Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, May 30, 2012

AMOSI MAKALA AKABIDHI BENDERA KWA WACHEZAJI WA GOFUNa Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala ameitaka timu ya Taifa ya Wanawake ya gofu kuhakikisha inapeperusha vyema bendera ya nchi katika mashindano ya All Africa Challenge yanayotarajia kuanza Juni 5, Botswana.

Timu hiyo inatarajia kuondoka nchini kesho kutwa huku ikiwa na Wachezaji watatu sambamba na mkuu wa msafara ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Maendeleo na watoto ya bunge Mary Chitanda.

Timu hiyo inaondoka nchini ikiwa tayari imeisha wahi kushika nafasi ya pili katika mashindano hayo yaliyofanyika mwaka 2010 ambapo hufanyika kila baada ya miaka miwili.

Akizungumza Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi bendera kwa timu hiyo Makala alisema watumie matoke hayo ya awali kwa kufanya vyema zaidi na kuweza kupeperusha vyema bendera ya nchi.

"Kama katika taarifa yenu ionavyosema mashindano ya mwisho mlishika nafasi ya pili sasa tunaimani mashindano haya mtakuwa wa kwanza na kuweza kututangaza vyema katika bara hili la Afrika, hivyo nendeni makaipiganie nchi yenu na kwa manufaa ya michezo," alisema.

Naye kwa upande wake Kepteni wa timu hiyo Madina Idd alisema kama waliweza kushika nafasi hiyo ya pili na wakati huo walikuwa katika maandalizi mabovu hivyo kwa sasa wanawahakikishia Watanzania wataibuka na ushindi.

"Mwaka 2010 tulishiriki na hata kufanikiwa kushika nafasi hiyo na huku tulikua katika maandalizi ya kusuasua lakini kwa sasa naimani tutafanya vyema zaidi," alisema.

Sambamba na hilo Shirika la ndege la Precion Air leo limekabidhi tiketi saba kwa timu  hiyo zikiwa ni za kwenda na kurudi ikiwa ni pamoja na tisheti na kofia vyote vikiwa na jumla ya sh. milion 7.3.

WAZIRI AMOS MAKALA AIKABIDHI BENDERA TIMU YA (TAIFA TAIFA STARS)Naibu waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh, Amos Makala akizungumza na waandishi wa habari leo hii jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi bendera kwa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars inayokwenda Nchini Ivory coast kucheza na timu ya taifa ya nchi hiyo  jumamosi ya wiki hii ambapo aliwataka wachezaji wa timu hiyo kuipa raha Tanzania kwa kishindo kizito na kuwatangazia kuwa wasiogope wachezaji wa Ivory coast makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA PHILEMONI SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Rais wa shirikisho la Mpira Tanzania TFF Bw, Leodger Tenga akiwatakia wachezaji hhao kila la heri katika safari yao na kuwatakia ushindi mwema.
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Kim Paulsen akiwahakikishia watanzania kuwa watakwenda kule Ivory Coast  kushinda kwani amewafundisha wachezaji wake namna ya kujiamini wenyewe na pia kuwa na nidhamu mchezoni ili waweze kupata ushindi.
Wachezaji wa timu ya Taifa waliohudhuria katika Tafrija hiyo ya kukabidhiwa Bendera.
Naibu waziri wa Utamaduni na Michezo Mh, Amos Makala (kushoto) akimkabidhi bendera ya taifa kapteni wa timu hiyo Mlinda mlango Juma Kaseja.

TUMBAKU HUUA WATU MILIONI 6 KWA MWAKA DUNIANI KOTE
NA MWANDISHI WETU
WAKATI Watanzania wakitarajia kudhimisha Siku ya Kutotumia Tumbaku Duniani kesho, imebainika kuwa tumbaku huua watu takribani milioni sita (6), kila mwaka.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Kumbana na Matumizi ya Tumbaku, Lutgard Kagaruki wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam kuhusu Siku ya Kutotumia Tumbaku Duniani.
Alisema maradhi yabayosababishwa na tumbaku huathiri nchi zite duniani, na ndiyo maana jumuiya ya kimataifa ikaungana na Mkataba wa Kimataifa wa Shirika la Afya Duniani wa kudhibiti matumizi ya tumbaku.
Kagaruki alisema  Mkataba huo umebeba misingi muhimu ya udhibiti wa matumizi ya tumbaku, itakayoweza kuokoa maisha ya watu milioni 200 ifikapo mwaka 2050, kama itatekeleza ipasavyo.
Alisema muingiliano wa kampuni za tumbaku umekuwa tishio kubwa kuliko yote kwa mikakati ya kutekeleza mkataba wa kimataifa wa kudhibiti matumizi ya tumbaku.
Kagaruki alibainisha kuwa mkataba huo unavipengele muhimu kwenye Kanuni namba  5.3 ambacho kinaeleza bayana mgongano mkubwa wa maslahi uliopo kati ya kampuni za tumbaku na afya ya jamii.

THABEET KUFUNDISHA KIKAPU WATOTO 200


NYOTA wa NBA, Hasheem Thabeet anategemea kutoa mafunzo ya siku mbili ya kucheza mpira wa kikapu kwa watoto 200 walio chini ya miaka umri wa miaka 17 kwenye  Uwanja wa Don Bosco kuanzia Juni 2 hadi Juni 3.

Thabeet anayechezea timu ya Portland Trail Blazers inayoshiriki Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) ataongoza kliniki hiyo yenye lengo la kuibua vipaji.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,Thabeet alisema  mafunzo ya mwaka huu yatakuwa ni tofauti kidogo na yale ya mwaka jana.

“Ninaimani kliniki hii itakuwa tofauti na ile iliyopita kwa sababu watoto wengi wamepata mwamko wa kucheza mpira wa kikapu baada ya kuona mafanikio ya wenzao,”anasema Thabeet.

Naye Meneja wa Sprite nchini Warda Kimaro wanadhamini wa mashindano hayo alisema baada ya mafunzo hayo vijana hao watakuwa kwenye mpango maalum wa kuendelezwa na kampuni yake.


Habari - Jackson Odoyo
Picha - globalpublishers.info
You might also like:

DIAMOND KUTUMBUIZA KATIKA SHINDANO LA MISS CHANG'OMBEBaada ya  kufanya  show ya Big Brother  Afrika Kusini MSANII Abdul Naasib ‘Diamond’ni mmoja wa wasanii watakaotoa burudani kamambe kulipamba  shindano la Redd’s Miss Chang’ombe 2012 shindano litakalofanyika Juni 9 mwaka huu  katika ukumbi wa Quality Centre barabara ya Nyerere Jijini Dar es Slaam.
Wengine watakaopamba shindano hilo la aina yake ni  kundi la Original Commedy akina Joti na bendi ya mapacha watatu ambayo kwa sasa imekuwa moja ya bendi zinayokonga  nyoyo za mashabiki wengi wa muziki hapa nchini.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam msemaji wa Kampuni ya King Promoters  ambao ndiyo waandaaji wa shindano hilo Martin Mauya ameaema kuwa kwa sasa warembo hao wameendelea kufanya mazoezi katika viwanja vya klabu ya TCC Chang’ombe Jijini Dar es Salaam.
Shindano hilo linatarajia kushirikisha warembo bomba 14 watakaopanda jukwaani kuchuana vikali kumpata mrembo wa mkoa huo wa kimashindano wa Chang’ombe huku baadhi ya wadau wa fani hiyo ya urembo nchini wakitabiri kuwa mrembo wa Tanzania mara hii atatokea katika mkoa huo wa kimashindano.
Mauya  amewataja warembo wanaotarajia kupanda jukwaani ni Elizabeth Mushi, Restituta Faustine, Miriam Ntakisivya, Flora Kazungu, Flora Robert,  Like Abraham, Clara Diu, Margareth Gerald, Jesca Haule, Deborah Nyakisinda, Suzan Paul, Wensley Matius, Zulfa Bundara na Catherine Masumbigana.
‘Kwa sasa warembo hao wanafanya mazoezi na kurudi nyumbani lakini Juni 3 warembo hao wataingia rasmi kambini katika Hoteli moja kubwa Jijini kabla ya kuapnda hiyo Juni 9’ alisema Mauya.
Shindano hilo limedhaminiwa na REDD’S ORIGINAL, NEXUS CONSULTING AGENCY, DODOMA WINE, CXC AFRIKA, PAPAZII INTERTAINMENT, KITWE GENERAL TRADERS,CHERISH, BEN EXPEDITION, SCREEN MASTERS, ARDHI PLAN LIMITED.

