Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, June 29, 2012

THE ORIGINAL COMEDY KUNOGEZA TAMASHA LA TIGO COCO BEACH DARMkurugenzi wa kikundi cha uigizaji cha The Original Comedy, Isaya Mwakilasa 'Wakuvanga' akielezea katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, jinsi walivyojiandaa kushiriki katika Bonanza la Tigo litakalofanyika kesho  na kesho kutwa kwenye ufukwe wa Coco, Oysterbay jijini. Kushoto ni Mratibu wa Promosheni wa Tigo, Edward Shila na Alice Maro ambaye ni Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo.(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

TBL FAMILY DAY YAFANA DARWafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), pamoja na ndugu zao wakishindana katika mchezo wa kuvuta kamba kwenye bonanza la kufurahi pamoja na familia zao, katika ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi Beach,Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.

 Wanafamilia wa TBL wakimuangalia mcheza sarakasi wa kikundi cha Black Texas, wakati akitembea juu ya waya.
 Mtoto wa moja ya familia ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambaye hakufahamika jina lake akitoa shoo ya bure katika bonanza la wafanyakazi hao kufurahi pamoja na familia zao, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja Usambazaji na Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kusini, James Bokela (kulia), akimkabidhi zawadi ya vifaa vya shule, mmoja wa mtoto wa wanafamilia ya TBL baada ya kushinda katika michezo wa mbio kwa watoto wa kiume bonanza la kufurahi pamoja na familia zao, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

 Ofisa Mnasihi wa VVU wa AMREF, Peace Kayoza (kushoto), akimchukua kipimo cha  damu Zaina Mohamed, mmoja wa wanafamilia ya TBL katika bonanza hilo.
 Meneja Uhusiano wa TBL, Editha Mushi akijadiliana jambo na viongozi wenzake wakati wa bonanza hilo.

                                                      Watoto wa familia ya TBL wakiogelea.

                                    Wafanyakazi wa TBL wakiwa wameshika zawadi za fulana.

Ofisa wa TBL Salvatory Rweimamu (kulia) akimkabidhi zawadi mtoto wa wanafamilia ya TBL aliyeshinda mbio.

MSAFARA WA RAIS WAZUIWA KWA KUWEKWA MAWE BARABARANI TEGETA, WALINZI 42, WANANCHI 56 WASHIKILIWA POLISI Askari wakilinda doria eneo ambalo lilitokea vurugu baada ya nyumba 10 na mabanda ya biashara kubomolea.

Baadhi ya akina mama wakiwa  na vyombo vyao  eneo la wazi  baada ya nyumba zao kubolewa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela akizungumza na wananchi wa Namanga Tegeta, ambao nyumba na mabanda yao vimebomolewa kimakosa jana na Kampuni ya Ulinzi ya Nassy ili kupisha upanuzi wa Barabara ya Bagamoyo.
Moja kati ya nyumba 10 zilizobomolewa na walinzi wa Kampuni ya Nassy katika eneo Namanga Tegeta, Dar es Salaam, leo, kiasi cha wenye nyumba na mabanda yaliyokuwa kando ya Barabara ya Bagamoyo, kuchukua hatua ya kuweka mawe na magogo barabarani wakitaka msafara wa Rais Jakaya Kikwete usimame wapate fursa ya kumueleza Rais kuhusu sakata hilo.  (PICHA ZOTE NA DOTTO MWAIBALE)

Mmoja wa wamiliki wa nyumba zilizobolewa katika eneo la Namanga Tegeta, Dar es Salaam, akilalamika mbele ya wanahabari jinsi walivyofanyiwa uonevu huo.

JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Dar es Salaam, linawashikilia walinzi 42 wa Kampuni ya Nassy, wananchi 56 na mmiliki wa Kituo cha kuuza mafuta cha Gapco cha Namanga Tegeta, wakituhumiwa kubomoa nyumba 10 za wakazi wa eneo hilo.

Tukio la kubolewa nyumba hizo lilifanyika katika eneo hilo jana asubuhi na kuzua tafrani kubwa iliyosababisha watu kadhaa kujeruhuiwa na kuurushia mawe msafara wa Rais Jakaya Kikwete uliokuwa ukielekea Bagamoyo.

Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Kamishina Msaidizi (ACP), Charles Kenyela alisema watu hao wanashikiliwa kwa ajili ya upelelezi kufuatia tukio hilo.

Alisema tukio hilo limetokana na mgogoro wa ardhi kati ya mmiliki wa kituo hicho Hemed Salum na wakazi wa eneo hilo ambapo jana alikwenda na walinzi hao na kuanza kubomoa nyumba hizo.

" Katika hali ambayo haikufahamika mara moja mmiliki wa eneo hilo licha ya kuwa jambo hilo lipo mahakamani alifika eneo hilo walinzi hao na kuanza kubomoa nyumba hizo'' alisema Kenyela.


Alisema watu hao wanashikiliwa kusaidia polisi na kuwa watu wawili waliojeruhiwa vibaya wapo Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.

Mmoja wa wananchi wa eneo hilo alisema hali hiyo imetokana na Polisi kushindwa kulifanyia kazi kwani mara kwa mara walikuwa wakipelekewa malalamiko lakini walikuwa wakipuuza.

"Haya ndio matokeo baada ya polisi kutupuuza na sasa yametokea madhara ndio wanakuwa wakwanza kufika tunaomba rais aingilie kati sula hili kwani naye amepata adha ya jambo hilo".  alisema mkazi huyo.

Kufuatia tukio hilo familia zilizokuwa zikishi katika nyumba hizo hazina mahali pa kuishi hadi tunaondoka eneo la tukio walikuwa wakiwasiliana na ofisi ya Serikali ya Mtaa wa eneo hilo kuona n jinsi ya kuwasaidia.

KHITMA YANGA YAISHA SALAMA 'ALHAMDULILLAH'Hitima Yanga imekwishasomwa, iliongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum. Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Wakili Imani Omar Madega, Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti katika uchaguzi wa Julai 15, Clement Sanga walikuwapo. Sasa watu wanakula, BIN ZUBEIRY anaondoka eneo la tukio.

Waungwana baada ya kisomo wakisubiri sadaka

Sheikh Mussa kulia, kushoto ni Katibu wake Almasi lailly Mussa na nyuma yao ni mwanachama wa Yanga, Mustafa Mohamed, Katibu wa Tawi la Kurasini

Madega kulia, akiwa na Sanga kushoto kwake

Waungwana wakisubiri sadaka baada ya dua

Katibu wa Yanga, Celestine Mwesigwa kulia, Madega na Sanga

Sheikh Mussa katikati, kulia Juma Mnonji mwanachama wa Simba, na kushoto Katibu wake, Almasi

Waungwana baada ya dua wakisubiri sadaka 


Maandalizi ya hitima katika klabu ya Yanga, makao makuu wa klabu, makutano ya mitaa ya twiga na Jangwani yanaendelea muda huu. Mboga zinakaribia kuiva, mchele umekwishaanza kuoshwa. Ng’ombe wawili wako jikoni. Ibada ya hitima yenyewe inakaribia kuanza kusomwa. Picha zote kwa msaada wa Blog ya BIN ZUBEIRY

Akina mama wakichambua mchele


Akina mama wakichambua mchelehttp://richard-mwaikenda.blogspot.com/
You might also like:

Tunawatambulisha Kwenu Blog maalum ya Miss Utalii Tanzania/Miss tourism Organisation.Miss Utalii Tanzania, tofauti na mashndano mengine ya urembo, ni zaidi ya shindano la urembo, kwani linalenga katika kutangaza na kuhamasisha Utalii,Utamaduni, Mianya ya Uwekezaji,Elimu,Afya ya Jamii,Utalii wa ndani,Utalii wa kitamaduni,Utalii wa Michezo na Utalii wa Mikitano Kitaifa na kimataifa. Shindano hili pia linahamasisha vita dhidi ya Umasikini,Iharibifu wa mazingira,uwindaji haramu,Uvuvi Haramu,Ujinga,Maradhi, Tamaduni kongwe na Potofu. Miss Utalii Tanzania pamoja na uchanga wake, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005, ni shindano lenye mafanikio makubwa kuliko shindano jingine lolote nchini kitaifa na kimataifa kwani pamoja na kuipa heshima Tanzania ya kuwa wenyeji wa shindano la Dunia la Miss Tourism World 2006, shindano hili ndilo lililo andika historia ya Tanzania kutwaa taji la kwanza la Dunia kabla na baada ya uhuru, pale tulipo twaa taji la Miss Tourism World 2006, pia shindano hili ndilo pekee nchini linashikilia rekodi ya kutwaa mataji ya dunia katika kila shindano tulilo shiriki,tumetwaa mataji 6 ya dunia tangu 2005. Kutokana na mafanikio haya , Tumepewa heshima ya kuaandaa shindano la Dunia la Miss Umoja wa Mataifa mwaka 2013 hapa Tanzania. Ni shindano pekee nchini ambalo washiriki wake hawavai mavazi ya kuogelea, bali mavazi ya heshima yasiyo mdhalilisha mvaaji wala mtazamaji na yaliyo buniwa na kushonwa kwa malighafi za tanzania tu.


MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM KATIKA MAONYESHO YA VIFAA VYA USAFI MANISPAA YA ILALA 
 Moja ya gari maalum kwa ajili ya kufagia barabara (Road sweeper) gari hilo linafagia barabara na kumwaga uchafu mbali zaidi.maonyesho hayo yamefanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe, Said Meck Sadick akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Operesheni ya usafi inayoendelea katika Manispaa ya Ilala ambapo aliwataka wananchi wa ilala kuwa na Ushirikiano kwa kutoegesha magari ovyo pasipo utaritibu ili waweze kupisha magari ya kufanyia usafi.

(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
 
Rachel Charles

MKURUGENZI Mtendaji wa Ear promotion Bw.Brian Kikoti amewaomba wafanyabishara ndogondogo wa soko  la wamachinga complex  kupeleka bidhaa zao  na sio kuliacha mpaka lichangamke.
Ameyasema hayo leo alipokuwa anaongea na wafanyabiashara katika soko la wamachinga jijini Dar es salaam, alisema wafanyabiashara ndogondogo hawapaswi kulikimbia soko hilo kwa madai kuwa hakuna wateja.
Bw.Kikoti alisema wamachinga wote wanapaswa kushirikiana na ear promotion ili kulitangaza soko hilo ndani na nje ya nchi ili kukuza uchumi kwa wafanyabiashara waweze kujikimu kimaisha na ata kukuza uchumi wa Taifa.
Pia alisema ili kulifanya soko hilo litambulike kimataifa watakuwa na maonyesho ya gulio litakalofanyika kila mwaka mwezi wa tisa kwa muda wa siku 14 ili kuwasaidia wafanyabiashara hao kutangaza bidhaa zao kwa uraisi.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ear Promotion Bw. Frank Miti alisema kila sikukuu  wataleta makampuni mbalimbali ili kuunga mkono mawazo na kuwawezesha wafanyabiashara hao  kupata faida kubwa.
Aidha  Wafanyabiashara ndogondogo wamelipongeza jambo hilo kwa kuwa litawapa fursa ya kuingia kwenye ushindani na kubadilishana  biashara na Nchi nyingine hivyo kupata misaada kutoka kwa wafadhili.

KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR LEOBaadhi ya maofisa mbalimbali na wananchi wakiwa katika Baraza la Wawakilishi wakisikiliza Hotuba na Michango mbalimbali inayotolewa na Wajumbe wa Baraza hilo.
 
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu mwenye kitabu akibadilishana mawazo na mwananchi ambae alienda kumuona huko katika Baraza la Wawakilishi nje ya mji wa Zanzibar.
 
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

RATIBA YA MICHUANO YA KOMBE LA KAGAME 2012KAGAME CUP 2012 FIXTURE
Sat. 14th July 1 APR vs WAU SALAAM Uwanja wa Taifa 2pm
2 YANGA vs ATLETICO Uwanja wa Taifa 4pm

Sun. 15th July 3 AZAM vs MAFUNZO Chamazi 4pm

Mon. 16th July 4 VITA CLUB vs PORTS Uwanja wa Taifa 2pm
5 SIMBA vs URA Uwanja wa Taifa 4pm

Tue. 17th July 6 ATLETICO vs APR Uwanja wa Taifa 2pm
7 WAU SALAAM vs YANGA Uwanja wa Taifa 4pm

Wed. 18th July 8 VITA CLUB vs URA Uwanja wa Taifa 2pm
9 PORTS vs SIMBA Uwanja wa Taifa 4pm

Thu. 19th July 10 ATLETICO vs WAU SALAAM Uwanja wa Taifa 2pm
11 MAFUNZO vs TUSKER Uwanja wa Taifa 4pm

Fri. 20th July 12 PORTS vs URA Uwanja wa Taifa 2pm
13 YANGA vs APR Uwanja wa Taifa 4pm

Sat. 21st July 14 AZAM vs TUSKER Uwanja wa Taifa 2pm
15 SIMBA vs VITA CLUB Uwanja wa Taifa 4pm

Sun. 22nd July REST DAY
QUARTER FINALS
Mon. 23rd July 16 B2 vs C2
17 A1 vs C3

Tue. 24th July 18 C1 vs A2
19 B1 vs A3

Wed. 25th July REST DAY

SEMI FINALS
Thu. 26th July 20 Winner 16 vs Winner 17

Thu. 26th July 21 Winner 18 vs Winner 19

Fri. 27th July REST DAY

FINALS AND 3rd PLACE PLAY OFFS
Sat. 28th July 22 Loser 20 vs Loser 21
23 Winner 20 vs Winner 21

WEMA SEPETU AAGANA NA OMOTOLA.Mwigizaji wa kimataifa kutoka nchini Nigeria Omotola Jalade, wapili kushoto akikabidhiwa zawadi za kanga, shanga na viatu kutoka kwa mwenyeji wake Wema Sepetu wakati akiondoka kuelekea Nigeria jana usiku. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions, Peter Mwendapole ambao waliratibu ziara ya msanii huyo mwingine ni msanii Snura Mushi.
Hapa Wema Sepetu akimvalisha kanga msanii huyo.

BIG RIGHT KUWAZAWADIA MABONDIA WAKE ENDAPO WATASHINDA Kocha wa ngumi wa Kambi ya mazoezi ya Big Right, Ibrahim (katikati) akiwa na mabondia wake wakati akiwasimamia katika Kambi yao ya mazozi ya pamoja kama timu kujiandaa na mapambano yao yanayotarajia kufanyika Julai 15 katika Ukumbi wa DDC Kariakoo, jijini Dar es Salaam, mwaka huu.
********************************************

KATIBU wa Vijana wa CCM Kata ya Kinondoni, Rehema Mbegu, ameahidi kutoa zawadi ya Baiskeli kwa Mabondo wa Klabu ya Mazoezi ya Big Right ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, iwapo watashinda katika mapambano yao yanayotarajia kufanyika hivi karibuni, ili kuwa moyo zaidi vijana kuupenda mchezo wa Masumbwi.

Rehema mbegu, mara kadhaa amekuwa akishirikiana na vijana wa Kata yake katika masuala mbalimbali ya Kijamii na ya kuendeleza michezo, ambapo amekuwa karibu zaidi na vijana wa rika zote na kuwapa sapoti kubwa ikiwa ni pamoja na kuwapa ushauri kujishughulisha na michezo zaidi ili kuepuka kutojiingiza katika mkumbo wa matumizi ya madawa ya kulevya.

Mabondia hao baada ya kuhakikishiwa zawadi nono ya kila atakayeshinda kuibuka na Baiskeli, wamezidi kuwa na morali zaidi na kutoa ahadi zao kwa Katibu huyo kuwa watafia ulingoni hadi kieleweke kwa kutupa mawe ya ukweli kwa wapinzani wao watakaokutana nao siku hiyo ya pambano.

