Saturday, July 18, 2009

ETHIOPIA YATOLEWA JELA NA FIFA BAADA YA UCHAGUZI

Shirikisho la kandanda la nchini Ethiopia EFF limeridhiwa na shirikisho la kandanda Duniani FIFA baada ya kufanya uchaguzi uliyofanyika mapema leo na kuweka uongozi mpya.
Ujumbe wa watu wa tatu toka FIFA umesema umeridhishwa na matokeo ya uchaguzi huo.
Mgogoro uliyokuwepo ndani ya EFF ulipelekea Ethiopia kuondolewa katika michuano ya kusaka nafasi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia nchini Afrika Kusini na mataifa ya Afrika nchini Angola mwaka 2010 mwezi Julai mwaka jana.
Sahlu Gebrewold Gebremariam amechaguliwa kuwa raisi wa EFF, akichukua nafasi ya Dr Ashebir Woldegiorgis, ambaye alijiuzulu mwezi May.
Sahlu alikuwa mgombea pekee katika nafasi ya uraisi katika uchaguzi uliyofanyika leo, baada ya wagombea wengine kujitoa siku ya Ijumaa.
Amesema dhamira yake kubwa ni kuhakikisha anafufua soka la Ethiopia.

No comments:

Post a Comment