Monday, July 11, 2011

YANGA BINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Wachezaji wa Yanga ya Dar es Salaam, wakishangilia ushindi na Komne lao baada ya kukabidhiwa kombe hilo kwa kuibuka kidedea baada ya kuwafunga watani wao wa jadi Simba kwa bao 1-0, katika mchezo wa fainali ya Kombe la Kagame uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Bao hilo lilifungwa na Asamoh baada ya krosi murua kutoka kwa Rashid Gumbo aliyemtoka Ulimboka mwakingwe katika dakika za nyongeza baada ya kumalizika dakika 90 bila kufungana.
Ubao ulisomeka hivi hadi mwisho wa mchezo huo.
Kipa wa Simba Juma Kaseja, akiruka kuokoa mpira bila mafanikio uliopigwa na Asamoh kwa kichwa na kuandika bao la kwanza na la ushindi kwa Yanga.
Liziwani Kikwete (kulia) akishangilia ushindi wa Yanga na shabiki mwenzake, Muddy Sebene, baada ya mchezo huo kumalizika.
Hekaheka langoni mwa Simba.

Kwa matokeo hayo Yanga ya Tanzania wanakuwa mabingwa wa Kombe CECAFA kwa upande wa vilabu Kagame Cup kwa 2011 na hivyo kuondoka na kitita cha dola za kimarekani 30,000.

Mshindi wa pili ambaye ni timu ya Simba amepata dola 20,000

Awali katika mechi ya kutafuta mchindi wa tatu wa mashindano hayo timu ya Al Mereikh ya Sudan iliifunga St. George ya Ethiopia magoli 2 - 0 na hivyo kuwa mshindi wa tatu wa michuano hiyo ambayo nayo imejinyakulia dola 10,000.

No comments:

Post a Comment