Ofisa wa Selcom Tumaini Mgori akiongea na wahandishi wa habari wakati wa huzinduzi wa huduma hiyo |
Wednesday, November 27, 2013
SELCOM,VODA COM NA OIL COM WAUNGANA KURAHISISHA UNUNUZI WA MAFUTA KWA NJIA YA MPESA
SELCOM,VODA COM NA OIL COM WAUNGANA KURAHISISHA UNUNUZI WA MAFUTA KWA NJIA YA MPESA
Ofisa wa Selcom Tumaini Mgori akiongea na wahandishi wa habari wakati wa huzinduzi wa huduma hiyo |
SELCOM,VODA COM NA OIL COM WAUNGANA KURAHISISHA UNUNUZI WA MAFUTA KWA NJIA YA MPESA
Ofisa wa Selcom Tumaini Mgori akiongea na wahandishi wa habari wakati wa huzinduzi wa huduma hiyo |
Tuesday, November 26, 2013
YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH AMPONGEZA CHEKA KUKIMBIA MBIO ZA UHURU MARATHON RAIS -TPBO
RAIS -TPBO
NDG WAANDISHI NA WADAU WA MICHEZO WOTE KWA UJUMLA WETU,
AWALI YA YOTE NAPENDA KUTUMIA FURSA HII KUMPONGEZA BONDIA BINGWA WA DUNIA WA WBF,FRANCIS CHEKA KWA KUKUBALIANA NA WAZO LANGU LA KUMUOMBA AJIUNGE NA KUWA MIONGONI MWA WATANZANIA WATAKOJITOKEZA TAREHE 08-12-2013 JIJINNI DAR-ES0SALAAM KUUNGANA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA MH, JAKAYA MRISHO KIKWETE KUKIMBIA MBIO ZA UHURU MARATHON ZENYE KUADHIMISHA UHURU WA TANGANYIKA.
KWA KWELI NILIKUWA NA MATEGEMEO MAKUBWA SANA KWAMBA FRANCIS CHEKA ANGENIKUBALIA WAZO LANGU HILO ,AKIWA KAMA NI MTANZANIA ANAYEIPENDA KWA DHATI NCHI YAKE KWANI AMESHAIPATIA SIFA KUBWA TANZANIA KWA KUTWAA TAJI LA UBINGWA WA NGUMI WA DUNIA DHIDI YA MMAREKANI PHILL WILLIAM HAPO TAREHE 30-08-2013 .
NA NILISHAWISHIKA KUMSHAURI CHEKA AINGIE KWENYE MBIO HIZI BAADA YA KUVUTIWA NA TAARIFA ZA WAANDAAJI KWAMBA KATIKA MBIO HIZO YUMO BINGWA WA DUNIA WA MBIO HIZO KUTOKA KENYA, NIKAONA IKO HAJA KWA MABINGWA WA TASNIA ZISIZOFANANA WAKANOGESHA MBIO HIZI ZA UHURU MARATHON HAPO 08-12-2013 PALE LEADERS CLUB.
NINAONA WAZI KWAMBA SASA IPO HAJA HATA KWA MAKAMPUNI MBALIMBALI YAKAMTUMIA FRNCIS CHEKA KATIKA SHUGHULI ZAO MBALIMBALI ZA KIJAMII NA HATA KUWATANGAZIA BIASHARA ZAO.
KWA KWELI HIZI NI MBIO AMBAZO ZINAPASWA KUUMGWA MKONO NA KILA MTANZANIA NA SIYO WANARIADHA PEKEE ,KWANI HAYATI BABA WA TAIFA HILI MWL JULIUS KAMBARAGE NYERERE ALIUPIGANIA UHURU WA NCHI HII KWA MASLAHI YA WATANZANIA WOTE, BILA KUJALI ITKADI ZA KIDINI, ZA KIMICHEZO ,NA HATA UKABILA.
NI JAMBO LA KUTIA MOYO KWAMBA WAMEJITOKEZA WATANZANIA WENYE NIA NJEMA KABISA YA KUUENZI UHURU WA TANGANYIKA KWA NJIA YA MICHEZO [KAMA HAWA WAANDAAJI WA UHURU MARATHON].
NI LAZIMA TUWAUNGE MKONO WAANDAAJI HAWA KWA HALI NA MALI ILI TUUENZI VYEMA UHURU WETU.