Vijana hi wamekwishaanza kambi yao ya pamoja na kufanya mazoezi ya pamoja kama timu chini ya Kocha wao, Ibrahim Bigright na kuongeza muda wa mazoezi ambapo kwa sasa wanafanya mara tatu hadi kwa siku.

Mabondia hao ambao wanategemea kupanda ulingoni july 15 DDC-kariakoo ni Issa Omar(bigright boxing) atakaechapana na Ramadhan Kumbele, kutoka Kambi ya Matumla, katika uzani wa fly weight, Mwaite Juma kutoka Bigright Boxing,ambaye atapigana mkongwe Anthony Mathias,  katika uzani wa Bantam.

Ambao watakuwa wakisindikiza pambano la ubingwa wa taifa ni kati ya JUMA
FUNDI wa keko na BAINA MAZOLA wa mabibo kutoka kambi ya mzazi
 
Katika Mchezo huo kutakua na DVD  Mpya kabisa za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha
wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri
Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa

MASANJA NA WAKUVANGA WA KUNZI NZIMA LA ORINGINAL COMEDY KUPAMBA TAMASHHA LA TIGO COCO BEACH KESHO


.

Msanii wa vichekesho wa kundi la Kome ZE KOMEDI nchni Tanzania Isaya Mwakilasa (Wakuvwanga) akitoa burudani ya kuchekesha mbele ya waandishi wa habari wakati wa kutangaza tamasha la Uzinduzi wa maonyesho ya sabasaba yatakayofanywa na kampuni ya Tigo kwenye Viwanja vya Coco Beach kuanzia kesho Jumamosi hadi July 1 mwaka huu, kulia ni Afisa habari wa Kampuni hiyo Alice Maro na kushoto ni Mtaalamu wa Promosheni Mahusiano na Udhamini wa kampuni hiyo.

Mtaalamu wa Promosheni, Mahusiano na Udhamini wa kampuni ya tigo Edward Shila, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu bonanza la uzinduzi wa maonyesho ya sabasaba litakalofanyika kwenye Viwanja vya Coco Beach jijini Dar es Salaa.

USIKU WA MTU MZIMA DAWA BI CHEKA
You might also like:

DEIDRE LORENZ KAINGIA KWENYE MAPENZI NA TANZANIA Deidre Lorenz akimkabidhi picha ya Ground Zero (New York) Rais wa Mt. Kili Marathon 1991 Onesmo Ngowi baada ya kukimbia mbio hizo.
Deidre Lorenz akiwa anahojiwa na waandishi wa Habari mjini Moshi.
---
Na Grace Soka, Afisa Uhusiano
MT. KILIMANJARO MARATHON 1991


Mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ameahidi kuleta wacheza sinema wenzake na kushiriki kwenye mbio za mwaka kesho za mt. Kilimanjaro Marathon zitakazokuwa zinatimiza miaka 23 tangu zianzishwe mwaka 1991.
  
Lorenz aliyekimbia mbio za mwaka huu ambazo zilipewa jina la “mbio za kutimiza miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika” na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) amesema kuwa atakuja na timu yake ya wapiga picha ili kupiga picha vivutio kadhaa vya Tanzania ikiwa ni pamoja na mlima Kilimanjaro. Qwiji hili la sinema za Santorini Blue, The Great Fight, Perfect Strangers na nyingine nyingi ameelezea kuipenda sana Tanzania.

“Sikutegemea kuikuta nchi nzuri kama hii” alisema mcheza sinema huyo ambaye ameshawahi kuchaguliwa zaidi ya mara 4 kugombea tuzo maarufu za Oscar. “Sasa nimeamini kuwa mlima Kilimanjaro ni mali ya Tanzania na nitautangaza katika sinema zangu zote” aliendelea kusema Deidre Lorenz.

Mcheza sinema huyu ambaye ameingia kwenye mkataba na kampuni kubwa ya Google hivi karibuni ili kuuza sinema zake katika mtandao aliielezea Tanzania kama nchi nzuri na yenye watu wakarimu sana.

