Saturday, June 23, 2012

MTANDAO WA WAANDISHI WA HABARI 'TAJONET' WAZINDULIWA


 Baadhi ya wanachama wa Mtandao wa Waandishi wa Habari Tanzania (TAJONET) wakiwa katika uzinduzi wa mtandao huo.
 Mjumbe wa Kamati ya TAJONET, Neema Mgonja akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Wanachama wa Mtandao huo.
Wanamtandao, Frank Balile, Juma Kasesa na Salum Mkandemba.
Angela Michael Msangi akizungumza kwenye uzinduzi wa mtandano huo.
 Zaituni Kibwana (kushoto) akiwa na mdau
Mwenyekiti wa muda wa Mtandao wa Waandishi wa Habari Tanzania (TAJONET), William Shao akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa mtandao huo uliofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Katibu wa Mtandao huo, Eben-Ezery Mende.
Chalila Kibuda akizungumza katika uzinduzi wa Mtandao huo.



WAANDISHI wa habari wamekutana jijini Dar es Salaam na kuanza mchakato wa kuunda mtandao utakaoweza kusimamia, kupigania na kutetea haki zao.

 Akizungumza katika kikao hicho, Katibu wa muda, Ebenezer Mende, alisema kuwa mtandao huo utajulikana kwa jina la ‘Waandishi wa Habari Tanzania (TAJONET) na utakuwa wa nchi nzima.
Alisema mtandao huo utatumika kama chachu ya kusaidiana katika matatizo mbalimbali, ukiwa na sauti moja katika kutetea maslahi yao na utahusika moja kwa moja katika kusimamia maadili ya tasnia ya habari.
Mende alisema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya wandishi wa habari kujikuta wakikabiliwa na matatizo mbalimbali huku wakikosa msaada.

 Aidha alibainisha kuwa TAJONET utakuwa bega kwa bega katika kuangalia suala zima la afya ya wanachama kwa kuanzia ngazi ya chini kama matibabu awapo hospitalini pamoja na misiba.
“Watu wengi wamekuwa wakichukulia matatizo ni kifo, bila kuangalia mambo mengine kama ugonjwa, sisi hatutaki kujielekeza hivyo bali tunataka tatizo la ugonjwa lipewe  kipaumbele  ili kuepusha vifo visivyo na ulazima,” alisema Mende.

Alibainisha kuwa  mkutano huo umeteua viongozi wa muda  14, ambao kati yao wataunda kamati ya rasimu ya upatikanaji wa katiba ya mtandao huo.

No comments:

Post a Comment