NINATUMIA FURSA HII KUWAOMBA MABONDIA WENGINE NA WADAU WA MCHEZO WA NGUMI WAJIUNGE KWENYE MBIO HIZI KWA LENGO MOJA TU NALO NI KUUENZI UHURU WA NCHI YETU ,KWANI BILA KUWA NA UHURU KTK NCHI YOYOTE , WAZALENDO WA NCHI ILE HUWA HAWANA TOFAUTI NA WATUMWA,KWANI WANAKUWA HAWANA MAAMUZI YAO BINAFSI ,KWA KUWA KILA JAMBO HUAMULIWA NA WATAWALA WAO BILA KUJALI JAMBO NI ZURI AU BAYA.
KWA KUWA WAANDAAJI WAMETUTANGAZIA KUPITIA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI KWAMBA KUNA MATAIFA ZAIDI YA 21 YAMETHIBITISHA KUSHIRIKI KATIKA UHURU MARATHON ,PIA MHESHIMIWA RAIS,NA WABUNGE , WAMETHIBITISHA USHIRIKI WAO,SIONI KWA NINI WATANZANIA WA KAWAIDA TUSISHIRIKI KATIKA TUKIO HILI LA KIHISTORIA LA UHURU MARATHON.
PIA NINAYAOMBA MAKAMPUNI MBALIMBALI YAZIDHAMINI MBIO HIZI ZA UHURU MARATHON KILA MWAKA ,NA ISIWE MWAKA HUU PEKEE.
NINA IMANI KUBWA SANA KWAMBA WATANZANIA WENGI TUTASHIRIKI MBIO HIZI ZA UHURU MARATHON SIKU HIYO YA TAREHE 08-12-2013 PALE LEADERS CLUB.
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE ,NA UDUMISHE UHURU NA AMANI NCHINI KWETU TANZANIA.
IMELETTWA KWENU NAMI;-
YASSIN ABDALLAH -USTAADH
RAIS; TPBO-LTD
+255 713-644974 752 335584
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA NCHI WANACHAMA WA SHIRIKISHO LA VIWANDA VYA UTENGENEZAJI NGUO KWA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA BARANI AFRIKA (CAPA)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikata utepe kuzindua rasmi Jarida la Wanachama wa Shirikisho la
Viwanda vya Utengenezaji nguo kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola
Barani Afrika (CAPA Journal), wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo
lililoanza leo katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha. Kushoto ni Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na (kulia) ni
Mwenyekiti wa Bodi ya CAPA,John Kondoro.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Nchi Wanachama wa
Shirikisho la Viwanda vya Utengenezaji Nguo kwa nchi Wanachama wa
Jumuiya ya Madola Barani Afrika,lililoanza leo katika Ukumbi wa AICC
jijini Arusha.
Baadhi
ya washiriki wa Kongamano hilo, wakiwa makini kumsikiliza Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
wakati alipokuwa akisoma hotuba ya ufunguzi.
Baadhi
ya washiriki wa Kongamano hilo, wakiwa makini kumsikiliza Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
wakati alipokuwa akisoma hotuba ya ufunguzi.
Baadhi
ya washiriki wa Kongamano hilo, wakiwa makini kumsikiliza Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
wakati alipokuwa akisoma hotuba ya ufunguzi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea zawadi ya Kinyago kutoka kwa Makamu wa Mwenyekiti wa CAPA wa
Kanda ya Afrika Magharibi, Prof. Daniel Nyarko, baada ya kufungua rasmi
Kongamano la Nchi Wanachama wa Shirikisho la Viwanda vya Utengenezaji
Nguo kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika,lililoanza
leo katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
(wa nne kushoto), Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru
Kawambwa (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya CAPA,John Kondoro
(kushoto kwa Makamu) na baadhi ya viongozi wa CAPA, wakifurahia kwa
pamoja baada ya kuzindua rasmi Jarida la Wanachama wa Shirikisho la
Viwanda vya Utengenezaji nguo kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola
Barani Afrika (CAPA Journal), wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo
lililoanza leo katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa
Kongamano hilo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa
Kongamano hilo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa
Kongamano hilo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifurahia burudani ya ngoma ya Kimasai, wakati akitoka kwenye Ukumbi
wa AICC, baada ya kufungua rasmi Kongamano la Wanachama wa Shirikisho la
Viwanda vya Utengenezaji nguo kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola
Barani Afrika (CAPA Journal)lililoanza leo katika jijini Arusha.
