Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, July 16, 2012

CHADEMA WASHINGTON DC YAPATA UONGOZI MPYA



Mwenyekiti mpya wa Chadema Washington Cosmas Wambura akipeana mikono ya pongezi na Katibu mpya Ndugu Isidori Lyamuya.

Tawi la Chadema Washington DC limepata Viongozi wapya walioshika nafasi za waliokuwa Viongozi wa muda. Katika Uchaguzi huo Cosmas Wambura amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda Kalley Pandukizi. Nafasi ya Katibu imechukuliwa na Isidori Lyamuya aliyechukua nafasi ya Liberatus Mwang’ombe aliyekuwa Katibu. Nafasi ya Mweka hazina imechukuliwa na Ludigo Mhagama na nafasi ya katibu mwenezi imechukuliwa na Hussein Kauzella. Nafasi nyingine zilizogombewa ni Wenyeviti na Makatibu wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee. Pia kulikuwa na nafasi ya Afisa Habari wa Chama. Akiongea baada ya Uchaguzi Mwenyekiti aliyechaguliwa ndugu Cosmas Wambura amesema atatoa ushirikiano mkubwa katika kuendeleza shughuli mbalimbaliza kukijenga Chama. Pia Katibu mpya amesema watashirikiana na Mwenyekiti na wanachama wengine wote kuhakikisha Chama kinzidi kuwa Imara na kupata wanachama zaidi.

No comments :

Post a Comment