Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, March 31, 2015

WATEJA WA SELCOM KUJINYAKULIA TSH 100,000 KILA SIKU



Meneja ukuzaji biashara na Masoko wa Selcom Tanzania, Juma Mgori kushoto akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya uzinduzi wa promosheni ya 'Shinda na Selcom' inayomwezesha mtumiaji wa huduma za kampuni hiyo kujishindia Tsh,100,000 ambapo washindi kumi watajishindia kitita hicho kila wiki na shindano hilo litadumu hadi mei 31 kulia ni Meneja Miradi wa Kampuni hiyo Gallus Runyeta
Meneja ukuzaji biashara na Masoko wa Selcom Tanzania, Juma Mgori kushoto akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi
 wa promosheni ya 'Shinda na Selcom' inayomwezesha mtumiaji wa huduma za kampuni hiyo kujishindia Tsh 100,000 ambapo washindi kumi watajishindia kitita hicho kila wiki na shindano hilo litadumu hadi mei 31 katikati ni Meneja Miradi wa Kampuni hiyo Gallus Runyeta na Meneja wa huduma za Ziada 'VAS', Chia Ngahyoma


 Meneja Miradi wa Kampuni ya Selcom Gallus Runyeta kushoto akimwelekeza Meneja ukuzaji biashara na Masoko wa kampuni hiyo, Juma Mgori jinsi shindano linavyo endelea katika mtandao



WASHINDI KUMI KILA WIKI

AIRTEL YAKARABATI DARASA SHULE YA MSINGI USHINDI


 


Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia), akizungumza kabla ya kukabidhi Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni Mwenyekiti wa Shule hiyo, Jumanne Konara na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elias Katunzi, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia), akimkabidhi Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Mikocheni ‘B’, Suleiman Sagong’o, Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni Mwenyekiti wa Shule hiyo, Jumanne Konara na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elias Katunzi, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia), akifungua mlango wa  Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Mwenyekiti wa Shule hiyo, Jumanne Konara, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elias Katunzi, Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Mikocheni ‘B’, Suleiman Sagong’o na baadhi ya wafanyakazi wa Airtel.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia), akiwasalimia watoto baada ya kukabidhi Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (mwenye miwani), na Afisa Mwandamizi wa Kitengo cha Biashara za Mashirika, Delfina Martin (mbele kulia), wakiwa wamekaa na watoto baada ya kukabidhi Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana.


Baadhi ya Wafanyakazi wa Airtel Tanzania, wakigawa zawadi kwa watoto baada ya kukabidhi Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
 
DAR ES SALAAM

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa “Airtel Tunakujali”  wakishirikiana na wafanyakazi wa kitengo cha Airtel Biashara za Mashirika ameendeleza dhamira ya kusaidia jamii kwa kukarabati darasa la chekechea katika shule ya msingi Ushindi iliyopo jijini Dar Es Salaam. Leo Airtel imebadili mtazamo wa darasa hilo kwa kuwa jengo la kisasa na kuwapatia vitendea kazi  ikiwemo madawati na  michezo mbalimbali kwa ajili ya watoto hao.

Shule ya Msingi Ushindi imekuwa miongoni mwa shule hapa nchini zilizoweza kuingia katika mfuko wa mradi wa  “Airtel Tunakujali” ili kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini. Baadhi ya shule ambazo zilishaweza kuingia  katika mradi huo ni Kumbukumbu Shule ya Msingi iliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam na shule ya Msingi Pongwe mjini Tanga. Lengo la mpango huu ni kuboresha mazingira ya wanafunzi na walimu mashuleni,kuwapataia wanafunzi elimu bora, kuhamasisha mahudhurio mazuri ya wanafunzi mashuleni na kunyanyua kiwango cha mfumo wa elimu katika katika taasisi hii.
Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano  , Mkurugenzi mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema, "Kutokana na dhamira ya Airtel tunafuraha kubwa sana kupata nafasi hii na kuwa ni wa moja wa makampuni yaliyopata nafasi ya kujenga mazingira bora na imara katika sekta ya elimu.  Leo hii tunakabidhi darasa zuri na la kisasa lenye Uwezo wa kukidhi idadi kubwa ya wanafunzi., hii itasaidia kupunguza shida iliyopo na kufanya mazingira ya kusomea kwa wanafunzi wengi kuwa rafiki. Tunaamini kwamba ubora wa elimu ni muhimu zaidi katika karne hii kwa ajili ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi hapa Tanzania. Sisi pia tunatambua changamoto nyingi katika ngazi zote za sekta hii muhimu.

Aliongeza " kwa kuboresha mazingira ya wanafunzi hawa ni kuchochea uelewa  na kuinua maisha yao ya hapo baadae. "Bila shaka, ubora wa elimu unawapa watoto nafasi bora katika maisha kutambua ndoto zao na kuwa viongozi bora wa kesho. Colaso aliendelea akisema, “anawaomba walimu na wanafunzi wa Ushindi watunze  rasilimali iliyotolewa kwao ili viweze kutumika na watoto wengine watakaokuja hapo baadae”.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi  ya Ushindi Elias Katunzi akitoa shukrani zake kwa Airtel alisema ,”kwa niaba ya walimu, wazazi na wanafunzi wa shule ya msingi ya Ushindi napenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kuweza kututengenezea  darasa lililobora na imara . 

Ningependa kuwashukuru Airtel kwa yote waliyotufanyia kwa ajili ya shule hii. Kutokana na msaada huu tuanaamini kabisa idadi ya watoto itaongezeka kwani kwa sasa tunawatoto wapatao 50 wa chekechea.Tunaamini kwamba idadi ya watoto itaongezeka na wazazi watapata moyo zaidi wa  kuwaandikisha watoto wao hapa shuleni. Tunatarajia uandikishaji utaongezeka katika kipindi kitakachofwata "alibainisha Katunzi.

Mwalimu mkuu akaongeza pia kuwa anafurahi kwamba Airtel wameweza kuwasaidia katika tatizo hilo la ukarabati wa jengo na kuziomba taasisi  nyingine kuchangia sekta ya elimu katika shule mbalimbali kwani matatizo yanafanana nchini kote.

Tuesday, March 24, 2015

BONDIA WANG XIN HUA KUTOKA CHINA AWASILI KUMKABILI MUDY MATUMLA IJUMAA


Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassini Abdalla kushoto akisalimiana na bondia Wang Xin Hua kutoka China mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam jana kwa ajili ya mpambano wake na mohamed Matumla utakaofanyika march 27 katika ukumbi wa diamond jubilee katikati ni Rais wa ngumi za kulipwa nchini PST Emanuel Mlundwa na kulia ni promota wa mpambano uho Jay Msangi Picha na SUPER D BOXING NEWS
Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassini Abdalla kushoto akisalimiana na bondia Wang Xin Hua kutoka China mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam jana kwa ajili ya mpambano wake na mohamed Matumla utakaofanyika march 27 katika ukumbi wa diamond jubilee katikati ni Rais wa ngumi za kulipwa nchini PST Emanuel Mlundwa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Wang Xin Hua kutoka China akilakiwa na mwenyeji wake Rais wa ngumi za kulipwa nchini PST Emanuel Mlundwa

bondia Wang Xin Hua kutoka Chinabondia Wang Xin Hua kutoka China
Bondia Wang Xin Hua kutoka China akiwasili nchini kwa ajili ya mpambano wake na Mohamed Matumla utakaopigwa March 27 katika ukumbi wa Diamond jubilee kulia ni promota wa mpambano uho Jay Msangi