Mkurugenzi wa shindano la kumsaka mwanamitindo mwenye vigezo vya kipekee nchini Tanzania(unique model) Methuselah Magese (kulia) akizungumza mbele ya waandishi |
Wednesday, October 31, 2012
UZINDUZI WA SHINDANO LA UNIQUE MODEL 2012 WAFANYIKA LEO
WAKAZI WA DAR WAFURAHIA USAFIRI WA GARI MOSHI
WAKAZI
wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, wamefurahia kuanza kwa
usafiri wa treni waliousubiri kwa muda mrefu ulioanza juzi.
Kamera
yetu leo ilitua katika ofisi ya mkuu wa kituo kinachodili na usafiri
huo, Bi. Rose Ngauga na kuzungumza mambo kadhaa kuhusiana na usafiri
huo.
Ngauga alisema kuwa usafiri huo siyo nguvu ya soda kama inavyodaiwa na baadhi ya watu na kwamba utakuwa endelevu.
Ngauga alisema kuwa usafiri huo siyo nguvu ya soda kama inavyodaiwa na baadhi ya watu na kwamba utakuwa endelevu.
YANGA YAIFUNGA MGAMBO 3-0
Beki wa Yanga, Mbuyi Twite akimpongeza Nadir
Haroub ‘Canavaro’ baada ya kufungia timu yake bao la kwanza dhidi ya Mgambo ya
Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Yanga ilishinda 3-0.
Mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva akimpongeza Nadir Haroub baada ya kufunga bao la kwanza
Didier Kavumbagu na Ramadhan Malima wa Mgambo kwenye mchezo wakichuana katika mchezo huo.
RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA BARABARA KWA SADALA-MASAMA HAI
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimpongezza Mbunge wa Hai na Kiongozi wa
Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe kwa hotuba
nzuri ya kumkaribisha na kumsifia kwa kazi anayofanya katika maendeleo
ya miundombinu nchini katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa
barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
Rais Jakaya Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Leonidas Gama (katikati) na
Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe wakizungumza wakati wa sherehe za
uzinduzi wa ujenzi wa Barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani Hai. (Picha
kwa hisani ya Ikulu)
Rais Jakaya Kikwete akisaidiwa
kuzindua jiwe la msingi na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, katika
eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani
Hai.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na kupewa shukurani na
Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe
Freeman Mbowe katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa
Sadala-Masama wilayani hai leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Miundombinu Mhe John Pombe
Magufuli Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe L:eonidas Gama na Mbunge wa Hai na
Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe
wakikata utepe mojawapo ya magreda katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi
wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Miundombinu Mhe John Pombe
Magufuli Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Leonidas Gama na Mbunge wa Hai na
Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika
picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaro baada ya uzinduzi
wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na wananchi katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
Serikali Kusaidia Kubana Wanaokiuka Sheria Za Filamu
Maelezo 31/10/2012
KAMPUNI ya usambazaji na utengenezaji filamu nchini Steps Entertainment imeahidi kushirikiana na serikali kupambana na wanaokiuka sheria ya filamu na michezo ya kuigiza ya mwaka 1976. Hayo yamesemwa jana na meneja Mkuu wa Steps Entertainment Bw. Jairaj Almoradan jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na Sekretatieti ya Bodi ya filamu Tanzania. Bw.Almoradan amesema kampuni yake haitapokea kazi za wasanii wasiofuata sheria kwa kutengeneza filamu zilizo kinyume na maadili na zilizo kinyume na sheria. Amesema kuwa sheria inawataka kutengeneza filamu zinazofuata maadili na kuwasilisha master kopi kwa ajili ya kuidhinishwa kuingia sokoni. “tutajitahidi kuwaeleza wasanii na tutakuwa wakali kutopokea filamu ambazo tunaona zipo kinyume na maadili na utamaduni wetu.”Amesema Bw. Almoradan. Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Bi. Joyce Fissoo amesema bodi imekuwa ikipata malalamiko kuhusiana na baadhi ya filamu kuwa kinyume na maadili ya Mtanzania. “Sisi kama bodi kazi yetu ni kukagua filamu na matangazo yake kama yapo kimaadili na yamefata sheria ikiwa ni pamoja na kuzipa madaraja filamu hizo kabla hazijaenda sokoni.”amesema Bi.Fissoo.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA NANE WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM-TAIFA, MJINI DODOMA LEO
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wazazi
CCM-Taifa. Mkutano huo unafanyika sambamba na uchaguzi wa Viongozi wapya
wa Jumuiya hiyo, katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Chuo cha Mipango, mjini
Dodoma leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwasili kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Chuo cha Mipango, mjini Dodoma
leo Oktoba 31, 2012 kwa ajili ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Nane wa
Jumuiya ya Wazazi CCM-Taifa. Mkutano huo unafanyika sambamba na uchaguzi wa
Viongozi wapya wa Jumuiya hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo
baada ya ufunguzi uliofanyika leo, mjini Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na William Malecela, wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa
Mwalimu Nyerere Chuo cha Mipango, mjini Dodoma leo, baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wazazi
CCM-Taifa. Mkutano huo unafanyika sambamba na uchaguzi wa Viongozi wapya wa
Jumuiya hiyo.
DOKEZO LA AMIR MHANDO KUTOKA TASWA
Naomba
kuwajulisha kuwa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) na Muungano wa
Kamati za Olimpiki za Afrika (ANOCA) kupitia Kamati ya Olimpiki Tanzania
(TOC) wameandaa mafunzo kwa waandishi wa habari wanawake wa Afrika
itakayofanyika Desemba 10 na 11 mwaka huu Nairobi, Kenya.
Kutokana na hali hiyo Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimepewa nafasi ya waandishi wa habari wanawake watatu washiriki kwenye mafunzo hayo na imepokea barua hiyo leo na inatakiwa hadi Ijumaa wiki hii iwe tayari majina hayo yametumwa pamoja na wasifu wa wahusika walioteuliwa.
Kwa msingi huo kwa kutumia njia hii ya uwazi zaidi, naomba waandishi wanawake wenye nia na muda wa kushiriki mafunzo hayo wawasilishe CV zao kabla ya Ijumaa (Novemba 2, 2012) saa sita mchana ofisini kwa Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto (Hifadhi House ghorofa ya 9 zilipo ofisi za JamboLeo, Posta) au kwangu mimi ofisi za Daily News Tazara, Dar es Salaam.
Masharti ya mafunzo ni kuwa yataendeshwa kwa lugha ya Kingereza na Kifaransa, lakini pia watakaoshiriki wawe tayari kuja kutoa elimu watakayaoipata huko kwa wenzao pindi watakaporudi nchini.
Suala la CV ni la umuhimu kupita maelezo, kwani baada ya hapo mchana siku hiyo TASWA itateua majina matatu na kuyatuma TOC kwa taratibu nyingine.
Watakaoteuliwa watalipiwa nauli ya kwenda Nairobi na kurudi Dar pamoja na malazi na chakula kwa siku zote watakazokuwa huko.Tuchangamkie nafasi, kumbuka ni kwa wanawake tu.
Nawasilisha kwa utekelezaji.(Kama hujaelewa tuwasiliane 0713415346)
Katibu

REDDS MISS TANZANIA YATANGAZA VIINGILIO NA WASANII 31 Oktoba 2012 .
Fainali za
shindano la Redds Miss Tanzania 2012 zitafanyika tarehe 3 Novemba 2012 katika
ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza jijini D’salaam
Akizungumza na waanmdishi
wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY Hashim
Lundenga alisema maandalizi yote yamekamilika na kila kitu kipo tayari na leo
tupo hapa kuwatangazia watanzania na washika dau wote wa tasnia ya Urembo kuwa
tiketi kwaajili ya shindano letu la mwaka huu zipo tayari na zipo kwa idadi
maalum na leo hii zinaanza kuuzwa katika vituo tulivyovipendekeza kulingana na
maoni ya wadau
Kutokana na
ukubwa wa shindano kwa mwaka huu wale wote watakaofanikiwa kuingia ukumbini
watakaa katika viti maalum vilivyowekwa katika hadhi ya kimataifa na kila
tiketi itagarimu kiasi cha shilingi laki moja (100,000) za kitanzania.
Katika
kufanikisha shindano hili kutakuwa na vitu tofauti na miaka ya nyuma na
tutarajie kuona shindano lenye ushindani mkubwa hasa kwa kuzingatia kuwa sehemu
kubwa ya warembo wetu ni wasomi walio katika ngazi ya elimu ya juu nchini
Vituo vinavyoanza
kuuza tiketi hii leo ni. Stears samora
Regency park
Hotel,Rose garden Mikocheni,Share illusion-Mlimani City,Giraffe Hotel,Ubungo
Plaza na ofisi za Lino.
Nitoe rai kwa
wapenzi wote waweze kupata tiketi mapema ili kuepuka usumbufu kwa sababu ya
kikomo cha tiketi kilichopo kama tulivyotangaza awali
Kwa upande wa
burudani kutakuwa na burudani nyingi sana na zitaongozwa nawasanii nguli hapa
nchini kama
1) Diamond Platnum
2) Winfrida Josephat’Rachel’
3) Wanne star ngoma troupe
Katika shindano
hilo ambalo ndani yake kuna mashindano mengine madogo yanayojulikana kama [Fast
Tract] Tayari washiriki 5 wameshajipatia tiketi ya kuingia katika kundi la
Warembo 15 Bora. [Top 15 Finalist]
Washiriki hao ni
Lucy Stephano –
Miss Photogenic
Magdalena Roy –
Top Model
Mary Chizi – Top
Sport Woman
Babylove Kalalaa
– Miss Talent
City sports
lounge-iliyopo posta mpya mkabala na mnara wa askari.
Happiness Daniel
– Miss Personality
Mwisho napenda
kutoa shukrani zangu kwa wadhamini wetu ambao ni TBL kupitia kinywaji chao cha
Redds Original,Star Tv na Giraffe Hotel
HASHIM LUNDENGA.
MKURUGENZI
DROO YA PILI YA SHINDA NOAH YAFANYIKA, WASHINDI WAZIDI KUPATIKANA
DROO
ya pili ya Bahati Nasibu ya Shinda Noah inayoendeshwa na Kampuni ya
Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi,
Risasi, Amani, Ijumaa na Championi leo imewapata washindi wengine katika
Viwanja vya Karume, jijini Dar.
Washindi
waliopatikana katika droo hiyo na kujinyakulia zawadi tofauti ni, Rukia
Vitali wa Boko, Dar (TV Flat Screen), Leah Andrew wa Mwananyamala
(Simu aina ya Samsung Galaxy), Rehema Kigadye wa Tegeta (Jezi) huku
wengine wakijinyakulia zawadi za papo kwa papo (kama wanavyoonekana
pichani).
Tuesday, October 30, 2012
KOCHA WA NGUMI C. MZAZI KUWAPOZA MACHUNGU MABONDIA WALIODHURUMIWA NA PROMOTA KAIKE

Mabondia
hao wanatarajia kupanda Ulingoni Novemba 18/2012 huko maeneo ya Mabibo
katika ukumbi wa D.I.D, ambapo pambano hilo litakuwa ni la upinzani
kubwa kutoka na mabondia hao kutambia na kufikia kutaka kuzichapa kavu
kavu mtaani.
Akilizungumzia
pambano hilo kocha mzazi alisema kuwa mabondia hao wote ni wazuri ambao
wanaofundishwa na kocha mzuri mwenye uwezo mkubwa pia ni mabondia
wazuri
na ni tegemeo zuri la baadae.

Hivyo
basi Mwaite Juma, kutoka BigRight boxing gym atacheza na Baina Mazola wa
No talking gym katika pambano la raundi nane.
Na Pambano hilo kali litasindikizwa na Karim
Ramadhan (mdogo wa Nasibu Ramadhan-bondia bora wa mwaka) atakaecheza
na Martin Richard.
Siku
hiyo pia kutakuwa na mapambano mengi ya kiushindani ya kuwekana sawa
nani zaidi ya mwingine kati ya mabondia wa mabibo na mwananyamala.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo,kupokea ripoti mikataba ya gesi Novemba 30

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
--
Na Gedius Rwiza
Na Gedius Rwiza
Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo atapokea ripoti mikataba ya gesi Novemba 30,
akizungumza na Wajumbe wa TPDC Waziri Muhoongo Alisema:
“Nawaombeni wajumbe wote wa TPDC, kuweni makini na mikataba ya
utafutaji wa mafuta na gesi, pia naomba mpitie mkataba mmoja baada ya
mwingine kwa umakini zaidi na ile yenye utata naomba taarifa kuhusu
utata huo,”alisema Profesa Muhongo.
MIKATABA 26 ya utafutaji na uchimbaji wa gesi ambayo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliliagiza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzani (TPDC)kuipitia upya na kutoa ripoti ,ripoti hiyo inatarajiwa kutolewa Novemba 30 mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es salaam jana, Mwenyekiti wa Bodi ya (TPDC), Michael Mwanda alisema kazi inaendelea vizuri na kwamba wanatarajia kutoa ripoti hiyo mwishoni mwa mwezi ujao.
Profesa Muhongo alitaka mikataba hiyo ipitiwe upya ili kuona kama kuna ambayo ilifanyika kinyume na sheria ili waliohusika waweze kuchukuliwa hatua.
Hatua hiyo ilikuja baada ya Profesa Muhongo kuiagiza TPDC kupitia upya mikataba yote iliyokuwa imefanyika na kutoa taarifa ya mikataba yote mibovu.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mwanda alisema kwa sasa zoezi hilo linakwenda vizuri na timu yake inaendelea kuipitia mikataba hiyo 26 na kwamba ana matumaini ifikapo mwishoni mwa Novemba watakabidhi ripoti kwa Waziri wa Nishati na Madini.
