Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, October 2, 2012

BREAKING NUUUZ; AJALI MBAYA IMETOKEA MUDA SI MREFU ENEO LA MBALIZI MBEYA, MAGARI MAWILI YAGONGANA NA KUWAKA MOTO . WATU KUMI WALIPOTIWA KUFARIKI DUNIA, MBUNGE WA VITI MAALUM MH.MARY MWANJELWA ALIKUWEMO KATIKA AJALI HIYO, KATIBU WAKE ATEKETEA KWA MOTO.





HIVI NDIVYO MAAFA YALIVYO
MKUU WA MKOA WA MBEYA ALIYE VAA SUTI YA BLUE MH. ABASS KANDORO AKIWA ENEO LA AJALI
HIVI NDIVYO HILI GARI LILIVYO UNGUA MOTO BAADA YA AJALI
MAMIA YA WATU WALIOFIKA KUSHUHUDIA AJALI HIYO MBALIZI
HIVI NDIVYO GARI HILI LILIVYO PINDUKA NA KUWAKA MOTO BAADA YA AJALI
HII NI GARI NYENGINE AMBAYO PIA ILIWAKA MOTO BAADA YA KUGONGANA
FIRE WAKIWA WAMEWAHI ENEO LA TUKIO KWA AJILI YA KUZIMA MOTO HUO
ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI WAKIWA WAMEFIKA ENEO LA TUKIO AMBAPO MAGARI HAYO YAMESABABISHA VIFO VYA WATU KUMI.
 
HUU NDIO MUONEKANO WA GARI HILI LIKIWA LIMEUNGUA LOTE
HAYA NI MABAKI YA GARI HILI AMBALO NALO LILIUNGUA LOTE
WANANCHI MBALI MBALI WAKIWA WANASHUHUDIA AJALI HUKU WENGINE WAKIWA WANAENDELEA KUOKOA WALIO PATA AJALI
KIKOSI CHA FFU NAO WALIKUWEPO SAMBAMBA KATIKA KUHAKIKISHA ZOEZI LA UOKOAJI LINAENDA KIKAMILIFU.
PIA KATIKA ENEO HILI MBUNGE WA VITI MAALUM MH.MARY MWANJELWAALIKUWEPO NDANI YA PICK UP ILIYO UNGUWA MOTO, KATIBU WAKE ATEKETEA KWA MOTO HUO.KWA HISANI YA MBEYA YETU BLOG

INDIA YAIKOPESHA TANZANIA Tsh.280Billioni.



Waziri wa fedha na Uchumi Dk.William Mgimwa (kushoto) akibadilishana hati ya mkopo wa Tsh 280Billioni kutoka kwa Meneja wa Benki ya Exim ya India Geeta Poojary (katikati) jijini Dar es Salaam leo kwaajili ya kusaidia usambazaji wa maji kwenye mji wa Chlinze kulia ni Balozi wa India Debnath Shaw

Mohamed Mwikongi 'Frank' na Rose Ndauka wana real promise


WASANII wa Filamu nchini Mohamed Mwikongi 'Frank' na Rose Ndauka wapo mbioni kuachia filamu ya real promise itakayotoka wiki hii akizungumzia filamu hiyo Frank amesema kuwa wapenzi wake wakae mkao wa kula kwani kazi imeshakamilika na sasa wasubili kuiona mtaani

Kazi hiyo itakayokuwa ikisambazwa na Kampuni ya SPLASH ya jijini Dar es salaam itatoka wiki hii ambayo ina mambo mengi ya kujifunza katika filamu hiyo inayozungumzia mapenzi ya kweli

Aidha aliongeza kwa kusema wapenzi wake wamuunge mkono kwa kununua nakara alisi ya filamu hiyo na kuacha uchakahuaji kwa watu wanaonyonya jasho la wasanii kwani wanadumaza maendeleo ya wasani

Filamu hiyo yenye mafundisho mbalimbali itatoka wiki hii kwa ajili wapenzi wapate burudani wakiwa majumbani na kujifunza mambo ya familia

REDDS MISS TANZANIA WAINGIA KAMBINI LEO.



Warembo wa Shindano la Redss Miss Tanzania wakifuatilia maelekezo mbalimbali mara baada ya kuwasili kambini kwenye Hoteli ya Girraffe jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya warembo 30 wameingia kwenye kambi hiyo.    




