Kopo jipya la Castle Lite linavyoonekana sasa

Wateja
wetu walihitaji kuipata bia yao popote pale walipo au kuwa nayo popote
waendapo, hivyo kupatikana kwa bia hii katika chupa peke yake
kulipunguza uhuru wa kuwa na bia yao popote waendapo kwani walihitaji
kurudisha chupa kila waitumiapo.
Uzinduzi
wa Castle lite ya kopo utasaidia zaidi kuongeza upatikanaji wa
kinywaji hiki katika maduka ya reja reja (super markets) n.k kote
nchini na kuwapa nafasi wapenzi wa castle lite kununua bia yao
waipendayo na kwenda nayo nyumbani. Bei ya reja reja kwa kopo ni
shilingi 1700/- na bei ya reja reja kwa chupa itaendelea kubaki ile ile
1700/-.
Kwa
upande wake Meneja mawasiliano na mahusiano ya jamii wa Tbl Edith
Mushi aliwashukuru wapenzi na watumiaji wa bia ya Castle Lite kwa
kuweza kuipa mafanikio makubwa katika soko la bia hapa nchini,
“ninawahakikishia kuwa mnafanya uamuzi ulio sahihi kwa kuchagua kutumia
Castle Lite” nasi tutaendelea kuwapatia bia iliyo bora siku zote.
Alisema Edith.
You might also like:
No comments :
Post a Comment