Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, October 12, 2010

WIZARA YA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO YAAGIZA TFF KUANZIA SAS A KUTUMIA BRASS BAND WAKATI WA MECHI ZA KIMATAIFA NA SI VINGINEVYO

Katikati ni katibu mkuu wa wizara ya habari utamaduni na michezo SETTI KAMHANDA kulia kwake ni mkurugenzi wa idara ya michezo THADEO na kushoto ni mkurugenzi wa MAELEZO CLEMENT MSHANA
Mkurngenzi wa idara ya michezo LEONARD THADEO akiju swali kwa waandishi wa habari
Katibu mkuu wa wizara ya habari utamaduni na michezo SETTI KAMHANDA akiwa na mkurugenzi wa idara ya michezo LEONARD THADEO .
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, GEROGE MKUCHIKA, ameliangiza shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kuhakikisha kuanzia sasa nyimbo za taifa katika michezo yeyote ya kimataifa zinapigwa na BRASS BAND, ili kuepuke aibu na fedheha kama zile zilizotokea juzi kwenye uwanja wa taifa wakati wa mechi kati ya TAIFA STARS na Morocco.

Akizungumza kwa niamba ya waziri Mkuchika,katibu mkuu wa Wizara Habari, Utamaduni na Michezo SETTI KAMHANDA amesema kitendo cha kutopingwa nyimbo za taifa kilichotokea siku ya jumamosi kilisababisha adha kubwa kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, JAKAYA KIKWETE,mashabiki waliohudhuria mchezo huo na wananchi.

KAMHANDA ameongeza kwamba WAZIRI MKUCHIKA ameliangiza shirikisho la soka nchini TFF, kuhakikisha linachukua hatua kali dhidi wale wote waliohusika kulitia aibu taifa kwa kushindwa kuwezesha kupingwa nyimbo za taifa wakati wa mchezo kati ya TAIFA STARS na Morocco

Wakati Mkuchika akitoa agizi hilo, tayari shirikisho la soka nchini TFF, kupitia kwa RAIS wake LEODGER TENGA tayai limeshamsimamaisha kazi Afisa habari wake FLORIAN KAIJAGE kwa uzembe huo na kwamba atisaidia tume itakayoundwa kulichnugza sakata hilo.

Katika mchezo huo kundi D, uliochezwa kwenye uwanja taifa jijini DSM STARS ilifungwa bao moja kwa bila na Morocco.

MSANII SALIF KEITA KUTOKA MALI KUTUMBUIZA MOVENPICK DSM JUMATANO KESHO

Msanii KEITA akisalimiana na kiongozi kutoka chama cha albino nchini wakti wa mkutano na waandishi wa habari
msanii SALIF KEITA
Msanii SALIF KEITA katika akiongea na waandishi kulia kwake ni meneja masoko kutoka banki ya stanbic singano

SALIF KEITA kutoka MALI kutumbuiza Dar

Mtuzi na Mwimbaji wa Mziki kutoka MALI, SALIF KEITA, maarufu kama,(GOLDEN VOICE OF AFRICA) anatarajiwa kukonga nyoyo za mashabiki wa mziki atakapopanda jukwaani kutupuiza jijini DSM hiyo kesho .

MENEJA MASOKO wa BANKI ya STANBIC ambao ndio wadhamini wakuu wa ziara ya mwanamziki huyo, ABDALLAH SINGANO amesema pamoja na kutumbiza kwa nyimbo mbalimbali pia ataimba nyimbo zinazohusu nyimbo zinazopinga unyanyasaji na mauja ya Albino nchini na Afrika kwa ujumla.

KEITA ambaye pia ni Albino, amesema binaandanu wote ni sawa,wameubwa kwa rangi na mabakila mbalimbali ili wapate kujuana,na kuzaliwa Albino hayo ni majaliwa ya mungu na si changuo la wao Albino kwa hivyo hawabanguliwe wala kuuawa.

Katika onyesho hilo litakalotubuizwa na SALIF KEITA,pia atazidikizwa na mwanamuziki wa tanzania mwanadada KEISHA.

KUZIONA SIMBA NA YANGA ELFU 30 KATIKA UWANJA WA CCM KIRUMBA MWANZA


Kaimu katibu mkuu wa TFF SUNDAY KAYUNI ametanganza viingirio katika mchezo wa watani wa jadi simba na yanga mchezo utakaofanyika jumamosi ijayo katika uwanja wa ccm kiruma mkoani MWANZA.
AMESEMA KIINGILIO KATIKA MCHEZO HUO NI, MZUNGUKO ELFU TANO WAKATI VIP SHILINGI ELFU THELATHINI.
Wakati huo huo KAYUNI amesema msafara wa viongozi watatu wa TFF wameondoka leo kwenda CAIRO MISRI kuhudhuria mkutano wa shirikisho la soka Afrika, CAF wa kutadhimini michuano ya fainali za kombe la mataifa Afrika CAN yaliyofanyika Angola mwaka 2008.

Viongozia waliondoka ni rais wa TFF leodiger tenga,kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday kayuni na kocha wa timu ya taifa JAN PAULSEN.