Kila mmoja akiwa makini kusikiliza maelezo ya maishamapya ya kambini.
Meneja wa Mikutano wa Hoteli ya Giraffe James Philbert akiwafundisha warembo hao namna ya kupiga menyu kwenye mahoteli kama hayo.
Hapa sasa wanapiga menyu.
Warembo wote wakapiga picha ya pamoja.

Tanesco waendelea kukamata wezi wa umeme.



Mafundi na wakaguzi wa mita za shirika la umeme Tanesco Mkoa wa shirika hilo Temeke,  wakikagua moja ya nyumba za eneo la Mtoni Relini Temeke baada ya nyumba hiyo kukutwa na mita mbili huku moja ikiwa haitumiki na hata inayotumika imekutwa ikiwa imeunganishwa umeme kabla haujafika kwenye mita hiyo na kusomwa.
Fundi akionyesha waya zilizounganishwa kuiba umeme kabla hazijafika kwenye mita.
Mkaguzi wa mita wa Shirika la Tanesco Mkoa wa shirika hilo Temeke Abrahamu Kalimile akimuonyesha mteja namna walivyoharibu mita ili waibe umeme mara baada ya kupima pamoja na  kuifungua na kugundua tatizo hilo.
 
 
KAZI ya ukaguzi wa mita za umeme kwa wateja wa Shirika La umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Shirika hilo Temeke iliendelea tena jana na kuwakatia umeme watu watano baada ya kukuta na makosa mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya operesheni ya ukaguzi wa mita hizo uliofanyika jana Mtoni Kwa Azizi Ally eneo la Relini msimamizi wa zoezi hilo Johari Nasibu, alisema jumla ya nyumba 80 walizifanyia ukaguzi.
“Kama tunavyofanya siku zote kwenye zoezi hili leo hii tumefanya hapa mtoni eneo la relini tumefanikiwa kukuta mita nane zikiwa na makosa mbalimbali na hatua za haraka tulizo zichukua ni kuwasitishia huduma kwanza kabla ya kufanya tathmini ya hasara tuliyopata ili waweze kutulipa na kama hawajalipa tunawafikisha mahakamani” alisema Nasibu.
Akifafanua zaidi makosa waliyowakutanayo wateja hao aliyataja kuwa ni pamoja na Wizi kwa njia ya kuharibu mita wateja watano, Kuiba umeme kabla haujafika kwenye mteja mmoja na Kujiunganishia umeme bila ya kufuata taratibu wateja wawili.
Aidha Johari alisema kiasi kikubwa cha umeme kimeibwa na shirika lazima litawachukulia hatua kali za kisheria endapo hawatakubali kulipia umeme walioutumia kwa kipindi chote.

I-VIEW STUDIOS KUSIMAMIA KAZI ZA DIAMOND PLATNUMZ




 Msanii wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ akisaini mkataba na kampuni ya One Touch Solution itakayosimamia kazi za msanii huyo.
JUU: Mkurugenzi wa Kampuni ya I-View Studios, Raqey Mohammed ( kushoto)na msanii Diamond Platnumz wakisaini mkatabawa kufanya kazi pamoja. Wanaoshuhudia ni Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View Dr. Peter Aringo na Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Petter Mwendapole
 
CHINI: Mkurugenzi wa Kampuni ya I-View Studios, Raqey Mohammed akibadilishana mkataba na msanii Diamond Platnumz baada ya kusaini. Wanaoshuhudia ni Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View Dr. Peter Aringo  na Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Petter Mwendapole.


DAR ES SALAAM, Tanzania
MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameingia mkataba na kampuni ya I-View Studios ya ili wasimamie kazi zote kwa muda wa miaka miwili.

Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solution ya mjini Dar es Salaam, Petter Mwendapole amesema I-View itasimamia mikataba yote ya kazi zote za msanii huyo na yeyote atakayetaka kufanya kazi na Diamond kwa sasa itabidi awasiliane I-View.

“Diamond ameamua kufanya kazi zake kimataifa, na ameingia mkataba na I-View ambapo wao ndio watakuwa wakisimamia maonyesho, matangazo, nyimbo kwenye simu, nguo kila kitu ambacho kinahusiana nay eye kinapaswa kupitia I-View,” amesema.

Mwendapole alisema pamoja na maonyesho, lakini I-View pia itawajibika katika muonekano mpya wa msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba ndani na nje ya Tanzania. One Touch Solutions ndio watakuwa wasemaji wa msanii huyo.

Diamond kwa upande wake alisema anataka kufungua ukurasa upya katika tasnia ya muziki nchini na kwa anaamini utasaidia katika kumfanya aongeze nguvu zaidi katika kutunga na kutengeneza nyimbo zake.

“Hii yote ni kuhakikisha nafanya kazi zangu kwa ufanisi badala ya kujirundikia mambo mengi, kuna watu walikuwa wakinitafuta wanashindwa kunipata lakini sasa watakuwa wanafahamu ofisi ziko wapi na wanawasiliana na menejimenti inawapa majibu, watu wa habari watakuwa na mtu wa kuwasiliana nae moja kwa moja hata kama sipatikani,” amesema.

Diamond anatarajia kutoa wimbo wake mpya ambao pia utarekodiwa na kampuni ya I-View. Tayari usaili umeshafanuyika kwa ajili ya wale ambao wataonekana kwenye video hiyo.

I-View mbali na kazi kupiga picha, lakini pia inatengeneza matangazo mbalimbali ya TV, Radio, mabango, ubunifu wa kazi mbalimbali za sanaa.

I-VIEW STUDIOS KUSIMAMIA KAZI ZA DIAMOND PLATNUMZ




 Msanii wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ akisaini mkataba na kampuni ya One Touch Solution itakayosimamia kazi za msanii huyo.
JUU: Mkurugenzi wa Kampuni ya I-View Studios, Raqey Mohammed ( kushoto)na msanii Diamond Platnumz wakisaini mkatabawa kufanya kazi pamoja. Wanaoshuhudia ni Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View Dr. Peter Aringo na Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Petter Mwendapole
 
CHINI: Mkurugenzi wa Kampuni ya I-View Studios, Raqey Mohammed akibadilishana mkataba na msanii Diamond Platnumz baada ya kusaini. Wanaoshuhudia ni Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View Dr. Peter Aringo  na Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Petter Mwendapole.


DAR ES SALAAM, Tanzania
MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameingia mkataba na kampuni ya I-View Studios ya ili wasimamie kazi zote kwa muda wa miaka miwili.

Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solution ya mjini Dar es Salaam, Petter Mwendapole amesema I-View itasimamia mikataba yote ya kazi zote za msanii huyo na yeyote atakayetaka kufanya kazi na Diamond kwa sasa itabidi awasiliane I-View.

“Diamond ameamua kufanya kazi zake kimataifa, na ameingia mkataba na I-View ambapo wao ndio watakuwa wakisimamia maonyesho, matangazo, nyimbo kwenye simu, nguo kila kitu ambacho kinahusiana nay eye kinapaswa kupitia I-View,” amesema.

Mwendapole alisema pamoja na maonyesho, lakini I-View pia itawajibika katika muonekano mpya wa msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba ndani na nje ya Tanzania. One Touch Solutions ndio watakuwa wasemaji wa msanii huyo.

Diamond kwa upande wake alisema anataka kufungua ukurasa upya katika tasnia ya muziki nchini na kwa anaamini utasaidia katika kumfanya aongeze nguvu zaidi katika kutunga na kutengeneza nyimbo zake.

“Hii yote ni kuhakikisha nafanya kazi zangu kwa ufanisi badala ya kujirundikia mambo mengi, kuna watu walikuwa wakinitafuta wanashindwa kunipata lakini sasa watakuwa wanafahamu ofisi ziko wapi na wanawasiliana na menejimenti inawapa majibu, watu wa habari watakuwa na mtu wa kuwasiliana nae moja kwa moja hata kama sipatikani,” amesema.

Diamond anatarajia kutoa wimbo wake mpya ambao pia utarekodiwa na kampuni ya I-View. Tayari usaili umeshafanuyika kwa ajili ya wale ambao wataonekana kwenye video hiyo.

I-View mbali na kazi kupiga picha, lakini pia inatengeneza matangazo mbalimbali ya TV, Radio, mabango, ubunifu wa kazi mbalimbali za sanaa.

MSAANII WA BONGO MOVIE " SINGLE MTAMBALIKE ( RICHIE ) " AMTWANGA MTANGAZAJI WA TBC 1





BAADA ya kumpiga na kumjeruhi Mpigapicha wa Runinga ya Taifa ya TBC1, Moses Friday na kisha kujisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Mabatini, Kijitonyama jijini Dar, mwigizaji Single Mtambalike ‘Richie’  anajutia kitendo hicho ambacho kimemfanya aendelee kusota  rumande

Kwa mujibu wa msanii mmoja aliyeenda kumtembelea Richie kituoni hapo, alitonya kuwa msanii huyo anajutia kitendo alichokifanya baada ya polisi kumzuia rumande mpaka Moses atakapopona.

Hata hivyo, jitihada za baadhi ya wasanii kwenda kwa ndugu wa Moses kumuombea msamaha Richie ziligonga mwamba baada ya familia ya mpigapicha huyo, kukataa msamaha huo kwa madai kwamba hali ya ndugu yao bado hairidhishi.

Wakati huohuo, baadhi ya wafanyakazi wa TBC1, wamekilaani kitendo alichokifanya msanii huyo kwa kumuumiza vibaya Moses kisa kikiwa ni kupigwa picha tu kitu ambacho ni cha kawaida kwa msanii kama yeye.

Habari za uhakika ni kwamba Moses amelazwa katika Hospitali ya Muhimbili na kwa jinsi alivyoumia inabidi aagiziwe ‘pleti’ za kuunganisha taya kutoka nchini Kenya.

UMEZISOMA HIZI?

 Hata hivyo Richie amekuwa na matukio ya kuwapiga watu na kuwaumiza vibaya miezi michache iliyopita alimtandika makonde ya kufa mtu msanii mwenzia ajulikanae kwa jina la Coreta na kuwekwa lupango ata hivyo msanii huyo kwa kitendo chake cha kuingia na kuanza kuwashambilia waandishi wa habari na kumfanyia mazara makubwa sana Mosese wa TBC si cha kiungwana kabisa kwa kuwa yeye ni kioo cha jamii

"NILIOLEWA NA KUACHIKA NDANI YA SIKU NNE.....KWA SASA SIKO TAYARI KUOLEWA TENA".....SKAINA





MIEZI kadhaa baada ya kuvunjika kwa ndoa yake iliyodumu kwa  siku nne, mwanadada  kutoka kiwanda cha filamu za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ ameiambia mpekuzi  kuwa kwa sasa hayupo tayari kuolewa tena kama ilivyokuwa mwanzo bali kuolewa kwake kutachukua muda mrefu.

Skaina alisema hana wazo la kuolewa ila akitokea mwanaume anayejitambua na ambaye anataka kuoa kweli, ataolewa, lakini siyo kama ilivyokuwa mwanzo kwani alipata mchumba kwa muda mfupi na kuolewa  jambo ambalo halikuwa na mafanikio.

KLABU YA KAYUMBA YA ILALA MABINGWA WAPYA WA SAFARI POOL 2012




 Mkurugenzi wa Wizara ya Habari,Utamaduni ,Michezo na Vijana, Leonard Thadeo (wapili kushoto) akimkabidhi Kikombe Nahodha wa Klabu ya Kayumba kutoka Mkoa wa kimichezo wa Ilala, Emmanuel Martin mara baada ya kutwaa ubingwa wa Taifa wa mashindano Safari Pool 2012.

Mabingwa wa Taifa Safari Pool 2012, Klabu ya Kayumba kutoka Mkoa wa kimichezo wa Ilala jijini Dar es Salaam wakishangilia na Kikombe mara baada ya kutwaa ubingwa huo jijini Mwanza juzi.
**************************
Na Mwandishi Wetu,Mwanza.
TIMU ya mchezo wa pool ya Klabu ya Kayumba kutoka mkoa maalum wa kimichezo wa Ilala jijini Dar es salaam, juzi ilitawazwa kuwa mabingwa wapya wa taifa wa  mashindano ya 'Safari Lager National Pool Championship 2012' baada ya kuikung'uta Meeda ya Kinondoni magoli 13-2 katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo.
Fainali hizo za taifa ambazo zilishirikisha jumla ya timu 16 ambazo zilikuwa mabingwa kwenye mikoa yao katika mashindano hayo ngazi ya mikoa, zilifanyikia kwenye ukumbi wa hoteli ya Monarch mkoani hapa na kudhaminiwa na wadhamini wakuu wa mchezo huo nchini, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safri Lager.
Kabla ya mchezo huo wa fainali ambao ulizikutanisha timu za mkoa  wa Dar es salaaam, mashabiki kibao ambao walikuwa wanausubiri kwa hamu kubwa walitegemea kuona upinzani wa hali ya juu lakini hali ilikuwa tofauti baada ya Meeda kukubali kufungwa kirahisi tofauti na mategemeo ya wengi.
Kayumba kwa kutwaa ubingwa huo walizawadiwa fedha taslim Sh.Mil. 5, kikombe kikubwa cha ubingwa huo na medali za dhahabu.
Meeda wenyewe kwa kushika nafasi ya pili waliondoka na fedha taslim Sh.Mil.2.5 , 2eyes ya Arusha iliyoshika nafasi ya tatu ilijinyakulia Sh.1,250,000 na Anatory ya mkoa wa Morogoro iliyoshika nafasi ya nne ilipewa Sh.750,000.
Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume), bingwa wa mkoa wa Mbeya, Solomon Elias ambaye ni bubu alitwaa ubingwa huo wa taifa baada ya kumkandamiza, Athuman Seleman wa Morogoro magoli 5-1 katika mchezo wa fainali na kujinyakulia Sh.500,000.
Athumani Seleman kwa kushika nafasi ya pili ilizawadiwa Sh.250,000, wakati ambapo Fayuu Staniley wa Arusha alipewa Sh.200,000 kwa kushika nafasi ya tatu na Ally Nada wa Manyara aliyeshika nafasi ya nne aliambulia Sh.150,000.
Mkoa wa Mbeya walionekana kujiandaa vizuri kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja baada ya Betty Sanga naye wa mkoa huo kutwaa ubingwa wa taifa wa mashindano hayo baada ya kumchapa Cecilia Kileo wa Kilimanjaro magoli 5-2 katika mchezo wa fainali.
Betty kwa kutwaa ubingwa huo alijinyakulia fedha taslim Sh.350,000, wakati ambapo Cecilia aliyeshika nafasi ya pili aliondoka na Sh.200,000, Sada Tulla wa mkoa wa Shinyanga aliyemaliza fainali hizo akiwa nafasi ya tatu alizawadiwa Sh.150,000 na Anna kutoka mkoa wa Iringa aliyeshika nafasi ya nne alipewa Sh.100,000.
Mbali ya zawadi kwa washindi hao lakini pia timu zote ambazo hazikushika nafasi hizo nne za juu zilizawadiwa fedha taslim kulingana na nafasi zilizoshika pamoja na wachezaji wote wa mchezaji mmoja mmoja ambao nao hawakushika nafasi za juu.
Zawadi zote kwa washindi zilikabidhiwa na Mkurugenzi wa Michezo Tanzania, Leonard Thadeo ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika kilele cha fainali hizo.

THOMAS MASHALI KUKIPIGA NA BONDIA WA UGANDA





Na Mwandishi Wetu


BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali amesaini mkataba wa kucheza pambano la ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati dhidi ya Bondia Medi Sebyala wa Uganda, litakalofanyika Oktoba 14 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Friends Corner.

Akizungumza hivi karibuni, Mratibu wa Pambano hilo linalosimamiwa na Shirikisho la Ngumi za kulipwa TPBO, Regina Gwae amesema mpambano huo ni maandalizi ya kuhakikisha bondia Mashali anavuka mipaka ya Tanzania baada ya kufanya vema nchini.


“Huwezi kwenda nje kama ndani hufanyi vizuri na huwezi kwenda Ulaya, ukaikimbia Afrika Mashariki, hivyo tumeona tumpe pambano Afrika Mashariki ili akifanya vyema aweze kuvuka mipaka hiyo sasa,” alisema Regina.


Aliongeza kuwa, mazungumzo na bondia Sebyala yamekamilika na tayari ameshatumiwa mkataba wake kwa ajili ya pambano hilo ili ausaini baada ya kuupitia.


“Pambano hilo litakuwa na raundi 10 na watacheza katika uzito wa kilo 72 na kama tujuavyo ukizungumzia mabondia wa uzito wa kati wanaotamba nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla, huwezi kuacha kuwataja Mashali na Sebyala,” alisema Regina.


Regina alisema wanataraji mpambano utakuwa mzuri wenye kuvutia kwa kuwa Mashali ni bondia mzuri na Sebyala naye ni mzuri aliyeweka historia ya kuwasumbua mabondia mahiri nchini Fransis Cheka na Rashidi Matumla kwa nyakati Tofauti.


Pia amewaomba wafadhili kujitokeza kudhamini mchezo huo unaotarajiwa kuwa na mapambano kadhaa ya utangulizi yenye kuvutia wakiwemo mabondia chipkizi Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Jonas Segu,  mabondia wengine watakacheza utangulizi  watatangazwa baadaye watakaosindikiza mpambano huo.


 Katika Mchezo huo kutakua na Uhuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.




Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

BFT YAMTAKA PROMOTA WA NGUMI, KAIKE SIRAJU KUWALIPA MABONDIA






Na Elizabeth John
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa (BFT), Makore Mashaga amemtaka Promota wa ngumi za kulipwa nchini, Kaike Siraju kuwalipa mabondia fedha zao kama walivyokubaliana kwa lengo la kuendeleza mchezo huo hapa nchini.
Kaike anadaiwa kuwafanyia kitendo ambacho si cha kiungwana mabondia chipukizi Issa Omar na Mwaite Juma kwa kuwapambanisha Julai 15 mwaka huu kwa makubaliano ya kuwalipa na baadae kutowalipa.
Juni 25 mwaka huu Kaike aliwasainisha mkataba mbele ya Katibu Mkuu wa Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Ibrahim Kamwe kuwa Omar kucheza na Ramadhan Kumbele kwa malipo ya sh. 80,000.

Pia Kaike alifanya hivyo kwa bondia, Juma aliyecheza na Anthony Mathias, ambapo vijana hao walicheza na hawakulipwa na promota huyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mashaga amesema kuwa kwa kufanya hivyo atawakatisha tamaa mabondia wakiwa bado hawajawa na uzoefu katika mchezo huo, hivyo anamshauri awalipe mapema.
Alisema kuwa mambo yaliyofanywa na promota huyo si ya kiungwana ni kuwavunja moyo mabondia chipukizi, kudumaza ngumi na kufanya mchezo wa ngumi uonekane ni mchezo wa wahuni kwa vitendo vya kihuni kama hivi.

MCHEZO WA MASUMBWI, TAA INAYOZIZIMA – SEHEMU YA SITA





Na Onesmo Ngowi

Masumbiwi au kwa majina mwengine ndondi au ngumi na kwa majina ya mitaani ndogwa, mawe n.k. ni mchezo unapoendwa sana na watu wengi. Aidha mchezo huu ni kati ya michezo inayoogopwa sana duniani. Mchezo wa ngumi uko hatarini kupoteza maana yake ya asili yaani kucheza kama burudani, kuwakilisha nchi na kujenga ushupavu wa mchezaji. Mamilioni ya watu wanaojazana kuutazama wasingependa kabisa kujiingiza kuucheza mchezo wa ngumi. Sasa endelea………………………………….!
  
Mabondia wengi na walio mabingwa wa dunia huajiri "cutman" kwa kipindi chote cha maisha yao ya ngumi. Kutokana na umuhimu wa kumhudumia bondia wake vizuri ma-cutman wengi wanalipwa fedha zaidi ya madaktari katika mpambano.
Katika mpambano wa ngumi kuna washika vibao (Card Girls) vinaoonyesha raundi inayofuata. Mara nyingi watu hawa huwa ni wasichana wanamitindo au waliobobea kwenye majukwaa kama wanamuziki, wanamitindo, wacheza shoo n.k. Kila raundi inapoisha mshika kibao huingia kwenye ulingo akitembea kwa maringo na kuonyesha raundi inayofuata.
Mara nyingi mwendo wake husaidiwa na musiki mororo unaopigwa na watazamaji hufuatilia kwa makelele ya furaha. Wapo vile vile washika vibao ambao ni wanaume wanaofanya mazoezi ya kutunisha musuli na haswa mpambano wenyewe unapokuwa ni wa wanawake.
Vile vile kuna mtangazaji (Commentator) ambaye anatakiwa kutangaza mpambano wenyewe. Mtangazaji wa mpambano hutangaza mpambano wenyewe kwa ujumla akianzia na aina ya mpambano, wageni waliohudhuria na mabondia wahusika.
Pengine ni wakati anapotangaza mabondia husika ndipo anapotakiwa kutumia madoido ya hali ya juu kumnadi kila bondia. Kazi yake nyingine ni kutangaza matokeo ya kila mpambano haswa inapozingatiwa kuwa mchezo wa ngumi unajumuisha mapambano mengi madogo madogo (supporting bouts) kabla ya mpambano mkubwa.
Waliotajwa hapo juu ndio wahusika muhimu mbali na promota na meneja kuendesha pambano la ngumi.
MIFUMO YA NGUMI NA MADHARA YAKE KWENYE MAENDELEO YAKE
Mifumo ya ngumi imekuwa inabadilika na wakati, tangu ngumi zilipoanza. Lakini nitaanzia na hapa kwetu Tanzania. Ipo mifano mingi inayoonyesha namna mabondia wetu wa kitanzania walivyo na uwezo mdogo wa maswala ya ngumi. Mfano mmoja ni jinsi Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) ilivyokwisha jitahidi kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha ili kuwawezesha baadhi ya mabondia kushindania tuzo mbalimbali za kimataifa.
Kana kwamba ni kazi ta TPBC kuhakikisha kwamba bondia bingwa wa tuzo hizi kuzitetea, mabondia hawa wanaishia kupoteza mataji yote waliyoyashinda kwa gharama kubwa na juhudi hizi za TPBC bila kuyatetea.
            Baadhi yao wakitumiwa na wababaishaji wachache wanaojiita mameneja feki wanaodiriki hata kuushutumu uongozi wa TPBC kwamba uliuuza mikanda yao ya ubingwa. Kuna usemi wa kiswahili unaosema kwamba “akutukanaye hakuchagulii tusi”. Ni kioja cha hali ya juu tena dhihaka isiyo na upeo kwa mtu kusema kwamba mkanda wake umeuzwa.
Mkanda wa bondia ni mali yake na haiwezekani tu mtu akajitokeza barabarani amevaa mkanda wa ubingwa asiokuwanao. Kufanya hivi ni sawa na mtu kuvaa nguo za askari wa zima moto na kwenda nazo disko.
            Dhihaka kama hizi na nyingine nyingi zilnaufanya uongozi wa TPBC uachane na kujishughulisha na maswala ya kupromoti na kumeneji. Kwa kuwa juhudi zake za kuwasaidia mabondia pale ambapo mapromota na mameneja hawakuwepo zinachukuliwa kama njia mbadala ya kujinufaisha kifedha, iliamua kukoma.
Mikanda ambayo TPBC iliigharamia ili kuhakikishia mabondia wa kitanzania wanayashinda ni pamoja na IBF/Afrika, CBC, ECAPBF na WBU.
            Ni vizuri nieleze tu kwamba bondia anayeshinda mkanda wa ubingwa anatakiwa awe ameutetea katika kipindi kati ya miezi minne na mwaka mmoja (Division ndogo kuanzia Light Fly mpaka Super Light Weight wanatakiwa wawe wametetea katika kipindi cha miezi sita, Kunzia Welterweight mpaka Heavyweight anatakiwa awe ametetea katika kipindi cha mwaka mmoja husuan ubingwa wa dunia). Mashirikisho mengi madogo mbali na IBF, WBA, WBO na WBC hayana sheria ngumu zinazomtaka bondia atetee ubingwa wake katika kipindi hiki kilichotajwa hapo juu.
Hivyo huwapa muda kati ya miezi sita mpaka mwaka mmoja an wakati mwingine bondi anakaa tu na mkanda mpaka atakapojitokeza bondia mwingne anayeutaka.
Lakini mashirikisho kama IBF, WBC, WBO na WBA ni lazima bondia bingwa acheze na bondia anayemfuata kwenye viwango katika kipindi kilichotajwa cha miezi sita kwa ubingwa wa bara (Continental) mpaka mabara (Intercontinental).
            Sheria za mashirikisho haya zimeufanya mchezo wa ngumi kuwa na upinzani wa hali ya juu. Bingwa anapotakiwa kutetea ubingwa na bondia anayemfuata kwenye viwango na kwa muda uliotakiwa kunaufanya mchezo wa ngumi kuwa na upinzani wa hali ya juu.
Bondia anaposhindwa kutetea ubingwa wake katika kipindi hiki hunyanganywa ubingwa na kutangazwa kuwa ubingwa wenyewe uko wazi. Ubingwa uliotangazwa kuwa wazi unawafanya mabondia walio namba moja hadi nne kucheza mapambano ya mtoano (Elimination Titles) ili kuwapata mabondia wawili watakaoshindania ubingwa.
Kwa ajili ya upinzani na malipo mazuri mapambano yote ya mashirikisho haya hutangazwa kwa njia ya tenda (bidding). Mapromota wanatakiwa watume ofa ya fedha watakazolipa mabondia na atakayetoa donge nono ndiye anayeshinda katika tenda ya kupromoti pambano husika.
Kwa wenzetu inakuwa rahisi kwani mifumo yao wa kupromoti ngumi inamruhusu promota kuweza kukubaliana na makampuni mbalimbali ya mitandao ya televisheni itakayomlipa fedha za kupromoti. Anapopiga mahesabu yake na kuona kuwa anazo fedha za kutosha na faida ndipo anapotuma tenda yake. Iaendelea………………………….!
Mwandishi wa makala haya ni; Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Shirkisho la Ngumi za Kulipwa Afrika Mashariki na Kati (ECAPBF), Shirikisho la Ngumi la Kimataifa bara la Afrika, Masharilki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi (IBF/AFRICA) na Mkurugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) E-mail: ibfafrica@yahoo.com

HAPPY BIRTHDAY MDAU ANGELA MSANGI WA TBC 1





 Mwandishi wa TBC Angela Msangi leo anatimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa kwake, SPORTS LADY mwenzako nakutakia kila la heri na afya njema katika maisha yako, AMIN!

 Hapa Angela akiwa na mbunge wa Viti Maalum (CCM), Esther Bulaya
 Angela na Dina 
 Angela na Sports Lady mwenzake, Jane John pia wa TBC hapa wako kikazi zaidi



Enzi hizooooooooooooooooooooooo, Dina na Angela katika kusaka...HHAHAHA, HAPPY BIRTHDAY MAMAA wa K&L MEDIA SOLUTIONS

DAR LIVE ILIVYOBANJUKA JUU NA 'DNA' , WASANII WA BONGO






DNA akiwapagawisha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia leo.
…Akifanya makamuzi ya nguvu.
Dully Sykes akiwapa ‘hi’ mashabiki.
Roma akiwahamasisha mashabiki wake.
Jhikoman alipokuwa akitoa burudani ya Jumapili.

Jike la Simba, Isha Mashauzi, akiwajibika.
DNA akiwasilisha ujumbe kwa mashabiki.
Shadrack Joseph (mwenye suruali nyeusi) akicheza na kundi lake kibao cha marehemu Michael Jackson kiitwacho Thriller.

Rukia Juma ‘Mamaa Mashauzi’ akikamua na kundi la Mashauzi Classic.
Sehemu ya wanamuziki wa Mashauzi Classic wakiwa kazini.
Mkali wa sarakasi, Zungu Tasha, akifanya vitu vyake.
Shabiki ‘aliyeleta za kuleta’ akiondolewa na mabaunsa.
UMATI wa wapenzi wa burudani jana walibanjuka na msanii Denis Kaggia ‘DNA’ kutoka nchini Kenya katika onesho

lililofanyika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam.

Burudani hiyo ilisindikizwa na wasanii mbalimbali wakiwemo mkali wa muziki wa reggae Jhikoman, Kundi la Taarab la

Mashauzi Classic, wanamuziki wa kizazi kipya, Shadrack Joseph, Roma, Dully Sykes na burudani ya sarakasi kutoka mkali wa ishu hizo, Zungu Tasha.

(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL)

AMIR KHAN KUMVAA CARLOS MOLINA DESEMBA




 
 
LONDON, England
 BONDIA Mwingereza Amir Khan anatarajia kurejea ulingoni Desemba mwaka huu, kupigana na Carlos Molina – huku akiwa chini ya ukufunzi wa kocha mpya Virgil Hunter anayemnoa kwa sasa.

Khan, 25, analichukulia pambano hilo kama hatua moja mbele kuelekea mchuano anaouwania wa kupimana ubavu na bondia kama Floyd Mayweather.
 
Bondia huyo mzaliwa wa jiji la Bolton, hivi karibuni alimfukuza kazi mkufunzi wake Freddie Roach, kufuatia kichapo kutoka kwa Danny Garcia Julai mwaka huu, akidai kocha huyo hakuwa na muda wa kutosha kumnoa, kutokana na majukumu mengine.
Mkali huyu kwa sasa yuko kwenye mazoezi makali chini Hunter nje ya ‘gym’ yake huko Hayward, California, tayari kumvaa Molina.
Khan alisema: “Kusema kweli nimeridhishwa mno Virgil kuwa mkufunzi wangu mpya. Kila mmoja miongoni mwa mabondia wanatambua uzoefu, ufundi na mafanikio ya Virgil aliyopata miaka michache iliyopita.
“Naangalia mbele kuanza kambi yangu mpya kwa bidii na kufanya baadhi ya mambo muhimu nikiwa chini yake. Kuwa na Virgil katika kona yangu ulingoni, najua kwamba itanirejesha katika kilele cha ubora wangu katika uzani wa ‘Light-welterweight’.