Meneja mkuu wa kampuni ya tigo atembelea kampuni ya Clouds Media Group leo jijini DarMeneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez akizungumza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga pichani kulia,mara baada ya kumaliza ziara ndani ya kampuni hiyo  na kujionea mambo mbalimbali,shoto ni Ofisa Mahusiano wa Tigo Alice Maro.
 Meneja Mkuu wa kampuni ya simu za mikononi ya Tigo akifanya mahojiano mafupi na mtangazaji wa Choice FM,aitwaye Thandi Kathembe mapema leo jioni.
Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga (pili kutoka kulia),akifafanua jambo kwa Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez alieambatana na Ofisa Mahusiano wake, Alice Maro,kulia ni Dj Fetty.
Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga akifafanua jambo kwa Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez (pichani kati),Kulia ni mmoja wa watangazaji wa Clouds FM,Ruben Ndege.
Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez akiperuzi moja ya jarida la Burudani hapa nchini la KITANGOMA,linalochapishwa na kampuni ya Prime Time Promotions LTD. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimuelekeza Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez namna ya baadhi ya vipindi vya Clouds TV vikiwa tayari kwa kurushwa hewani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimuelekeza Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez namna ya baadhi ya vipindi vya Clouds TV vikitayarishwa kabla ya kwenda kurushwa hewani.

WANASHERIA WA KIMATAIFA WASAIDIA KUWAJENGEA UWEZO WANASHERIA WA KITANZANIA Mkuu wa Chuo cha Sheria cha Tanzania Dr. Gerald Ndiku akiongea katika ufunguzi wa mafunzo kwa ajili ya wanasheria wa hapa nchini kuwajengea uwezo na mbinu za uandika maandiko ya kisheria, namna ya kutengeneza vipengele vya upatanishi wa mizozo, mwenendo wa kesi mahakamani, mikataba ya kuuza na kununua, mikataba ya mikopo pamoja na mbinu na taratibu zake na maandishi mengine ya kisheria kwa ujumla.
 Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Bi. Angellah Kairuki akisoma risala yake kuashiria ufunguzi wa mafunzo ya sheria kupitia Chuo Cha Taifa Cha Sheria kupitia shirika la kujitolea lijulikanalo kwa jina la New Perimeter lililoanzishwa na DLA Piper kwa muda wa wiki 2 kwa wanafunzi wapatao 240 yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Bw. Simon Boon kutoka DLA Piper- London Kitengo Maalum cha Restructuring ambaye pia ni kiongozi wa mradi akiongea machache.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Sheria cha Tanzania Dr. Gerald Ndiku, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Bi. Angellah Kairuki  wakiwa pamja na Bw. Lawrence Masha kutoka IMMMA Advocates.
 Wageni waalikwa wakiwa na wanafunzi.
Mshereheshaji wa sherehe hiyo, Bw. Sebo akiongea machache kabla ya kumaliza ufunguzi.
 Wageni wakiwa katika picha ya pamoja.
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Bi. Angellah Kairuki akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baaya ya kufungua mafunzo hayo.

WAZIRI AMOS MAKALA NA MATUKIO JIJINI DAR ES SALAAMNaibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla akikabidhi bendera kwa Timu  ya Taifa ya mchezo wa Golf inayotarajiwa kusafiri kwenda  Gaborone Botwsana kwa ajili ya mashindano ya chalenji ya Afrika kwa upande wa Wanawake.Wapili kushoto ni  Mh. Mery Chatanda (Mbunge).(Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla akikabidhi kiasi cha shilingi milioni kumi kwa mama wa marehemu Steven Kanumba ikiwa ni rambirambi ya Serikali kwa familia. (Picha na Benjamn Sawe wa WHVUM)
You might also like:

WEMA SEPETU AMRUSHA ROHO JOKETE


Msanii ambaye hajawahi kukaukiwa na matukio yenye kufaa kutengeneza vichwa vya habari katika vyombo vya habari nchini, Wema Abraham Sepetu, kwa mara nyingine ametawala vyombo vya habari baada ya tukio lake la usiku wa jana la kuvishwa pete ya uchumba na msanii wa bendi ya Machozi, anayekwenda kwa jina la Mwinyi.
Tukio hilo ambalo limevuta hisia za wapenzi wa masuala ya udaku na burudani nchini, lilijiri katika ukumbi wa Maisha Club, jijini dar es salaam, usiku wa kuamkia leo, ambapo lilishuhudiwa na mashabiki lukuki wa bendi ya Machozi waliokuwa wamejazana hapo kwa ajili ya burudani ya muziki uliokuwa ukiporomoshwa na bendi hiyo.
Hata hivyo, tofauti na ambavyo imechukuliwa na watu wengi kuwa Wema amepata mchumba mpya na ndio alikuwa akimvisha rasmi pete ya uchumba, ukweli ambao umewekwa wazi ni kuwa, mwanadada huyo alihusika katika tukio hilo kama sehemu ya maandalizi ya filamu yake mpya itakayokwenda kwa jina la Super Star.
Movie hiyo inatarajiwa kuelezea maisha halisi ya msanii huyo ambaye pia aliwika katika medani za ulimbwende, na Mwinyi atashiriki katika filamu hiyo akiigiza nafasi ya mwanamuziki Diamond, ambaye alikuwa mpenzi wa Wema na ambaye alimvisha pete ya uchumba lakini wakamwagana baadae kutokana na mikasa baina yao kuzidi kushamiri.
Kibwagizo: Hata hivyo, Wema anajulikana kuwa hajatulia, unadhani itashangaza kesho kusikia kuwa tukio hilo mbali ya kuwa sehemu ya filamu, lilikuwa pia tukio rasmi la kuwaunganisha wawili hao?

manny pacquiao ajifua kwa ajili ya kumdunda bondia timothy bradley

 manny pacquiao akifanya mazoezi kwa ajili ya mpambano wake june 9 na timothy bradley


Tuesday, May 29, 2012

MSANII WA BONGO FLAVA KASSIM MGANGA AWAPAGAWISHA MASHABIKI WA EXTRA BONGO MEEDA Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Kassim Mganga, (kushoto) akiimba katika jukwaa moja na wanamuziki wa bendi ya Extra Bongo wakati wa onyesho la bendi hiyo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Meeda uliopo Sinza Dar es Salaam. Mashabiki wa bendi hiyo walisikika kumshangilia baada ya kupanda jukwaani na kuimba kipande cha wimbo wa Rejina Zanzibar, huku wengine wakimtaka kuendelea kuimba bila kushuka jukwaani hapo.

 'Mkaanga Chips' Martine Kibosho, akizicharaza Drams, kwa umahiri mkubwa wakati wa onyesho lao hilo.
 Mwimbaji wa Bendi hiyo, Bob Kissa, akiimba jukwaani.
 Huyu yeye ni kiraka katika bendi hiyo, kwani anauwezo wa kuimba, kurap, kupiga Tumba na kucheza, ambapo ndani ya bendi hii ni Kiongozi wa Wanenguaji na tayari ametunga wimbo wake utakaokuwa ndani ya albam ya bendi hiyo ijayo unaokwenda kwa jina la Bakutuka.
 Mpiga Gitaa la Besi, mahiri Hosea Bass, akiliungirumisha gitaa katika onyesho hilo.
Wanenguaji wa bendi hiyo wakishambuliwa jukwaa wakati wa onyesho lao na kuwapagawisha mashabiki wao ambao kamwe hawakuvumilia kuketi vitini bali waliamka kila dakika na kwenda kuwatunza.

KAMATI YA MISS TANZANIA YATANGAZA SHINDANO DOGO LA KUMSAKA MWAKILISHI WA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA DUNIA

LINO INTERNATIONAL AGENCY LIMITED
P.O. BOX. 53069 DAR ES SALAAM, TELEFAX :+255 22 2120201,
SAMORA AVENUE AND MKWEPU, MOBILE: +255 753 764156,   DAR ES SALAAM.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABAR
29 MEI 2012

WAREMBO wanaotaka kushindana katika shindano dogo la kumsaka mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Dunia (Miss World 2012) wameombwa kuendelea kuchukua fomu za kushindana katika kinyang’anyiro hicho na kuzirudisha kabla ya Juni 

.Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga amesema  kuwa wanatarajia kufanya mchujo wa washiriki Juni 5 kwa ajili ya kubakiza warembo 10 kwa ajili ya kuwania nafasi ya kushiriki katika mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika Agosti 18 kwenye ukumbi wa Dongsheng Fitness Center Stadium,  mjini Ordos, Inner Mongolia, China.

Lundenga alisema kuwa  zoezi hilo lilisimamishwa kutokana na zuio la Serikali na  wakati huo, jumla ya warembo 12 walikuwa wamekwisha chukua fomu za kushiriki. Alisema kuwa muda wa kufanya mashindano hayo umekaribia na wanatarajia kuitangaza tarehe mpya hivi karibuni.

Alisema kuwa amefurahishwa na kasi ya kuchukua na kurejesha fomu, hata hivyo wanahitaji warembo wengi zaidi ili kuweza kupata wigo mpana kwa ajili ya kumsaka mrembo atakayewania taji la Dunia ambalo kwa sasa lina mikononi mwa mrembo kutoka Venezuela, Ivian Sarcos.

“Tunakaribia kufanya mashindano madogo hivi karibuni, hivyo ni wajibu wetu kuwakumbusha warembo wanaotaka kuwania taji hilo kufanya hivyo kabla ya Juni 4 ili kuweza kuingia katika zoezi la mchujo,” alisema Lundenga.

Alisema kuwa mpaka sasa jumla ya nchi 84 zimekwisha pata wawakilishi wao kwa ajili ya mashindano hayo. Nchi 32 pamoja na Tanzania bado hazija chagua wawakilishi wao katika mashindano hayo.

 Fomu za kuomba kushiriki zinapatikana katika ofisi za Miss Tanzania za jijini na mawakala wote wa mashindano hayo katika mikoa ya Tanzania Bara.

HIDAN .O. RICCO.
PRO.
LINO INTERNATIONAL AGENCY LIMITED
0715 019288

BAADA YA KUTANGAZWA KUTIMULIWA TWANGA PEPETA MARTINE SOSPETER ATANGAZA KUJIUNGA NA BENDI YA MASHUJAAAliyekuwa Meneja wa Bendi ya Twanga Pepeta, Martin Sospeter (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Busness uliopo Kijitonyama wakati akitoa malalamiko yake kuhusu tuhuma zilizoelezwa ndiyo chanzo cha kufukuzwa katika bendi ya Twanga majuzi, (kulia)  ni Kaimu Meneja wa bendi ya Mashujaa Muzika King Dodoo (kushoto) ni Rais wa Bendi ya Mashujaa Charles Baba.
****************************************
Akizungumza na waandishi wa habari Martine, alisema kuwa ''Juzi usiku nilishangazwa na kauli ya mkurugenzi wangu wa zamani, Asha Baraka, katika taarifa aliyoitoa katika vyombo vya habari  na mitandao ya kijamii kuwa amenifukuza kazi kutokana kuihujumu bendi ikiwemo kushawishi wanamuziki kujiunga na bendi ya Mashujaa,

Kwa kweli kauli ile ilinisikitisha sana kutokana na ukweli kwamba Asha, nilimchukulia kama zaidi ya dada kwani nilifanya naye kazi kwa  miaka 14 iweje hii leo aje anitolee maneno ya kunichafua katika vyombo vya habari?,

Mimi sijawahi kuhusika na mpango wowote wa wasanii wa Twanga kuhamia Mashujaa na wala sikuwa nafahamu mpango huo zaidi ya mwisho wa siku kusikia fununu za chinichini na mwishowe wasanii hao kutanghazwa kuhamia Mashujaa.

Leo napenda nitangaze rasmi kwamba nimeachana na African Stars na kujunga na Mashujaa Entertainment na tayari nimeshasaini mkataba wa kazi katika bendi hii, 

“Nilipanga nifanye taratibu za kumuaga kutokana na kuwa nilikuwa nafanya kazi kwake bila ya mkataba lakini nimepata bendi hii ambayo tulikaa na kukubaliana mambo kadhaa na kuona kuwa yana maslahi kwangu, 

Mbali na mkataba baadhi ya makubaliano na uongozi wa mashujaa ni pamoja na kunipangishia nyumba hali itakayonilazimu kuhama ile iliyokuwa chini ya Twanga.

Ninaamini nitafanya vizuri kazi zangu katika bendi hii mpya kama ilivyokuwa Twanga ambapo nilidumu kwa muda mrefu na kuchangia kufika hadi hapo nilipoachia, hivyo naomba ushirikiano kwa uongozi, wanamuziki, Wadau na hata ninyi wanahabari.

KUNANI WANAMUZIKI WOTE KUTIMKA TWANGA NA KUJIUNGA NA MASHUJAA??

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA MAENDELEO WA FINLAND NA UJUMBE WAKE IKULU DAR ES SALAAM LEO. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wa Waziri wa Maendeleo wa nchini Finland, Heidi Hautala (wa pili kushoto kwa Makamu) aliyeongozana na ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo asubuhi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wajumbe walioongozana na Waziri wa Maendeleo wa Finland, Heidi Hautala (wa pili kutoka kwa Makamu) baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam leo asubuhi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Waziri wa Maendeleo wa Finland na Ujumbe wake mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo asubuhi.
*********************************

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA FINLAND
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amekutana na Waziri wa Maendeleo wa Finland Mheshimiwa Deidi Hautala ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano na maendeleo wa nchi hizi mbili.
Katika mazungumzo hayo Dk. Bilal alimweleza Waziri huyo hatua zinazochukuliwa na serikali ya Awamu ya Nne katika kufikia dira ya Taifa ya maendeleo 2025 ikiwa ni pamoja na kutekeleza kauli mbiu ya kilimo kwanza na kuhakikisha kila mtoto anapata elimu.
Alisema katika kutekeleza kilimo kwanza, serikali inafanya jitihada ya kuhakikisha maafisa ugani wa kutosha wanapatikana ili kusaidia wakulima vijijini kujua mbinu bora za kilimo cha kisasa na namna zitakavyowawezesha kuzalisha kwa tija.
“Hata hivyo, tunajaribu kuongea na taasisi za fedha waweze kuwasaidia wakulima kwa kuwapatia mikopo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao,” alisema na kuongeza
“Tuna tatizo la soko kwani vijiji vingi havijaunganishwa na barabara, bado tunawapa msaada wa kutosha kuhakikisha mazao yao yanafika sokoni. Tunaamini kupitia kilimo kwanza tutawawezesha wakulima wetu kutoka kwenye kilimo cha mashamba madogo na kwenda kwenye mashamba makubwa ya biashara.”
Alipotakiwa kuzungumzia kuhusu mabadiliko ya hivi karibuni ya Baraza la Mawaziri Dk. Bilal alisema hali hiyo inatokana na serikali kutoa madaraka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali na kuruhusu Bunge kuwa huru zaidi.
Makamu wa Rais alimhakikishia Waziri huyo kuwa, wale wote watakaobainika na ubadhirifu wa mali za umma watafikishwa kwenye vyombo vya sheria na kusema kwamba serikali inatambua kuwa Mahakama ni chombo muhimu na kamwe hakuna mwenye mamlaka ya kuingilia katika kutimiza majukumu yake.
Akiwa nchini, Waziri Hautala ambaye anafuatana na ujumbe wa watu 12 anatarajia kuhudhuria mkutano wa Benki ya Maendeleo Afrika utakaofanyika mjini Arusha.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es slaam
Mei 29, 2012

USIKOSE USIKU WA HIP HOP
KESI YA LULU FULL ULIZI KILA KONA


LULU AFIKISHWA MAHAKAMANI, KESI YAKE YA AHIRISHWA MPAKA JUNI 11.

