Friday, November 2, 2012

POLISI WAMEFANIKIWA KUZUIA MAANDAMANO YA WAISILAMU JIJINI DAR LEO.



 Kariakoo ilivyokuwa leo mara baada ya sala ya Ijumaa, maduka yalifungwa na watu kulikimbia eneo hilo kukwepa mabomu, ya polisi ambao walizingira misikiti yote ya Kariakoo kwa kuweka ulinzi mkali.
Polisi wakiweka Doria kali kwenye mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam leo wakati wa Sala ya Ijumaa, ambapo walidhibiti kila msikiti kwa kuweka ulinzi mkali kuhakikisha hakuna maandamano yanayofanyika. Hata hivyo mabomu kadhaa yalipigwa kwa watu waliojaribu kutaka kuandamana na kusababisha eneo la Kariakoo kukimbiwa na watu na maduka kufungwa.
BAADHI ya waisilamu waliozungumza na mtandao huu walisema wamejisikia faraja kufanya ibada huku wakiwa na ulinzi wakutosha na kulitaka jeshi la polisi kufanya hivyo kila ijumaa inapofika kwasababu siko wasiyokwenda kuwalinda ndio siku watakayo andamana.

Aidha mmoja wa wafanya biashara Ally Saidi alisema serikali bora itangaze tu kama ijumaa ni siku ya mapumziko maana wao hawafanyi biashara kutokana na mabomu kila inapofika siku ya Ijumaa.
"Serikali wangetumia akili kwa kuwaruhusu hawa watu waandamane kisha wakawalinda waone kama ijumaa nyengine wataandamana badala ya kutumia nguvu nyingi na pesa kulinda misikiti halafu hakuna kinachopatikana zaidi ya vurugu. ZAID TEMBELEA http://saidpowa.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment