Friday, December 6, 2013

BALOZI SEIF ALI IDDI ATEMBELEA HOTELI YENYE CHUMBA NDANI YA BAHARI "MANTA RESORT " PEMBA ZANZIBAR



Balozi Seif akiwa pembezoni mwa dirisha ndani ya  chumba cha chini ya Bahari akiangalia  samaki na mazingira yake mara baada ya kuuzindua mradi huo hapo Manta Resort Hoteli Makangale.
Balozi Seif akiangalia ngazi ya kutokea juu ya chumba cha chini ya Bahari katika Hoteli ya Manta Resort Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba kwenye sherehe za uzinduzi wa chumba hicho ikiwa ni 
muendelezo wa sherehe za kutimia miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimpongeza Meneja  
Mkuu wa Hoteli ya Manta Resort Bwana Methew Saus  kwa kukamilisha 
ujenzi wa chumba cha chini ya Bahari kwenye hoteli yake iliyopo 
Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba huku Waziri wa Habari Mh. 
Marouk akifurahia kitendo hicho.
Kitanda na mandhari halisi na nzuri iliyomo ndani ya chumba cha chini ya Bahari katika hoteli ya 
Manta Resort Makangale Kaskazini Pemba mradi uliozinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa 
Zanzibar balozi Seif.
Sehemu ya choo katika chumba cha chini ya Bahari kilichopo kwenye Hoteli ya Manta Resort huko Makangale Pemba.
Meneja  Mkuu wa Hoteli ya Manta Resort Bwana Methew Saus Maarufu 
“ Babu kwa Nini  “akitoa maelezo ya hatua zilizochukuliwa kukamilisha 
ujenzi wa chumba cha chini ya Bahari  katika Hoteli ya Manta Resort 
iliyoko Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba.Kushoto ya Balozi
 Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi, Waziri wa Habari, Utamaduni, 
Utalii na Michezo  Mh. Said Ali Mbarouk na Naibu wake Mh. Bihindi Hamad.
Meneja  Mkuu wa Hoteli ya Manta Resort Bwana Methew Saus akionyesha 
eneo la juu la chumba cha chini ya bahari ambapo mgeni atapata fursa ya kupunga upepo pamoja na kuota jua.
Mandhari nzuri ya Hoteli ya Manta Resort ya Makangale Mkoa wa 
Kaskazini Pemba eneo ambalo  kipo chumba cha chini ya Bahari.
Na Othman Khamis Ame  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 

Mradi mpya wa ujenzi wa Chumba cha chini ya Bahari uliofanywa na Hoteli ya Manta Resort iliyopo   katika Kijiji cha Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba umeiweka Zanzibar katika ramani mpya ya Dunia katika harakati za kuimarisha sekta ya Utalii unaobeba nafasi kubwa ya Uchumi katika 
Mataifa mengi Ulimwenguni.

No comments:

Post a Comment