Kamisheni
ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) inatambua mkataba (mikataba) kati ya
Francis Cheka na Kaike Siraju aliyosaini kupigana na Japhet Kaseba siku
ya July 7, mwaka huu.
Aidha Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) inamshauri bondia
Francsi Cheka awe na mawasiliano mazuri na promota wa pambano hilo ili
hali ya kutoelewana iliyokwisha kujitokeza imalizwe kwa manufaa ya
tasnia ya ngumi nchini.
TPBC inawashauri wadau wote wanaotaka kufikia makubaliano na mabondia
kutofanya hivyo nje ya utaratibu wa mchezo wa ngumi ambao ni kusaini
mikataba mbele ya Kamisheni na wakili ili maslahi ya wote yalindwe.
Tunapenda pia kuwashauri mabondia wote kuacha tabia ya kusaini mikataba
zaidi ya mmoja hususan wakati bado wakiwa na pambano mkononi.
No comments :
Post a Comment