Rais Kikwete ndani kamata Fursa Twenzetu
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Wadau mbali mbali
walioshiriki kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika leo
kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.Mh. Rais
ameupongeza uongozi wa Kampuni ya Clouds Media Group kwa ubunifu wao wa
Kampeni ya Fusra inayowakutanisha na kuwahamasisha vijana mbali mbali
nchini kujituma na kufanya kazi ili kutokomeza swala zima la ukosefu wa
ajira,Pia Rais Kikwete ameahidi kuwasaidia waendeshaji wa Warsha
hiyo.Picha zote na Othman Michuzi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumza
machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi,Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete,ili aweze kuzungumza na Wadau mbali mbali walioshiriki kwenye
Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa
Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa,Ahmed Lussasi akizunguma katika Warsha ya Fursa namba alivyo
Mwanamuziki
wa Muziki wa Kizazi Kipya,Nasseb Abdul a.k.a Diamond akitoa ushuhuda
wake wa namna alivyoanza na mpaka alipofikia sasa,ambapo ameweza kuiona
Fursa na kuweza kugawana fursha hiyo na vijana wenzake anaofanya nao
kazi kila siku.Kushoto ni Mwanafursa Mwingine,ambaye pia ni Msanii wa
Mashairi,Mrisho Mpoto.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi. Fatma Ally akielezea namna alivyoipata Fursa kwa kupitia Ufugaji wa Nyuki.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasikiliza vijana mbali mbali walopata Fursa na kuweza kufanikiwa katika maisha yao.
Mrisho Mpoto akizungumzia Fursa yake.

Wadau mbalimbali wa Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu wakimsikiliza kwa makini Mwenyeshaji wa Kampeni hiyo ya Fursa,Ruge Mutahaba.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Naseeb Abdul a.k.a Diamond.Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akiwapongeza vijana walioiona Fursa.
Wadau
mbali mbali wakiwa kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu iliyofanyika
leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya pamoja.
K-Guitar wa Bana Marquis wala hajutii
Kelvin Nyoni 'K Guitar' kaika pozi |
Tayari wimbo huo umeanza kurushwa hewani na baadhi ya vituo vya redio nchini na kwa sasa anajipanga kwa ajili ya kufyatua video yake ili mashabiki wapoate uhondo kamili.
Akizungumza na MICHARAZO, mwanamuziki huyo anayecharaza pia gitaa la rythm alisema wimbo huo ameurekodia katika studio za Swadt Records chini ya prodyuza T-Tach kwa msaada mkubwa wa mameneja wake watatu akiwamo mchora katuni wa gazeti hili, Abdul King'O.
Kelvin alisema wimbo huo ni mwanzo wa safari ndefu ya kuwapa burudani mashabiki wa muziki kupitia albamu yake binafsi itakayokuwa na nyimbo zaidi ya sita katikka miondoko tofauti za Zouk, Bongofleva na Rhumba.
"Baada ya kukamilisha kutoa video ndipo nitaanza kurekodi nyimbo nyingine ambapo mpaka sasa tayari ninazo kama tatu zilizokamilisha mashairi yake," alisema Kelvin.
Kelvin kabla ya kuingia kwenye muziki wa dansi akijiunga na bendi ya Bana Marquiz inayoongozwa na mwanamuziki nyota wa kimataifa, Tshimanga Assosa Kalala 'Mtoto Mzuri', alishawahi kutoa wimbo wa Bongofleva wa 'Mapenzi Siyo Pesa' kabla ya kuurudia tena katika bendi hiyo
Mechi ya Tanzanite sasa kuchezwa Dar
Mashujaa wa Tanzania, Tanzanite |
Baada ya ukaguzi uliofanywa na maofisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imebainika uwanja huo unatakiwa ufanyiwe marekebisho ambayo hayawezi kuwahi Desemba 7 mwaka huu, siku ambayo ndiyo mechi hiyo inatakiwa kuchezwa.
