Friday, October 23, 2009

SERENGETI YAITAKA TAIFA STARS KUIFUNGA MISRI

Wadhamini wakuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambao ni watengenezaji wa Kinywaji cha Bia ya Serengeti wamesema watashirikiana bega kwa bega kuhakikisha Timu hiyo inawabwaga mafarao wa Misri katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaochezwa Novemba 5 mwaka huu Cairo, Misri.
Akizungumza na kipindi cha michezo na burudani cha radio Times FM Afisa uhusiano wa kampuni hiyo Teddy Mapunda amesema ijapokuwa taarifa ya mwaliko huo wameupata muda mfupi lakini watajitahidi kadri ya uwezo wao kuwapatia mahitaji muhimu wachezaji ili wapate ushindi kwenye mchezo huo.
Mapunda ameongeza kuwa atafurahishwa endapo Timu hiyo ya Misri itakubali mwaliko wa kuja Tanzania, kwani mbali na kuja kucheza lakini watawatembeza kwenye vivutio vyetu ili wajionee.

No comments:

Post a Comment