Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, July 21, 2011

Airtel Yagawa Madawati kwa shule Mwanza







Kutoka kulia ni Meneja wa huduma kwa jamii Airtel Tunu Kavishe akiwa na Meneja wa Kanda ya Ziwa Airtel Ally Maswanya wakikabidhi madawati kwa mkuu wa shule Kangaye Bi Josephine Mlundwa na mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Fweka Ndawala wapili kushoto. Waliohudhuria hafla fupi ya makabidhiano shuleni hapo ni mgeni Rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Francis Mkabengwa (watatu toka kushoto) na anaefuata ni Mstahiki meya wa kata ya Kangale Joseph .K.Manyelele.

Airtel Tanzania kampuni ya simu za mkononi yenye kutoa huduma bora nchini kote, leo imegawa madawaka katika shule ya sekondari Kangaye ikiwa ni sehumu ya shughuli zao za kusaidia jamii.

Katika kauli iliyotoleawa na kampuni ya Airtel Tanzania kupitia Meneja Biashara Kanda Ziwa Ally Maswanya alisema”Airtel imedhamiria kusaidia shule kwa kutoa vifaa vya mbalimbali ikiwepo vya kufundishia ili kuahakikisha elimu bora inatolewa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla. Tunatambua elimu ndiyo ufunguo wa mafanikio hivyo basi tunashirikiana na wizara ya elimu katika kuinua kiwango cha elimu sio Mwanza tu bali Tanzania kwa ujumla. Airtel itaendelea kusaidia mashule kwa kutoa vitabu na madawati ikiwa ni sehemu ya shughuli zetu za kusaidia jamii, nia yetu ni kuwafikia shule nyingi zaidi katika mikoa yote ya Tanzania alioongeza.





Akiongea wakati wa shughuli ya kugawa vitabu iliyofanyika Kanyaye Secondary katika wilaya ya ilemela, meneja wa shughuli za kijamii, Tunu Towo Kavishe alisema, tunaelewa uhaba wa madawati na vifaa vya kufundishia na tunaongeza nguvu zetu kusaidia sekta ya elimu, Airtel Tanzania inatoa fulsa sawa kwa shule zote katika mikoa yote nchini na kuhakikisha misaada tunayotoa inawafikia wanafunzi nchini kote. Leo Airtel inatoa msaada wa madawati 50 kwa shule ya sekondari Kanyaye.





“Tunayo malengo ya dhati kabisa katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini na kuhakikisha kinaongezeka, hasa kupitia upatikanaji wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za sekondari. Tangu tulipoanza mpango wetu wa kusaidia vitabu kwa shule mbali mbali za sekondari hapa nchini, takribani miaka saba iliyopita, tumeshazifikia zaidi ya shule za sekondari tofauti zipatazo 800 nchini na leo tunathibitisha dhamira yetu ya kusaidia mashule kwa kutoa madawati kanyaze secondari”, alisema Kavishe





Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia sekta ya elimu hapa nchini.

No comments :

Post a Comment