RAIS WA TFF TENGA ATANGAZA KUMSIMAMISHA KAZI MSEMAJI WA TFF KAIJAGE

Rais wa tff tenga kulia akiwa na mkurugenzi wa ufundi sunday kayuni.

Shirikisho la soka nchini TFF limemsimamisha kazi Afisa habari wake FLORIAN KAIJAGE kutokana na tuhuma za uzembe uliochangia kushindwa kukamilishwa kwa itifaki ya kupigwa kwa nyimbo za taifa katika mchezo kati ya TAIFA STARS dhidi ya MOROCCO uliofanyika siku ya Jumamosi.

Rais wa shirikisho la soka hapa nchini-TFF- LEODGAR TENGA amemwomba radhi rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, JAKAYA MRISHO KIKWETE,serikali ya MOROCCO, mashabiki waliokuja uwanjani siku ile na WATANZANIA kwa ujumla kwa tukio hilo.

Aidha TENGA anasema hatua ya kumsimamisha kazi KAIJAGE imechukuliwa ili kutafuta chanzo cha sababu zilizopelekea kushindwa kupigwa kwa nyimbo za TAIFA siku hiyo na TFF imeunda tume maalumu kuchunguza suala hilo.

Kufuatia kutokea kwa tatizo la kugoma kwa wimbo wa taifa mara kwa mara TFF imeamua kuanzia sasa kutumia bendi ya polisi -‘BRASS BAND’ kama njia mbadala ya kucheza nyimbo za taifa pindi timu ya taifa inapocheza na timu ya taifa jingine.
Wakati huohuo TFF imeahidi kukaa meza moja na vyombo vya habari kutatua

kasoro zilizojitokeza katika mechi iliyopita ambapo waandishi wa habari walilazimika kuingia uwanjani kwa kutumia tiketi badala ya utaratibu uliozoeleka wa kutumuia kadi maalumu.

ALIYEKUWA MSEMAJI WA TFF KAIJAGE.

Monday, October 11, 2010

TAIFA STARS HOI KWA MOROCCO YALALA 1-0 NYUMBANI

Kipa wa timu ya Taifa ya Moroco, akiruka kuokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake wakati wa mchezo baina ya timu hiyo na Moroco, wa kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afri, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijiji Dar es Salaam leo jioni. Moroco ilishinda bao 1-0. Picha na (SPM)
Beki wa kushoto wa Taifa Stars, Stephano Mwasika, akiwatoka mabeki wa Moroco, wakati wa mchezo huo.
Winga wa Stars, Idrisa Rajab, akiruka kumiliki mpira mbele ya beki wa Moroco.
Kiungo mshambuliaji wa Stars Nizar Khalfan, akiwahadaa ambeki wa Moroco.
Screen ya Uwanjani humo nayo pia ilifanya kazi na kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki waliokuwa na huzuni ya kufungwa na wengine wakijikuta wanafuraha baada ya kujiona katika Screen hizo japo tayari timu yao ilikwisha fungwa.
Mrisho Ngasa, akichuana na beki wa Moroco...
Mshambuliaji wa Moroco, ambaye pia mchezaji wa Arsenal akimiliki mpira mbele ya mabeki wa Stars Nadiri Haroub (kushoto)hadrac na Shadrack Nsajigwa.
Sehemu ya mashabiki wa soka waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.
Hatari langoni mwa Moroco.......
Beki wa Stars, Shadrack Nsajigwa, akibadilishana jezi na mchezaji wa Moroco baada ya mchezo huo kumalizika

Saturday, October 9, 2010

TASWA YAIJIA JUU TFF JUU YA UINGIAJI WA WANAHABARI KATIKA MECHI

TASWA YAIJIA JUU TFF JUU YA UINGIAJI WA WANAHABARI KATIKA MECHI


Katika hatua nyingine CHAMA cha waandishi wa habari za michezo TASWA na kinakusudia kuvunja uhusiano wake na shirikisho la soka nchini TFF endapo halitafuata maelekezo ya mapendekezo yao ya waandishi wa habari kuingia uwanjani bila kuwa na utaratibu wenye kikwanzo.

Taarifa ya TASWA iliyosambazwa na katibu mkuu wa chama hicho, AMIR MHANDO ametaja mapendekezo ya makubaliano ya kikao chao na baadhi ya wahariri wa habari nchini na kubainisha kuwa endapo TFF itapuuza mapendekezo yao.

Miongoni mwa mapendekezo waliyotaka kutekelezwa ni pamoja na TFF itenge tiketi 120 kwa ajili ya wanahabari kuanzia mchezo wa kesho kati ya TAIFA STARS na MOROCCO na si tiketi SABINI ambazo TFF ilibainisha kuzitoa katika mchezo huo.