Vyumba vya wachezaji vya uwanja huo ndilo eneo ambalo linatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa
Zitto Kabwe, Dk Kitila wana mashtaka 11 ya kujibu CHADEMA
Zitto Kabwe |
Akizungumza katika makao makuu ya chama hicho, Mkurugenzi wa habari na Uenezi John Mnyika, alisema barua hizo zipo tayari na wahusika watapatiwa wakati wowote kuanzia leo Novemba 26.
Mnyika alikuwa akitoa taarifa ya kikao cha Utekelezaji cha sekretarieti ya chama hicho iliyoketi baada ya mkutano wa kamati kuu iliyoketi tarehe 20 – 22 Novemba mwaka huu.
Ni katika Mkutano huo, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu alisema kuwa mkutano uliofanywa na Zitto na Dk Kitila mbele ya waandishi hawajazungumzia tuhuma zinazowakabili, badala yake walichofanya ni kujitungia tuhuma ambazo kimsingi sizo zilizo wavua nafasi zao.
Lissu alisema, Zitto na Dk Kitila hawakusimamishwa nyadhifa zao kwa masuala ya PAC, Uchaguzi wa mwaka 2010, wala kutoshiriki kwenye operesheni za chama au sababu zingine, na walitaja hizo sababu ili kupotosha tuhuma zinazowakabili kwa jamii.
“Walichokifanya kina Zitto na Kitilla ni "Diversion" (kubadili mwelekeo) wa mashtaka yao yanatokana na waraka wa kihaini wa mabadiliko ambao ni kinyume na katiba, kanuni na maadili na itifaki ya Chama. anawaambia waandishi, "wamevuliwa nafasi zao na kamati kuu kwa sababu ya waraka wenye nia ovu" alisema Lissu.
Aliongeza kuwa Chadema kina mwongozo wa uchaguzi uliopitishwa na kamati kuu, Zitto na Kitila wanaufahamu ingawa haijulikani ni kwanini wao walienda kinyume na mambo yanayojadiliwa katika kamati kuuu
Aidha Lissu alieleza kuwa Dk Kitilla anapotosha umma na wanachaka kwa kauli yake kuwa kamati kuu haina mamlaka ya kumvua yeye nafasi yake ya ujumbe wa kamati kuu maana amechaguliwa na baraza kuu, alimtaka Kitila na Zitto waangalie vema katiba ya chama hasa majukumu ya kamati kuu, pale yanaporuhusu Mwanachama yeyote kusimamishwa au kufutiwa uanachama haraka kama kamati kuu itaona kuna umuhimu wa kufanya vile.
Kigaila alisema, Kamati kuu iliyoketi Novemba 20-22/2013 ilipitisha ratiba ya uchaguzi wa ndani ya chama kama ifuatavyo.
22/11/2013-14/12/2013 ni kukamilisha zoezi la usajili wa wanachama, 15 Desemba hadi 15 Januari uchaguzi ngazi za vitongoji, 16 januari 30 Januari 2014 Rufaa naukaguzi, ambapo tarehe 01 Februari hadi 15 Februari ni uchaguzi wa matawi.
Chadema pia ilisema 16 Februari hadi 29 mwezi huo huo ni kusikiliza rufaa na ukaguzi, ambapo uchaguzi wa majimbo utaanza rasmi 1 Aprili hadi Aprili 10, huku uchaguzi ngazi ya Wilaya ukitarajiwa kufanyika 25 Aprili hadi mei 5 mwaka 2014, na ngazi ya Mikoa ni 20 Mei hadi 25 Mei.
Huku uchaguzi wa kanda ukitarajiwa kufanyika Julai 9, na haada ya hapo Julai 23 hadi Julai 30 utakuwa ndio muda wa uchaguzi ngazi ya Taifa, utakaoanza na baraza la Wazee, Baraza la Vijana, Baraza la Wanawake kisha uchaguzi wa ndaniya chama.
KINANA ATEMBELEA KUKAGUA MAENDELEA YA MIRADI JIMBO LA RUNGWE MASHARIKI
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya Sekondari ya Mwakaleli.
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akikata ubao
akiwa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakikata
mbao kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara na madarasa ya shule ya
Sekondari ya Mwakaleli.
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiongea na
wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mwakaleli na kuwataka wanafunzi
waongeze bidii kwenye masomo kwani elimu haina mwisho.