Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, July 11, 2012

MARADONA ATIMULIWA UKOCHA AL WASL YA DUBAI



Diego Armando Maradona - Kocha aliyetimuliwa klabu ya Al Wasl

DUBAI, Falme za Kiarabu

NGULI wa soka duniani raia wa Argentina, Diego Maradona amefukuzwa kazi huko Falme za Kiarabu, alikokuwa akiinoa klabu ya Al Wasl, baada ya miezi 14 ya kufanya kazi hiyo.

Kufukuzwa kazi kwa Maradona kulitarajiwa tangu Juni, wakati bodi nzima ya klabu ya Al Wasl ilipojiuzulu, kufuatia hitimisho la msimu usio na taji.

Maradona, 51, alijiunga na Al Wasl ya Dubai Mei 2011 na hadi anafukuzwa ana salio la mwaka mzima la mkataba ambao kimsingi klabu imeuvunja rasmi.

Nyota huyo wa zamani wa soka ametimuliwa, baada ya kutoipa mafanikio tarajiwa Al Wasl, iliyomaliza ligi ikiwa nafasi ya nane kwenye msimamo.

"Kufuatia majadiliano ya pamoja kati ya Bodi ya Wakurugenzi wa Al Wasl kupitia nakutathmini benchi la ufundi chini ya kocha Diego Maradona, imeamua kusitisha kazi ya Maradona na dawati zima la ufundi," ilisomeka taarifa ya klabu kwenye tovuti yake.

Maradona, mshindi wa Kombe la Dunia akiwa na Argentina mwaka 1986, alipamba vichwa vya habari huko Falme za Kiarabu hapo Machi mwaka huu, wakati alipojiingiza katika mabishano na mgogoro na mashabiki wa timu yake.

Katika mechi hiyo ambayo Al Wasl ilifungwa mabao 2-0 kwenye Ligi ya Kulipwa ya Falme za Kiarabu ‘UAE Pro League’ kutoka kwa Al Shabab, alipanda jukwaani kujaribu kumlinda mke wake, baada ya mashabiki kuonekana kupanga kuwafanyia vurugu wake na wapenzi wa wachezaji.

Maradona alichukuliwa ili kufufua heshima ya Al Wasl ndani na nje ya dimba, lakini ikajikuta ikimaliza pointi 29 nyuma ya mabingwa Al Ain.

No comments :

Post a Comment