Mbio za Mount Kilimanjaro Marathon zilianzishwa mwaka 1991 na Marie Frances anayetoka katika jiji la matajiri la Bethesda nchini Marekani baada ya kuombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri. Tangu kuanzishwa kwake mbio hizi zimekuwa zinaleta watalii matajiri katika mji wa Moshi kupanda mlima Kilimanjaro na kukimbia mbio hizi zinazojulikana kama Seven Continental Races.
  
Hakuna masharti yote ya kukimbia mbio hizi na watanzania wanaoshiriki katika mbio hizi huwa hawatozwi pesa za kiingilio.
  
Kwa kutambua mchango wake katika uchumi wake Manispaa ya Moshi iliibadilisha jina barabara ya zamani ya Bustani Ale na kuiita Marie Frances Boulevard ili kumuenzi mama huyu aliyejitolea maisha yake kuutangaza mlima Kilimanjaro.

“Kila siku napokea ujumbe kutoka nchi mbalimbali niende huko kuanzisha mbio za marathon lakini kwa sasa basi” alisema mama huyo aliyekuwa mtayarishaji wa vipindi vya televisheni ya ABC kabla ya kunzisha Mt. Kilimanjaro Marathon.
  
Alisema kuwa mwaka jana yeye na Rais wa klabu ya Mt. Kilimanjaro Marathon mtanzania Onesmo Ngowi walifanya makubaliano ya Ethiopia Airlines (ET) jijini Addis Ababa kuzifanya mbio hizo kuwa za kimataifa zaidi. “ET walikubali kutoa ufadhili kwetu na pia kugharamia kushiriki kwetu katika mbio za New York Marathon, Boston Marathon na Los Angelos Maratthon ili kuitangaza vyema Tanznaia” alibainisha Frances.
  
Katika makubaliano hayo, Ngowi na Frances pia wataanzisha mbio za “King Solomon Marathon” zitakazofanyika katika jiji la Addis Ababa nchini Ethiopia.
  
Deidee Lorenz amefungua pazia kwa watu mashuhuri kushiriki katika mbio za marathon nchini Tanzania na ni jukumu la Watanzania kuchangamkia fursa zinazoletwa na ujio wao.

JOIN TO GROOVEBACK WITH BACKARD THIS SATURDAY AT NYUMBANI LOUNGE, DARZANZIBAR FILM FESTIVAL July 5 Mwaka huu mastaa kibao watashuka Bongo. Kutoka Marekani anakuja Mario
Van Peebles. Kama umeangalia filamu ya All Things Fall Apart ya 50
Cent utakuwa umewahi kumuona huyu jamaa, mle ndani aliigiza kama baba
wa 50 Cent.

Cabo Snoop naye atadondoka kutoka Angola, yote ni kuzifanya siku tisa

za tamasha zisimchoshe mtu yoyote, bila kwuasahau mastaa wetu Bongo
kama Diamond, Linah, Barnaba, Roma na Sultan King.

Bongo Movies wao ndio wataongoza jahazi la filamu, JB, Davina, Irene

Uwoya, Jackline Wolper, Cloud na wengine wengi wataheadline katika
tamasha.
 
JB akizungumza katika mkutano na wanahabari, pembeni ni Davina

AZAM MARINE KUMALIZA TATIZO ZANZIBARa
 Meli hiyo inavyoonekana kwa Nje
 Meli hiyo inavyoonekana kwa ndani.
Meli hiyo inavyoonekana kwa Ujumla
Azam yaamua kufanya kweli na hivi karibuni meli ya kisasa iko mbioni  kuzinduliwa ambayo ikawezesha watu kwenda na magari yao Zanzibar. Meli hiyo inauwezo kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo tani 500.KAMPUNI ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa ya kisasa kwaajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja. Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa. 
 Mohamedi alisema shida ya usafiri itapungua kwa asilimia kubwa kutokana na meli hiyo kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1500, Mizigo tani 500 na magari 200 ambapo abiria atakae jisikia kwenda na gari lake Zanzibar, Pemba au Dar es Salaam ataweza kufanya hivyo.
Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20.

KUMEKUCHA MISS UTALII KINONDONI 2012
baadhi ya washirki wa miss utalii kinondoni 2012