Thursday, December 13, 2012

SHEREHE YA MIAKA 15 YA BENDI YA FM ACADEMI KUFANYIKA DESEMBA 14 JIJINI DAR ES SALAAM




Ofisa Masoko wa Kampuni ya Tigo Bw.Alex Msigara.(kulia)Akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo kwenye Hotel ya Southen Sun jijini Dar es salaam juu ya kudhamini maadhimisho ya miaka 15 ya bendi ya muziki ya FM Academia,Sherehe hiyo itafanyika tarehe 14 Desemba mwaka huu msasani Beach Club ,Ambapo amesema wao  kama Tigo wameamua kufunga mwaka kwa kusaidia jamii wanayoihudumia katika Nyanja zote ikiwemo ya burudani kama sehemu ya shughuli zao za kijamii .
Amesema Tigo itatuma ujumbe mfupi wa maneno kwa wateja wote wa jiji la Dar es salaam kuwapa taarifa kuhusu maadhimisho hayo ya miaka ya 15 ya bendi ya FM Academia.(katikati)Mwimbaji wa bendi hiyo Bw.Nyoshi El Sadaat.(kushoto)mratibu wa onesho hilo  Bw.Nasibu Mahinya. Ofisa Masoko wa Tigo, Alex Msigara akielezea kuhusu udhamini wao katika maadhimisho ya miaka 15 ya bendi hiyo Mwingine ni Kiongozi wa Bendi ya FM Academia 'Wana Ngwasuma', Nyoshi El-Sadaat

No comments:

Post a Comment