Tuesday, October 28, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONESHO YA MWEZI WA WANAWAKE WAJASILIAMALI (MOWE) JIJINI DAR ES SALAAM.




 Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, wakati aliwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 28, 2014 kwa ajili ya kufungua rasmi Maonesho ya mwezi wa Wanawake Wajasiliamali (MOWE).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya GS 1, Ester Budili, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.Oktoba 28, 2014. Kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene.

No comments:

Post a Comment