Friday, March 16, 2012

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ateua wakuu wa mikoa wapya

Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao
kuwa Wakuu wa Mikoa
.
Dkt. Rajab Mtumwa
RUTENGWE
ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa KATAVI.Kabla ya
hapo Dkt. Rutengwe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda.
Ndugu Magalula Saidi MAGALULA ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa GEITA.Kabla ya hapo Ndugu MAGALULA alikuwa Mkuu wa Wilaya ya
Lindi.
Ndugu Paschal Kulwa
MABITI
ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa SIMIYU.Kabla ya
hapo Ndugu MABITI alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida.
Kapt. Asery MSANGI ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE.Kabla ya hapo Kapt. MSANGI alikuwa Mkuu wa Wilaya ya
Iringa.
Uteuzi huu
unaanza tarehe 15 Machi, 2012.Wataapishwa Ikulu, Dar es
Salaam, Jumatano tarehe 21 Machi, 2012 saa 04:00 asubuhi
.
Imetolewa
na
:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
15 Machi,
2012

No comments:

Post a Comment