Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, July 19, 2012

NMB Yajenga Bwawa La Maji Iganda






Benki ya NMB mnamo tarehe 12 July, 2012 ilifungua rasmi bwawa la Iganda wilaya ya mbozi mkoa wa mbeya. Ujenzi wa bwawa hilo ulitokana na ziara ya benki hiyo kijijini hapo na kubaini kuwa na tatizo la maji kama kikwazo katika uzalishaji wa kahawa katika eneo hil. NMB iliahidi kuwasaidia wakulima katika kujenga bwawa litakalotumika kukusanya maji wakati wa mvua na kuyahifadhi kwa ajili ya matumizi wakati wa vipindi vya uhaba wa mvua.

Akizungumza katika uzinduzi huo Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB Bw. Mark Wiessing alisema “NMB ikiwa mfadhili mkuu wa mradi huo inaamini matumizi ya maji yaliyohifadhiwa katika bwawa, yanagusa maisha ya wananchi wengi wa kijiji cha Iganda na Vijiji vya jirani vinavyokizunguka, kwa vile umeongeza uzalishaji wa kahawa na ubora ambapo matokeo yake itakuwa kuuza kahawa kwa bei nzuri kwa wakulima, hatua ambayo itawawezesha kuboresha hali yao ya maisha ambalo ni lengo kuu la benki ya NMB”

 NMB imechangia jumla ya shilingi milioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa bwawa hilo wakati mchango wa nguvu za wananchi wa eneo hilo kwa njia ya Kujitolea ukiwa ni kiasi kilichobaki cha Tshs 10 million na kufanya jumla ya gharama zote za ujenzi wa bwawa kufikia shilingi milioni 40.

Katika kipindi cha zaidi ya miaka minne iliyopita tangu mwaka 2008, NMB Kanda ya nyanda za juu, imekua ikielekeza juhudi zake katika uboreshaji na uendelezaji wa zao la kahawa kwa kupitia mikopo ya Stakabadhi ya mazao ghalani. Mpango huo ulianza kwa kuanza kutoa mafunzo kwa vikundi na vyama vya ushirika vya mazao (AMCOS) vilivyotarajiwa kufanya kazi na NMB. Mpango huo wa mafunzo ulikuwa ni kuwaelimisha kuhusiana na namna mfumo wa Stakabadhi ya mazao ghalani unavyofanya kazi na mahusiano yake na wadau mbalimbali katika mnyororo wa thamani. Wadau mbalimbali waliohusika ni kama vile, viwanda vya ukoboaji wa kahawa, Bodi ya Kahawa (TBC) na idara za serikali.

Madhumuni ya uhusiano huo na benki ni kuwawezesha wakulima kunufaika na bei nzuri ya kahawa iliyopo katika soko. Pia ni kuhakikisha ya kuwa wanazalisha kahawa iliyo bora ambayo itawawezesha kuuzwa kwa bei nzuri katika mnada.Kwa kahawa kuuzwa kwa bei nzuri, tunatarajia ya kwamba wakulima wengi wapya wataanza kujihusisha na uzalishaji wa zao la kahawa na hivyo kuongeza kiwango cha uzalishaji.

Kikundi cha wakulima wa kahawa Iganda ni kimojawapo cha vikundi vinavyofanya kazi na NMB,toka mwaka 2008 uhusiano huu umekuwa ukiimarika mwaka hadi mwaka katika uzalishaji wa zao la kahawa na hivyo kukifanya kuwa ni moja wapo ya kikundi kinachofanya vizuri katika uzalishaji wa kahawa nyingi na yenye ubora. Ufanisi huu umetokana na uimara wa uongozi na uwajibikaji wa wanachama.
Kwa niaba ya wanakijiji /wanachama wa iganda mwenyekiti wa Iganda Cofee Group aliishukuru benki ya NMB kwa kuleta maendeleo kijijini hapo. Hafla hito fupi ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Kadeghe Michael,afisa Mtendaji wa Kata, Eckson Mdollo,Afisa Mtendaji wa Kijiji,Juma Shantiwa,Viongozi na wanachama wa Kikundi cha wakulima wa kahawa Iganda

No comments :

Post a Comment