STARS NGUO KUCHANIKA UWANJA WA TAIFA DHIDI YA MOROCCO

Naibu waziri wa habari utamaduni na michezo joel bendera akizungumza na wachezaji wa stars
nahodha shadrack

meneja wa timu ya stars mbele kabisa akiwa na wachezaji wakati wa mkutano na waandishi wa habari

BALOZI WA JAPAN AKABIDHI MIPIRA OFISI YA TAMISEMI

Balozi wa japan akitoa mipira

naibu katibu mkuu tamisemi akikabidhi mipira kwa mmoja wa viongozi kutoka namtumbo.
BALOZI wa JAPAN nchini TANZANIA, HIROSHI NAKAGAWA amekabidhi mipira MIA MBILI ya soka kwaajili ya watoto wa shule za wilaya ya NAMTUMBO mipira ambayo ilitolewa na wananchi WANNE wa JAPAN kuunga mkono maendeleo ya mchezo huo nchini.

Wakati akikabidhi mipira hiyo, Naibu katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini na kutaka mipira hiyo iwafikie walengwa

SAGINI, ameonyesha imani ya kuwa na wachezaji wa baadae wenye vipaji na hakusita kumweleza balozi HIROSHI NAKAGAWA kuwa mchezo wa soka ni moja kati ya michezo inayotoa ajira kwa vijana wengi nchini ndo mana serikali imeamua kurudisha michezo ya UMISETA na UMITASHUMTA kwani vipaji huanza kuonekana tangu utotoni.

MABONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA KUZICHAPA JUMAMOSI KATIKA UKUMBI WA TEMEKE STEREO

mabondia wakitambiana
mabondia wakiwa na promota
mabondia wakipima uzito

MAZOEZI YA TIMU YA MOROCCO YALIVYOKUWA SIKU YA ALHAMIS

MOROCCO WAINGIA DSM KWA KASI YA AJABU

mazoezi kama kawaida



mazoezi kama kawa

morocco wakiwa mazoezini

Friday, October 8, 2010

LIVERPOOL HATARINI KUPOTEZA POINTI

Klabu ya Liverpool inakabiliwa na hatari ya kukatwa pointi tisa iwapo kampuni inayoimiliki ya Kop Holdings itafilisiwa wiki ijayo.

Liverpool hatarini kufilisiwa

Liverpool hatarini kufilisiwa

Kanuni za ligi zinaeleza pointi zinaweza kukatwa iwapo kampuni inayoimiliki inakabiliwa na hatari ya kufilisika kutokana na mzozo wa utawala.

Taarifa zilizopatikana zinasema wamiliki wa klabu hiyo Tom Hicks na George Gillett watakuwa na kibarua kigumu kujieleza kwamba uendeshaji wa klabu hiyo hauathiri kampuni yao.

Liverpool inaweza ikaingia katika wimbi la kutangazwa imefilisika iwapo uuzwaji wa klabu hiyo hautakuwa umekubalika itakapofika tarehe 15 mwezi huu wa Oktoba.

Iwapo Hicks na Gillett watafanikiwa kuzuia uuzwaji wa klabu hiyo kwa gharama ya paundi milioni 300 kutoka kwa kampuni ya New England Sports Ventures (NESV), wanaomiliki timu ya mchezo wa baseball ya Marekani ya Boston Red Sox , kampuni yao inaweza kutangazwa imefilisiwa na Royal Bank of Scotland kutokana na deni inayodai ya paundi milioni 280.

Mtendaji Mkuu wa bodi inayoendesha Ligi kuu ya England Richard Scudmore, mwenyekiti Sir Dave Richards na katibu Mike Foster ndio watakaoamua kama kuna haja ya kuikata pointi klabu hiyo.

Liverpool tayari ipo katika wimbi la timu tatu zilizo chini ya msimamo wa Ligi Kuu ya England, baada ya kuanza vibaya msimu huu ikiwa na pointi sita tu kutokana na michezo saba iliyocheza hadi sasa.

Awali ilifikiriwa klabu hiyo ingeweza kuepuka adhabu hiyo, lakini sasa inakabiliwa na hatari iliyo wazi ya kukatwa pointi iwapo uuzaji wa klabu hiyo kwa kampuni ya NESV utacheleweshwa.

WATOTO WA MOMBASA KATIKA ZIARA UINGEREZA


Watoto 14 kutoka mjini Mombasa, Kenya, wenye umri wa chini ya miaka 13, wamekuwa nchini Uingereza kushiriki katika mechi kadhaa za kandanda.

Kundi hilo la watoto likifahamika kwa jina la Coastal Kings, yaani Wafalme wa Pwani, liliweza kupambana katika soka na watoto wa shule ya Uingereza ya Elstree.

Katika kipindi cha wiki moja, watoto hao waliweza kupata jumla ya magoli tisa, na muhimu zaidi, kupata marafiki watakaodumu katika maisha yao yote.

Vijana hao waliweza kutoka sare katika mechi tatu, na kupata ushindi katika moja.

Mwalimu mkuu wa shule ya Elstree, Mark Sayer, alisema alipendezwa mno na namna vijana hao kwa upesi walivyoweza kujumuika katika jamii ya Elstree.

Mara tu walipofika walishangazwa na maisha ya Elstree, lakini baada ya muda mfupi tu, waliweza kwa ujasiri mkubwa kuyazoea masiha ya Elstree.

Safari ya vijana hao nchini Uingereza ilipangwa na shirika linalofahamika kama Touraid.