Sunday, March 4, 2012
BANDARI MABINGWA LIGI DARAJA LA PILI NETBOL

NETIBOLI LINDI HOI KWA BANDARI DAR
Mbunge wa viti maalum Merry Mwanjelwa, akiwasalimia wachezaji wa timu ya RAS ya Lindi muda mfupi kabla ya kuanza kwa mpambano wao dhidi ya timu ya Bandari ya Dar es Salaam, hadi blog inatoka uwanjani RAS ilikuwa imeshafungwa magoli 25 kwa 5.
Wachezaji wa Lindi wakimsikiliza Mbunge wa viti maalum Merry Mwanjelwa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kufunga mashindano ya ligi ya Netboli daraja la pili taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa bandari wakiigaragaza timu ya RAS Lindi bila huruma.
Kikosi Kinachotarajiwa kuwa cha timu ya taifa ya Netiboli (rangi ya kijani) wakipimana ubavu na wachezaji wa timu ya Netiboli ya Shule ya Sekondari ya Filbert Bayi (rangi nyekundu) jijini Dar es Salaam. Hata hivyo kikosi hicho kilibugizwa mabao 6-2 na watoto wa Bayi.
Friday, March 2, 2012
WAZIRI WA ELIMU AZINDUA KAMPENI YA TIGO TUCHANGE SAA 5 MPAKA 6 UNACHANGIA ELIMU KWA KUNUNUA TIGO RUSHA KWA MDA HUO
Mheshimiwa
Waziri Shukuru Kawamba,
Wawakilishi
kutoka Hassan Maajar Trust,
Wafanyakazi
wa Tigo,
Ndugu
waandishi wa habari,
Mabibi
na mabwana,
Naomba
mniruhusu kuongea na nyie leo na kiswahili changu ambacho sio kizuri sana,
lakini kwenye hii siku maalum ningependa nijaribu
Nina
furaha kuwakaribisha wote katika siku hii nzuri ya kampeni ya Tigo Tuchange.
Tuna furaha kumkaribisha Waziri wa Elimu na Ufundi Stadi, mheshimiwa Shukuru
Kawambwa kama mgeni rasmi.
Tigo
Tuchange ni moja ya sehemu yetu ya kusaidia jamii nchini Tanzania. Mchango wa
leo unalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi katika shule zenye
upungufu wa vifaa, hivyo kuwawezesha kufanya vyema katika masomo yao.
Kati
ya saa tano asubuhi na saa sita mchana leo, muda wa maongezi utakaonunuliwa
kupitia Tigo Rusha,utaongezwa na Kampuni yetu,
kwa kiwango kile kile na fedha zote zitaingia moja kwa moja kwenye
kampeni.
Tulizindua
Tigo Tuchange mwaka jana,na tulipata mafanikio makubwa kwani tuliweza kukusanya
kiasi cha shilingi milioni ishirini na tano nukta tisa,ambazo zilitumika
kununua vitabu na vifaa vingine katika shule mbalimbali nchini. Mwaka huu
tunatarajia mafanikio zaidi. Hassan Maajar Trust ni moja kati ya watakaofaidika
na kampeni hii,vifaa vingine vya elimu vitatolewa ambavyo vitanufaisha
wanafunzi wa shule za msingi.
Asanteni, na kwa pamoja tufaye mabadiliko yatakayoboresha mazingira ya wanafunzi!
TIGO TUCHANGE KUPITIA TIGO RUSHA SAA 5 HADI SAA 6 LEO
Thursday, March 1, 2012
Homa pambano la komedi wa Dar na Mwanza yapanda, Kingwendu atua mapema
NETBOL LIGI DARAJA LA PILI YAENDEREA KUTIMUA VUMBI VIWANJA VYA KLABU YA SIGARA
Timu ya Bandari ya Dar es salaam wakiwa bkatika picha ya pamoja
Mchezaji wa timu ya Ras Lindi GS,Roza Issa akitafuta mbinu ya kumtoka mchezaji wa timu ya Temeke wD, Ailat John wakati wa mashindano ya taifa ya netbol ligi daraja la pili, Dar es salaam jana Temeke ilishinda bao 21 kwa 18.(Picha na www.burudan.blogspot.com)
SHUKRANI
Ndugu John Hans Badi (PICHANI) ambaye ni mmiliki na Mhariri Mkuu wa Daily Mitikasi Blog, anachukua fursa hii kutoa shukrani za dhati kwa watu wote walioshiriki, kwa namna moja au nyingine katika kumuuguza hadi maziko ya mpendwa Mama yake Mzazi, Esther Nyimbo Badi aliyefariki dunia siku ya Jumatano Feb. 22, 2012 Majira ya Saa 12:30 jioni katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam na baadaye kuzikwa Kijijini Ilembula (W) Njombe, Iringa.Shukrani za pekee ziwaendee Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Aga Khan ambao walikuwa wakipigania ili kuokoa maisha ya mpendwa marehemu Mama yetu bila kuchoka hadi dakika ya mwisho neno la Mungu lilipotimia.
Shukrani pia ziwaendee Familia yote ya Marehemu Dr. Luhangano Joseph Badi ikiongozwa na Dada yetu Mkubwa Mama Blandina Nyoni, shemeji zetu kwa jitihada walizozifanya za kujaribu kuokoa maisha ya Mama yetu.
Pia nawashukuru Wanahabari, Bloggers na wadau wote ambao kwa namna moja ama nyingine walijumuika nami katika kunifariji na kunitia moyo katika kipindi hiki kigumu, ama kwa njia ya simu, E-mails, ana kwa ana.
Si rahisi kumtaja mtu mmoja mmoja ila shukrani pia ziwaendee Mama Mdogo Eliza, Binamu zetu pamoja ndugu jamaa na marafiki.
Sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mungu abariki kila jambo mnalolifanya hapa duniani na hakika mmejiwekea thawabu nyingi kwake. Kwa kuwa kila nafsi itaonja mauti, basi hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kutimiza ahadi yake na tuseme: Yeye (Mama Esther Nyimbo Badi) ni wa Mwenyezimungu na kwake Mungu sote tutarejea!
Mungu ampumzishe Mama Esther Nyimbo Badi Mahala Pema Peponi – Amen!
NHIF YAZINDUA BODABODA KWA AFYA NA CHF MKOANI RUVUMA

WATUMISHI WA SERIKALI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII KISHA KUDAI HAKI ZAO
Watumishi wa serikali ambao ni wanachama wa TUGHE wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza wajibu wao na hatimaye waweze kupata haki ya kudai nyongeza ya maslahi kwa mwajili.
Rai hiyo Imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Tughe Taifa Ally Kiwenge wakati akiongea na watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali hiyo.
Bw Kiwenge alisema ili Wafanyakazi waweze kuwa na sauti ya kudai hali bora ya maslahi kwa mwajili ni budi wao kwanza wakafanya kazi kwa bidii na kuzingatia taratibu.
Alizitaja taratibu kama kuwahi kazini na kuwajibika katika sehemu zao za kazi pia kuacha uzembe,uzururaji na kupiga majungu kuwa ndio nguzo za kuwa na Utendaji mzuri mahala pa kazi
“Watumishi wa serikali tuache maneno ya kejeli na uchochezi na tutumie vikao halali kuwasilisha kero na matatizo yetu kwa mwajili” alisema Bw Kiwenge na kuongeza kuwa kwa watumishi wazembe na wapika maneno sehemu za kazi Tughe haitojishughulisha kuwatetea endapo hatua za kinidhamu zitachukuliwa na waajiri.
Aidha katika hatua nyingine Katibu huyo wa Tughe Taifa amepongeza kitendo cha Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kwa hotuba yake ya mwisho wa mwezi Februari kwa kuonyesha umakini wa kushughulikia kero za watumishi wa sekta ya afya kupitia tume iliyoundwa na Waziri Mkuu kufuatia mgogoro wa madaktari nchini.
Alisema “namshukuru Rais Kikwete kwa kuwahakikishia watumishi wa sekta ya afya nchini kuwa atahakikisha kero za Wafanyakazi kama si kuzimaliza zote basi atasimamia kuona zinapungua “.na kuongeza kuwa Rais akishasema wao viongozi wa vyama vya Wafanyakazi wanafarijika kuona serikali inasikia kilio cha watumishi nchini.
Katika kikao hicho Bw Kiwenge alitaja matatizo makuu manne ambayo serikali inapaswa kuyafanyia kazi kwa kipindi hiki .Kwanza,watumishi wanahitaji nyenzo za kufanyia kazi za kisasa katika hospitali zote nchini ili wananchama wa Tughe watekeleze vema majukumu yao.
Aliongeza na kuiomba serikali na kuishauri ihangaike na kutoa nyenzo za kufanyia kazi kwenye hospitali zote nchini.
Pili,Wafanyakazi wanataka kuwa na majadiliano na viongozi wao ili kuwe na ushirikiano katika kutatua kero zinazojitokeza mahala pa kazi kabla madhara hayajawafika wananchi.
Tatu,amewasihi na kuwaonya watumishi wa serikali kutojiingiza katika siasa.”Kuwa na chama chako na hisia zako ni haki ya mtumishi lakini usilete na kuingiza siasa zako kazini” alisema Kiwenge
Nne,ameitaka serikali ichukue maamuzi magumu ya kuboresha maslahi ya watumishi wake wa sekta ya afya kama kweli inasema sekta hii ni muhimu . “Tughe inaishauri serikali ifanye maamuzi magumu ya kupandisha mishahara ya watumishi ili ikidhi mahitaji ya mwezi mzima ”.
Ameongeza kusisitiza kuwa kiwango cha kima chini i kinacholipwa sasa na serikali cha shilingi laki moja na nusu hakitoshi kumwezesha mtumishi kukidhi mahitaji yake kwa mwezi mzima ambapo kwa wastani mtumishi mwenye familia yenye mke na watoto wanne anaishi kwa shilingi mia nane .
Alisema Tughe inaiomba na kuisisitiza serikali anagalau ihakikishe mtumishi anaishi kwa zaidi ya dola moja yaani shilingi elfu moja na mia sita kwa siku kwani kinyume na hapo watumishi wa serikali wataendela kuishi katika umasikini kinyume na sera ya maisha bora kwa mtanzania.
“Mtumishi yeyote anyeishi chini ya dola moja kwa siku anaishi katika umasikini mkubwa” alisema Bw.Kiwenge na kusisitiza kuwa ni wakati sasa umefika kwa serikali kusikia kilio cha watumishi na kupandisha mishahara kwa kima cha chini hadi shilingi 350,000/=kwa mwezi.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Dkt.Benedict Ngaiza aliwataka viongozi wa Tughe kuwa mfano wa kuigwa kwa kuonyesha njia badala ya wao kuwa walalamikaji kwani hilo likifanyika litaendeleza na kudumisha ushirikiano mahala pa kazi.
Na Revocatus A.Kassimba
Afisa Habari