Lulu akishuka kutoka katika Basi la Mahabusu
Lulu akiwa katika viti akisubiri kusomewa mashtaka.
Askari magereza wakiimarisha ulinzi mahakamani hapo.

JOYCE KIRIA- KUTOKA U'HOSEGIRL MPAKA UTANGAZI
Na HERIETH MAKWETTA
'UGUMU wa Maisha ni Kipimo cha Akili'. Huu ni usemi uliozoeleka katika maisha ya kijamii hasa kwenye miaka ya sasa ambapo hali ya uchumi imekuwa ikizidi kuwa ngumu.
Katika ugumu wa maisha huo kuna walioshindwa kabisa kujikwamua hadi kukata tamaa. Lakini kuna ambao wameutumia ugumu huo kutafuta namna ya kujikomboa, ndiyo wanaozungumzia kwenye usemi huu.
Mmoja wa watu hao ni mtangazaji ambaye pia ni Mmiliki wa Local Media Entertainment, kampuni inayoendesha vipindi vya televisheni vya 'Wanawake Live' na 'Bongo Movie', vinavyorushwa na Kituo cha EATV, mwanadada Joyce Kiria.
Utumwa pasipo malipo sahihi na kutokuwa na uhuru wa maamuzi, vilikuwa sehemu ya maisha yake kwa muda mrefu. Ilikuwa ni baada ya kumaliza elimu yake ya msingi.
"Unajua natoka katika familia ya hali ya chini, hivyo nilipomaliza Darasa la Saba sikuwa na namna ya kuendelea na masomo," anasema.
"Nilianza kwa kufanya kazi za ndani za u-hausigeli, nilifanya kazi hii kwa miaka miwili. Sikuifurahia sana.
"Baadaye niliona nisonge mbele, niliiacha kazi hiyo na nikajiunga katika genge la mama ntilie, nilifanya kazi hapo kwa muda mpaka nilipoamua kuanza kuchoma chapati."
Hata hivyo anasema hakudumu na kazi hiyo kwani hakuwa akipatana na moto hivyo akatafuta kazi katika kiwanda cha mablanketi, Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
"Nikafanya kazi kwa muda pale lakini baadaye nikapata nafasi ya kazi katika duka moja Kariakoo, jijini Dar es Salaam, hapo ilikuwa tayari imefikia mwaka 2000," anaongeza.
"Niliendelea na kazi yangu na baadaye nilipata mtaji wa kuniwezesha kufungua biashara yangu."
Anasema alianza biashara zake rasmi kwa kupigisha simu katika vibanda vidogo, mtaji ulikua na baadaye alifungua duka la vifaa vya shule na mapambo, lakini baadaye akairudia biashara ya nguo.
"Baada ya kufanikiwa kukuza mtaji wangu, niliingia tena katika biashara ya nguo, na nikaanza kununua nguo za jumla kutoka Dubai, Falme za Kiarabu," anasema.
"Siku moja nikaenda na kununua nguo mwenyewe huko Falme za Kiarabu. Nilirudi na kuona nguo hizo zimejaa sana Kariakoo na bei yake ipo chini, hapo ndipo mtaji wangu ukafa au kwa maneno mengine nifilisika."
Anasema baada ya kushindwa biashara akaamua kumwona, Amina Chifupa (sasa marehemu) ambaye alikuwa mteja wake wa nguo na kumweleza shida yake.
"Amina ambaye wakati huo alikuwa anafanya kazi redio ya Clouds akanishauri nianze utangazaji kwani aliona nina kipaji, hivyo nilianza kazi hiyo pale Clouds mwaka 2006. Mwaka 2008 nikaolewa," anasema.

