Mcheza sinema
maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ambaye alitua mjini Moshi jana kushiriki
kwenye mbio za kimataifa za Mt. Kilimanjaro Marathon leo alikaa na watoto wa
kituo cha yatima cha Upendo kinachoendeshwa na masista wa shirika la Precious
Blood mjini Moshi. Lorenz aliingia kwa kishindo katika Manispaa ya Moshi na
kueleza juu ya nia yake ya kuitangaza Tanzania nchini Marekni kwa kutumia
usanii wake wa filamu.
Deidre Lorenz
anashiriki katika mashindano ya Mt. Kilimanjaro Marathon ambayo yanaanza
kutimua vumbi tarehe 24 Jumapili kuanzia Moshi klabu hadi Rau madukani na
kurudi. Mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na Marie Frances kutoka
katika mji wa Bethesda nchini Marekni mwaka 1991 baada ya kuombwa na balozi wa
zamani wa Tanzania nchini Misri kuja Tanzania kuanzisha mbio za marathon.
Deidre Lorenz
anawakilisha kikundi cha Actors Guild ambacho kina lengo la kukusanya pesa kwa
ajili ya kutibu ugonjwa wa saratani. Katika ziara yake kwenye kituo cha watoto
yatima cha Upendo Deidre aliwasomea watoto hao hadithi mbalimbali za watoto.
Aidha, aliwapa zawadi za fangi za kuchora, vitabu, daftari, kalamu, chocolate
na zawadi nyingine kemkem zinazowaelimisha watoto.
Lorenz ameshiriki
pia katika mahojiano na waandishi mbalimbali wa habari mjini Moshi na kueleza
kuhusu nia yake ya kuitembelea Tanzania mara kwa mara. Amesema kuwa wazazi wake
hususan bibi yake alimwambia kuwa Tanzania ni nchi yenye wanawake wenye sura
nzuri sana. Aidha marafiki zake wamemwambia kuwa aje yeye kwanza ili wao waje
katika mbio zinazofuata.
You might also like:
No comments :
Post a Comment