Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, December 2, 2012

PROFESIONAL KIBAO NDANI YA NDONDO DAR ES SALAAM




Mshambuliaji wa Mpumalanga Adam Kingwande (Anachezea African Lyon)  mwenye mpira akijaribu kumtoka mshambuliaji wa Vuguvugu Husein Kicheche (Anachezea Bandari ya Kenya) kwenye mchezo wa fainali ya mashindano ya jezi uliochezwa juzi uwanja wa Chuo cha Bandari, Vuguvugu ilitwaa kombe baada ya kuifunga Mpumalanga mabao 4-2





Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Tandika wilaya ya Temeke akikabidhi zawadi ya mbuzi nahodha wa timu ya Mpumalanga amabo ni washindi wa pili wa mashindano ya jezi yaliyokuwa yameandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi kata ya Tandika kwenye uwanja wa Chuo cha Bandari, Temeke jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Kimataifa anayechezea Bandari ya Kenya inayoshiriki ligi kuu nchini humo Husein Kicheche jana aliisaidia timu ya mtaani kwake ijulikanayo kama Vuguvugu kutwaa kombe la jezi lililochezwa uwanja wa Chuo cha Bandari.


Mchezo huo ambao ulikuwa wa fainali ya mashindano ya kuwania jezi uliandaliwa na Umoja wa Vijana Kata ya Tandika wilaya ya Temeke na ulizikutanisha timu zaidi ya 30.

Fainali ilichezwa katti ya Vuguvugu na Mpumalanga, mchezo ambao ulivuta hisia za mashabiki kiasi cha kujaza uwanja wa Chuo cha Bandari kutokana na timu zote kuwa na wachezaji wa wanaocheza ligi kuu Bara na Zanzibar.

Timu ya Vuguvugu ambayo ilikuwa ikicheza mchezo wa kasi iliifunga wapinzani wake timu ya Mpumalanga mabao 4-2.

Mabao ya Vuguvugu yalifungwa na Babu Deo dakika ya 8 ya mchezo baada ya kupokea pasi toka kwa Husein Kicheche na la pili lilifungwa na Oseja Said dakika ya 30.


Kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana iliwachukua dakika mbili kuongeza bao la tatu lililofungwa na Kimbu Musa anayechezea Toto African kwa shuti la mbali na karamu ya mabao ilihitishwa na Mponda Nurdin dakika ya 78.

Mpumalanga walipata bao la kwanza kwa njia ya penalti lililofungwa na Adam Kingwande dakika ya 58 na bao pili lilifungwa na Muhaji Kampala dakika ya 82.

Wachezaji wanaochezaji ligi kuu wamekuwa wakichezea timu za mtaani kwa kipindi hiki cha mapumziko.

Baada ya mchezo kumalizika mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Tandika alitoa zawadi ambapo timu ya Vuguvugu walikabidhiwa seti ya jezi na Mpumalanga walipewa zawadi ya mbuzi.

Pia aliwaasa wachezaji kutumia michezo kama ajira hivyo nidhamu ni muhimu ili kufikia malengo yao.
"Mnatakiwa mcheze michezo mkijua ndio ajira yenu hivyo nidhamu ni muhimu ili kufikia malengo mliojiwekea", alisema.

WEMA SEPETU NA DIAMOND PENZI LAO LAFUKUTA UPYAA..!!




 Penzi la Wema sepetu na Diamond platnum inaonekana kushika kasi upya baada ya kuendelea kuwepo kwa ukaribu ambao umezua minong'ono mingi jiji hapa.
 Wema amekuwa msaada mkubwa kwa Diamond kwa vitu mbalimbali na hii imethibishwa na Diamond mwenyewe kuwa kati ya wanawake waliomsaidia kufika hapo alipo ni Wema sepetu.
 Kuthibitisha hayo ni kutokana na muoendelezo wa nyimbo anazozitoa Diamond ambazo zina baadhi ya mistari katika mashairi yaliotungwa na Wema ikiwepo nyimbo ya 'nataka kulewa' ambayo inamtambisha msanii huyo kwa sasa.
 Katika hali ya uperuzi na kudadisikuhusiana na kuwepo kwa mahusiano yanayoendelea kati ya wawili hao kuna asilimia nyingi zaidi zinazoshabikiana na ukweli wa jambo hili ingawa Diamond amekuwa katika mahusiano ya wasichana wengi tofauti lakini ni wazi anamzimia sana Wema kuliko wanawake wote aliowahi kuwa nao katika maisha ya ujana wake.

MNYIKA AIPIGA TAFU MBURAHATI QUEENS




Mbunge wa jimbo la Ubungo, John Mnyika akikabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalmbali vikiwemo, Shuka, Godoro na Chandarua pamoja na fedha taslimu kiasi cha sh. laki saba kwa Makamu Mwenyekiti wa timu ya soka ya Wanawake ya Mburahati Queens, Ridhwan Mkasa kwa ajili ya kuisaidi timu hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake jimbo la Ubungo (Chadema), Hawa Mwaifunga. (Picha na Habari Mseto Blog)  

Na Elizabeth John

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema ) amelitaka Shilikisho la saka Tanzania (TFF) kutoa mchanganuo kwa dola 250 za Marekani zinazotolewa na Shirikisho la soka Duniani (FIFA) kila mwaka kwa ajili ya kuendeleza soka nchini.
Mnyika aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati alipokabidhi msaada wa shilingi milion 1.5  pamoja na godoro moja likijumuishwa kwenye fedha hizo kwa timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Mburahati Queens.
“TFF inaulazima wa kutoa ufafanuzi kuhusu fedha hizo ambazo zinatolewa kwaajili ya kukuza soka la vijana na wanawake, wanatakiwa kuchanganua kwa kiwango ambacho kulitumika kuanzia Juni mwaka jana hadi Juni mwaka huu na matumizi yaliyoanza kutumika Julai yanatakiwa yaelekeze ni kiasi gani kimetengwa kwaajili ya vijana na wanawake,” alisema Mnyika.
Mburahati Queens ilipewa msaada huo baada ya timu hiyo kutembelea bungeni mjini Dodoma kwaajili ya kuhamasisha upatikanaji wa Katiba mpya.
Mnyika alisema shilingi laki tano zilichangwa na wabunge viti maalumu  na kukabidhiwa kwake na Waziri kivuli wa Habari Utamaduni na Michezo Joseph Mbilinyi  ‘Sugu’  katika kikao kilichopita.
Pia baada ya kurudi kutoka bengeni katika kikao kilichopita Mnyika alikusanya michango mingine kwa wadau wengine na michezo na hadi kufikia kiwango kicho.
Mnyika aliuomba uongozi wa timu hiyo kuandaa mchezo mwingine wa kuwahamisisha wananchi wa Jimbo la Ubungo kujitokeza kutoa maoni yao kwa wajumbe wa tume ya kukusanya maoni ya Katiba mpya.
“Kutokana na Kamati ya Katiba kufika katika Jimbo letu mnatakiwa kujitahidi kuandaa mchezo wa kirafiki ili kuhamisisha wananchi kujitokeza katika utoaji wa maoni ya Katiba Mpya,” alisema Mnyika.

MIAKA 20 YA CLUB BILICANAS NA MIAKA 13 YA CLOUDS FM KATIKA PICHA




Bendi ya muziki ya dansi ya Sky Light ikitumbuiza katika sherehe za kutimiza miaka 20 ya Club Bilicanas na miaka 13 ya Clouds FM. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
Sherehe hizo zilipambwa na shamrashamra za aina mbalimabli ikiwemo kukati keki pamoja na kufungua shampeni
Dk. Lilian Mtei akizungumza katika hafla hiyo.
Mwakilishi wa Clouds FM, Wasiwasi Mwabulambo akizungumza katika hafla hiyo
 Tukate keki
 Mmoja kati ya wafanyakazi wa kwanza wakati Bilicanas Club inaanzishwa miaka 20 iliyopita, Monika Victor akimlisha keki, Dk. Lilian Mtei wakati wa hafla ya kutimiza miaka 20 ya klabu hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. 
 Maandalizi ya keki
 Pili Mitemo  ambaye alimwakilisha mumewe aliyekuwa Meneja wa kwanza wa klabu hiyo, ambaye kwa sasa ni marehemu akipokea keki kutoka kwa Dk. Lilian Mbowe kwa ajili ya kuwapa wadau waliojitokeza katika hafla hiyo
 Mzee Ali Ramadhan Mkude nae akuwa mbali katika mnuso wa Bilicanas Club kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa
 Mdau Bi. Agnes Mbowe akillishwa kipande cha keki na Dk. Lilian Mtei.
 DJ Ibrahim Tuwa 'Dj Ibra' akilishwa keki wakati wa hafla hiyo
Dk. Lilian Mtei akimlisha kipande cha keki Meneja Msaidizi wa Vinywaji wa Club Bilicanas, Amandus Agant wakati wa Birthday ya Bilicanas Club kutimiza miaka 20.
 Monica Victor akigawa keki kwa wadau waliofika katika sherehe hizo.
 Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka akiwa na mmiliki wa blog ya Bongoweekend, Khadija Kalili pamoja na wadau wengine. 
Watu wa mataifa mbalimbali wakicheza muziki katika ukumbi wa Bilicanas. 
Na Andrew Chale

