Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, June 20, 2010

Priscus Nyoni mshindi wa gofu

Priscus Nyoni akijiandaa kuingiza mpira katika shimo wakati wa mashindano ya gofu ya Zain Lugalo Fiddle yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa TPDF Lugalo jijini Dar es Salaam .

Priscus Nyoni amefanikiwa kuwa mshindi katika mashindano ya mchezo wa gofu yaliyofanyika juzi katika viwanja vya mchezo huo vya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kupata pointi 31.

Nyoni aliyekuwa akichuana vikali na Terence Mwakaliku alifanikiwa kumshinda kwa tofauti ya pointi 2 baada ya mpinzani wake kujipatia pointi 29.Ushindi huo ulimpatia Nyoni zawadi mbalimbali kutoka Zain ikiwemo seti ya vyombo vya ndani.

Nyoni alisema kuwa zawadi aliyoipata itakuwa changamoto kwake ili azidi kufanya vizuri katika mashindano ya mchezo huo yatakayofanyika wiki ijayo.

Zawadi hii kwangu ni changamoto kubwa kwasababu kama nimeweza kuipata leo sitaki kuikosa tena,” alisema Nyoni

Nyoni ambaye ni mchezaji kijana wa gofu alisema kuwa hakuamini kama atashinda kwani mchezo ulikuwa mgumu na upinzani mkali na kusema kuwa siri ya mafanikio ni kufanya mazoezi kwa bidii.

Mbali na Nyoni washindi wengine ni Terence Mwakaliku , Simon Sayore na Stephania Sayore. Washindi hawa pia walijipatia zawadi mbalimbali ikiwemo miavuli,vyombo vya nyumbani pamoja na muda wa maongozi vyote kutoka Zain.

Michuano hiyo ambayo imekuwa ikifanyika kila mwisho wa wiki chini ya udhamini wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zain itaendelea wiki ijayo katika viwanja hivyo kwa kuwashirikisha wachezaji wa rika mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

MWANAIDI HASSAN NDIYE MWANAMICHEZO BORA 2009

MWANAIDI HASSAN NDIYE MWANAMICHEZO BORA 2009

Mwanaidi Hassan,akilia kilio cha furaha na kutoamini alipotangazwa kuwa Mwanamichezo Bora nchini Tanzania kwa mwaka uliopita wa 2009.Mwanaidi anacheza mchezo wa Netball.Anachezea timu ya JKT Mbweni na Timu ya Taifa ya Netball.Utoaji wa tuzo hizo ulifanyikia New Africa Hotel jijini Dar-es-salaam.

Mwanaidi Hassan(katikati) akikabidhiwa Tuzo ya Uanamichezo Bora na kitita cha shilingi Milioni Moja(1m Tshs).Anayemkabidhi ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania(BMT),Kanali Iddi Kipingu.Wanaoshuhudia pembeni,kutoka kulia kwenda kushoto ni David Nyombo,aliyechukua Ushindi wa Tatu kupitia mchezo wa kunyanyua vyuma vizito(body building),Juma Kaseja,aliyechukua ushindi wa pili kupitia mchezo wa Soka.Kaseja ni golikipa wa Simba Sports Club ya jijini Dar-es-salaam.Mwingine pichani ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo(TASWA),Boniface Wambura.TASWA ndio waandaji wa tuzo hizo.

Juma Kaseja(kulia) akipokea Tuzo ya ushindi wa pili.Kaseja, golikipa nambari moja wa Simba.Anayemkabidhi ni Jaji Mark Bomani,Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni ya Serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa tuzo hizo.

David Nyombo,mnyanyua vyuma vizito,akikabidhiwa tuzo yake ya ushindi wa tatu.

Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini na wadau wa TASWA.

Picha zote na Richard Mwaikenda.

NANI ATAIBUKA MWANAMICHEZO BORA?

Posted: 18 Jun 2010 09:59 AM PDT

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), leo kinatarajiwa kumtangaza mwanamichezo bora wa mwaka jana(2009) baada ya zoezi la kuwapigia kura wanamichezo waliofanya vema katika mwaka huo kukamilika jana.

