Friday, March 16, 2012

WANAFUNZI WA UDOM WAFANYA ZIARA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA VIWANDANI ILIYOPO DODOMA MJINI NA KUKABIDHI MSAADA WA VIFAA VYA USAFI LEO

Mmoja wa Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)
akishusha Baadhi ya vifaa vya kufanyia usafi wakati wanafunzi wa UDOM
walipowasili Shule ya Sekondari ya Viwandani iliyopo Manispaa ya Dodoma Mjini
mchana wa leo.
Picha Zote na Josephat Lukaza wa
Lukaza Blog - http://josephatlukaza.blogspot.com
Picha hapo juu ni Mwanafunzi wa UDOM Josephat Lukaza
akitoa Maelezo jinsi ya matumizi sahihi ya vifaa vya kufanyia na kutunzia uchafu
kwa wanafunzi wa klabu ya mazingira ya shule ya sekondari ya viwandani iliyopo
Dodoma mjini
Mwalimu wa Klabu ya Mazingira ya Shule ya Sekondari ya
Viwandani Bi Ester Bahati akitoa shukrani za dhati kwa wanafunzi wa UDOM
waliotembelea Shule hiyo na Kutoa Misaada ya Vifaa vya Kufanyia Usafi leo Mchana
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma wakiwa
makini kusikiliza Wanafunzi wa Klabu ya Mazingira Wakichangia Mada mbalimbali
kuhusu Umuhimu wa Kutunza mazingira wakati walipotembelewa na Wanafunzi kutoka
Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) leo mchana

No comments:

Post a Comment