WADAU  mbalimbali  wa burudani  usiku  wa kuamkia jana walifurahia kwa pamoja  na kula keki ya miaka 20 ya klabu ya Kimataifa ya Bilicanas na miaka 13, ya Clouds Fm,  iliyoambatana na shamrashamra mbalimbali ndani  na nje ya  ukumbi huo.

Sherehe hizo ziliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bilicanas Group, Dk. Lilian Mtei  ambapo aliwashukuru wadau hao kwa kuwa bega kwa bega na klabu hiyo, tangu 1992. “Tunawashukuru sana kwa kuwa nanyi mara zote inatia faraja kwetu na tutaendelea kutoa huduma bora siku zote|” alisema Mbowe.

Mtei pia aliwashukuru wafanyakazi mbalimbali waliofanikisha ukumbi huo kufikia hapo na kutoa heshima ya kipekee kwa wafanyakazi  waliokuwapo  tokea inaanza hadi ilipofikia miaka 20 na hatimaye  kukata keki hiyo.

“Uwepo wa miaka 20, tuna kila sababu ya kuwapongeza wafanyakazi  tuliokuwa nao toka mwanzo hadi leo, na kwa heshima ya pekee  Mama Victor na Mrs Mitemo  ndiyo watakao kata keki hii” alisema Mtei.

Keki hiyo ilikatwa na wafanyakazi   hao  Monica  Victor   na Pili Mitemo  ambaye alimwakilisha mumewe aliyekuwa Meneja wa kwanza wa klabu hiyo, ambaye kwa sasa ni marehemu.

Aidha, kwa upande  Clouds FM, iliwakilishwa na Wasiwasi Mwabulambo ambaye alipongeza klabu Bilicanas kwa kuwa mstari wa mbele katika kuinua sanaa nchini hasa kwa kuwasaidia wasaidia wasanii kufikia malengo yao.

Kwa upande wake  Ibrahim Tuwa ‘Dj Ibra’ aliyekuwa akisherehesha  shughuli hiyo, aliwaomba wadau kuendelea kuwaunga mkono na wataendelea na huduma bora zaidi ha hapo. Dj Ibra alijiunga na Bilicanas tokea 2002,ambapo mpaka sasa ana miaka 10 kwenye klabu hiyo  iliyowahi kuwa na madj maarufu waliopita  hapo ambao wengi wao wapo kwenye vituo vya televisheni na redio.

JUMUIYA YA WAZAZI KURUDISHA MALI ZAKE ZILIZOVAMIWA KINYUME CHA SHERIA





DAR ES SALAAM, Tanzania

JUMUIYA ya Wazazi nchini imesema itahakikisha inarudisha mali zake zote zilizovamiwa kinyume cha sheria ikiwemo Shule ya Kaole ambayo ni ya kihistoria kati ya nchi ya Msumbiji na Tanzania.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo alisema huo ni mkakati wa uongozi mpya uliyoingia madarakani hivi karibuni.
Alisema kitendo alichofanya Mkurugenzi wa shule za Green Acle, Julian Bujugo hakikubaliki kwani kimevunja mikatiba ya nchi mbili ya kulifanya eneo hilo kuendelea kuwa la kumbukumbu ya wapigania uhuru wa nchi ya Msumbiji.
“Haitafika Januari mwaka ujao Shule ya Kaole itakuwa imeisharudishwa mikononi mwa Jumuiya kwani shule ile ni ya nchi mbili naitaendelea kuwa ya kumbkumbu ya FLELIMO”alisema Bulembo.
Bulembo alisema eneo la Kaole haliwezi kuuzwa na kumilikiwa na watu wengine na baadala yake litabaki kuwa la watu wa msumbiji kutokana na ukweli kwamba kuna makaburi ya ndugu zaao ambapo hutembelea eneo hilo mara kwa mara.
“Tumemuita Bujugo kesho tukutane naye na kumjulisha kuwa alichofanya ni ukiukaji wa sheria hivyo anapaswa kuanza mchakato wa kukabidhi shule hiyo haraka kwa jumuiya”alisema.
Akifafanua zaidi, Bulembo alisema Jumuiya hiyo ilikumbwa na matatizo mengi hapo awali kutokana na baadhi ya watendaji kutokuwa waaminifu kuuza baadhi ya mali.
Alisema baada ya uongozi mpya kuyabaini hayo, inawatahadharisha wale wote waliyovamia mali za jumuiya hiyo kutambua kuwa wakati umefika kwa kuzirudisha hata kama ni kwa fidia kidogo watakayopewa na Jumuiya kinyume chake watawaburuza mahakamani.
Akizungumzaia maendeleo ya shule za jumuiya hiyo, Bulembo alisema zipo shule 71 ambapo kati hizo, 53 zimekuwa zikifanya vizuri kitaaluma.
Alisema kutokana na hali hiyo wamefikia muafaka na Kamati ya Shule hizo kuanza mchakato wa kuzibadili zile 18 ambazo hazifanyi fizuri  kuwa za ufundi (VETA), ambapo alisema Veta yao itakuwa tofauti kwani itapokea vijana wengi wanaomaliza darasa la saba na siyo kidato cha nne, kwani kundi hilo linasahaulika pindi liingiapo mitaani.
“Niwatowe wasiwasi wazazi wenzangu kuwa Jumuiya haina mpango wa kuuza baadhi ya shule zake zinazofanya vibaya bali mpango wetu ni kuziimalisha kiufundi ili ziweze kupokea kundi hilo la watoto wetu wanaomaliza elimu ya msingi” alisema Bulembo
Vilevile alisema kuwa hivi sasa shule zao siyo za huduma tena bali zitakuwa za kibiashara kama nyingine kwa sababu sera zilizoanzisha shule hizo awali zimepitwa na wakati.

WAMA YATOA MSAADA WA BOTI NA VIFAA VYA UVUVI KWA KIKUNDI CHA VIJANA MANISPAA YA LINDI





Boti ya Kikundi cha  Mwambao Fishing group iliyopewa jina la” Nani Kama Mama” wakati wa uzinduzi jana  ikiondoka katika bandari ya Lindi tayari kwa kazi ya uvuvi (Picha na Freddy Maro)


 Mke Wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa msaada vifaa vya kwa wawakilishi wa kinduchi cha Mwambao Fishing Group katika bandari ya Lindi jana jioni.
 Mke Wa Rais Mama Salma Kikwete na viongozi wengine pamoja na wawakilishi wa kikundi cha Mwambao Fishing group waki vuta kamba kuzindua rasmi Boti ya kikundi hicho jana wakati wa sherehe za makabidhiano yaliyofanyika katika bandari ya Lindi jana jioni
Na Freddy Maro, Lindi
 Vijana kikundi cha Mwambao Fishing Group  wa Mji ya Lindi wamemshukuru mke Rais mama Salma Kikwete baada ya kuwakabidhi Boti ya Uvuvi na vifa vyake katika hafla fupi iliyofanyika katika bandari ya Lindi jana jioni.

Akisoma risala kwa niaba ya wanachama wa kikundi hicho, Katibu Msadizi wa kikundi Bwana Jackson John Mnenje alitoa ahadi ya kutunza boti hiyo na na kuvitumia kwa malengo  waliyojiwekea ikiwamo kununua boti nyingine baada ya mwaka mmoja kutokana na faida itakayo tokana na biashara za uvuvi.
“Juhudi alizofanya Mama Salma, zinaonyesha jinsi anavyoguswa na hali ngumu ya maisha ya Watanzania na dhamira aliyonayo ya kutukwamua kutoka katika hali hii.Tunamshukuru Mungu kwani leo sisi tumebahatika na kujiunga na Watanzania wengi wanaofaidika na juhudi zake za kuboresha maisha ya Watanzania,” wanakikundi hao walisema katika risala hiyo.

