Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, July 29, 2011

MABONDIA WA ZANZIBAR NA BARA KUONESHANA KAZI DDC KEKO KESHO
Alphonce Mchumiatumbo akipima uzito Dar es Salaam jana kwa ajili ya mpambano wake KESHO na Amour Zungu utakaofanyika katika ukumbi wa DDC Keko leo kulia ni msimamizi wa mabondia hawo. Kanda Kabongo

TENDE HIZOOOO MSIMU WAKE UHO EHEEE

Wafanyabiashara ya tende wakipima kwa kilo kwa ajili ya kuweka kwenye mifuko kuuza kushoto ni Sadam Mubaraq na Said Makingo kama walivyokutwa makutano ya mtaa wa Mafia na Swahili DAr es Salaam jana zao la tende upendwa kununuliwa sana katika kipindi cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani itakayoanza mwanzoni mwa mwezi ujao

NANI KUIBUKA MSHINDI WA MISS ILALA LEO


REDDS MISS ILALA KUNYAKUA MILIONI 1.500.000 IJUMAA

Shindano la kumtafuta Mrembo wa Kanda ya Ilala linafikia kilele ijumaa wakati Walimbwende kumi na saba watakapo panda jukwaani kumenyana wakishindania Taji la Redds Miss Ilala ikiwa ni kwenye mchakato wa kuelekea kumpata Mrembo wa Tanzania.
Kila kitu kiko tayari kwa ajili ya Mashindano haya ambayo yatafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja. Warembo wamekamilika, maandalizi yote yako sawa sawa ikiwa ni kubadilisha kabisa maandhali ya viwanja vya Mnazi mmoja kutoka katika hali ya kuwa vya mikutano ya hadhara na kuwa katika hali ya viwanja vya starehe na burudani.
Michoro ya jinsi viwanja vitavyo onekana imetokana na Taman min Indonesia park iliyoko katika jiji la Jakarta na tunategemea kuwa kila atakayefika mahala pale atapata burdani tosha na kumfanya kuweka shindano la mrembo wa Ilala mwaka huu kuwa kumbukumbu kwake.
Bendi ya African Stars Twanga Pepeta itaanza kutumbuiza kuanzia saa moja kamili jioni na kutoa burdani kwa watu watakaokuwa wanaingia uwanjani hapo. Burdani pia itaporomoshwa na Mwanamuziki wa ngoma za asili Wanne Star na Warembo walioingia fainali katika Shindano la Vipaji.
Zawadi zitakazo tolewa kwa warembo ni kama ifuatavyo:
1. Redds Miss Ilala atapata Tshs 1,500,000/=
2. First Runner Up atapata Tshs 1,000,000/=
3. Second Runner Up atapata Tshs 850,000/=
Hawa watapata pia tiketi ya kuwakilisha Miss Ilala katika shindano la Vodacom Miss Tanzania.
4. Third Runner Up atapata Tshs, 500,000/=
5. Fourth Runner Up atapata Tshs. 500,000/=
6. Kifuta Jasho kila mmoja atapata Tshs 200,000/=

LUDACRIS: NINAZO NYIMBO ZA KUTOSHA KUKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WANGU KATIKA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA JUMAMOSIMwanamuziki Ludacris kutoka nchini Marekani akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika asubuhi hii kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dare es salaam, Ludacris alikuwa akizungumzia onyesho lake atakalolifanya kesho, katika tamasha la Mwendelezo wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwabja vya Leaders Club jijini Dar es salaam, katika picha kulia ni Mkurugenzi wa radio Clouds Ruge Mutahaba. Ludacris amesema anazo albam saba hivyo katika albam hizo anatarajia kutoa burudani ya kutosha ili kukonga mioyo ya mashabiki wa wa muziki wake nchini Tanzania
Mwanamuziki Ludacris wa pili kutoka kulia akiwa katika mkutano huo kulia ni Ruge Mutahaba mkurugenzi Clouds kushoto ni Caroline Ndungu, aliyekuwa mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweriers na Meneja wa bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo.
Meneja wa bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo akizungamza katika mkutano wa waandishi wa habari wakati alipozunguzia tamasha la Serengeti Fiesta, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders Club, katikati ni Mwanamuziki Ludacris na mwisho ni Mkurugenzi wa Clouds Ruge Mutahaba.
http://fullshangwe.blogspot.com/

Wednesday, July 27, 2011

JOACHIMU CHISANO ATEMBELEA WAKULIMA WA ZAO LA MLONGE BAGAMOYO

Joachim Chissano akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Bi,Eileen Kasubi
Bi,Eileen Kasubi katikati akiwa katika shamba la zao la mlonge na mgeni wake Joachim ChissanoJoachim Chissano kushoto akitembezwa katika shamba la zao la mlonge na mwenyeji wake Eileen Kasubi

Rais Mstaafu wa Msumbiji, Bw. Joachim Chisano kushot
o akitoa neno la shuklani baada ya kutembelea katika shamba la zao la mlongejoachim Chissaibishwano akikar

Thursday, July 21, 2011

TOTO ZE BINGWA NA SHARAMA WAZUNGUMZIA UZINDUZI WA ALBAMU ZAO UTAKAOFANYIKA JULY 23
Totoo ze Bingwa akiongea na waandishi wa habari asubuhi ya leo katika ukumbi wa habari maelezo, kushoto ni msanii Sharama kutoka nchini Kenya
Rapa wa bendi ya akudo impact Totoo Ze Bingwa (katikati) akiongea na waandishi wa habari katika ukubi wa habari maelezo leo asubuhi alipokuwa akizungumzia uzinduzi wa albam yake ya Hii Mambo haieleweki utakaofanyika siku ya jumamosi tarehe 23/07/2011. Kushoto ni msanii kutoka Kenya naefahamika kwa jina la Sharama ambae nae pia siku hiyo atazindua albamu yake ya VUNJA WINGA na kulia ni msanii Lai K kutoka kundi la Ukoo Flani maumau ambao watasindikiza uzinduzi huo.

VIDEO YA MIAKA 50 YAZINDULIWA RASMI
Mwenyekiti wa chama cha Wanamuziki,Tanzania Flava Unit akizungumza mapema leo kuhusiana na uzinduzi wa video ya miaka 50 ya uhuru wa sanaa ya Muziki,video hiyo imefanywa na kampuni ya Visual Lab,ina jumla ya dakika zisizozidi nne ili watazamaji wasichoke, na ina wasanii zaidi ya 50 huku walioingiza sauti wakiwa 36. Watayarishaji wa Audio ni Marco Challi na Lamar, wakati video imefanywa na Adam Juma wa Visual Lab.


Msemaji Mkuu wa Tanzania Flava Unit,Mkubwa Fella akiwatambulisha viongozi waandamini wa chama hicho,mapema leo kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.kushoto kabisa ni Mjumbe wa chama hicho Keisha.


Msemaji mkuuu wa chama cha Tanzania Flava Unit,Mkubwa Said Fella akiendelea kuwatambulisha viongozi wa chama hicho,wa kwanza kulia ni Mjumbe Banana Zorro,Prodyuza wa Chama hicho Lamar Niekamp kutoka Fish Crub,Katibu Kalla Pina na anaefuata kushoto ni Khalid Mohamed ambaye ni Mwenyekiti Msaidizi wa Tanzania Flava Unit.


