Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, July 18, 2010

Thierry Henry astaafu soka ya kimataifa

Mchezaji mashuhuri wa timu ya Taifa ya Ufaransa na Barcelona Thierry Henry ametangaza kustaafu soka ya kimataifa na timu ya Taifa.

Henry mwenye umri wa miaka 32 ametangaza uamuzi huo wakati wa mahojiano na shirika la habari AP kabla ya kufikia uamuzi wa kujiunga na klabu ya mpira wa miguu ya New York Red Bulls.

Amesema kuwa anajiunga na klabu ya Red Bulls nchini Marekani, siyo kwa kutaka kumuiga David Beckham kwa kusafiri mara kwa mara baina ya Ulaya na Marekani.

Amesema huu ndiyo mwisho kwake kushiriki timu ya Taifa.

Thierry Henry

Thierry Henry

Tangu ajiunge na timu ya Taifa, Henry amefunga magoli 51 mara 123 alizoshiriki michuano ya kimataifa kwa niaba ya Ufaransa kuanzia mwaka 1997.

Alitia fora wakati akichezea klabu ya Arsenal ambako alikuwa nahodha na anatazamiwa kushiriki pambano la Red Bulls dhidi ya mahasimu wakuu wa klabu yake ya zamani, Tottenham hotspurs hapo tarehe 22 Julai.

Alipohama kutoka Arsenal mnamo mwaka 2007, Henry alijiunga na Barcelona ya Uhispania na alikuwa na mwaka mmoja uliosalia kwenye mkataba wake aliporuhusiwa na Barcelona kuweza kuihama.

Kocha mpya kijana kumsaidia Capello

Capello amesema ataelekeza nguvu zaidi kuendeleza wachezaji vijana.

Meneja wa timu ya England, Fabio Capello, amekubali kuteua kocha kijana ambaye ni mzawa wa England ajumuike na Stuart Pearce kwenye kikosi chake cha ufundi, BBC Sport imefahamishwa.

Mkurugenzi wa maendeleo wa chama cha soka cha England, Sir Trevor Brooking, amesema atasaidia kuteua kocha huyo na kuwasilisha mapendekezo yake ifikapo mwezi Disemba.

Pearce, ambaye pia ndiye kocha wa timu ya England ya wachezaji wa chini ya umri wa miaka 21, tayari yumo katika kikosi cha makocha cha Capello.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya bodi ya FA kukutana kujadili ufanisi mbovu wa timu ya England kwenye mashindano ya Kombe la Dunia.

Nafasi kwa vijana

Mwandishi wa maswala ya michezo wa BBC, Dan Roan alisema: "FA inataka Brooking na Capello kutafuta kocha mwingine kijana kusaidia katika kikosi cha ufundi cha timu ya taifa ya England, bega kwa bega na Stuart Pearce.

Wawili hao watawasilisha mapendekezo yao kuhusiana na mpango wa kuendeleza wachezaji wa kimataifa na mafunzo ya makocha, huku chama cha soka, FA, kikiwa na shauriku ya kujifunza kutokana na England iliyokuwa ikimwagiwa sifa, kushinda mechi moja tu.

Capello, ambaye aliendelea na kazi yake baada ya mashindano, alisema ataelekeza zaidi nguvu zake kuendeleza wachezaji vijana. Hatua za kwanza zitaanza kuonekana wakati England itakapocheza na Hungaru katika mechi ya kirafiki kwenye uwanja wa Wembley, tarehe 11 Agosti.

ZAIN YAKABIDHI KOMPYUTA ST. JOSEPH

Mkuu wa shule ya Sekondari ya St. Joseph ya jijini DSM, SR. Edwardina Frederick (kati), akipokea msaada wa kompyuta kutoka kampuni ya simu ya Zain. Wanaokabidhi msaada huo ni mameneja wa Teknohama wa Zain, Asupya Nalingigwa (Kushoto) na Godfrey Masanja (kulia). Jumla ya kompyuta 4 zenye thamani ya Shilingi Milioni sita zimetolewa mwishoni mwa wiki kwa shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya St. Joseph iliyopo Salasala jijini DSM wakifurahia moja ya kompyuta kati ya nne zilizokabidhiwa na kampuni ya simu ya Zain kwa shule hiyo. Kulia ni meneja wa Teknohama wa Zain Asupya Nalingigwa. Jumla ya kompyuta 4 zenye thamani ya Shilingi Milioni sita zimetolewa mwishoni mwa wiki kwa shule hiyo.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya St. Joseph ya jijini DSM, SR. Edwardina Frederick (kushoto), akiwashukuru mameneja wa kampuni simu ya Zain kwa msaada wa kompyuta walioutoa kwa shule hiyo. Kutoka kulia, wanaosikiliza ni Tunu Kavishe (Meneja Huduma za Jamii), Godfrey Masanja na Asupya Nalingigwa (Mameneja wa Teknohama). Jumla ya kompyuta 4 zenye thamani ya Shilingi Milioni sita zimetolewa mwishoni mwa wiki kwa shule hiyo.

