Filamu ya Senior Bachelor imepangwa kufunga pazia la wiki ya maonyesho ya wazi ya filamu yanayoendelea katika viwanja ya Tangamano Mjini Tanga. Filamu hiyo ambayo itaonyeshwa jumaamosi hii katika Tamasha la Grand Malt la wazi la filamu linaloendelea viwanjani hapo imeongozwa na Single Mtambalike(RICHIE) na production manager ni Suleiman Said Barafu. Akiongea nasi Musa Kissoki Mkurugenzi wa Sofia Production waandaaji wa Tamasha hilo amesema anaamini filamu itasisimua wengi kwenye maonyesho hayo hasa kutokana na uigizaji wake. "JB ni moja ya waigizaji wenye mbwembwe sana, hivyo hii imetoka kuwa moja ya kazi zake nzuri ambazo tutazionyesha katika tamasha hili la GrandMalt la wazi la filamu Tanzanial. MUIGIZAJI wa filamu hiyo Jacob Stiven maarufu kama JB amejizolea umaarufu kutokana na filamu hiyo hadi kupelekea kupachikwa jina la Erick Ford alilotumia katika muvi hiyo; Senior Bachelor ni moja ya filamu pendwa kuonyeshwa katika Tamasha hili JB anatarajiwa kuwepo mjini Tanga kufungua filamu hiyo katika hadhara kwa ajili ya maonyesho yake.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment