Friday, November 13, 2009

YANGA - KWAHERI BARASA

Uongozi wa klabu ya Yanga umempa mkono wa kheri popote aendako Winga machachari atumiae guu la kushoto Mkenya Mike Barasa kufuatia mchezaji huyo kutoonyesha ushirikiano wa kutosha kama atabakia Jangwani ama laa.
Luis Sendeu Akizungumza bila kumeza mate wala kusita na waandishi wa vyombo mbali mbali vya Habari za michezo katika Jengo lenye Mvuto pengine kuliko vilabu vyote amesema wameamua kuutangazia Umma juu ya hatma ya mchezaji huyo kuwa kwa sasa hawatakuwa naye.
Yanga katika hatua nyingine wamewakumbusha Wanachama wao kuwa waanze kuzilipia kadi zao kabla ya uchaguzi hapo mewakani.

No comments:

Post a Comment