Saturday, October 17, 2009

UCHAGUZI MKUU YANGA JANUARI 2010

Mwenyekiti wa timu ya Dar es Salaam Yang African Bw. Imani Madega (kulia)akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu uchaguzi wa timu hiyo utakaofanyika Januari 3 mwakani, kushoto ni Katibu Mkuu wa timu hiyo Lawrence Mwalusako.
Akizungumza na kipindi cha michezo na burudani cha Radio Times FM Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Imani Mahugira Madega amesema sababu kubwa za kurudishwa nyuma kwa uchaguzi huokufanyika may mwakani ni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba mwakani hivyo wameona bora warudishe nyuma uchaguzi wa Yanga kwa maslahi ya Taifa.

No comments:

Post a Comment