Monday, July 30, 2012

Mama Pinda azindua mradi wa maji wa Hospitali ya Mawenzi mjini Moshi leo



Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizindua mradi wa maji katika Hospitali ya Mawenzi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti anaemaliza Muda wake wa, Richard Wells. Hadi kukamilika kwa mradi huo wa maji safi, Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited imetumia zaidi ya milioni 55 za kitanzania kujenga tanki kubwa la kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro.
 Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bi. Teddy Mapunda, akifafanua juu ya gharama halisi za mradi huo. 
 
“Sisi kampuni ya bia ya Serengeti tunatambua sana changamoto zinazowakabili watanzania, taasisi na mashirika mbalimbali hususani hospitali juu ya upatikanaji wa maji safi na salama, na kwasababu hiyo kampuni ya bia ya Serengeti imeona hilo na kuamua kusadia kutatua tatizo hilo katika maeneo mbalimbali ikianza katika maeneo yanayohitaji huduma ya maji kwa haraka zaidi” alisema Mapunda na kuongeza kuwa kujitolea kusaidia jamii ni moja yab sera za kampuni hiyo kama njia mojawapo ya kurudisha shukrani zake kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla.

Mgeni rasmi akifungua maji yanayotoka katika bomba lililounganishwa katika matanki hayo.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji wa SBL, Nandi Mwiyombela 
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Mtumwa Mwako
 Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bi. Teddy Mapunda, akifafanua juu ya gharama halisi za mradi huo. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, anaemaliza muda wake Richard Wells akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment