Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
KAMPUNI
ya simu za mkononi ya Halotel ndio mtandao pekee unaotoa huduma za
mawasiliano kwa njia ya Simu za mkononi katika kata ya Namayuni iliyopo
Kilwa Masoko Mkoani Lindi.
Mtandao
huu ndio unawasaidia wakazi wa kata ya Namayuni kuweza kuwasiliana na
ndugu na jamaa wa maeneo hayo na sehemu nyingine kwa njia ya simu ya
mkononi kwa kuwa wamejengewa mnara unao wawezesha kuwasiliana kwa njia
simu za mkononi.
Diwani
wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura
amepongeza mtandao wa simu za mkononi wa Halotel na kusema kuwa
umeisaidia sana jamii ya wakazi wa kata ya Namayuni mkoani humo kutokana
na hapo awali kutokuwepo na mtandao wowote wa simu.
"
Tunawashukuru sana Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel kukumbuka kama
kunaviumbe huku na kutuwekea mnara katika kata yetu kwakua kabla ya
mtandao huu tulisafiri na kupanda juu ya vilima ili kutafuta
mtandao(network) ili tuweze kuwasiliana na watu wengine kwa njia ya
simu."
Nao
wakazi wa Kijiji cha Namayuni wamesema kuwa Mtandao huu wa Halotel
"umetusaidi sana katika huduma mbalimbali hasa kutufichia siri katika
mawasiliano kwani tulikuwa tunaenda umbali mrefu kwenda kutafuta
mtandao, kwa sasa tunakaa ndani tuu na tunawasiliana na ndugu na jamaa
bila mtu yoyote kujua kama tumewasilana na nani".
Wafanyakazi
wa mtandao wa Halotel wametembelea kata ya Namayuni kwaajili ya
Kampeni ya HALO MAISHA inayoendelea katika maeneo mbalimbali
yaliyofikiwa na mtandao huo nchi zima ili kila jamii ifaidike na spidi
kubwa ya intaneti na upatikanaji wa huduma nzuri za mtandao huo.
Wanafunzi
wakisoma kupitia Kompyuta zilizounganishwa na intaneti ya spidi kubwa
walizopewa na kampuni ya Simu za mkononi ya Halotel katika shule ya
sekondari ya Lugoba iliyopo Msata- Bagamoyo Mkoani Pwani.
Mtaalamu
wa masuala ya mtandao wa kampuni ya Halotel, Kilwa Masoko Mkoani
Lindi, Sebastian Inocent akifafanua changamoto mbalimbali zinazo wapata
wakazi wa kijiji cha Namayuni.
Afisa
habari wa kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Halotel, Frank
Mwakyoma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namayuni kilichopo kata
ya Namayuni Kilwa Masoko Mkoani lindi mara baada ya wafanyakazi wa
kampuni hiyo kuwatembelea katika kijijini hapo.
Wakazi wa Kijiji cha Namayuni wakipata maelekezo walipo tembelea kibanda cha kusajili laini jijini hapo.
Vijana wakipiga simu kwa ndugu na jamaa wakiwa kijijini hapo.
Baadhi ya waandishi wa habari.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Lugoba iliyopo Msata mkoani Pwani, Abdala
Sakasa akizungumza wakati wafanyakazi wa kampuni ya Simu za Mkononi ya
Halotel walipotembea katika shule hiyo kujionea jinsi wanafunzi
wanavyotumia Kompyuta zilizounganishwa na intaneti yenye spidi ya kazi
ili kusaidia wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Lugoba hasa wa kidato
cha tano na cha sita kwa kusoma na kuongeza uwezo wao katika masoma
kutokana na wanafunzi hao kukosa baadhi ya vitabu. Wanafunzi wa shule
hiyo wamefurahia uwepo wa mtandao wa Halotel kwani ndio mtandao pekee
uliochelewa kufika hapa nchini na kuweza kutoa kompyuta 19
zilizounganishwa na intaneti katika shule hiyo.
Mwalimu
wa somo la Kompyuta na maswala ya mawasiliano(ICT), Emmanuel Mhizi
akifafanua jambo mbele ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya
Halotel walipotembelea shuleni hapo mkoani Pwani. Mwalimu wa Kulia ni
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Lugoba, Benjamini Nyamatwema.
Mhizi
amesema kuwa wanachangamoto kubwa katika kupanga zamu za wanafunzi wa
shule hiyo kwani shule hiyo inawanafunzi 1391 na kompyuta zenye intaneti
ni 19 tuu, kwa mujibu wa ratiba ya wanafunzi kuingia kwenye chumba
hicho wanaingia wanafunzi 30 kwa kila kipindi ili kila mwanafunzi aweze
kuingia katika chumba cha kompyuta.
Wanafunzi
wakiwa katika Darasa la kompyuta ambalo Kampuni ya Halotel walijitolea
kwa kuwapa kompyuta hizo pamoja na kuwaunganishia Intaneti spidi kubwa
ya bure kwa miaka mitatu mfurulizo iki kuweza kuwasaidia wanafunzi hao
katika kujisomea machapisho mbalimbali yaliyopo kwenye mitandao
mbalimbali.
Mwalimu
wa somo la Kompyuta na maswala ya mawasiliano(ICT), Emmanuel Mhizi
akiwakagua wanafunzi kwa uangalifu katika darasa hilo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lugoba akiendelea kujisomea somo alilolifungua walipotembelewa na wafanyakazi wa Kampuni ya Halotel mkoani humo.
Walimu wa Shule ya Sekondari ya Lugoba iliyopo Msata- Bagamoyo Mkoani Pwani wakijadiliana jambo wakati wanatembea.
Diwani wa
Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura
akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wakazi wa kijiji cha
Namayuni mkoani humo walipotembelewa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya
Halotel ambayo ndio mtandao pekee uliowafikia wananchi na wakazi wa kata
hiyo.
Wakazi wa kata ya Namayuni na wanakijiji cha Namanyuni wakimsikiliza Diwani
wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura
mara baada ya kutemelewa na wafanyakazi wa kampuni ya Simu za Mkononi yz
Halotel mkoani humo.
Mkazi
wa Kijiji cha Namayuni akizungumza na simu wakati amekaa akitumia
mtandao wa simu wa Halotel akiwasiliana na mtu aliyepo Zanzibar bila
kwenda kupanda kwenye kilima kama zamani.
Aidha
mzee huyo alielezea furaha yake kwa ujio wa mtandao wa Halotel
unavyowasaidia na kuwafichia siri zao, kwani mwanzoni kila mtu alijua
kuwa ndio anaenda kuongea na simu na mpaka kusababisha kuaga na kwenda
umbali furani kwaajili ya kutafuta netiweki ili aweze kuzungumza na mtu
ambaye anamtafuta.
Mwenyekiti
wa Kijini cha Namayuni, Ally Mtumbwe akizungumza na waandishi wa habari
Kilwa Masoko Mkoani Lindi kata ya ya Namayuni kijijini cha namayuni
mara baada ya wafanyakazi wa mtandao wa Halotel kutembelea kijijini
hapo.
Mkazi
wa Kijiji cha Namayuni akielezea jinsi mtandao huo ulivyorahisisha
biashara kutokana na kujengewa mtandao wa Halotel amesema kuwa mtandao
huo umewasaidia kwa kuagiza bidhaa anazozihitaji ukitofautisha na zamani
ambapo ilibidi kuzifuata hata kama hajui kama bidhaa anayoitaka ipo au
haipo, hata hivyo amesema kuwa Halotel imewasaidia kuokoa muda sana.
Mkazi wa kijiji cha Namayuni akiuliza swali kuhusiana na mtandao huo kuhusiana na kama unaweza kutuma pesa au kupokea pesa.
Watoto wa Kijijini cha Namayuni wakipata picha na mwandishi wa gazeti la The Citizen kijijini hapo.
Afisa
masoko wa kampuni ya Halotel , Charle anayepiga picha kwa simu akiwa na
baadhi ya waandishi wa habari katika kijini cha Namayuni, Klwa Masoko
mkoani Lindi.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.