Wanamichezo waliofanikiwa kuingia katika hatua ya fainali ni kipa mahiri wa Simba, Juma Kaseja, mfungaji mahiri wa timu ya netiboli ya Jeshi Stars, Mwanaidi Hassan na mtunisha misuli, David Nyombo. Kwa undani zaidi wa habarii hii bonyeza hapa.

David Nyombo

Juma Kaseja

Friday, June 11, 2010

ZAIN YAUZWA, YANUNULIWA NA AIRTEL

Airtel Yaunganika na Afrika – Yakamilisha makubaliano ya kibiashara ya kuvuka mipaka makubwa kuliko yote katika masoko yanayoendelea

Imeingia Ligi ya simu tano za mkononi zinazoongoza duniani

Nembo ya Airtel sasa yaenda kimataifa ikiwafikia watu bilioni 1.8

Yasisitiza nia yake kwa Afrika na Yaahidi huduma za bei nafuu, kusambaza mtandao na kutoa huduma kabambe

Yazishukuru serikali za nchi 15 Afrika kwa kuiunga mkono

New Delhi, Juni 8, 2010: Bharti Airtel Limited (“Bharti”) leo imechukua hatua kubwa ya kuelekea kuwa kampuni ya simu za mkononi ya kimataifa baada ya kukamilisha ununuzi wa shughuli za biashara ya Zain Group (Zain) katika nchi 15 Afrika kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 10.7. Kwa ununuzi huu, chapa ya Airtel sasa itakuwa ya kimataifa ikiwa inawafikia zaidi ya watu 1.8 bilion barani Asia na Afrika na wateja wakiwa zaidi ya milioni 180.

Makubaliano haya ya kibiashara ya kuvuka mipaka ni makubwa kuliko yote katika masoko yanayoendelea na yatapelekea kupatikana kwa mapato ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 12.4 na mapato kabla ya riba, kodi, uchakavu (EBITDA) ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 4.7, kwa kuzingatia mahesabu ya mwisho. Bharti sasa ni miongoni mwa makampuni matano makubwa ya simu za mkononi duniani.

Bw. Sunil Bharti Mittal, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Bharti amesema, “Tumefurahi kukamilisha makubaliano haya kwa ajili ya India na Bharti. Tunapenda kuzishukuru kwa dhati serikali za nchi zote 15 pamoja na serikali ya India kwa kutuunga mkono katika hatua hii muhimu. Na hii itakuza zaidi uhusiano wa kihistoria baina ya India na Afrika katika masuala ya kiuchumi na kijamii na kupelekea kuboresha ushirikiano kati ya Kusini na Kusini.

Bharti, ambayo imekuwa ikijizatiti kufikia dira yake ya kusambaa Afrika, imedhamiria kuchangia kukua kwa mawasiliano ya simu katika bara kwa kusambaza huduma ndani ya nchi hizo na kutoa huduma zenye bei nafuu ambazo zinawagusa watu wa kawaida. Pia tunawaadhidi wateja wetu wa Afrika mambo kabambe na bidhaa na huduma kadhaa zenye ubunifu wa hali ya juu.

Tunapenda kuwakaribisha zaidi ya wafanyakazi 6500 wenye vipaji na taaluma ya hali ya juu kwenye familia ya Bharti na tunasubiri kwa hamu kufanya kazi nao kupeleka kampuni zao kwenye hatua nyingine ya mafanikio. Tunapenda kuishukuru timu ya Zain kwa utaalamu wao, ambao umetuwezesha kukamilisha makubaliano haya katika muda unaoweka rekodi.’’

Bw. Asaad Al-Banwan, Mwenyekiti, Zain, said “Tunawatakia mafanikio makubwa Bharti Airtel katika kuendeleza kukua kwa mawasiliano ya simu katika bara la Afrika na tunauhakika watu wa Afrika wataipokea kampuni yenye nia dhabiti na inayotambulika duniani.’’

Ununuzi wa Bharti wa shughuli za Zain unahusisha nchi 15 zenye wateja 42 milioni. Idadi ya watu wanaoishi ni zaidi ya milioni 450 na mwingiliano wa simu ni takriban asilimia 32. Nchi ambazo Bharti imenunua shughuli zake ni; - Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Gabon, Ghana, Kenya, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Sierra Leone, Tanzania, Uganda, na Zambia. Zain inaongoza katika nchi 10 kati ya hizo nchi 15, na ni ya pili katika nchi zilizosalia nne.

Bharti ilishauriwa kuhusu makubaliano haya ya kibiashara na Standard Chartered Bank ambao walikuwa washauri wakuu, Barclays Capital kama mshauri mkuu mbia na SBI Group kama mshauri mkuu wa biashara (Onshore Advisor). Global Investment House , Kuwait walikuwa washauri wa kanda ( Regional Advisor).

Standard Chartered Bank, Barclays, SBI Group, ANZ , BNP , Bank of America Merrill Lynch, Credit Agricole CIB , DBS, HSBC, Bank of Tokyo Mitsubishi UFJ na Sumitomo Mitsui Banking Corporation ni wafadhili wa Bharti katika makubaliano haya.

Herbert Smith LLP walikuwa Washauri wa Kimataifa wa masuala ya Sheria, Milbank Tweed Hadley & McCloy LLP walikuwa washauri wa masuala ya Fedha na Sheria na AZB & Partners walikuwa washauri wa Sheria wa India, wakati Ernst & Young walikuwa washauri wa Mahesabu.

Kuhusu Bharti Airtel Limited

Bharti Airtel Limited, ni kundi la makampuni ya Bharti, na inaongoza katika masoko yanayoendelea ya simu za mkononi katika nchi 18 Asia na Afrika. Kampuni ina zaidi ya wateja milioni 180.

Bharti Airtel imewekwa katika nafasi ya makampuni sita ya teknolojia yanayoongoza duniani na Business Week. Bharti Airtel inamuundo wa vitengo vinne vya biashara, simu za mkononi, (mobile), Telemedia, Kitengo cha Biashara ( Enterprise ) na TV za Digital,

Biashara ya simu za mkononi inatoa huduma katika nchi 18 Asia na Afrika. Biashara ya Telemedia inatoa huduma za data (broadband), IPTV na huduma za simu katika miji 89 India . Kitengo cha Biashara (Enterprise business) hutoa suluhisho kwa wateja wa makampuni, na huduma kwa makampuni yanayojihusisha na usafirishaji wa ndani na wa kimataifa. Huduma ya TV ya digital inatoa huduma nchini India . Huduma zote hizi zinapatikana chini ya chapa ya Airtel, (bila kuhusiha Bangaladesh na Africa ).

Miundombinu ya kimataifa ya mtandao wa Airtel inajumuisha umiliki wa mfumo wa mkongo wa baharini wa i2i na ushirika pamoja na umiliki katika mfumo wa mikongo mitano ya kimataifa ya baharini, SEA -ME-WE 4, EIG, I-ME-WE, AAG na UNITY. Kwa maelezo zaidi. Tembelea; www.airtel.in.

Zain yakabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya SMS- JIVUNIE

Zain, Kampuni ya simu za mkononi inayoheshimika kwa kutoa huduma ya mawasiliano na kusambaa maeneo mengi zaidi hapa nchini imekabidhi jumla shilingi milioni mbili kwa washindi Promosheni ya SMS JIVUNIE.

Washindi waliokabidhiwa zawadi zao za pesa taslimu ambazo ni sh. 500,000/- kwa kila mmoja ni wale ambao ni wakazi wa jijini la Dar es Salaam wakati washindi wa kutoka nje ya Dar es Salaam taratibu za kuwakabidhi zawadi zao zinafanyika kuhakikisha kuwa nao pia wanakabidhiwa zawadi zao.

Washindi waliokabidhiwa zawadi ni Mashimba Mashimba, Chemu Hassani, Philip Masonda, Osole David Gilina, Godwin Joseph na Enock Dodan. Washindi hawa ni kati ya washindi 19 waliojishindia fedha taslimu ambazo jumla yake ni sh. Milioni 9.5 kutoka Zain.

Tangu kuanza kwa promosheni , Jumla ya washindi 26 kutoka mikoa mbalimbali wamejishindia zawadi mbalimbali zikiwemo Bajaj, baiskeli, na tiketi ya kushuhudia kombe la Dunia.

Meneja Masoko wa Zain Tanzania Costantine Magavilla alisema kuwa promosheni hiyo inaendelea kuchezeshwa ambapo washindi wataendelea kujishindia Zawadi mbalimbali kutoka Kampuni ya Simu za mkononi ya Zain Tanzania.

“Na leo hii kwa mara ya kwanza pia mtaweza kushuhudia tukimpa mshindi mwingine ambaye anajishindia tiketi ya kwenda kushuhudia kombe la Dunia, akiwa amelipiwa gharama zote yeye na mtu mwingine atakayemchagua kwenda naye, Kabla na baada kuisha kwa mwezi huu wa sita, tukiwa tumepata watanzania 12 watakaokwenda kushuhudia kombe la dunia nchini Afrika ya Kusini,”alisema Magavilla

Katika Promosheni ya JIVUNIE SMS kampuni ya Zain itatoa bajaj 10, baiskeli Toyota Corola 5, tiketi 12 za kushuhudia fainali za kombe la Dunia pamoja na fedha Taslimu 500,000/- kwa mshindi mmoja kwa kila siku. Zawadi kubwa katika promosheni hii itakuwa ni gari aina ya RAV 4 SUV.


Ili kushiriki katika promosheni hii ambayo inaendeshwa katika stahili ambayo mshiriki anajikusanyia pointi kutokana na maswali aliyoyajibu, mteja wa Zain anatakiwa kujisajili kwa kutuma neno JIVUNIE kwenda namba 15656.

Baada ya hapo mteja atapata ujumbe wa kumtaarifu kuwa sasa amesajiliwa na swali la kwanza litafuatia na maswali mengine pia yataendelea kuulizwa ambapo mshindi atapata pointi kutokana na kujibu majibu kwa usahihi.

Pointi za upendeleo zinatolewa endapo mshiriki atakuwa amefikia kiwango cha pointi ambazo zinatakiwa, na hii inaweza kumpa nafasi ya ushindi zaidi mshiriki na kujinyakulia zawadi za kila siku na zile za mwisho wa wiki.

Sunday, June 6, 2010

RAIS WA RBP KUIPELEKA TWIGA STARS KAMBINI MAREKANI!!

Rais wa RBP OIL & Industrial Technology Tanzania Limited Rahma Al Kharoos akiongea na waandishi wa habari leo kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam kulia ni Meneja Huduma wa kampuni hiyo Ibrahim Khatrush


Rais wa kapuni ya mafuta ya RBP Oil & Industrial Technology Tanzania Limited Rahma Al Kharoos ametangaza ziara ya timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars kwnda nchini Marekani kwa mafunzo mbalimbali wiki ya kwanza ya mwezi Agosti.

Akizungumza kwenye mkutano na wandishi wa habari katika hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam Rais huyo amesema anaamini kuwa ziara hiyo itakuwa ni chachu ya mafanikio ya timu hiyo wakati itakapokwenda kucheza katika fainali za kombe la mataifa ya afrika kwa wanawake mwezi septemba nchini Afrika Kusini.

Amesema akiwa kama mlezi na mdhamini wa Twiga Stars na kwa kushirikiana na wenyeji wa ziara hiyo huko Marekani ambao ni taasisi ya FREEDOM WASHINGTON wamejipanga kuhakikisha ziara hiyo inakuwa ni ya mafanikio hasa ukizingatia kwamba timu ya Twiga Stars imeweka historia kwa nchi yetu kushiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo makubwa ya mpira wa miguu kwa wanawake.

Ameongeza kuwa Twiga Stars ikiwa Merekani itacheza michezo minne wa kwanza utakuwa ni wa kuchangia timu hiyo (Charity) ambapo watu mbalimbali watachangia timu yetu ili iweze kujiandaa vyema na mashindano hayo.

Jana Twiga Stars ilifanikiwa kukata tiketi ya kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake nchini Afrika kusini ambazo zitafanyika mwezi septemba mwaka huu baada ya kutoka sale ya magoli 3-3 na timu ya Eritrea.
Naomba wadau, wapenzi wa soka la wanawake kuiunga mkono timu hii ambayo imeleleta sifa na heshima taifa la TANZANIA kwa kupata nafasi hiyo ya kushiriki michuano mikubwa zaidi baraNI Afrika kwa wanawake. Naamini kuwa sasa milango ya wachezaji wanawake kucheza soka la kulipwa nje itatimia.

Mikel kutocheza Kombe la Dunia, majeruhi

Kukosekana kwa Obi Mikel ni pigo kwa safu ya kiungo ya Nigeria.

Kiungo wa timu ya taifa ya Nigeria, John Mikel Obi, ametangaza kujitoa katika michuano ya Kombe la Dunia 2010 huko Afrika Kusini kutokana na majeraha ya goti.

Mikel anaungana na nyota wengine wa Chelsea, Michael Essien na Michael Ballack ambao watakosa michuano hiyo mikubwa kutokana na majeraha, pia kuna wasi wasi kuwa Didier Drogba naye huenda asicheze.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, alifanyiwa upasuaji wa goti mwezi Mei, lakini amesema bado hajisikii kuwa amepona kikamilifu kiasi cha kucheza katika Kombe la Dunia.

"Tumemwondoa Mikel kutoka kikosi chetu baada ya kueleza kuwa asingependa kuhatarisha uchezaji wake," msemaji wa timu ya Nigeria alieleza.

Nafasi yake Obi Mikel itajazwa na Brown Ideye, mshambuliaji kutoka klabu ya Sochaux ya Ufaransa, ambaye hajawahi kuchezea timu ya taifa ya Nigeria.

Osward Mweyunge mshindi wa Gofu Lugalo

Prev 38 of 120
  Tiger Woods Hits

Osward Mweyunge ameibuka mshindi katika mashindano ya mchezo wa gofu yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya mchezo huo vya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kujipatia pointi 39.


Mashindano hayo ambayo yalishirikisha wachezaji wa rika mbalimbali yanadhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania.


Kufuatia ushindi huo Osward ambaye ni kati ya vijana wanaochipukia katika mchezo wa gofu, alizawadiwa Seti ya vyombo vya ndani kutoka kampuni ya Zain pamoja na zawadi nyingine.


Mbali na Mweyunge washindi wengine ni Juma Likuli aliyepata point 37, Terence Mwakaluka aliyejipati point 31, Joseph Taird aliyejipatia point 38, Mohamed Rweyemamu aliyejipatia pointi 34 na Simon Sayore aliyejipatia point 31.


Washindi hawa pia walizawadiwa zawadi mbalimbali kutoka Kampuni ya Zain ikiwemo muda wa maongezi wa mtandao wa Zain.


Mweyunge alitoa wito kwa wadhamini wengine kujitokeza ili kuhakikisha kuwa mchezo wa gofu unachezwa katika kiwango kinachokubalika kitaifa na hata kimataifa.


“Sasa tuna Zain ambao kwa kiasi kikubwa wanahamasisha watanzania kucheza gofu lakini kwa kutoa zawadi ambazo pia zinawatia moyo wachezaji, bado tunaomba wafadhili wengine kujitokeza kudhamini mchezo huu,” alisema.


Kampuni ya Simu za mkononi ya Zain Tanzania ina mkakati wa muda mrefu wa kuendeleza mchezo wa gofu hapa nchini kwa kushirikiana na klabu ya gofu ya Lugalo ya jijini Dar es Salaam kuanzia kwa vijana wadogo ambao wana vipaji vya mchezo huo..

Ends.