Kutokana na bei kubwa ya vifaa hivyo, vijana hao wamesema kati ka risala yao kuwa, wasingeweza kamwe kununua vifaa hivyo bila msaada huo uliotolewa na Mama Salma Kikwete na kwamba utakuwa kichocheo kikubwa  cha kukabiliana na na changamoto  za maisha zinazowakabili.

Akizungumza kabla ya kukabidhi Msaada huo,mke wa Rais Mama Salma Kikwete alisema msaada huo ni utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2010 na 2015 inayolenga kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuongeza kuwa ilani hiyo imetambua kuwa uvuvi ni moja ya sekta za uchumi ambazo hazijapatiwa msukumo wa kutosha.

“Kuongeza ufanisi na tija na kubadili maisha ya wavuvi ni moja ya Mapinduzi yanayolengwa katika ilani ya CCM ya 2010 -2015 na mpango uliopo ni wa kuimarisha ushirika wa makundi ya ujasiriamali ikiwa ni njia moja kubwa ya kuwawezesha  wananchi  wa kawaida kumiliki na kuendesha uchumi,” alisema Mama Salma.

Mama Salma amesema kuwa Taasisi anayoingoza ya Wanawake na Maendeleo WAMA itaendelea kuwasaidi wananchi katika maeneo yao ya kujenga ushirika ulio imara na unaojitegemea kiuchumi na unaoendeshwa na wao wenyewe katika misingi wa uwazi na uwajibikaji.

Mama Kikwete amesema pia kuwa WAMA  inalo jukumu la kuhamasisha na kutoa msaada wa hali na mali kwa wananchi na kuwawezesha kufikia malengo wali yojiwekea kwa kuwapatia nyenzo na vifaa mbalimbali,lakini wajibu wa kujiendeleza na kujisimamia unabakia  wa watu wenyewe.

Mke wa Rais amewahimiza wanachama wa Mwambao Fishing group kujenga mshikamano ili kikundi hicho kipate utulivu utakao wapa fursa ya kupanga mipango ya kujenga na kuimarisha kikundi na kufanya kazi kwa uwazi,kuaminiana na kupeana moyo.

Kikundi cha Mwambao Fishing Group chanye wanachama  25 kilianzishwa mwaka huu katika manispaa ya Lindi kutokana na ushari wa Mama Salma Kikwete aliyewashaur i vijana hao kuunda kikundi na kubuni mradi wa maendeleo utakao wasaidia  kuboresha masiha yao

MPIGA PICHA MKUU TANZANIA DAIMA AACHANA NA UKAPERA


  


Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga akiwa na mke wake, Fridah Mockray wakati wa ibada ya ndoa takatifu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Sinza jijini Dar es Salaam jioni hii. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
 Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga akiwa katika pozi na mke wake, Fridah Mockray mara baada ya kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki Sinza jijini Dar es Salaam jioni hii. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga akipongezwa na mama yake mzazi
Pozi la harusi
Picha ya pamoja
Maharusi wakitoka Kanisani
Matron akisaini cheti

UZINDUZI WA ALBAM YA MASHUJAA LEADERS CLUB ILIVYOJILI





 Wanenguaji wa Mashujaa Band, wakikamua jukwaani wakati wa shoo ya ufunguzi wa uzinduzi wa albam yao, ambao shoo hii waliicheza jukwaani bila kumalizika kutokana na matatizo ya umeme.
 'Mkaanga Chips' wa Mashujaa, akizicharaza Drams.
 Wanamuziki wa Bendi ya Mashujaa wakiingia kwa staili yao ya kucheza muziki wa Kihindi, wakati wa shoo yao ya pamoja, ambayo hata hivyo haikuweza kumalizika.
 Wanenguaji wa Mashujaa, wakikamua jukwaani..
 Makamuzi yakiendelea..
 Shoo ilikuwa ni tamu kwa kweli, lakini haikuwa na raha kutokana na karaha ya umeme.
 Mpiga Tumba wa bendi hiyo, MCD, akizicharaza tumba....
 Sehemu ya mashabiki wa VIP waliolipa kiingilio cha Sh. 100, 000 kila mmoja, wakiwa katika eneo lao la VIP.