Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, February 6, 2012

JERUSALEM GROUP YAZINDUA KATIBA YAKE


Mgeni rasmi akigawa katiba kwa wanachama
Katiba zikiendelea kugaiwa baada ya uzinduzi wake
Mkurugenzi Msaididi toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Vick Mwakasege akimkabidhi Katiba mweka hazina wa Jerusalem Group Bi, Rose Mkisi baada ya kuizindua Dar es salaam jana
Mkurugenzi Msaididi toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Vick Mwakasege akionesha katiba aliyozindua
Mkurugenzi Msaididi toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Vick Mwakasege Katiba mweka hazina wa Jerusalem Group Bi, Rose Mkisi baada ya kuizindua Dar es salaam jana
Baadhi ya wanachama wakiburudika na mziki wakati wa uzinduzi wa katiba hiyo
Makamu Mwenyekiti wa Jerusalem Group Bi, Eddah Mwakasege akisoma lisara kwa mgeni rasmi
Ni Burudan Mwanzo Mwishooo
Kaimu Mwenyekiti Dr Asajile Mwakasole akitoa neno
Kaimu Mwenyekiti Dr Asajile Mwakasole kulia akimkabidhi katiba mgeni rasmi kwa ajili ya kuizindua

AUT EZEKIEL NA KAJALA WAGOMBEA BWANA..!!



URAFIKI wa wasanii wawili wa tasnia ya filamu bongo, Kajala na Aunty Ezekiel, umeanza kuingia dosari, baada ya tetesi kwamba wamechukuliana bwana huku wakijua kuwa wao ni marafiki wa karibu.

Baadhi ya watu wa karibu na mastaa hao, walifunguka na kusema kuwa dalili hizo mbaya zimejitokeza hivi karibuni ambapo nyota hao walionekana wakipigiana simu za kutukanana.

Kajala na Aunty hivi karibuni urafiki wao ulikuwa ni wa hali ya juu ambapo hata hivyo baadhi ya watu walitabiri kuwa hawawezi kufika mbali kwani wote ni wanawake ambao wanapenda kujirusha.

Mmoja wa wasanii ambae anafanya kazi na nyota hao, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kuwa siku ambayo Kajala anatoroka na mpenzi wa rafiki yake walikuwa sehemu moja wanakunywa, baada ya wote kulewa ndiyo mchezo huo ulipofanyika.

Alisema baada ya kufanya kitendo hicho alimtaarifu Aunty, kuwa asiwe na wasiwasi kwani mpenzi wake ameondoka naye na hawezi kurudi eneo la tukio kwani wako mbali.

“Unajua hawa walikuwa ni marafiki sana na naweza kusema awali walikuwa kama ndugu lakini baada ya kuchukuliana wanaume basi hali imekuwa mbaya na kwa sasa hawapeani hata salamu.” alisema msanii huyo.
Baada ya warembo hao kutafutwa, Kajala, alisema kuwa hana bifu na Aunty lakini tatizo ambalo lipo ni dogo na watalimaliza kwani mapenzi hayana mwisho katika hii dunia.

Alisema alimchukua mpenzi wa rafiki yake lakini siku hiyo alikuwa amelewa na hakujua kama anafanya makosa makubwa kama hayo.

“Unajua pombe zikiwa zimepanda kichwani unaweza kufanya kitu ambacho hukutegemea kukifanya, lakini kuhusu hilo naweza kusema kwamba yataisha kwa sababu sisi marafiki wa kushibana,” alisema Kajala.

Kwa upande wa Aunty alidai kuwa hawezi kurudiana tena na mpenzi wake huyo ambaye tayari amelala na Kajala kwani haitaji kutoka na mwanaume ambaye tayari ametembea na msanii.

Aliongeza kwa kusema kuwa endapo Kajala, anahitaji waendelea kuwa marafiki basi amuombe msamaha kupitia vyombo vya habari ili kila mtu aweze kujua kilichotokea kati yao.

