Thursday, June 16, 2011

SHINDANO LA VODACOM DAR INTER COLLEGE KUFANYIKA LEO

Warembo wanaotarajia kupanda jukwaani Juni 17 wiki hii, kuwania Taji la Vodacom Miss Dar Inter College, wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja kwa ajili ya kujiandaa na shindano hili litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Sunciro ar es Salaam. Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE MicrosoftInternetExplorer4

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye kambi ya warembo hao, jijini Dar es Salaam leo, mratibu wa shindano hilo, Angela Msangi, amesema kuwa katika kunogesha fainali ya shindano hilo wamemwalika msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo flava’, Dully Skyes ambaye atatoa burudani sambamba na wasanii wengine walioalkwa.


Baadhi ya warembo hao wakipozi kwa picha wakati wa mazoezi yao kwenye Ukumbi wa Sunciro.
Warembo wanatarajia kushiriki shindano hilo wakipozi kwa picha wakati wa mazoezi yao.
Warembo hao wakiwa katika mazoezi ya shoo yao ya ufunguzi.

No comments:

Post a Comment