Saturday, March 10, 2012

MICHUANO YA KOMBE LA (NSSF) YAZINDULIWA RASMI LEO, JAMBO LEO YAIBANJUA TBC 2-1

Nahodha wa timu ya Jambo Leo Said Mwishehe
akimkabidhi zawadi ya majarida ya Jambo mgeni rasmi Mh. Gaudensia Kabaka Waziri wa Kazi na Ajira mara baada ya kuzindua rasmi mashindano ya
kombe la NSSF kwenye viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe jijini Dar es salaam leo
asubuhi.
Katika
mchezo wa soka auliokutanisha timu za Jambo Leo na TBC timu ya Jambo Leo ambao
ndiyo mabingwa watetezi wa kombe hilo wameibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi
ya TBC hivyo kuanza vyema utetezi wa kubaki na kombe hilo.
Wachezaji wa TBC na Jambo Leo wakichuana vikali
katika mchezo huo kwenye viwanja vya TCC Sigara
Chang'ombe.
Timu zikisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo
huo.
Kwa upande wa Netboli timu za IPP na Mwananchi
Communication zikichuana vikali hata hivyo IPP wamekuwa washindi baada ya
kuikandamiza timu ya Mwananchi magoli 16-12 na kuibuka na ushindi.
Kikosi cha timu ya TBC kikiwa katika picha ya
pamoja.
Kikosi cha timu ya
Jambo Leo kikiwa katika picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment