Tuesday, April 10, 2012

KANUMBA KWELI ALIKUWA MTU WA WATU, MAELFU WAKO LEADERS KUMUAGA MCHANA HUU

Mwigizaji Clouds pamoja na
waombolezaji wengine wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa Mwigizaji mwenzao
marehemu Steven Kanumba aliyefariki hivi karibuni kwa ajili ya kuuweka mahali
palipoandaliwa kwa ajili ya waombolezaji kuuaga mwili wa mpedwa wao katika
viwanja vya Leadres jijini dar es salaam, Marehemu Kanumba ataagwa leo hapo na
kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Fullshangweblog inarusha matukio haya kutoka
mjini Dodoma kupitia sitelite zilizotegwa kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar
es salaam

(PICHA NA MP)



Mwili wa marehemu Kanumba ukiwa umewekwa tayari kw
awaombolezaji kuuaga kwa mara ya mwisho.
Waombolezaji wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya
Leaders jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuuaga mwili wa Marehemu
Kanumba.
Wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu wakiwa wamembeba mmoja
wa waombolezaji aliyepoteza fahamu kwa ajili ya majozi ya msiba
huo.
Wafanyakazi wa msalaba mwekundu wakiwa tayari kwa
kuwahudumia watu watakaopata matatizo yoyote kutokana na msiba huo.
Mmoja wa waombolezaji akiwa anasaidiwa na mwenzake
Usalama umeimarishwa katika viwanja vya Leaders jijini
Dar es salaam kwa ajili ya msiba huo.
Kama unavyoona katika picha usalama ni mkubwa na watu
wameandaliwa maeneo ya kukaa kwa ajili ya msiba huo.
Waombolezaji mbalimbali wakiingia katika viwanja vya
Leaders jijini Dar es salaam.
Ni hali ya majonzi pamoja na kwamba kuna jua kali
lakini waombolezaji wengi wamejitokeza katika viwanja hivi.
Makapeti
mekundu yametandikwa katika viwanja hivyo kwa ajili ya kupita viongozi na watu
maarufu.

No comments:

Post a Comment