Thursday, November 5, 2009

TIMU YA TAIFA YA SOKA YA WANAWAKE YAINGIA KAMBINI

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania Twiga Stars jumla ya wachezaji 20 wametangazwa leo kwa ajili ya kuanza mazoezi ili kujiandaa na Mashindano ya Afrika kwa nchi za Magharibi yatakayofanyika Nigeria mwishoni mwa mwezi huu,
Akizungumza na waandishi wa habari Kocha mkuu wa Timu hiyo Charles Bonifas Mkwasa amesema wachezaji wote wanatakiwa waripoti Ijumaa jioni mazoezini kwa kipindi chote kabla ya kwenda Nigeria.
Mashindano hayo yajulikanayo West Africa Football Union ambapo kuna timu kama Nigeria ,Ghana,Guinea,Senegal,Sieraleon Mali, na Tanzania kama wageni waalikwa.

No comments:

Post a Comment