Sunday, August 19, 2012

MSAMA AMSAIDIA SH. MILIONI MOJA MCHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA,TAIFA STARS, ALPHONCE MODEST KWA AJILI YA MATIBABU YA MIGUU



 Mratibu wa Tamasha la Injili la Pasaka Tanzania, Alex Msama (kushoto), akimkabidhi msaada wa sh. mil. 1, mchezaji wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Alphonce Modest za kusaidia matibabu ya miguu inayosumbuliwa na baridi yabisi. Msaada huo uliokabidhiwa Dar es Salaam leo, ulihamasishwa na Mhariri Kiongozi wa gazeti la Champion, Saleh Ali (wa pili kushoto) pamoja na Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten na Radio Magic FM, Said Kilumanga (wa pili kulia). Wameiomba Jamii yenye huruma kumsaidia kwa hali na mali mchezaji huyo ambaye wamemsafirisha kwa gharama zao kutoka Mwanza. (PICHA ZOTE NA KAMANDA  RICHARD MWAIKENDA)
Modest akitembea kwa taabu huku akisaidiwa na mdogo wake Francis

No comments:

Post a Comment