Friday, October 11, 2013

PSPF YAKUTANA NA WADAU WAKE KATIKA CHAKULA CHA JIONI, YAELEZA FAIDA ZA KUJIUNGA NA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI

  


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni PSPF, Adam Mayingu akitoa taarifa za majukumu, mafanikio, changamoto na mipango ya mfuko kwa wadau wa mfuko huo waliohudhuria kwenye hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na PSPF.
Wakurugenzi wa idara tano za PSPF katika picha ya pamoja wakati wa utambulisho kwa wadau wa mfuko huo, kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani, Godfrey Ngonyani, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Gabriel Silayo, Kaimu Mkurugenzi wa Technohama, Andrew Mkangaa, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji, Francis Mselemu na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Masha Mshomba.  

Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji PSPF, Gabriel Silayo akieleza namna mfuko unavyowekeza ili kulinda thamani ya michango ya wanachama dhidi ya mfumuko wa bei na changamoto nyingine za kiuchumi
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji PSPF, Francis Mselemu akifafanua jambo kwa wadau wa mfuko huo
Afisa Mahusiano na Masoko wa PSPF, Hawa Kikeke na Mshereheshaji wa hafla hiyo Ephraim Kibonde 
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala PSPF, Masha Mshomba akifafanua jambo kwa wadau wa mfuko huo waliohudhuria hafla ya chakula cha jioni

No comments:

Post a Comment