KUVUNJIKA KWA NDOA YA AWALI
Joyce, ambaye sasa ni mke halali wa Henry Kilewo, ndoa yake ya kwanza ilikuwa mwaka 2008 alipooana na Nelson Joshua 'DJ Nelly'.
"Muda mfupi baada ya ndoa nikaanza kuonja machungu yake, niliishi maisha ambayo sikuchagua, hii ilikuwa ni baada ya kuolewa," anasema.
"Niliamua kuachana na mume, unajua ilifikia hatua nilihisi ningeweza hata kuwekewa sumu katika chakula, yalikuwa ni maisha ya chuki.
"Hapo ndipo ukawa mwanzo wa kuyajua mengi ambayo niliamua rasmi kuanza kuyafanyia kazi nikiwa kama mwanamke niliyejitolea kutetea haki za wanawake."
Anasema alianza kwa kudai talaka ambayo ilikuwa ngumu kutolewa kwani ndoa aliyofunga ilikuwa ni ya Kikristo.
"Nilifanikiwa kupewa talaka yangu na hapo ndipo ukawa mwanzo wa kuanzisha kipindi cha Wanawake Live nikiwa na dhamira ya kweli ya kutetea Haki za Wanawake.

WITO WAKE KWA JAMII
Joyce ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro, anasema tatizo lililopo hapa nchini ni mfumo dume, ambao umekithiri.
"Mwanaume anasahau kutunza familia yake na kutokomea kusikojulikana, kwa sababu ya uchumi mdogo familia yake inaingia kwenye taabu, hali hii haivumiliki na ndiyo mwanzo wa kuvunjika kwa ndoa nyingi," anasema.
"Pia changamoto za kimaisha ni nyingi, wapo wanawake wenye kipato, lakini kutokana na mfumo dume wanalazimika kuacha kila kitu kikiwa chini ya waume zao ambao baadaye huwasaliti."
Anasema kupitia kazi yake ya sasa amepania kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili iachane na na mfumo huo kuweza kutoa haki sawa kwa wote.
Habari hii kwa hisani ya gazeti la Mwanaspot.

HOSPITALI YA TUMBI YAANZA KUPOKEA MSAADA WA MASHUKA Afisa Uhusiano wa Maxinsure akiongea na waandishi wa habari walipoenda kukabidhi  misaada  katika hospitali ya Tumbi, kushoto kwake ni Mganga mkuu wa Hospitali ya Tumbi Dk. Issac  Lwari
 Afisa Uhusiano wa Maxinsure akionyesha mashuka alioyakabithi katika hosptali ya Tumbi hivi karibuni
 Meneja Madai wa Kampuni ya Maxinsure  ,Bw. Ian Kifunta akishikilia mashuka ya msaada wakati walipokua wanatembelea hospitali ya  Tumbi hivi karibuni
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Tumbi Dk Issach Lwari akiwaonyesha wafanyakazi wa Maxinsure mashine mbovu,iliyokua ikinyooshea  nguo za hospitalini hapo.

Hospitali ya Tumbi ya mjini kibaha yapokea msaada wa mashuka 50 yenye thamani ya shillingi za kitanzania 500,000 kutoka katika kampuni ya Bima ya Maxinsure hivi karibuni, Msaada huo ukiwa umetokana na na taaarifa iliyotoka katika gazeti maarufu moja nchini,likiwa linaelezea kuhusu upungufu wa mashuka katika hospitali hiyo.

Kampuni ya Maxinsure ndio imekua kampuni ya kwanza kabisa nchini kuitikia wito huo, huku Bima kuu ya Afya ya nchini ikihahidi kutoa mashuka pia hivi karibuni.

“Tunashukuru sana kampuni ya Maxinsure kwa kuguswa na tatizo letu,tunategemea kupata mashuka zaidi na tunaomba makampuni mengine yaweze kujitokeza kutusaidia, kwani hili sio tatizo pekee linaloikabili hospitali yetu”.Alisema Mganga mkuu wa hospitali ya Tumbi,Dk.Issach Lwari akishukuru kwa msaada alioupokea

Kwasasa Hospitali ya Tumbi ina mashuka yapatayo 900 huku ikiwa bado na uhitaji wa mashuka yasiopungua 1,124.

DK. Lwari alitaja matatizo mengine kama ,mashine za kufulia, upungufu wa damu na pia hospitali iyo inakabiliwa na ukosefu wa Vipimo mbalimbali ,swala linalopelekea kuwashauri wagonjwa wachukue vipimo katika hospitali nyingine