Alisema kamati hiyo ambayo ilipewa kazi hiyo, inafanya kazi kwa makini kama ilivyoagizwa na Waziri, na kwamba wanazingatia muda waliopewa ukifika wawe wamemaliza suala hilo.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, alifanya mkutano na wajumbe wa bodi ya TPDC, Septemba 15 mwaka huu na kuwaagiza kupitia upya mikataba ambayo tayari ilishaingiwa na kuwakataza kusaini mikataba mipya hadi pale watakapokuwa wametoa ripoti ya mikataba hiyo.
Waziri alisema kuna mikataba mingi yenye utata katika mikataba hiyo 26 na kuwaomba wajumbe hao kuhakikisha wanaipitia kwa umakini na kwamba ile ambayo itakuwa na makosa wahusika watatakiwa kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.
“Nawaombeni wajumbe wote wa TPDC, kuweni makini na mikataba ya utafutaji wa mafuta na gesi, pia naomba mpitie mkataba mmoja baada ya mwingine kwa umakini zaidi na ile yenye utata naomba taarifa kuhusu utata huo,”alisema Profesa Muhongo.
Alisema kwa sasa mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo vya mikataba ya kifisadi katika wizara yake na mashirika ambayo yapo chini ya wizara watafukuzwa kazi na kufunguliwa mashitaka.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba Yakusanya Maoni Kaskazini Unguja
Bw. Issa Seremani Issa (60), mkazi wa Shehia ya Mangapwani Mdodoni, Wilaya yaKaskazini
B, Mkoa wa Kaskazini Unguja akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati
Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipofanya mkutano wa kukusanya maoni jana
(Oktoba 28, 2012).
Bi. Khadija Abas Haji (49), mkazi wa Shehia ya Bumbwini Misufini, Wilaya ya Kaskazini
B, Mkoa wa Kaskazini Unguja akitoa maoni yake Katiba Mpya wakati Tume
ya Mabadiliko ya Katiba ilipofanya mkutano wa kukusanya maoni jana
Bw. Ame Khamis Ame (38) mkazi wa Shehia ya Mangapwani Mdodoni, Wilaya yaKaskazini
B, Mkoa wa Kaskazini Unguja akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati
Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipofanya mkutano wa kukusanya maoni jana
(Oktoba 28, 2012).
Bw. Mbaruku Muhamad Mbaruku (65), mkazi wa Shehia ya Bumbwini Misufini, Wilaya yaKaskazini
B, Mkoa wa Kaskazini Unguja Katiba Mpya wakati Tume ya Mabadiliko ya
Katiba ilipofanya mkutano wa kukusanya maoni jana (Oktoba 28, 2012).
Wakazi wa Shehia ya Bumbwini Misufini, Wilaya yaKaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifuatilia mkutano wakutoa
maoni kuhusu Katiba Mpya wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipofanya
mkutano wa kukusanya maoni jana (Oktoba 28, 2012).Picha zote na Tume
ya Mabadiliko ya Katiba
Tamasha Kuhamasisha Ngumi Mtwara
Bakari dunda akivishwa mkanda na mbunge wa mtwara baada ya kuchukuwa ubingwa huo katika ukumbi wa makonde
Tamasha la kuhamasisha masumbwi mkoani mtwara lilimalizika kwa
mafanikio mazuri kwa watu kuitikia na kukubali mapambano mengine mengi
ya ngumi kufanyika mkoani humo.
katika tamasha hilo lililosindikizwa na pambano la ubingwa wa taifa
la uzito wa unyoya kati ya Bakari mohamed'dunda wa blackmamba ya mtwara
alimshinda abdala seleman wa dar es salaam,
Nae mkongwe Rashid 'snake man" matumla alimshinda kiaina yake
bondia Patrick amote wa kenya katika pambano ambalo liliwasimua sana
mashabiki na kuwafanya kushindwa kukaa vitini muda wote wa pambano na
hasa pale mkenya alipokwenda chini kwa konde zito lililotupwa na matumla
baada ya kukwepa ngumi na kutupa hilo konde kwa kushtukiza,mwanzo
alianza taratibu na kuonekana kama mchovu kutokana na kitambi
alichonacho na kujikwaakwaa ulingoni lakini kadiri muda ulivyosogea
ndivyo alivyobadirika na kuonekana mzuri zaidi.
pambano jingine lililowaacha hoi wapenzi wa mtwara na kukaa kimyaaa
na kuduwaa kwa mshangao ni la haruna mnyalukolo wa dar na ashraf wa
blacmamba kwani ngumi zilipoanza tu walianza kwa nguvu sana na kutupiana
makonde mfululizo yaliyomuingia kila mmoja na kupelekana chini kwa zamu
na wote walivimba nyuso na kutokwa na damu baada ya kupasukapasuka
mpaka mwishowe ashraf spidi na uvumilivu ulipomshinda na kukubali
kuliachia pambano kwa kukataa kurudi ulingoni raundi ya nne pambano
lilikuwa la raundi sita.