Friday, July 9, 2010

Kila mmoja adai Spian ndio mabingwa wapya wa dunia ?

Spain-mabingwa wapya wa dunia ?

Na je, Paul na Pauline wasemaje ?

Wakati Ujerumani ina miadi na Uruguay leo usiku kuania mshindi watatu, wapiga-ramli wote na mashabiki wa dimba wadai Spain na sio Holland ndiyo itakayotawazwa bingwa mpya wa dunia hapo kesho huko City Stadium,Johannesberg.

Pweza wa Ujerumani- Paul- ametabiri Spain ndio mabingwa wakati mkewe- Pauline , ameelemea timu ya nyumbani Holland. Nani kati yao atashinda finali hii kati ya Spain na Holland na Paul na Pauline ?

Kuanzia watoto wa shule huko Soweto, Afrika Kusini, hadi vituo vya kamari ulimwenguni na hata pweza-dume, Paul wa Oberhausen , Ujerumani, upatu unapigwa na kuhanikiza Kombe la dunia kesho Jumapili linakwenda Spain, Na hiyo itakuwa mara ya kwanza .

"Wanacheza dimba maridadi ajabu.Tunataka kuwa kama wao. Bila shaka, watashinda Jumapili hii- fanyeni hivyo Spain."-alisema shabiki chipukizi wa miaka 13, Dumisani Motye, aliekuwa akimuigiza David Villa wa Spain katika uwanja wa vumbi mtaani Soweto.

Kabla ya changamoto hiyo, Ujerumani na Uruguay zitateremka uwanjani huko Port Elizabeth leo usiku kuamua finali ndogo ya Kombe la dunia mwaka 2010: Nani ni mshindi wa tatu ? Baada ya kumaliza wapili mwaka 2002 na watatu nyumbani mwaka 2006, Ujerumani leo haitaki chochote kasoro ya taji hilo la mshindi watatu kufuta machozi ya pigo la pweza Paul,alieangusha juzi kwa kutabiri ushindi wa Spain.

Lakini, Waspain, waliopigiwa debe tangu mwanzo kuwa ndio mabingwa wapya wa dunia, baada ya kuanza taratibu wamepata kasi wakati muwafaka-hatua za mwisho za kombe hili baada ya kuwaambia Wajerumani,kutangulia si kufika. Nani sasa atazuwia "kikosi cha manuwari za Spain" kutia gati bandarini City Stadium?

Manahodha wa Holland pia ni maarufu na wanadai ni jahazi la kocha Bert van Marwijk lililowafungisha virago mabingwa mara tano, Brazil, seuze Waspain.

Kama Spain, Holland, haikuwahi kutwaa kombe la dunia na mara hii, wanataka kufuta madhambi ya 1974 na 1978 walipofika finali na kupokonywa Kombe na Ujerumani na Argentina. Wanadai, halali ni mara tatu.

Vyovyote mpambano wa kesho utakavyomalizika, jina jipya litaandikwa katika Kombe la FIFA. Isitoshe, utakuwa ushindi wa kwanza wa timu ya Ulaya wa Kombe la dunia nje ya bara lao.

Na sura hii haikuonesha hivyo pale firimbi ilipolia Juni,11 kuanzisha kombe la kwanza la dunia barani Afrika. Kwani,timu za kanda ya Amerika kusini,zilitia fora ,lakini mwishoe, ilidhihirika vishindo vyao vilikuwa vya darini vilivyoishia sakafuni. Na hii, licha ya mabingwa wa dunia, Itali, makamo-bingwa ,Ufaransa na England, mabingwa 1966 kuanguka. Hata Spain, utakumbuka ilishindwa mpambano wake wa kwanza na Uswisi.

Holland, haikufungwa hata mechi moja katika Kombe hili la dunia na mpambano wa kesho utakuwa wa 14 mfululizo bila kushindwa.

Hizo ni salamu akina Arjen Robben, van Marwijk, van Bommel, van der vaart, van Persie na van Brockhorst wanazompelekea Del Bosco na La Roja,timu yake ya Spain.

Wakati salamu za pweza "Paul" kutoka Ujerumani kuwa ni Spain itakayoshinda kesho, amezipokea mkewe "Pauline" huko The Hague,Holland, mashabiki wa Afrika kusini,wanadai Wadachi-Holland, asili ya makaburu, wamerudi nyunmbani, na mcheza kwaohutunzwa-Pauline amkumbusha pweza Paul.

Wednesday, July 7, 2010

Uholanzi yalenga kutimiza ndoto

Ni mara ya tatu kufuzu fainali, lakini bado hawajapata kushinda Kombe la Dunia.

Uholanzi inapania kupiga hatua moja zaidi na kutwaa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza, licha ya kucheza fainali mara mbili.

Mabao mawili yaliyofungwa katika muda wa dakika tatu kipindi cha pili na Wesley Sneijder na Arjen Robben yaliisaidia Uholanzi kuishinda Uruguay na kuingia fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978.

Giovanni van Bronckhorst alikuwa ameifungia Uholanzi bao la mapema, lakini Diego Forlan akaisawazishia Uruguay kwa shuti la mbali muda mfupi kabla ya mapumziko.

Katika muda wa majeruhi Uholanzi walijikuta kwenye hatari ya ushindi kuwaponyoka wakati Maxi Pereira alipofunga bao la pili la Uruguay, lakini mchezo ukamalizikia hapo.

Kabla ya mwaka 1978 Uholanzi ilikuwa imecheza fainali ya mwaka 1974 mjini Munich ambapo ilishindwa na Ujerumani 2-1.

Mwaka 1978 Uholanzi walishindwa kwenye fainali na wenyeji Argentina mabao 3-1 mjini Buenos Aires.

Fainali ya Jumapili itakuwa ya tatu kwa Uholanzi, na mshambuliaji wa Liverpool, Dirk Kuyt anasema anaamini wakati umewadia kutwaa Kombe hilo baada ya 'kulinusa' mara mbili.

Ghana yataka FIFA ibadili sheria

Uruguay dhidi ya Ghana

Diego Forlan (kushoto) na Asamoah Gyan (kulia)

Waziri wa michezo wa Ghana amesema shirikisho la soka duniani FIFA linatakiwa kubadilisha sheria za mchezo wa soka kufuatia kuondolewa kwa Ghana kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya kutumika mikono.

Waziri huyo Akua Sena Dansua hajasema ni sheria zipi angetaka zibadilishwe, lakini watu wengi wamekuwa wakisema mwamuzi wa mchuano wa robo fainali kati ya Ghana na Uruguay angetakiwa kuipa Ghana goli, wakati mchezaji wa Uruguay Luis Suarez alipoondosha kwa mikono mpira uliokuwa unaingia kwenye lango la timu yake.

Kwenye mechi hiyo mshambuliaji wa Ghana Dominic Adiyah alipiga mpira kwa kichwa ukaeleka kuingia katika lango la Uruguay ukibakia muda mfupi sana kabla ya mechi kumalizika, lakini Suarez ambaye ni mchezaji wa ndani akauondosha kwa mikono.

Mwamuzi alimwonyesha kadi nyekundu Suarez na akawapa Ghana penati ambayo Asamoah Gyan alipiga nje.

Adhabu hiyo ni kulingana na sheria zilizopo za shirikisho la soka dunia FIFA.

Mechi ilimalizika kwa sare, ikalazimika kuingia mikwaju ya penalti na Uruguay wakaibuka washindi wa mabao 4-2.

Ghana ilikuwa timu ya Afrika kufikia hatua ya robo fainali katika Kombe la Dunia.

Baada ya kurejea nyumbani Black Stars walipokelewa kwa shangwe na nderemo mjini Accra.

Rais wa Ghana John Atta Mills alisema wachezaji hao watapewa tuzo za kitaifa na pia dola 20,000 kila mmoja.

Mashabiki wa soka kote barani Afrika waliishabikia Ghana wakati wa mchuano huo, na wengi walipigika sana baada ya Black Stars kuondolewa.

Ilikuwa ni timu pekee ya Afrika iliyobakia kwenye mashindano baada ya timu zingine tano za Afrika kuondolewa kwenye raundi ya kwanza ya michuano hiyo.

ZAINI YAKABIDHI MADAWATI SHULE YA MSINGI KASULU


Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Azan akiongea na Meneja wa Shughuli za Kijamii wa Zain Tanzania Tunu Kavishe (Kushoto) mara baada ya kukabidhi madawati yaliyotolewa hivi karibuni na kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania kwa shule ya msingi ya Kasulu iliyoko katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya Kasulu iliyoko katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Moshi Mikidadi (kushoto) akipokea msaada wa madawati mia moja yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni saba kutoka kwa Meneja wa Shughuli za Kijamii wa Zain Tanzania Tunu Kavishe (Kushoto) mara baada ya kukabidhi madawati yaliyotolewa hivi karibuni na kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania kwa shule ya msingi ya Kasulu iliyoko katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Azan (katikati) akimpongeza Meneja wa shughuli za Kijamii ya Zain Tanzania Tunu Kavishe (kushoto) mara baada ya kukabidhi madawati mia moja yenye thamani ya zaidi ya milioni saba kutoka kampuni ya Zain Tanzania kwa shule ya msingi Kasulu . Makabidhiano hayo yamefanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Moshi Mikidadi.

Saturday, July 3, 2010

ziff kuanza rasmi julai 10,2010


Mkurugenzi wa Tamasha la ZIFF,Dr. Martin Mhando akifafanua jambo kwa wadau waliofika katika mkutano wa ufunguzi rasmi wa tamasha hilo uliofanyika leo katika ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar.
Mratibu wa Maswala ya Muziki wa ZIFF,Edward Lusala (kushoto) akitaja list ya wasanii watakao panda jukwaani katika tamasha hilo linalotazamiwa kuanza rasmi Julai 10 mpaka Julai 18 huko kisiwani Zanzibar.wengine toka kulia ni Dean Nyalusi (Meneja wa ZIFF),Dr. Martin Mhando (Mkurugenzi wa ZIFF) na Ibrahim Mitawi (Msaidizi wa mambo ya Kiufundi ZIFF).
Baadhi ya wadau walifika leo katika ufunguzi rasmi wa tamasha la ZIFF katika ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar wakifuatilia kwa makini maelezo ya Dr. Mhando (hayupo pichani)..


ZANZIBAR INTERNATIONAL FILM FESTIVAL


Zanzibar International Film Festival (July 10th-18th) ni tamasha kubwa kuliko yote ya utamaduni ya aina yake kwenye ukanda wa Afrika mashariki. Ikiwa imetimiza miaka 13 na kuudhuriwa kila mwaka na zaidi ya wageni 200,000 na kushirikisha nchi 43, ZIFF ni taasisi ya wazanzibari yenye kulenga zaidi filamu za kiafrika huku ikisherehekea na kuthamini utajiri wa tamaduni zilizopo ndani ya ukanda huu na zaidi

Tofauti na tamasha lingine lolote, hili ni tajiriba ya aina yake ya tamaduni za kiafrika. Hakuna zuria jekundu, Umaridadi na waandishi wa habari za udaku.

ZIFF ni tamasha linalokuja mara mmoja tu kwa mwaka, ni nafasi ya pekee kwa Wazanzibari kujumuika pamoja na kutazama filamu kwenye viwambo vikubwa. Kwa mwaka huu filamu zote zitaonyeshwa bure kwa wakazi wote wa Zanzibar!


ZIFF’s theme this year’s is Hopes in Harmony.
Mwishoni mwa mwaka huu Zanzibar itafanya uchaguzi mkuu wa serikali. Kuna historia ya machafuko kipindi cha uchaguzi kwa kutazama uchaguzi uliopita mwaka 2005 kati ya wanaounga mkono upinzania na polisi. Mbiu ya tamasha kwa mwaka huu ina angaz matakwa ya watu wa kisiwa hiki ya amani na muafaka.

Filamu ya ufunguzi, ni filamu yenye tunzo inayo muhusu mwanamziki maarufu Youssou N’Dour, I Bring What I love (Naleta nachokipenda), inayozungumzia ]addresses the themes of religious tolerance, harmony and peace.

“I Bring What I Love” imedhaminiwa na SIGNIS.


Key Facts & Figures in 2009
• Waudhuriaji Mji Mkongwe: 45,000
• Waudhuriaji Dar es salaam: 200,000
• Wageni toka nje: 12,000
• Nchi zilizo shiriki: 43
• Filamu zitakazoonyeshwa mwaka huu: 100


Vitu Vya Kutazamia Mwaka Huu…
Fainali ya Kombe la dunia! Kwa kuzindua tamasha 2010 tutaonyesha mechi ya fainali ya kombe la dunia ndani ya Ngome Kongwe.

Filamu ya ufunguzi
Youssou N’Dour. I Bring What I Love Ni filamu yenye tunzo nyingi. Ya kuhamasisha, inayotupeleka kwenye safari ya kimziki, yenye ushuhuda wa nguvu ya sauti ya mtu mmoja kuhamasisha mamilioni. Muongozaji wa Filamu: Elizabeth Chai Vasarhelyi. Imedhaminiwa na SIGNIS.

Nipe Jibu: Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza . Filamu ya kwanza ya kuchanganya Muziki na kuigiza Muongozaji Nadine Louise Fasera. Nipe Jibu ni filamu nzuri ya Kiswahili yenye kuchanganya muziki iliyotengenezwa kwa mtazamo wa kisasa na kitamaduni kwa simulizi iliyochangamka juu ya binti yatima anayeishi kwenye maisha ya ndoto.

My Policy: Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza. Kijana mdogo mfanya biashara anapigwa risasi kwenye siku yake ya kuzaliwa akiwa anarejea nyumbani kwake akitokea kwenye tafrija yake kusherehekea siku hii muhimu akiwa na mchumba wake, Victoria. Wiki chache baadae, Yule aliyempiga risasi amjia na kumchoma kisu hadi kufa. Kwa kupagawa na pigo hili, Victoria aamua kuhama Montreal na kuanza maisha mapya, Lakini muuaji amjia nay eye pia.... Muongozaji: Phad Mutumba

Motherland: African premiere - Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza Africa

Ana’s Playground: African premiere

Lamu’s Maulid: world premiere

Inside Life: world premiere
Pumzi: East Africa’s first ever science fiction film
A sneak preview of Twiga Stars

Muziki
ZIFF 2010 Itakua ikisakata kwenye burudani ya muziki na… Dully Sykes – AKA Mr Misifa ama Mr Chicks, Msanii anayetambulika sana kwa miondoko ya dancehall Tanzania. AY, Msanii anayengara ndani ya Africa Mashariki akiwakilisha vyema Tanznia na balozi wa burudani Tanzania, Kidumu , Ndiye mwanamuziki maarufu Africa Mashariki toka Burundi anayeshikilia Tunzo nyingi ikiwemo tunzo ya Muziki bora wa Afrika Mashariki kwa Tunzo za Tanzania Music Awards, Body Mind Soul Bendi ya watu 6 kutoka Kaskazini mwa Malawi wanaopiga mziki wa kiafrika wenye vionjo vya Jazz, Windhund featuring Sekembuke & Siga bendi kutoka Austria inayotumia vionjo vya kizungu na kiafrika, ushairi na sanaa ya simulizi ili kuleto vionjo vipya na vya aina yake kwenye ulimwengu wa muziki.

Filamu za Watoto!
Kwa kushirikiana na taasisi ya filamu ya Kidanish, Maonyesho ya filamu za Watoto zitaonyeshwa makundi makubwa ya Watoto, zikiwa zimetafsiriwa kwa Kiswahili kwajili ya Watoto na vijana wa Mji mkongwe.

Art exhibtions
"Hopes in Harmony" (Matumaini yenye Kuafikiana) – Onyesho la picha yanayoletwa na mpiga picha toka Italy, Carlo Deste
"Colour Bash" – Uchoraji wa vitenge kutoka pande mbalimbali za Afrika, na Mahelia de Randamie
Artwork kutoka wakina mama wa Iranian, Hii inaletwa na Ubalozi wa Iranian embassy
kwa kushirikiana na Soko Filam, ambapo watengeneza filamu na wachongaji toka Zanzibar wanakuja kuonyesha na kuuza bidhaa zao..

Tasnia
ZIFF ni tukio muimu kwenye jumuiya ya Cinema duniani. Festival Forum na Festival of Festival program inatoa nafasi kwa wasambazaji, mapromota, waongozaji wa filamu na waandaji kukutana ili kukomaza mizizi kwenye tasnia ya filamu kwenye nchi zinazoendelea. Mwaka huu wawakilishi toka Trinidad na Tobago, Uganda, Holland, Iran, Mexico and Italy watashiriki ZIFF kujadili nafasi ya matamasha ya filamu kwenye nchi zinazoendelea.

Warsha
ZIFF itaendesha warsha tatu wakitoa upendeleo kwa ushiriki wa waandaji filamu toka ukanda huu wa Afrika mashariki kwa waandaji wenye kuonyesha hari na vipaji vyenye mlengo wa kuibuka kwenye tasnia hii.

WARSHA ZA NAMNA YA KUOMBA MISAADA YA KIFEDHA KUANDAA FILAMU NA WARSHA – warsha itaongozwa na wakufunzi toka Sweden and Uganda

UANDAAJI WA MAKALA: CONNIE FIELD – Warsha hii ya siku nzima italeta mtazamo mzima wa namna ya kuandaa makala chini ya usimamizi wa mshikiliaji wa tunzo ya uandaaji wa makala(producer / director), Connie Field.

CINEPHILMS:UTENGENEZAJI WA FILAMU KUTUMIA SIMU YA MKONONI – Hii warsha ya aina yake itaongozwa na Jonathan Dockney wa chuo kikuu cha Natal South Africa. Utengenezaji wa filamu kwa kutumia simu za mkononi ni teknolojia inayo ibuka kwa kasi sana. Njo ujifunze jinsi ya kutengeneza filamu kwa simu!

Tafadhali bonyeza hapO kwa maelezo zaidi:
www.ziff.or.tz
ama
www.ziff.or.tz/press

Asmah Makua
(Swahili Press)
asmahmakau@yahoo.co.in
Tel no: 0713711413
Laura Martin-Robinson
(English language Press)
press@ziff.or.tz
Tel: +255 782689845

TBL yaipiga jeki timu ya taswa fc ya arusha

Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za michezo ambaye pia ni Mratibu wa tamasha la waandishi wa habari za michezo,Jamila Omari akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha hilo la michezo linalotarajia kufanyika Agost 1 mwaka huu.katikati ni Meneja matukio wakanda ya kaskazini wa TBL,George Mombeki na kushoto ni Katibu wa chamacha waandishi wa habari za michezo,Mussa Juma
Nahodha wa timu ya Taswa FC ya mkoa wa Arusha Moses Kilinga akikabithiwa jezi na mpira na mratibu wa tamasha hilo Jamila Omary kwa ajili ya maandalizi ya timu yake.
Meneja matukio wakanda ya kaskazini wa TBL,George Mombeki akimkabithi Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za michezo ambaye pia ni Mratibuwa tamasha la waandishi wa habari za michezo,Jamila Omari mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni mbili iliyotolewa na kampuniya bia ya TBl kwa ajili ya mashindano hayo.


Na Woinde Shizza,Arusha

kampuni ya bia ya TBL imetoa cheki ya shilingi milioni mbili kwa ajili ya kudhamini Tamasha michezo la waandishi wa habari linalotarajia kufanyika Agosti moja mwaka huu katika kiwanja cha kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za michezo mkoani hapa ambaye pia ni mratibu wa mashindano haya Jamila Omary wakati akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa tamasha hili linatarajia kufanyika Agosti moja mwaka huu na litashirikisha jumla ya timu kumi na mbili zilizopo mkoani hapa.

Alisema kuwa tamasha hili hufanyika kila mara na linashirisha timu za waandishi wa habari kutoka katika mikoa mbalimbali ikiwemo timu ya waandishi wa habarikutoka mkoani Dar es salaam,Arusha pamoja na mkoa wa Manyara.

Alitaja nia ya tamasha hili ni kuwakutanisha pamoja waandishiwa habari kutoka katika mikoa mbalimbali pamoja na kuwapa burudani ikiwemo yamichezo mbalimbali na kubadilishana ujuzi na mawazo kwa ujumla.

Jamila alitaja timu ambazo zimejitokeza kushiriki katika mashindano haya kuwa ni Taswa FC ya Arusha,Taswa ya Dar ,timu ya chuo cha waandishi wabahari cha Arusha (AJTC),chuo cha waandishi wa habari east afrika ,radio five,triple A radio,Ormame radio ,timu ya CRDB,timu ya NMB,timu ya NSSF,timu ya Pepsi pamoja na timu kutoka kampuni ya bia ya TBL.

Akikabithi cheki hiyo meneja matukio wa kanda ya kaskazini kutoka TBL George Mombeki alisema kuwa kampuniu yao imehamua kuthamini tamasha hili kwani waandishi wa habariwamekuwa wakiwapa ushirikiano mkubwa sana.

"tumeamua kuwaunga mkono waandishi wa habari kwakuwa wamekuwa wakitupa ushirikiano mkubwa sisi pamoja na wananchi kwa ujumla na tunahaidi kuthamini mashindano haya mpaka mwisho hatutaishia hapa"alisema Mombeki.

Ujerumani yaiadhibu Argentina 4-0

Mashabiki wa Ujerumani wakishangilia ushindi wa timu yao dhidi ya Argentina.

Ujerumani imeiadhibu Argentina kwa kuifunga mabao 4-0 kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia katika uwanja wa Green Point mjini Cape Town na kujipatia nafasi katika nusu fainali.

Juhudi za Ujerumani kutaka kufuzu miongoni mwa nne bora zilianza katika dakika ya tatu wakati Thomas Muller alipofunga kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Bastian Schweinsteiger.

Kipindi cha kwanza kilimalizika Ujerumani wakiongoza 1-0 na katika dakika ya 68, Miroslav Klose akiichezea nchi yake mechi ya 100 aliongeza bao la pili kukamilisha pasi ya Lukas Podolski.

Podolski aliendelea kupenyeza pasi za kupendeza kutokea upande wa kushoto, na katika dakika ya 74 alitoa moja ambayo mlinzi Arne Friedrich alifunga bila matatizo, na kuipatia Ujerumani bao la 3.

Klose alipata fursa nyingine katika dakika ya 89 kumalizia pasi nyingine kutoka Podolski na kuandikisha bao lake la pili, na la nne kwa Ujerumani.

Uhasama

Katika mashindano ya Kombe la Dunia yaliyopita timu hizo mbili zilikutakana katika hatua ya robo fainali ambapo Ujerumani walishinda kupitia mikwaju ya penati.

Kwenye mechi ya Jumamosi, Ujerumani waliwavuta Argentina upande wao mara kwa mara kisha kuwavamia haraka, mkakati ambao uliwawezesha kupata ushindi mkubwa.

Walinzi wa Ujerumani walimdhibiti nyota wa Argentina Lionel Messi ambaye aliweka juhudi nyingi za kutaka kurudisha goli kwa mikwaju ya mbali.

Sasa Ujerumani inatarajia kuchuana kwenye nusu fainali na mshindi kati ya Uhispania na Paraguay.

Miroslav Klose anahitaji kufunga mabao mawili tu kwenye michuano iliyosalia ili kuwa mchezaji anayeongoza kwa ufungaji wa mabao mengi katika historia ya michuano ya Kombe la Dunia. Kwa sasa analingana na Gerd Muller pia wa Ujerumani ambaye amefunga magoli 14, anayeshikilia rekodi ni Ronaldo wa Brazil akiwa na magoli 15.

Serena atwaa taji la tennis Wimbledon

Serena Williams ameshinda taji lake la nne la Wimbledon.

Serena Williams ameshinda taji lake la nne la ubingwa wa Wimbledon katika mchezo wa tennis kwa kumshinda Vera Zvonareva wa Urusi kwa seti mbili kwa mfuto katika fainali ya wanawake. Hii inakua ni mara ya 13 kwa Serena kunyakua ubingwa wa mashindano makuu ya kimataifa ya Grand Slam.

Serena ambaye ndiye mchezaji nambari moja dunia alitetea taji lake dhidi ya mrusi huyo 6-3, 6-2 katika muda wa dakika 67 na kuongeza udhibiti wa familia ya Williams katika Wimbledon.

Serena amemaliza mashindano ya mwaka huu bila ya kupoteza hata seti moja na kuongezea mataji aliyokwishajinyakulia ya Wimbledon katika miaka ya 2002, 2003 na 2009.

Hii ni mara ya kwanza kumshinda mtu ambaye si dada yake Venus katika fainali ya Wimbledon.

Dada hawa wawili kwa jumla wameshinda mara tisa ubingwa wa Wimbledon katika miaka 11 iliyopita.