Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, October 30, 2014

SHIWATA WAGAWA MASHAMBA KWA WANACHAMA WAKE



Msanii Maarufu nchini Ahmed Olotu 'Mzee Chilo' wa kwanza kulia akimsikiliza mwenyekita wa SHIWATA Cassim Taalib wa pili kushoto  walipokuwa wakigawa mashamba kwa ajili ya wanachama wao
Watakaohamia kijiji cha wasanii kupewa bustani bure

Na Mwandishi Wetu

MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umetoa bure kwa wanachama wake wanaomiliki nyumba katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga ya eneo la kulima bustani.

Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa watakaonufanika na ofa hiyo ni wale watakaohamia katika nyumba zao kabla ya Desemba mwaka huu ambapo mtandao unaadhimisha miaka 10 kutoka uanzishwe.

Alisema wanachama hao wanatakiwa kufika SHIWATA kugaiwa maeneo hayo ambayo yatalimwa mazao ya muda mfupi (ambayo si ya kudumu) kama vile pilipili,mahindi, matango, pilipili hoho, mananasi, mbogamboga, matikiti maji ambayo hustawi kwa wingi maeneo hayo.

Katika hatua nyingine SHIWATA imeamua kusafisha shamba la ekari 200 ambazo zimekwisha gaiwa kwa wanachama ambao walijitokeza kulima katika shamba hilo la 500 zinazomilikiwa na mtandao huo kwa ajili ya maandalizi ya kilimo kwanza msimu huu katika kijiji cha Ngarambe, Mkuranga.

Mwenyekiti Taalib alisema SHIWATA imeingia mkataba na Kampuni ya Willy Enterprises Ltd ya Dar es Salaam kukodisha mtambo wa kusafisha shamba (Buldoza) kwa ajili ya wanachama zaidi ya 100 waliojitokeza kulima.

Alisema SHIWATA itatumia sh. mil. 22.2 kukodisha buldoza hilo kusafisha shamba la ekari 200 zilizogaiwa kwa wanachama ambapo kila mmoja atalipa gharama ya sh. 111,000 kwa ekari moja.

Jitihada za kusafisha shamba hilo zinafanywa na SHIWATA ikiwa ni maandalizi ya kufikiwa kwa malengo ya kuanzishwa mtandao huo utakaoadhimisha miaka 10 ya kuanzishwa mwaka 2004.

Mpaka sasa SHIWATA inao wanachama 8,000 kutoka fani mbalimbali za uigizaji, muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya, taarab, soka, netiboli, vijana na waandishi wa habari.
Mwanachama wa siku nyingi wa Shiwata Manase Zabron ambaye ni kocha wa mpira wa kikapu nchiniakienda kuoneshwa shamba lake
Baadhi ya viongozi wa Mtandao wa wasanii Tanzania 'SHIWATA' wakishudia ugawaji wa mashamba kwa wanachama wake juzi Ngarambe Mkulanga Mkoa wa Pwani

Tuesday, October 28, 2014

BONDIA FADHILI MAJIHA AONESHA MAAJABU KWA KUPIGWA KWA POINT THAILAND MCHEZO WA RAUNDI 12







Bondia Pungluang Sor Singyu wa Thailand kushoto akipambana na Fadhili Majiha wa Tanzania  wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia WBO Asia Pacific bantamweight title   uliofanyika katika uwanja wa shule ya Amphawa iliyopo Bangkok, Thailand Majiha alipigwa kwa point
Bondia Fadhili Majiha wa Tanzania kushoto akipambana na Pungluang Sor Singyu wa Thailand  wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia WBO Asia Pacific bantamweight title   uliofanyika katika uwanja wa shule ya Amphawa iliyopo Bangkok, Thailand Majiha alipigwa kwa point

 Na Mwandishi Wetu


akizungumzia matokeo hayo ya kupigwa kwa point bondia huyo amejigamba na kusema kuwa yeye alistaili ushindi hivyo wamempa kwa kuwa kacheza kwao na mcheza kwao utunzwa mana nilicheza kwa ustadi wa ali ya juu na wapenzi wote wa ngumi walikuwa upande wangu wakitafakali kwa nini nilinyimwa ushindi

bondia huyo ambaye anatamba sana hapa nchini kuwa akuna wa kumbabaisha ambapo anadai kukimbiwa mara mbili na bondia Fransic Miyeyusho pamoja na Nassibu Ramadhani ambao wote amewapa onyo ole wake mmoja wao akaingia anga zake atakiona cha moto kwa kuwa mechi zao nyingi wanapenda kupangiana wenyewe kwa wenyewe

nimerudi nyumbani nipo fit sina ata kovu la aina yoyote hile hivyo nitahakikisha nafanya mazoezi kuendeleza ufiti niliokuwa nao na napenda kutoa tahadhali kwa bondia yoyote mtanzania atakayejitokeza kwa sasa mbele yangu yeye atakuwa halali yangu 
nae  Kocha wake Waziri Chara amejigamba kwa kusema kuwa bondia wake ni wa kimataifa ambapo michezo yake karibia mitatu kacheza
Philippines na mwingine Thailand hivyo wao ni wa kimataifa zaidi mana mapambano aliyocheza nje yote yalikuwa magumu na raundi ni 12 ambapo zote alimaliza kwa kuwa nilimjenga katika mazingira mazuri mabondia wengi wakienda nje ya nchi wengiwao wanapigwa raundi ya kwanza ya pili awafiki ya nne

CHIDI BENZ APANDISHWA KIZIMBANI, AKOSA DHAMANA NA APELEKWA SEGEREA



 Msanii wa muziki wa kizazi kipya miondoko ya Hip Hop, Rashid Makwiro, ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiwasili katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. 
**************************************
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benzi’ leo amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la matumizi ya dawa za kulevya.

Chid Benzi, alipandishwa kizimbani majira ya saa nane mchana, mbele ya Hakimu Warialwande Lema, ambaye alimtaka msanii huyo atolewe nje kutokana na uvaaji mbaya wa suruali yake kwani alivaa ‘Kata kei’ ili avae vizuri nguo.

Akisomewa mashitaka yake, na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono, alidai kwamba mnamo 24 Oktoba 2014, Chidi Benzi alikutwa na dawa hizo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Alidai kwamba, shitaka la kwanza linalomkabili ni kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya sh.38, 638. Pia shitaka la pili ni kukutwa na gramu 1.72 za dawa kulevya aina ya Bangi yenye thamani 1,720.

Mbali na hilo, shitaka la tatu ni kukutwa na vifaa vinavyotumika kuvutia dawa hizo za kulevya, ambapo alikutwa na Kifuu cha nazi kitupu na kijiko kimoja.

Hata hivyo, wakili huyo alidai kwamba upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika. Hakimu Lema alihairisha kesi hiyo hadi Novemba 11, mwaka huu baada wadhamini kushindwa kujitokeza kwa haraka.

Hakimu Lema alisema, mshitakiwa huyo anatakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili wa kudumu pamoja na bonfdi ya Sh.milioni 1.

Hali hiyo ya kushindwa kupata dhamana ilizua hali ya simanzi kwa familia yake, kutokana na kuchelewa kujitokeza kwa wadhamini wake mbele ya Hakimu na hivyo kushindwa kupata dhamana.

Chidi Benzi alikamatwa na dawa za kulevya katika hatua ya ukaguzi kwaajili ya kupanda ndege ya Fastjet akielekea jijini Mbeya, juzi jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akiingia Mahakamani leo.
Chidi Benzi akipanda karandinga kwa ajili ya kuelekea katika mahabusu ya Segerea.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONESHO YA MWEZI WA WANAWAKE WAJASILIAMALI (MOWE) JIJINI DAR ES SALAAM.




 Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, wakati aliwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 28, 2014 kwa ajili ya kufungua rasmi Maonesho ya mwezi wa Wanawake Wajasiliamali (MOWE).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya GS 1, Ester Budili, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.Oktoba 28, 2014. Kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene.

CHEKA AONA NGUMI HAZILIPI, SASA ARUDI KUOKOTA CHUPA

Francis Boniface Cheka 'Maputo'
Na Imani Makongoro, Mwananchi
Nyumbani kwa bondia Francis ‘SMG’ Cheka hakuishi pilika ambazo zinatokana na kazi ya chupa za plastiki anayofanya bingwa huyo wa zamani wa dunia wa WBF.
Nje ya nyumba yake kuna mafurushi kila kona yakiwa na ‘bidhaa’ tofauti ikiwamo chupa za plastiki, chupa za konyagi, chibuku na plastiki ngumu (ndoo na madumu) yaliyopasuka.
Cheka anavyookota chupa
“Mimi ndiyo mwanzilishi wa biashara hii hapa Morogoro, niliianza 2004 baada ya kuamua kuingia mtaani kuokota na kuziuza mwenyewe, wakati huo kilo moja niliuza kwa Sh100 na nilikuwa nikizunguka kutwa nzima kutafuta chupa mtaani,” anasema Cheka.
Anasema wakati anaanza kuokota chupa alikuwa na miaka mitano tangu aingie kwenye ngumi za kulipwa, lakini hakuwa maarufu.
“Nilikuwa nina uwezo wa kuzunguka na kuokota hadi kilo 100 kwa siku, japo ilikuwa kazi ngumu, lakini nilipata fedha nikanunua kiwanja maeneo ya Kilimahewa na kujenga nyumba kwa kazi ya kuokota chupa.
“Pia niliweza kujiandalia mapambano peke yangu kwa kazi hii, ambayo yalinijenga na kunipa umaarufu kwenye ngumi, nimejiandalia mapambano zaidi ya 15 kwa fedha niliyopata kwa kuokota chupa,” anasema Cheka.
Anasema vijana wengi wa Morogoro walianza kuokota chupa baada ya kuona Cheka amejenga nyumba kwa kazi hiyo, hivyo hakuwa na hiyana aliwafundisha kazi hiyo na wengine aliingia nao mtaani kuokota.
“Nilipoanza kucheza mapambano ya ubingwa wa Afrika nilisimama kuokota chupa nikawaachia wengine na mimi kuelekeza nguvu zangu kwenye ngumi, kijiwe changu nikamweka mtu wa kufanya hiyo kazi na nikawa na nanunua kwa watu wengine kisha mimi nauza tena.
“Kwa kipindi chote ambacho nilikuwa nimebanwa na masuala ya ngumi, mradi wangu huu uliyumba kwani kila niliyemwachia alikuwa na fikra za kuniibia, ilifikia mahali nikakwama kwani nilikopa fedha benki kuongezea nguvu kwenye biashara yangu ya makopo hivyo nilipaswa kulipa,” anasema Cheka.
Anavyookota chupa mtaani
“Watu wanashangaa mtu kama mimi kuokota chupa, lakini ndiyo kazi inayoniweka mjini, wiki iliyopita nilikuwa Msamvu (stendi kuu ya Morogoro) nakusanya chupa kwa bahati nikakutana na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia alishangaa kuniona naokota Chupa.
“Hakuamini kama mimi bingwa wa dunia na bondia namba moja Tanzania ndiyo naokota chupa mtaani, lakini ukweli nisipofanya kazi hii na nikabaki kutegemea ngumi, maisha yatakuwa magumu kwangu,” anasema Cheka.
Anasema haoni aibu kufanya kazi hiyo kwani ni kazi iliyompa mafanikio na kujenga nyumba mbili, moja ikiwa Kilimahewa ambako anaishi hivi sasa na nyingine Kihonda alikowapangisha watu wengine.
“Muda wangu mwingi nimeelekeza kwenye chupa, mazoezi sasa sifanyi kwani nina muda sijafanya mazoezi ya ngumi, nasimamia mwenyewe biashara yangu ya chupa ambayo mbali na kuokota mwenyewe pia kuna watu ambao wanaokota na kuniuzia.
“Chupa za maji nanunua kilo moja Sh250 na mimi nauza 700 baada ya kusaga, kwa mwezi nina uhakika wa kuuza kilo 4,500 mpaka 6,000 na plastiki ngumu nanunua Sh350 na mimi nauza Sh 2,000 baada ya kusaga hivyo kwa mwezi nauza zaidi ya kilo 3,000, pia naokota chupa za konyagi na chibuku ambazo naziosha na kuwauzia watu wa kampuni hizo,” anasema Cheka.
Ameamua kuingia mtaani kutembeza CD
“Sijapata mafanikio yoyote kwenye ngumi hadi sasa hivyo nimeona nijaribu kuuza CD za mapambano yangu labda nitafanikiwa,” anasema Cheka.
Anasema kazi hiyo anaifanya kwa kutembeza CD zake mkononi na kuwapelekea watu kwenye maeneo tofauti mjini Morogoro na amekwishauza CD 200 hadi sasa.
“Nilitoa CD 200 ambazo niliziuza kwa kutembeza mwenyewe mkononi zikaisha na sasa nimetoa nyingine 200, najitangazia biashara mwenyewe kwani napeleka kwenye mkusanyiko wa watu, vituo vya daladala, Stendi ya Msamvu na maeneo ambayo najua nikienda sikosi wateja, CD moja nauza Sh 3000,” anasema Cheka.
Fedha nyingi aliyowahi kupata katika ngumi
“Fedha nyingi niliyopata ni Sh10 milioni ambayo nilicheza pambano Russia mwezi Desemba 2012 na kupigwa kwa Knock Out (KO) raundi ya nne, pambano lile nilicheza bila kujiandaa na nilipata fedha hiyo kwa kuwa sikuitumia kwenye maandalizi,” anasema Cheka.
Anasema mapambano mengi anayocheza nchini amekuwa akiambulia Sh3 milioni mpaka Sh4 milioni baada ya kutoa fedha za maandalizi, kumlipa kocha na kununua vifaa.
“Pambano nililocheza na Mmarekani la ubingwa wa dunia nilipewa Sh4 milioni za maandalizi, nikaweka kambi Nairobi kila kitu nalipa mwenyewe mpaka kumlipa kocha, hadi narudi sina fedha baada ya pambano nikapewa Sh3 milioni, nilikuwa na madeni nikalipa na kubaki sina kitu.
“Hata wakati nafanyiwa sherehe ya kupongezwa Morogoro, sikuwa na hata shilingi, siku nawekewa dau la Sh10 milioni nikacheze Russia, sikukataa japo nilijua sina mazoezi, nilipigwa KO kihalali na kuvuliwa ubingwa wa dunia,” anasema Cheka.
Mkakati wake wa kurudi shule
Cheka alipewa ofa ya masomo kwenye Chuo cha St Joseph cha mjini Morogoro na aliingia darasani siku moja kisha akatokomea hadi leo hajawahi kurudi.
“Mimi ni baba wa familia ambayo inanitegemea, siyo kama sipendi kusoma, lakini nikiwa shule majukumu ya familia nitayatekeleza vipi? Hivi sasa nimeamua habari ya kusoma niiweke kando niboreshe biashara yangu, Mungu akiniweka hai, nitasoma miaka ijayo,” anasema Cheka.
Kwa nini anaitwa Kazimoyo?
Akiwa Morogoro, Cheka anajulikana pia kwa jina la Kazimoyo.
“Hili jina nimepewa na marafiki zangu ambao wananiita Kazimoyo kutokana na kazi ninazozifanya, ambazo wanasema nina moyo mgumu ndiyo sababu nazifanya, hivyo kazi ninazofanya sasa na nilizowahi kufanya nimefanya kwa moyo tu,” anasema Cheka.
Historia fupi ya maisha yake
Cheka alizaliwa miaka 32 iliyopita jijini Dar es Salaam, akiwa mtoto wa kwanza kwa baba yake, Boniface Cheka na alisoma Shule ya Msingi Kinondoni Hananasifu.
Alianza kucheza ngumi akiwa darasa la tatu na wakati huo baba yake alipenda kumfundisha ngumi.
“Nilipohitimu shule ya msingi, nilipata kazi kwenye gari la taka la Manispaa ya Kinondoni, nilifanya kazi hiyo pia nikijifua ngumi kwenye Ukumbi wa Arnautoglu, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
“Baada ya kuona maisha magumu Dar es Salaam, Nilikwenda Morogoro, sikuwa na mahali pa kufikia hivyo nikaomba kazi ya kufagia Stendi ya Msamvu na usiku hapo ndipo nikawa nalala,” anasema Cheka.
Anasema alilazimika kutandika maboksi na kulala kituoni hapo usiku ulipoingia na asubuhi anaamkia kwenye kibarua cha kufagia kituo hicho.
“Nilipata fedha kidogo na kupanga chumba, nakumbuka kitanda changu nilinunua kwa fedha niliyopata kwenye kazi ya kuzibua choo, sikuwa na ujuzi huo, lakini rafiki zangu waliponiambia kuna kazi hiyo nilienda kufanya na kulipwa Sh50,000 ambayo ilikuwa fedha nyingi kuwahi kulipwa,” anasema Cheka.
Anasema baada ya muda ndipo aliingia mtaani kuokota chupa, kazi iliyompa mafanikio na kujenga nyumba, na kutumia fedha aliyopata kujitangaza kwenye ngumi.
CREDIT: MWANANCHI

Sunday, October 26, 2014

BONDIA SAIDI MBELWA APIGA GEORGE DIMOSO KWA POINT




Bondia Georger Dimoso kushoto akipambana na Said Mbelwa wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamoso iliyopita Mbelwa alishinda kwa point mpambano huo wa raundi nane Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Said Mbelwa kushoto akioneshana umwamba na Geore Dimoso wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi jana Mbelwa alishinda kwa point Picha na SUPER D BLOG


 Mashabiki wa mchezo wa masumbwi wakifatilia kwa makini mchezo huo
Bondia Said Mbelwa akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi wa mpambano huo

S
Bondia Hamza Mchanjo kushoto akipambana na Juma Fundi wakati
wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Fundi alishinda kwa point mpambano huo wa raundi sita picha na SUPER D BLOG
Baadhi ya mashabiki kutoka Tanzani Boxing Fans Group Watssup wakijadili jambo na bondia Thomasi Mashali wa pili kushoto anae ongea nae ni Rajabu Mkamba mwenye tai
Bondia Aman Bariko 'Manny Chuga' akioneshana umwamba na Ally Bugingo wakati wa mpambano wao Bariki alishinda kwa point picha na SUPER D BLOG

Bondia Zamoyoni Mbishi kushoto akipambana na Sadiq Nuru wakati wa mpambano wao uliofanyika jana Mbishi alishinda kwa pointi picha na SUPER D BLOG


Bondia Hassan Mandula kulia akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Mohamed Jaka Mandula alishinda kwa TKO ya raundi ya pili picha na SUPER D BLOG

UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA), WASAINI WARAKA WA USHIRIKIANO JANGWANI DAR ES SALAAM LEO


 -Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakionesha hati za waraka walizotiliana saini za ushirikiano katika viwanja vya Jangwani Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalimu Seif Sharifu Hamad , Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
 Waendesha bodaboda ambao ni wafuasi wa Ukawa wakiingia kwa maandamano katika viwanja vya Jangwani.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalimu Seif Sharifu Hamad , akihutubia kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Emanuel Makaidi akihutubia kwenye hafla hiyo kabla ya kutiliana saini waraka wa ushirikiano.
 Makatibu wakuu wa vyama vinavyuunda Ukawa, wakionesha ishara ya mshikamano baada ya kusaini waraka huo wa ushirikiano. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrord Slaa, Katibu Mkuu wa CUF, Maalimu, Seif Sharifu Hamad na Katibu Mkuu wa Chama NLD, Tozi Matwange.
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tundu Lisu (kulia), akimkaribisha Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jusa Ladhu, kuzungumza katika mkutano huo.
 Wafuasi wa ukawa wakionesha vidole vitatu juu wakimaanisha kuikubali serekali tatu inayotakiwa na Ukawa.
 Wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), wakiwa 
kwenye mkutano huo.
Vijana wa chama cha chadema wakiwa juu ya gari wakifuatilia matukio mbalimba yaliyokuwa yakiendelea uwanjani hapo. Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com

MAKAMU WA RAIS AHUTUBIA WASANII KWENYE MADHIMISHO YA SIKU YA MSANII MLIMANI CITY JANA USIKU OCTOBA 25-2014



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Msanii yaliyofanyika jana usiku Octoba 25-2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi tunzo Edward Said Tingatinga msanii aliyejitolea maisha yake kwa Jamii, kwenye maadhimisho ya siku ya Msanii
yaliyofanyika jana usiku Octoba 25-2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi tunzo Josephat Kanuti msanii aliyejitolea maisha yake katika tasnia ya sanaa Nchini,   kwenye maadhimisho ya siku ya Msanii yaliyofanyika jana usiku Octoba 25-2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
 Wasanii na wananchi mbalimbali waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo wakifuatilia kwa karibu matukio mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika kwenye ukumbi huo. (Picha na OMR).

Friday, October 24, 2014

NGUMI KUPIGWA KESHO OKTOBER 25 FRENDS CORNER MANZESE

Bondia Ally Bugingo akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Amani Bariki 'Manny Chuga' mpambano utakaofanyika Oktoba 25 katika ukumbi wa Frends corner Manzese Dar es salaam katikati ni Antony Rutta picha na SUPER D BLOG
Bondia Sadiki Nuru akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa kesho jumamosi
Bondia Said Mbelwa akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika kesho oktoba 25 katika ukumbi wa frends corner manzese ambapo anapambana na George Dimoso mpambano wa raundi nane picha na SUPER D BLOG
Bondia Fadhili Boika kushoto akitunishiana misuli na Robinson Msimbe baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utajkaofanyika jumamosi ya oktoba 25 katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam picha na SUPER D BLOG



 Mwandishi Wetu

MPAMBANO wa mchezo wa masumbwi mkali utakaokutanisha mabondia mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania utafanyika

October 25 katika ukumbi wa friends Corner manzese jijini Dar es salaam akizingumza na waandishi wa habari mratibu wa mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'


amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mpambano wa mahasimu katika mchezo wa ngumi kati ya bondia Saidi Mbelwa 'Moto wa Gesi'  na George Dimos mpambano mwingine utawakutanisha Amani Bariki 'Manny Chuga' na Ally Bugingo mpambano unaosubiliwa kwa hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo mabondia hawo wamejizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo


pambano jingine ni kati ya Juma Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati Hasani Mandula ataonyeshana kazi na Mohamedi Jaka na Shabani Kaoneka atazipiga na Ibrahimu Maokola anaejiandaa kuwania kucheza ubingwa wa taifa mwishoni mwa mwaka huu Fadhili Boika atazipiga na Godfrey Silver  na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje, Kashinde Mohamedi atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru atakumbana na Mohamed Mbishi


katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo  kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali 



siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika


mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd

Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

NGUMI KUPIGWA KESHO OKTOBER 25 FRENDS CORNER MANZESE

Bondia Ally Bugingo akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Amani Bariki 'Manny Chuga' mpambano utakaofanyika Oktoba 25 katika ukumbi wa Frends corner Manzese Dar es salaam katikati ni Antony Rutta picha na SUPER D BLOG
Bondia Sadiki Nuru akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa kesho jumamosi
Bondia Said Mbelwa akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika kesho oktoba 25 katika ukumbi wa frends corner manzese ambapo anapambana na George Dimoso mpambano wa raundi nane picha na SUPER D BLOG
Bondia Fadhili Boika kushoto akitunishiana misuli na Robinson Msimbe baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utajkaofanyika jumamosi ya oktoba 25 katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam picha na SUPER D BLOG



 Mwandishi Wetu

MPAMBANO wa mchezo wa masumbwi mkali utakaokutanisha mabondia mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania utafanyika

October 25 katika ukumbi wa friends Corner manzese jijini Dar es salaam akizingumza na waandishi wa habari mratibu wa mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'


amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mpambano wa mahasimu katika mchezo wa ngumi kati ya bondia Saidi Mbelwa 'Moto wa Gesi'  na George Dimos mpambano mwingine utawakutanisha Amani Bariki 'Manny Chuga' na Ally Bugingo mpambano unaosubiliwa kwa hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo mabondia hawo wamejizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo


pambano jingine ni kati ya Juma Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati Hasani Mandula ataonyeshana kazi na Mohamedi Jaka na Shabani Kaoneka atazipiga na Ibrahimu Maokola anaejiandaa kuwania kucheza ubingwa wa taifa mwishoni mwa mwaka huu Fadhili Boika atazipiga na Godfrey Silver  na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje, Kashinde Mohamedi atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru atakumbana na Mohamed Mbishi


katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo  kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali 



siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika


mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd

Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

Thursday, October 23, 2014

WABUNGE WA KAMATI YA UCHUMI VIWANDA NA BIASHARA WATEMBELEA KIWANDA CHA KONYAGI





Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'KONYAGI' Bw. David Mgwassa wa pili  kulia akiwaongoza wabunge wa kamati ya uchumi viwanda na biashara  kutembelea kiwanda hicho kilichopo Dar es salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'KONYAGI' Bw. David Mgwassa kushoto akifafanua jambo mbele ya
wabunge wa kamati ya uchumi viwanda na biashara  walipotembelea kiwanda hicho kilichopo Dar es salaam
Ofisa wa Kampuni ya Konyagi Bw, Alex Sanamba kulia akiwaonesha kinywaji cha zanzi wabunge wa kamati ya uchumi viwanda na biashara  walipotembelea kiwanda hicho



Wabunge wa kamati ya uchumi viwanda na biashara wakiangalia mashine inayotengeneza konyagi ya kiroba

Mjumbe wa kamati ya Uchumi viwanda na biashara Bi. Naomi Kaihula kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'KONYAGI' Bw. David Mgwassa pamoja na Mkurugenzi msaidizi kutoka wizara ya viwanda na biashara Bw. Deo Ndunguru walipotembelea kiwanda cha Konyagi kujionea mambo mbalimbali