Baadhi ya Waandishi wa habari pamoja na wadau wengeine wakiangalia 'DEMO' ya video hiyo iliyozinduliwa leo kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.Ndugu zangu habari za mchana,Nachukua fursa hii kuwakaribisha katika uzinduzi wa video ya wasanii inayohusiana na sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania, hii ni sehemu yetu na sisi ya kusherehekea kama vijana tukionesha kuguswa kwetu na hili, na wakati huo huo tukijaribu kuonesha mchango wetu kama vijana kwa serikali yetu ambayo kwa njia moja ama nyingine inahitaji shukrani, kwani ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo.Tuna uhuru, tuna amani na mambo yanaenda ingawa matatizo ya hapa na pale yapo, lakini tumeangalia upande mzuri zaidi na tumeona kabisa huu ndio muda muafaka wa kukumbushana pale tuilipojikwaa, ili tupate kwernda kwa mwendo mzuri.Katika miaka hii 50 ya Uhuru sanaa ya muziki ni moja kati ya sekta ambazo zimeleta ajira kwa vijana. Unaweza kuona jinsi wasanii mbali mbali walivyojikwamua kupitia muziki, mifano hai imo hata humu ndani, watu wanaendesha magari, watu wanaishi kwenye nyumba nzuri na wana miradi yao kupitia muziki huu wa kizazi kipya.Si vibaya basi kwa kile kidogo unachokipata kukitolea shukrani, kuonesha kwamba unakithamini, sisi twajivunia miaka 50 ya uhuru na tunahisi kwamba tuna kila haja ya kusherehekea.Sisi kama Tanzania Flava Unit, vijana ambao tuko katika sekta ya muziki tuliojikusanya kwa lengo la kuufikisha muziki wetu katika eneo jingine kimaudhui tumepania kufanya matamasha mengi tu nchi nzima, katika kusherehekea hili na yote haya yatakuwa ya wazi, na tutakuwa tukitoa burudani kwa watanzania, tukisherehekea nao pamoja miaka hii 50.Kwa fikra zetu hii ni muhimu, kuna wakati mtanzania anahitaji burudani na hawezi kuingia sehemu kulipa wala hawezi kufika mahali mbali kabisa akaniona ama mimi, au Chegge ama temba, kwa nini tusimfikie na kumpa burudani?

Hilo lilikuwa wazo la kwanza.Lakini jingine ni kwamba kuna wakati mtanzania anahitaji kuburudika, kashafikiria sana mfumuko wa bei, kafikiria sana suala la umeme ambalo linatusumbua wengi na kafikiria sana ugumu wa maisha, na mwisho wa siku akitoka nje katika uwanja wa karibu anapata burudani angalau anachangamsha ubongo wake na kuanza kujua kesho atakabiliana vipi na ugumu huu wa maisha ambao kila kukicha tunajitahidi kuhakikisha kwamba tufike sehemu, ila mtu apate unafuu.

Tuko katika hatua za mwisho kabisa kupata udhamini wa kufanya matamasha haya, na tukiwa tayari tutawafahamisha.Video hii imefanywa na kampuni ya Visual Lab, ina jumla ya Dakika zisizozidi nne ili msichoke, na ina wasanii zaidi ya 50 huku walioingiza sauti wakiwa 36.Watayarishaji wa Audio ni Marco Challi na Lamar, wakati video imefanywa na Adam Juma wa Visual Lab.

Hili ndio kubwa kwa leo kaka na dada zangu iwapo kuna la ziada tutaambiana!Hamis Mwinjuma.

Mkurugenzi

Tanzania Flava Unit

GRAND MALT YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO VYA SH. M. 10 KWA TIMU YA BARAZA LA WAWAKILISHI
Waziri wa Habari, Utalii,Utamaduni na Michezo, Abdilah Jihad (kushoto) akipokea jezi kutoka kwa Meneja wa kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt, Consolata Adam, kwa ajili ya timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar itakayopambana na timu ya Klabu ya Wazee ya Arusha Septemba 8, mwaka huu. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa timu ya Baraza, Mbarouk Mussa. Kampuni hiyo ya Grand Malt imetoa vifaa hivyo vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 10. Picha na Martine Kabemba


Waziri wa Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Abdilah Jihad akionyesha viatu walivyokabidhiwa.


Waziri wa Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Abdilah Jihad (wa pili kushoto), Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Mbarouk Mussa (kushoto), pamoja na Meneja wa kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt, Consolata Adam (kulia) wakigonganisha vinywaji vyao vya kopo za kinywaji hicho wakati wa hafla ya timu hiyo kukabidhiwa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 10, mjini Zanzibar.Waziri wa Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo, Abdilah Jihad akizungumza ikiwa ni sehemu ya kushukuru kinywaji cha Grand Malt kwa kuruhusiwa kudhamini michezo na shughuli mbalimbali katika Visiwa vya Zanzibar.

HAPO ZAMANI (HII ILIKUWA NI MWAKA 2000).

