Wednesday, September 12, 2012

RAIS KIKWETE KATIKA ZIARA RASMI YA KISERIKALI (STATE VISIT) YA SIKU TATU NCHINI KENYA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya pamoja na ujumbe wake wakiingia Ikulu ya Nairobi Jumanne, 11 Septemba , 2012, alipoanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Waziri wa Elimu ya Juu wa Kenya, Mheshimiwa Margaret Kamar alipowasili Chuo Kikuu cha Kenyatta kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. Kulia kwake ni Waziri wa Elimu ya Juu, Mheshimiwa Margaret Kamar na kuhsoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Olive Mugendi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi baada ya kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na wanafunzi wawili waliotoa burudani ya vichekesho wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba ya kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa zawadi ya picha ya kuchora baada ya kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.

No comments:

Post a Comment