Sunday, February 5, 2012

SUPER D BOXING COACH AJIDHATITI KUENDELEZA MCHEZO WA NGUMI 2012


Baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Olimpic Tanzania 'TOC' na viongozi wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa Nchini 'BFT' wakiwa katika picha ya pamoja na makocha wa mchezo wa ngumi toka mikoa mbalimbali nchini Tanzania baada ya kupatiwa vyeti vya kutambulika kimataifa baada ya kuhitimu kozi kwa makocha hao
Baadhi ya makocha wa mchezo wa ngumi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa vyeti vyao wakati wa mafunzo ya kimataifa ya mchezo huo yaliyomalizika Kibaha Mkoa wa Pwani jana huku wakiwa wameng'arishwa na fulana zilizotolewa na SUPER D BOXING COACH kama zawadi kwa makocha hao.Baadhi ya makocha wa mchezo wa ngumi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa vyeti vyao wakati wa mafunzo ya kimataifa ya mchezo huo yaliyomalizika Kibaha Mkoa wa Pwani jana huku wakiwa wameng'arishwa na fulana zilizotolewa na SUPER D BOXING COACH kama zawadi kwa makocha hao.
Mkufunzi Mkuu wa Makocha wa Ngumi kutoka Chama cha Mchezo wa Ngumi za Ridhaa Duniani ( AIBA), Josephe Diouf, akimkabidhi cheti cha kufuzu ukocha wa mchezo wa ngumi Kimataifa, Rajabu Mhamila 'Super D' wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani
Kocha wa KImataifa wa Mchezo wa Ngumi Rajabu Mhamila 'Super d' akiwa ameshika cheti chake alichopewa baada ya kufuzu mafunzo ya ukocha kimataifa yaliyoandaliwa na Kamati ya Olimpic Tanzania kwa kushirikiana na chama cha ngumi cha Dunia 'AIBA'

klabu ya Bigrayt Mwananyamala yaendelea kuwanowa vijana


Kocha wa mchezo wa Ngumi Ibrahimu Kamwe 'Bigrayt' (kulia) akimwelekeza bondia Issa Omari jinsi ya kutupa masumbwi katika klabu ya Bigrayt Mwananyamala Dar es salaam jana (PIcha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

MASHINDANO YA KWANZA YA MCHUJO KUTAFUTA MABONDIA WATAKAOWAKILISHA TAIFA LA TANZANIA



3 February 2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Yah;- MASHINDANO YA KWANZA YA MCHUJO KUTAFUTA MABONDIA
WATAKAOWAKILISHA TAIFA LA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA
KUFUZU KUSHIRIKI MASHINDANO YA OLIMPIKI CASABLANCA
MOROCCO APRIL 2012.
Mashindano ya kwanza ya mchujo kwa ajili ya kuwapata wachezaji wa timu ya taifa ya mchezo wa ngumi.yatafanyika jijini Dare s salaam katika ukumbi wa uwanja wa taifa wa ndani tarehe 15-18/02/2012.
Watakao husika katika mchujo huo ni mabondia ambao wapo mazoezi,katika vituo vilivyoainishwa na BFT kwa ajili ya mazoezi ya awali kwa wachezaji walioteuliwa kwa kuzingatia vigezo vya kuwa wamefanya vizuri sana katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa yaliyoandaliwa au kutambuliwa na BFT.
Vituo hivyo ni uwanja wa ndani wa Taifa,Magereza Ukonga,mwenge JWTZ,mgulani JKT na kituo kilichopo jijini Mwanza.
Kwa umuhimu na ubora wa mashindano BFT inawaomba wale wote ambao wanahitaji kucheza na kujima na wachezaji walioteuliwa awali waende kujiandikisha katika vituo hivyo kwa kuwa watakao ruhusiwa kucheza ni wale tu ambao watakuwa wamepitishwa na makocha wa timu ya taifa waliopo katika vituo hivyo.

Katika mashindano hayo tunategemea kupata ufadhiri kutoka katika mamlaka ya usajiri wa biashara na makampuni (BRELA)
Hali ya mazoezi katika kambi zote inaendelea vizur hadi kufikia leo hakuna majeruhi na katika kituo cha mwenge leo watakuwa na zoezi la kucheza wao kwa wao kwa nia ya kujiimalisha zaidi na kuzoea hali ya mashindano kwa maandalizi ya tarehe 15.

Mako.re Mashaga
KATIBU MKUU
Mob;0713588818

MCHEZO WA POOL UNAZIDI KUPANDA CHATI NCHINI



Mchezaji wa Mchezo wa pool Shafii Namkanda akijitaalisha kupaga mpira wakati wa mazoezi katika klab ya mkunguni Kota za Bandari jijini Dar es salaam leo

FRANCIS CHEKA MADA MAUGO KUGOMBEA UBINGWA WA IBF RAUNDI 12 APRIL 28 PTA SABASABA




Makamu Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) , Madaraka Nyerere (Kushoto) akiwaelekeza mabondia Fransc Cheka kulia na Mada Maugo jinsi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kupigania ubingwa IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Aprilo 28.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

GRAND MALT KUNOGESHA SAUTI ZA BUSARA.



Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt Consolata Adama akizungumza na waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu udhamini wa kinywaji cha Grandmalt kwenye Tamasha la Sauti za Busara litakaloanza Jumatano 08/02/2012 hadi jumapili 12/02/2012 kwenye kiwanya cha Ngome Kongwe Zanzibar.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Toleo la Leo


GRAND MALT KUNOGESHA SAUTI ZA BUSARA.

Dar es Salaam, FEBRUARY 6, 2012:

Kinywaji maarufu cha Grand Malt leo kimethibitisha kukamilisha maandalizi ya kuliongezea raha tamasha la Sauti za Busara linalofanyika Zanzibar kuanzia tarehe 8 hadi tarehe 12 Februari.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa kinywaji cha Grand Malt; Bi Consolata Adam alisema; Sauti za Busara ni tamasha muhimu sana kwa nchi yetu, kwani linatangazwa ulimwengu mzima na hivyo kuvutia watu wa mataifa mbali mbali kuja kushuhudia tamasha hili, hii ni fursa kubwa kwa kutangaza vivutio vya utalii vya nchi yetu. Pia tamasha hili linaleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya muziki hapa nchini, kwa kuwaalika wasanii mbalimbali toka kila kona ya bara la Afrika, hii pia ni fursa kwa wasanii wa nyumbani kujifunza mengi toka kwa wasanii hawa.

Kufuatia umuhimu wa tamasha hili, Grand Malt imekuwa mstari wa mbele kama mmoja wa wadhamini, kuhakikisha kuwa tamasha hili litakuwa na hamasa ya aina yake, tumeweka vikundi ya kutoa burudani katika maeneo mbalimbali ambapo maandamano ya Sauti za Busara yatapita siku ya tarehe 9, ikiwemo viwanja vya Kisonge, ambapo pia wakazi wa Zanzibar watapata nafasi ya kupata kinywaji chao cha Grand Malt bila wasiwasi. Hivyo tunawakaribisha wakazi wa Zanzibar na watu wote watakahudhuria tamasha hili kuja kuburudika na Grand Malt huku tukifurahia burudani za Tamasha la Sauti za Busara 2012. Alisema Consolata.

Aidha alisema Kinywaji cha Grand Malt kitakuwa katika eneo la Ngome kongwe kwa siku zote za tamasha ili kuongeza furusa kwa watu mbalimbali kupata nafasi ya kuburudika na kinywaji kisichokuwa na kilevi na kilichotengenezwa kwa kutumia virutubisho vilivyo bora kabisa cha Grand Malt.

-MWISHO-

Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:

Consolata Adam – Grand Malt Brand Manager, +255767266766, consolata.adam@tz.sabmiller.com

Editha Mushi, Communications & Media Manager, +255767266420, editha.mushi@tz.sabmiller.com

TANGAZO LA DAWA YENYE NGUVU




DAWA YA NGUVU ZA KIUME NA MSIMKO KWA WANAWAKE WASIO NA HAMU YA TENDO LA NDOA AMBAYO HULETA MSISIMKO KWA WANAUME NA WAKE WAKUTANAPO.KWA SASA INAPATIKANA KWA BEI NAFUU HAPA JIJINI DAR ES SALAAM MAKUTANO YA MTAA WA KIPATA NA BARABARA YA MSIMBAZI
ALLY WA YANGA BOMBA UHURU NA MSIMBAZI 0787230551 AU 0652755838


PIGA NO O713827689, 0755074505 , au 0719 541366
,0652755838 UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM

BUGURUNI LOZANA STENDI YA TAX ULIZIA ADAMU KIBANDANI 0755875884

KARIAKOO SHULE YA UHURU STENDI YA MABASI YA TANDIKA ULIZIA ZUNGU MUHUZA TIKETI 0712743870

NA UKIWA ILALA SHARIF SHAMBA FIKA DSJ BANDA NAMBA 14 SIMU 0718718671

NA UKIWA KOTA ZA BANDARI KARIAKOO FIKA MKUNGUNI KIBANDANI KWA HUSEIN 0753893295

MWANANYAMALA FIKA JABA KLABU ULIZA MACHELLAH 0713470492

ENZOY INALETA HESHIMA

MECHI KUPIGWA LEO TAIFA


SHEREHE ZA MAULID YA KUZALIWA BWANA MTUME MUHAMMAD S.A.W



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) akiwa katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume S.A.W zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Zanzibar,(kushoto) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabbi,(wa kwanza kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Othman Makungu,na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji. (05/02/2012) (PICHA NA RAMADHAN OTHMAN IKULU)
Ustadhi Salum Rashid wa Madrsa Qadiria ya Amani akisoma Maulid Barzanji Mlango wa nne,ambao Waislamu husimama na kumswalia Bwana Mtume,S.A.W,wakati wa sherehe za Maulid zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,( katikati wakiitikia Dua katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume S.A.W zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Zanzibar,ikiombwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabbi,(wa pili kushoto)(wa kwanza kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Othman Makungu,na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,Wazri wa Katiba na Sheria Sheikh Abuu Bakar Khamis,(kushoto). (05/02/2012)
Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Pili Balozi Seif,pamoja na viongozi wengine ni miongoni mwa waliohudhuria katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa kwa Bwana Mtume S.A.W. zilizofanyika katika viwanja vya maisara Suleiman Mjini Unguja.
Baadhi ya Waumini wa mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja na viongozi wa Dini wakiwa katika kiwanja cha Maisara Suleiman,katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa kwa Bwana Mtume S.A.W. yaliyofanyika jana.

Thursday, February 2, 2012

Abdalah Mohamed 'Prins Naseem KUTETEA UBINGWA WAKE NA Salehe Mkalekwa .Februari 24



BINGWA wa mkanda wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (PST) Abdalah Mohamed 'Prins Naseem' atapanda ulingoni kutetea mkanda wake wa PST Februari 24 mwaka huu dhidi ya Salehe Mkalekwa.
Pambano hilo la ubingwa wa PST litakuwa ni pambano la uzito wa kg 57 na litashirikisha mapambano mengine manne ya utangulizi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Shaban Adiosi 'Mwayamwaya' alisema pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa New Kibeta uliopo mbagala kuu Dar es Salaam.
Alisema pambano hilo la ubingwa wa PST ni muendelezo wa shirikisho hilo kuendelea kuwainua mabondia chipkizi ambao hawajawa na majina makubwa ili nao waweze kufikia kiwango kizuri cha mchezo huo.

"Ubingwa huu wa PST ni maalum kwa ajili ya mabondia chipkizi na ndio maana mabondia wanaoshirikishwa wengi ni chipkizi na lengo ni kuendeleza vipaji vyao,"alisema Mwayamwaya.

Aliyataja mapambano ya utangulizi yatakayopamba pambano hilo yatakuwa kati ya Shaaban Zungu na Hasan Salehe watakaopigana uzito wa kg 55, Safari Mbeyu na Ibrahim Maokola watakaopigana uzito wa kg 67, Jofrey Pacho atakayetwangana na Seleman Shaaban na Abdalah Yusuph atakayepigana na Omari Kijepa.

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila ‘Super ‘D’.


“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’.

Rashidi MATUMLA VS MANENO OSWARD KUPAMBANA TENA Februar 25 UKUMBI WA PTA SABASABA DAR



BONDIA wa ngumi za kulipwa Rashid Matumla 'Snek man' amesema kukutana ulingoni mara kwa mara na bondia Maneno Osward 'Mtambo wa gongo' hawachezei njaa isipokuwa ni mapenzi ya ngumi aliyokuwa nayo.

Matumla na Maneno wanakutana ulingoni kwa mara ya tano sasa ambapo baadhi ya wadau wamekuwa wakihisi labda mabondia hao hupigana kwa sababu ya kutafuta fedha.

Akizungumza kwa njia ya simu Dar es Salaam jana, Matumla alisema yeye binafsi bado anauwezo wa kupigana katika mchezo huo na kama angetaka kustaafu angeweza kufanya hivyo ila bado anayo nafasi ya kufanya vizuri katika mapambano yake.

Alisema pambano lake dhidi ya Maneno litakalopigwa Februari 25 mwaka huu katika ukumbi wa PTA Sabasaba litakuwa ni pambano lake la tano kukutana na bondia huyo.

"Mimi na Maneno tumeshakutana mara nne ulingoni hadi sasa na hili litakuwa ni pambano letu la tano kupigana,"alisema Matumla na kuongeza kuwa.

"Katika mapambano hayo nimemshinda Maneno mapambano mawili, amenipiga pambano moja na tumetoka sare pambano moja lakini kama itawezekana nitamtwanga katika pambano lijalo,"alisema Matumla.

Alisema kwa sasa anajifua chini ya kocha wake Habibu Kinyogoli ambaye ameingia naye mkataba wa kumnoa na anainami atafanikiwa kumtwanga Maneno katika mchezo huo.

Pambano hilo la Februari 25 litakuwa ni pambano la marudiano kwa mabondia hao baada ya kutoka sare katika pambano la kwanza lililofanyika katika ukumbi wa Henken Mtoni Desemba 25 mwaka jana.

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila ‘Super ‘D’.


“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’.

TIGO YAONGOZA KUWA NA MASHABIKI WENGI FACEBOOK



Ulimwengu uliotawaliwa na mitandao ya kijamii, ni ule unao wasaidia wafanyabiashara kufikia malengo yao. Tigo kwa kulitambua hilo ikafungua ukurasa katika mtandao wa facebook,na kujikuta kwa kipindi kifupi inaibuka kuwa na mashabiki wengi wanaotembelea ukurasa huo kuliko kurasa za makampuni mengine ya simu nchini.

Ukurasa wa Tigo katika face book unatoa habari mbalimbali kuhusu Tigo pamoja na huduma zake, ni sehemu inayowaunganisha mashabiki wa Tigo na kuwawezesha kuchangia mambo na kampeni mbalimbali zinazoanzishwa na Tigo,vilevile mashabiki wanapata fursa ya kujua huduma na bidhaa mpya zinazotolewa na Tigo
“kuhakikisha tunakuwa karibu na wateja wetu katika ukurasa wetu wa face book tunahakikisha wateja wetu wanaendelea kuridhika na huduma zetu” anaelezea Mr. Gonzaga Rugambwa msimamizi wa ukurasa wa Tigo katika face book anaongeza kuwa “face book inatoa nafasi ya kubadilishana mawazo na ndiyo maana tumechagua kuutumia mtandao huu wa kijamii”

Mr. Rugambwa anaendelea kwa kusema kwamba Tigo ina furaha sana kuwa moja ya kampuni inayopendwa sana nchini Tanzania hasa kwenye mitandao ya kijamii,na ana waomba mashabiki wake kuendelea kuwapa ushirikiano na anasisitiza kuwa kujitolea kwao katika ukurasa wa Tigo facebook ndio unaosababisha ukurasa huo kuwa mahali pazuri pa kupata taarifa na kujadiliana.

Kwa kujiunga na ukurasa huo mashabiki wanapata nafasi ya kupewa taarifa za mambo muhimu yanayoendelea, pia mashabiki wana uwezo wa kuwaalika marafiki na jamaa zao kwa kubonyeza sehemu iliyoandikwa ‘share’ pia kwa kutumia upande wa kushoto katika ukurasa wa Tigo mashabiki wanaweza kuangalia video kutoka ‘you tube’,kutembelea mtandao wa ‘ tweeter’ na kupata huduma kwa mteja kwa saa ishirini na nne,ambapo wanaweza kutuma malalamiko na mapendekezo yao na kujibiwa katika muda muafaka.

Ukurasa wa Tigo facebook ni sehemu nzuri ambayo wateja wa Tigo wanapata huduma kwa mteja ya hali ya juu pia ukurasa wa Tigo face book unawapa fursa wateja kutoa dukuduku zao kwa mtandao wao wanaoupenda wa Tigo.

BONGO MOVIES VS WANAMZIKI WA DANSI KUKIPIGA JUMAPILI KUCHANGIA WAATHILIKA WA MAFULIKO


katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Compact Media Company, Eliya Mjatt Timu meneja wa timu ya wanamziki wa dansi, Mwijuma Muhumini 'Kocha wa Dunia' (kushoto) wakizungumza na wahandishi wa habari, Dar es salaam leo kuhusu mechi yao ya hisani na wachekeshaji na waigizaji 'Bongo Movies' kwa ajili ya kuchangia waathilika wa mafuriko, utakaofanyika jumapili katika uwanja wa taifa kulia ni Kocha mchezaji wa timu ya 'Bongo Movies' Chiki Mchoma

BONGO MOVIES VS WANAMZIKI WA DANSI KUKIPIGA JUMAPILI KUCHANGIA WAATHILIKA WA MAFULIKO


katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Compact Media Company, Eliya Mjatt Timu meneja wa timu ya wanamziki wa dansi, Mwijuma Muhumini 'Kocha wa Dunia' (kushoto) wakizungumza na wahandishi wa habari, Dar es salaam leo kuhusu mechi yao ya hisani na wachekeshaji na waigizaji 'Bongo Movies' kwa ajili ya kuchangia waathilika wa mafuriko, utakaofanyika jumapili katika uwanja wa taifa kulia ni Kocha mchezaji wa timu ya 'Bongo Movies' Chiki Mchoma

ZANTEL MAKES NEW APPOINTMENTS
























Ahmed Seif – Commercial Director PMO




Zantel, part of Etisalat Group and the most innovative mobile company in Tanzania in its endeavor to grow local talent has made 2 new appointments as it realigns its Commercial department. The new appointees are Ahmed Seif who is now the Commercial Director/Project Management Office and Sarah Mwigune who becomes the Customer Experience Director. The appointments were effective from January 15, 2012.







Ahmed Mokhles, Zantel Chief Commercial Officer commenting on the appointments said that they are in line with company strategy to realign the commercial department to be headed by qualified and experienced personnel who will be key in growing the business. “Their roles are quite crucial to the business and we are proud that local Tanzanians are taking up the lead in the company to ensure we keep growing not only in terms of business but in nurturing local talents as well.” said Mr. Mokhles.












Sarah Mwigune – Customer Experience Director



Ahmed Seif Holds Bsc in Engineering from the University of Dar es Salaam. I will be dealing with Projects in line with Zantel Commercial strategy in Tanzania. Among the projects which Ahmed was involved in is the East African submarine cable system (EASSy), Epiq Nation, Consortium Fibre Project in Tanzania, Seychelles Submarine Cable system, Zantel Network Rollout and various Zantel commercial products in the market. With a background in technology Ahmed will add value to the commercial team by bring more technological innovation in the Tanzanian Market.




As the new Director of Customer Experience Sarah Mwigune is in responsible for ensuring Zantel customers are satisfied with our services as well as champion marketing initiatives. Prior to her appointment she was in charge of Zantel Retention team a section of customer experience department. She has over 11 years work experience on customer service.









About Zantel:




Zantel is the official brand name for Zanzibar Telecom Limited, the fourth mobile service provider in Tanzania. Zantel is a home-grown Tanzanian company that seeks to positively enhance the lives of all its customers through improved communications. By providing value, high quality and smooth services, Zantel seeks to present customers with service they can rely on whether to conduct business efficiently or simply stay in touch with friends and family.







Zantel offers fixed/wireless services, international traffic and carrier service, data communications service and the Internet, CDMA, IP telephony and VOIP (Voice over Internet Protocol) as well as Value-Added Network Service (VANS).







Zantel was the first private telecom company in Tanzania to own an international gateway that enabled Zantel to reduce the rates for international calls by 60% that paved way for cheaper international calls in the country. It offers the most affordable and competitive international rates in the country to all the popular international destinations in the world and is partnering with more mobile companies to ensure customers roam with Zantel anywhere in the world. Today, Zantel's network covers all cities, major towns, highways and rural areas in Tanzania.

ONYESHO LA LADY IN READ 'RELOADED' 2012 KUCHANGISHA PESA KWA AJILI YA KUJENGA KITUO CHA KUSAIDIA WAATHIRIKA WA MADAWA YA KULEVYA.











Mbunifu wa mavazi mama Asia Idarous Khamsin wa Fabak Fashion ambaye pia ni muandaaji wa onyesho la Lady and Red 'Reloaded ' 2012 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia onyesho linalotarajiwa kufanyika Februari 10, 2011 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.


Meneja wa kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro ambao ni wadhamini wakuu wa onyesho hilo.


Mbunifu wa mavazi mama Asia Idarous Khamsin (wa pili kulia) wa Fabak Fashion ambaye pia ni muandaaji wa onyesho la Lady and Red 'Reloaded ' 2012 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia onyesho linalotarajiwa kufanyika Februari 10, 2011 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bw. Mauldi Mlawa ambaye ni Katibu wa Kikundi cha Kikale Youth Care kilichipo wilayani Rufiji na Meneja wa kinywaji cha Redds Original, Victoria Kimaro ambao ni wadhamini wakuu wa onyesho hilo. Onyesho hilo linatarajiwa kuwakutanisha wabunifu wapatao 30 ambao wataonyesha mavazi yao

SIMBA YAICHAPA JKT OLJORON











Club ya simba imeibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya timu ya JKT Oljoro katika mchezo uliofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam mabao hayo yalifungwa na mchezaji wa simba Emanuel Okwi.
Simba walicheza pungufu baada ya mchezaji Haruna Moshi kutolewa nnje kwa kadi nyekundu

Wednesday, February 1, 2012

FRANCIS CHEKA MADA MAUGO KUGOMBEA UBINGWA WA IBF RAUNDI 12 APRIL 28 PTA SABASABA



Bondia Fransic Cheka akizungumza na waandishi wa habari leo kupigania ubingwa IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Aprilo 28.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Bondia Mada Maugo akiongea na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba uho leokupigania ubingwa IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Aprilo 28.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Makamu mwenyekiti wa Oganaizesheni ya ngumi za Kulipwa Nchini, Madaraka Nyerere (Kushoto) akiwaelekeza mabondia Fransc Cheka kulia na Mada Maugo jinsi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kupigania ubingwa IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba April 28.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Abdallah Mohamed 'Prince Nassime' kugombania ubingwa wa PST na Swaleh Mkalwekwa feb.24


Bondia Abdallah Mohamed 'Prince Nassime' kulia akifuliwa na kocha wake msaidizi Rajabu
Bondia Abdallah Mohamed 'Prince Nassime' kulia akifuliwa na kocha wake msaidizi Rajabu
Bondia Abdallah Mohamed 'Prince Nassime' (kulia) akioneshana ufundi wa kutupa makonde na Jofray Sadiq wakati wa mazoezi ya kujiandaa kugombania ubingwa wa taifa Kg.67 unaotambuliwa na shilikisho la kumi za kulipwa PST na Swaleh Mkalwekwa feb.24