Hapa ilikuwa mbelembele kuanzia kushoto ni Mtoto wa Dandu, Alex Kajumulo na Rashid Matula mwaka 2000

TOTO ZE BINGWA KUZINDUA ALBAM YA MAMBO HAIELEWEKI JULY 23
Art in Tanzania Mzuka Records Album Launch - New albums of Totoo ze Bingwa and Sharamaa (Kenya), also 20%, Benjamin Mambo Jambo, Sanaa Sanaa Band, Zola D, Richie Rich, Akudo Impact Band and others. This is an event not to miss. Diamond Jubilee 23rd July 2011. Tickets available at numerous sales points in town

Airtel Yagawa Madawati kwa shule MwanzaKutoka kulia ni Meneja wa huduma kwa jamii Airtel Tunu Kavishe akiwa na Meneja wa Kanda ya Ziwa Airtel Ally Maswanya wakikabidhi madawati kwa mkuu wa shule Kangaye Bi Josephine Mlundwa na mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Fweka Ndawala wapili kushoto. Waliohudhuria hafla fupi ya makabidhiano shuleni hapo ni mgeni Rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Francis Mkabengwa (watatu toka kushoto) na anaefuata ni Mstahiki meya wa kata ya Kangale Joseph .K.Manyelele.

Airtel Tanzania kampuni ya simu za mkononi yenye kutoa huduma bora nchini kote, leo imegawa madawaka katika shule ya sekondari Kangaye ikiwa ni sehumu ya shughuli zao za kusaidia jamii.

Katika kauli iliyotoleawa na kampuni ya Airtel Tanzania kupitia Meneja Biashara Kanda Ziwa Ally Maswanya alisema”Airtel imedhamiria kusaidia shule kwa kutoa vifaa vya mbalimbali ikiwepo vya kufundishia ili kuahakikisha elimu bora inatolewa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla. Tunatambua elimu ndiyo ufunguo wa mafanikio hivyo basi tunashirikiana na wizara ya elimu katika kuinua kiwango cha elimu sio Mwanza tu bali Tanzania kwa ujumla. Airtel itaendelea kusaidia mashule kwa kutoa vitabu na madawati ikiwa ni sehemu ya shughuli zetu za kusaidia jamii, nia yetu ni kuwafikia shule nyingi zaidi katika mikoa yote ya Tanzania alioongeza.

Akiongea wakati wa shughuli ya kugawa vitabu iliyofanyika Kanyaye Secondary katika wilaya ya ilemela, meneja wa shughuli za kijamii, Tunu Towo Kavishe alisema, tunaelewa uhaba wa madawati na vifaa vya kufundishia na tunaongeza nguvu zetu kusaidia sekta ya elimu, Airtel Tanzania inatoa fulsa sawa kwa shule zote katika mikoa yote nchini na kuhakikisha misaada tunayotoa inawafikia wanafunzi nchini kote. Leo Airtel inatoa msaada wa madawati 50 kwa shule ya sekondari Kanyaye.

“Tunayo malengo ya dhati kabisa katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini na kuhakikisha kinaongezeka, hasa kupitia upatikanaji wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za sekondari. Tangu tulipoanza mpango wetu wa kusaidia vitabu kwa shule mbali mbali za sekondari hapa nchini, takribani miaka saba iliyopita, tumeshazifikia zaidi ya shule za sekondari tofauti zipatazo 800 nchini na leo tunathibitisha dhamira yetu ya kusaidia mashule kwa kutoa madawati kanyaze secondari”, alisema Kavishe

Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia sekta ya elimu hapa nchini.

Nibu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Danny Mwakitereko Apata Ajali Jijini Dar
Naibu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New habari (2006) Danny Mwakitereko(Pichani) amepata ajali ya gari siku wa kuamkia leo, jijini Dar es Salaam.Amefanyiwa upasuaji wa kichwa katika Taasisi ya mifupa Muhimbili. Hivi sasa yuko ICU Muhimbili kama anavyoonekana kwenye picha hapo juu leo hii.Tumwombee ndugu yetu Mungu amponye haraka ili tuungane naye katika kusukuma gurudumu la maendeleo kwa manufaa ya taifa. By Arodia Journalist, Mtanzania

WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNENI DODOMA L EO


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Bunda na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais , Siasa na Uhusiano wa Jamii, Stephen Wasira (kushoto), Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Idris Kikula (wapili kushoto), Mbunge wa Viti Maalum, Martha Mlata na Waziri wa Ujenziri wa Ujenzi, John Magufuli, kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 20,2011.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Magdalena Sakaya kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 20,2011.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
http://fullshangwe.blogspot.com/

MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo (jana) mara baada ya kuzindua mahabara ya kutembea.


