu.

Tuesday, August 18, 2009

SIKU YANGA WALIPOFULIA KWA MTIBWA, NGAO YA HISANI IKAENDA MORO!


Makamu wa pili wa Raisi wa shirikisho la kandanda Tanzania Ramadhani Nasib akimkabidhi kapteni wa klabu ya soka ya Mtibwa Suger NGAO YA HISANI
Kushinda raha bwana asikwambie mtu, cheki jamaa wanavyofurahia ubingwa wa kihistoria kwa mara ya kwanza halafu wanatwaa Ngao ya Hisani!
Kado naye alifanya kazi kubwa kulinda lango la Mtibwa
Hapa haendi mtu!

JE HUU NAO NI MCHEZO WADAU ???



Hapo je?
Jamaa huyu ni noma!
Vipi wewe unaweza kufanya hivi?
Hapo vipi ?
Hii ilikuwa ni wakati wa mapumziko katika mchezo dhidi ya Yanga na Mtibwa katika mechi ya Ngao ya Hisani

Monday, August 17, 2009

YANGA NA SIMBA WANG`ARISHWA NA KILIMANJARO


Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) David Minja (kulia) akipeana mkono na Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Dar es salaam Lucas Antoni KIsasa baada ya makabidhiano ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi.milion.65 kwa timu za Simba na Yanga anaeshuudia wa pili kushoto ni Meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe na Mkurugenzi wa utawala na uwanachama kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) Mtemi Ramadhani.(Picha na Rajabu Mhamilaa onblur="try {parent.deselectBloggerImageGracefully();} catch(e) {}" href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhxVZK7APklDPgsZ0namtZraghTqfGvoYR6AP3JmjiBeBeDYfO7reYTG7mIf45tVM1FC0l9d65SNeJPko7BhyZKd1UWVdETUaandmrZFeOy4xs6PLWhkHx2KXMzZeCg1jZ1ZlcnWclkPQ/s1600-h/Kaduguda+vifaa.JPG">
Katibu mkuu wa kuajiriwa wa klabu ya Simba Mwina Sefu Kaduguda akikabidhiwa uzi mpya wa mnyama.

NAIBU KATIBU MKUU WA UVCCM AZURU TEMEKE!!!


Wacheza ngoma wa kikundi cha Vihata Group wakiwajibika wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Bara, Mfaume KIzigo ayupo pichani alivyofanya zihara na kufunguwa matawi ya CCM katika Wilaya ya Temeke mwishoni mwa wiki.(Picha na Rajabu Mhamila)a onblur="try {parent.deselectBloggerImageGracefully();} catch(e) {}" href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhFb1SGhC5R5PH0lvS7vixcOWgKhUKypmsf7EgFsSr7dxPAGxzbWLB01I9iOWFIjTH7y4vXldixBoGyrZRyf6JR5OVHTGgA5z7CVpKUukQ_hyaBniG9XXmlqaqp3QIm9iIxyosXkyAsIw/s1600-h/UDUKWI.JPG">

Wasiliana na mpiga picha wetu +255787406938

Thursday, August 13, 2009

VODACOM YAKABIDHI VIFAA KWA KLABU ZA LIGI KUU TANZANIA BARA

Naibu waziri wa habari, utamaduni na michezo Joel Bendera (kulia) akimpa vifaa vya ushiriki wa ligi kuu ya vodacom katibu Mkuu wa Club ya Simba, Mwina Swif Kaduguda, wakati wa sherehe za kugawa vifaa kwa Club zinazoshiriki Ligi Kuu Hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika, Dar es salaam, wanaoshuudia wa pili kushoto ni Meneja udhamini wa kampuni ya VodaCom, George Rwehumbiza na Mkuu wa kitengo cha Udhamini wa kampuni hiyo Ephraim Mafuru. Picha na Rajabu Mhamila
Mchezaji Uhuru Seleman kushoto akimtoka mchezaji mwenzake Mohamed Banka wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Kinesi Dar es Salaam jana nyuma ni kocha wa timu hiyo Patrick Phiri.

Wednesday, August 12, 2009

EAST AFRICAN MELODY KAZINI !!!


Mwanamuziki wa Taarabu Hafua Suleiman akifanya vitu vyake katika miondoko ya mitikisiko ya pwani na kundi zima la Melody Picha na Rajabu Mhamila.
Kundi la Melody likifanya vitu vyake katika ukumbi wa DDC Kariakoo Picha na Rajabu Mhamila.Mwanamuziki wa Taarabu Husna Omary akifanya vitu vyake katika onyesho la MElody lililofanyika katika ukumbi wa DDC Kariakoo Dar es Salaam.Picha na Rajabu Mhamila a.k.a Super D

Monday, August 10, 2009

STARS YAENDA RWANDA!!!


Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ama The Blues of Africa imeagwa rasmi tayari kuelekea nchini Rwanda kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya taifa ya nchi hiyo.
wakati wakiagwa wamekabidhiwa bendera na Kaimu Mkurugenzi wa Wizara ya habari utamaduni na michezo, Charles Matoke na kuwataka kurudi na ushindi.
Wachezaji watakaosafiri na timu hiyo ni Shabani Dihile, Ali Mustapha, Juma Jabu, Erasto Nyoni, David Naftar, Stephano Mwasika, Shabani Nditi, Kelvin Yondani, Juma Nyoso, Mwinyi Kazimoto, Nurdin Bakari, Razack Khalfan, Mrisho Ngassa, Jerry Tegete, Danny Mrwanda, Rashid Gumbo, Kigi Makasi, John Bocco, Zahoro Pazi na Salum Sued.
Shadrack Nsajigwa ameacha kutokana na kuwa majeruhi hivyo asingeweza kucheza katika mchezo huo lakini pia hayumo Musa Hassan 'Mgosi' katika kikosi hicho kutokana na kwenda Norway katika majaribio.
Imebainishwa pamoja ya kuwepo katika msafara huo mshambuliaji Tegete ataanzia benchi kwani alikuwa majeruhi lakini sasa ameanza kufanya mazoezi mepesi.
Naye kipa Shabani Kado anaweza kuchukua nafasi ya Dihile ambaye hali bado sio nzuri lakini amemweka katika msafara huo huku akimwangalia maendeleo ya afya yake.

TAMASHA LA SIMBA LA FANA


Na hichi ndicho kikosi kamili cha Simba
Mwenyekiti wa klabu ya Simba Hassan Dalali akimkabidhi Mheshimiwa Spika Samweli Sita moja ya Jezi mpya za klabu ambazo zitatumiwa katika msimu wa ligi kuu Tanzania bara unaotaraji kuanza Agosti 23.
Mashabiki wa Simba katika tamasha la Simba "Simba Day" ambalo lilitumiwa na klabu hiyo kutambulisha Jezi mpya za klabu hiyo pamoja na wachezaji wapya.
Simba katika SImba Day ilicheza mchezo wa kirafiki na klabu ya Sports Club Villa ya Uganda na kuibuka na ushindi wa goli 1-0.