Friday, March 9, 2012

NBC yadhamini tuzo za mwanamakuka

Meneja Udhamini na Matukio wa Benki ya NBC,
Rachel Remona Kimambo (kushoto) akikabidhi mfano ya hundi ya shs milioni sita
kwa Tatu Ngao aliyeibuka kidedea katika Tuzo ya Heshima ya Mwanamakuka katika
hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi sambamba na Maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani. Tuzo hizo ambazo NBC ilikuwa mdhamini mkuu ziliandaliwa na
Umoja wa Wanawake Marafiki (UWF). Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa UWF, Mwate
Madinda na Dina Marios mmoja wa waratibu wa tuzo hizo.
Meneja Udhamini na Matukio wa Benki ya NBC, Rachel
Remona Kimambo (kushoto) akikabidhi mfano ya hundi ya shs milioni mbili na nusu
kwa Mwanne Msekalile, mshindi wa pili wa Tuzo ya Heshima ya Mwanamakuka 2012
katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi sambamba na Maadhimisho ya
Siku ya Wanawake Duniani. Tuzo hizo ambazo NBC ilikuwa mdhamini mkuu
ziliandaliwa na Umoja wa Wanawake Marafiki (UWF). Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa
UWF, Mwate Madinda na Dina Marios mmoja wa waratibu wa tuzo hizo.
Baadhi ya wanawake
waliohudhuria hafla ya utoaji tuzo ya Heshima
ya Mwanamakuka katika Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam juzi
usiku

No comments:

Post a Comment