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa(katikati) na(kushoto) mbunge wa Jimbo la Kinondoni (CCM) na (kulia) ni mbunge wa jimbo la Kawe ,Halima Mdee (CHADEMA) wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Zanaki sekondari ambao walikuwa Bungeni leo(jana) kushuhudia bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.


PICHA ZOTE NA KINABO - MAELEZO

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akitoa changamoto kwa wanafunzi wa sekondari ya Zanaki na Shule ya Sekondari Dodoma kuwa wasome kwa bidii na kuepuka migomo . Wanafunzi hao walikuwa Bungeni leo(jana) ili kushuhudia bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kuangalia shughuli za Bunge.

Mafunzo ya walimu wa awali yaliyotolewa na kampuni ya uchapishaji wa vitabu nchini ya Long man

Baadhi ya Walimu kutoka jijini Dar es Salaam waliohudhulia mafunzo ya siku tatu ya Uwezeshaji wa Walimu wa awali wa shule za Msingi yanayoendelea katika Taasisi ya Elimu Tanzania wakijifunza kwa vitendo Mafunzo hayo yamedhaminiwa na kampuni ya uchapishaji wa vitabu nchi ya Pearson Long Man


Baadhi ya Walimu kutoka jijini Dar es Salaam waliohudhulia mafunzo ya siku tatu ya Uwezeshaji wa Walimu wa awali wa shule za Msingi yanayoendelea katika Taasisi ya Elimu Tanzania wakijifunza kwa vitendo Mafunzo hayo yamedhaminiwa na kampuni ya uchapishaji wa vitabu nchi ya Pearson Long Man

.Mmoja wa Walimu kati ya 90 waliohudhuria mafunzo ya siku tatu ya Uwezeshaji wa walimu wa shule za msingi jijini Dar es Salaam,Getruda John kushoto akimwonyesha Mratibu wa Elimu ya Awali Clarence Mwinuka wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa pili kulia ni fisa mwandamizi wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Long Man,Belinda Mafuru mafundho hayo yamedhaminiwa na Kampuni ya Uchapishaji wa vitabu nchini ya Pearson Long Man.

Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Upendp iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam wapili (kulia) akijibu swali wakati wa mafunzo ya uwezeshaji wa Walimu ,kutoka kwa Muwezeshaji wa Kampuni ya Pearson Long Man Tanzania inayojihusisha na uchapaji wa Vitabu vya shule za awali na vyuo nchini, Maria Ellokelo, ali yeshika karatasi kushoto ni Ofisa Mauzo wa Long Man Salama Hamza na Mwalimu wa Shule ya Mkamba ya Temeke Jayneth Gideon


VODACOM KUWAPA RAHA WABUNGE IJUMAA HII


Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Ijuma hii itajumuika pamoja na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla ya chakula cha usiku pamoja na burudani ya muziki katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma. Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba chakula hicho ni sehemu ya utamaduni wa kampuni hiyo wa kuimarisha mahusiano na wadau wake mbalimbali ikiwemo Bunge na Serikali pamoja na kutambua juhudi za wadau hao katika maendeleo ya taifa na watu wake. "Tumekuwa na utamaduni wa kuandaa hafla za aina hii wakati wa Bunge ila ya mwaka huu mambo yatakuwa mazuri na ya aina yake ikilinganishwa na tulizowahi kufanya miaka ya nyuma na kwa mantiki hiyo kauli mbiu ya mwaka huu ni "More Than Ever Before" na tunamaanisha"Alisema Mwamvita. "Vodacom Tanzania inakwenda Bungeni mjini Dodoma ikiwa na sura mpya kufuatia mabadiliko makubwa katika muonekanao wake wa rangi na kauli mbiu ambayo sasa ni "kazi ni kwako" na hivyo tunataka kuwadhihirishia waheshimiwa wabunge upya wetu katika kila jambo tunalolifanya si tu katika utoaji wa huduma za mawasiliano ya mkononi nchini"Aliongeza Mwamvita Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda anatarajiwa kuongoza hafla hiyo itakayohudhuriwa pia na Spika wa Bunge Mama Anne Makinda, Kiongozi wa Kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe pamoja na wabunge wakiwemo mawaziri na naibu mawaziri watakaojumuika na viongozi wa Vodacom Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Dietlof Mare. Mwamvita alisema anatambua kuwa wabunge kwa sasa wapo katika kazi nzito ya kujadili bajeti ya Serikali kazi ambayo Vodacom inaitambua na kuiheshimu na hivyo pamoja na mambo mengine bado suala la kuwaandalia hafla za aina hiyo nalo lina sehemu yake ili kuwapatia fursa ya kukutana nje ya mazingira ya kazi. "Kwa niaba ya Uongozi wa Vodacom na wafanyakazi wake napenda kutumia fursa hii kwa heshima na taadhima kuwakaribisha waheshimiwa wabunge wote kujumuika pamoka katika usiku wa Vodacom na Bunge utakaoburudishwa na Mwanamuziki Banana Zorro, Diamond pamoja na Bi. Shakira ikiwa ni kuendeleza mahusiano mema yaliyopo yenye azma ya kujenga taifa lenye maendeleo makubwa katika nyanja ya mawasiliano ya simu za mkononi."Amesema

KAMBI YA ILALA YAKABIZIWA MAJI KWA AJILI YA MPAMBANO WA JUMAPILI JULAI 17
Rajabu Mhamila Super D Boxing Coach akiwa pamoja na Amir Mohamedi ' Msauzi' baada ya kukabidhi maji katoni 15 alizokabidhi kwa niaba ya Muddy Kalla Mtoto wa Ilala

Super D Boxing Coach akipokea maji toka kwa Amir Mohamedi ' Msauzi' baada ya kukabidhi maji katoni 15 alizokabidhi kwa niaba ya Muddy Kalla Mtoto wa IlalaBaadhi ya vijana wanaonolewa na kambi ya Ilala wakiwa mazoezini

AISHA MADINDA ATAMBULISHWA KUTUA JUKWAA LA EXTRA BONGO


Na Michael Machellah, jijini Dar

MNENGUAJI mahiri wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Aisha Madinda leo ametangazwa kujiunga rasmi na bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Ally Choki.Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa mnenguaji huyo Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki, alisema kuwa anajisikia faraja zaidi kumnasa mnenguaji huyo ikiwa ni sehemu ya kuzidi kuimarisha safu ya unenguaji kwa kuwa na watu wa sekta hiyo walio mahiri na uzoefu.Aidha Choki, alisema kuwa baada ya kuwanasa wanenguaji mahiri wa kiume wenye uzoefu wa siku nyimgi, Super Nyamwela na wenzake, alikuwa bado anandoto za kuwa na wanenguaji wa kike wenye uzoefu kama Aisha ambaye tayari amekwisha mnasa, huku akiamini kuzidi kuimarihs kikosi chake na kujiongezea mashabiki.Naye Aisha Madinda, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa rasmi, alisema kuwa ameamua kutua jukwaa la Extra Bongo ili kuweza kuungana na wacheza shoo wenzake wenye uzoefu ambao anaamini nao wametua jukwaa hilo kulingana na uzoefu wa wanamuziki wanaounda bendi hiyo.“Unajua siku zote ukifanya kazi na wanamuziki wazoefu na moyo wa kufanya kazi hata wewe pia unakuwa na moyo wa kufanya kazi na kukuza kipaji zaidi na kuongeza ozoefu na hata kupiga hatua na hasa katika anga hii ya muziki wa dansi.” Alisema AishaAisha tayari ameshaanza mazoezi na atatambulishwa rasmi kwa mashabiki jumatno katika onyesho lake la kwanza litakalofanyika kwenye ukumbi wa Klabu Masai Ilala jijini Dar es Salaam.


Kiongozi wa wacheza Shoo, Super Nyamwela alimkaribisha Aisha kwa mikono miwili na kusema sasa kazi imekamilika na kuwataka mashabiki na wapenzi wa bendi hiyo kujitokeza ili kushuhudia mambo mapya ya mnenguaji huyo aliyotuanayo katika bendi hiyo

Ashraf Na Chiku Wameremeta Ugiriki!Ashraf Hassan na Chiku Hamidu. Ndoa ilifungwa Julai 15 mwaka huu nchini Ugiriki.