Wednesday, September 26, 2012

REA KUENDESHA SHINDANO KUPATA TAASISI ZA KUWAPA UMEME VIJIJINI. Shule Hospitali na zahanati kunufaika. Jumla ya miradi 15 maeneo mbalimbali.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) Lutengano Mwakahesya (PhD) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuanza kwa shindano la usambazaji wa umeme vijijini, ambapo taasisi mbalimbali za vijijini ziliwasilisha maombi yao, ambapo mchujo wa shindano hilo unatarajiwa kufanyika Mkoani Arusha Oktoba 1 na 2. Mradi huo ni wa ushirikiano kati ya Serikali na Benki ya Dunia (WB), kulia ni Mkurugenzi wa fedha wa REA George Nchwali.
 Baadhi ya wafanyakazi wa REA wakifuatilia mkutano huo kati ya waandishi wa habari na Mkurugenzi wa wakala huyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.

No comments:

Post a Comment