Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, June 15, 2013

WAFANYAKAZI WA BARCLAYS WAWAFARIJI WATOTO WALIOLAZWA-MUHIMBILI



 Wafanyakazi wa Benki ya Barclays wakitoa msaada wa vitu ,mbalimbali katika wodi ya watoto Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, vikiwemo sabuni, vyandaru, miswaki, vinywaji baridi pamoja na dawa za meno, vitu hivyo vimetokana na michango ya wafanyakazi wanawake wa benki hiyo.
 Mwanasheria wa Benki ya Barclays, Farija Ghilas akimkabidhi sehemu ya msaada waliotoa kwa watoto waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, Sakina Hassani. Vitu hivyo vimetokana na michango ya wafanyakazi wanawake wanaofanyakazi katika benki hivyo. 
 Rahma Said mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam akipokea sehemu ya msaada uliotolewa na wafanyakazi wanawake wa benki ya Barclays wakati walipofika kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika wodi ya watoto katika hospitali ta Taifa Muhimbili. Vitu vilivyokabidhiwa leo ni pamoja na sabuni, vyandaru, miswaki, vinywaji baridi pamoja na dawa za meno, vitu hivyo vimetokana na michango ya wafanyakazi wanawake wa benki hiyo.
 Mwanasheria wa Benki ya Barclays, Farija Ghilas akimkabidhi sehemu ya msaada waliotoa kwa watoto waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam jana, Sakina Hassani. Vitu vimetokana na michango ya wafanyakazi wanawake wanaofanyakazi katika benki hivyo. 
Ahsante kwa zawadi.
 Poa zawadi ya mafuta mama.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays, Neema Sengo akizungumza na waandishi wa habari baada kutembelea wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam na kwafariji watoto walolazwa katika wodi hiyo na kuwabidhi vitu mbalimbali vikiwemo sabuni, miswaki, vyandarua, mafuta, pamoja na vinywaji baridi kwa watoto waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam,

SHOO YA 'KIJANJA YA THE FINEST' MWANA FA YAWAPAGAWISHA MAKAMBA NA ZITTO UKUMBINI


Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma Mwana FA na Linah, wakiimba kwa pamoja jukwaani, wakati wa shoo yake ya 'The Finest' iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana usiku. Katika onyesho hilo lilihudhuliwa na baadhi ya Viongozi wa vyama vya Siasa pamoja na wasomi kibao kutoka Vyuo mbalimbali. Miongoni mwa wanasiasa walioonekana kwa haraka haraka ukumbini hapo ni pamoja na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, aliyeketi na kuparty pamoja na Mbune wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
********************************
Halima Kambi, Dar
KATIKA Shoo hiyo ya 'Kijanja' pia ilihudhuliwa na wasomi kibao huku baadhi ya wabunge kama Zitto Kabwe na January Makamba wakiwa ni miongoni mwa mashabiki wajanja waliohudhuria katika shoo hiyo ya "kijanja" ya The Finest Kama Zamani iliyofanyika  katika Ukumbi Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam, jana usiku.

Mwana FA, pia alisindikizwa na na baadhi ya wasanii kama, Ben Paul, Linah, Maua, Dully Sykes na wengine kibao pamoja na bendi ya Njenje

Kiukweli show ilifana sana kutokana na utaratibu na mpangilio na maandalizi ya shoo yenyewe na MwanaFA aliweza kufanya yake jukwaani na kuwapagawisha mashabiki wake katika usiku ule.

Kutoka (kulia) ni Mbune wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, akiwa na Mbunge wa Bumbuli (CCM) January Makamba, wakiwa ni miongoni mwa mashabiki wa Mwana FA, waliohudhulia shoo hiyo. Kushoto ni Mtangazaji wa Clouds FM, Gerald Hando.
 Mwana FA, akishambulia jukwaa kwa mistari ya kina.....
 Sehemu ya warembo mashabiki wa Mwana FA, wakijitahidi kunasa matukio kupitia simu zao za mkononi.

SHEREHE YA UWT KWA CHAMA CHA UKOMBOZI CHA PALESTINA (PLO) ZAFANA DAR




 Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza wakati sherehe maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (Wapili kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
 Mamia ya wanachama wapya wa CCM ambao wengi wao ni vijana, wakiwa katika picha ya p0amoja na viongozi baada ya kupewa kadi zao katika sherehe maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (Wapili kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
 Kinamama wakimwayamwaya wakati wa sherehe hiyo
 Wengine wakigaragara chini kwa furaha wakati wa sherehe hiyo
 Kikundi cha Vijana wa CCM cha Ilala wakionyesha umahiri wao wa kuchgeza sarakasi wakati wa sherehe hiyo
 Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi akimwekeza jambo, Mwenyekiti wake, Sophia Simba wakati wa sherehe hiyo

Watatu wafa wa bomu mkutano wa CHADEMA






Uwanja wa Soweto ambapo Mkutano wa Chadema kufunga kampeni za kuwania Udiwani Kata ya Kaloleni Jijini Arusha ulikuwa unafanyika umegeuka kuwa uwanja wa vilio baada ya kinachodhaniwa kuwa bomu kulipuka na kuua watu watatu na zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya huku baadhi yao wakiwa wamevunjika miguu.
Katika Mkutano huo walikuwapo pia Mwenyekiti wa Chadema na  Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema sambamba na viongozi wengine wa Chadema Mkoa wa Arusha lakini bahati nzuri Mbowe na Lema   hawakudhurika moja kwa moja na mlipuko huo.

Mlipuko huo ulitokea mbele ya gari ambalo lilikuwa ni jukwaa la matangazo mara  tu baada ya Mh Mbowe, Lema na viongozi wote waliokuwa jukwaa kuu kushuka chini na kujichanganya katikati ya watu wakikusanya michango ya watu, hali inayoashiria mrushaji huenda alilenga kuwajeruhi viongozi hao.

Miili ya marehemu na majeruhi walipelekwa hospitali ya Mt Meru lakini hawakupokelewa baada ya kilichoelezwa ni vurumai iliiyoletwa na mamia ya wafuasi wa Chadema waliokuwa na hasira baada ya wenzao kuuawa.

Hali ikiwa bado tete viwanjani hapo, magari kadhaa ya askari polisi yalifika huku askari wakiwa na silaha lakini walilazimika kupiga mabomu ya machozi kadhaa hewani na kisha kuondoka kutokana na baadhi ya wananchi waliokuwa na hasira kuwafuata na kupaza sauti wakitaka wawaue pia.

Kijana mmoja muuza machungwa aliieleza blogu hii kuwa aliyerusha bomu hilo alitokea upande wa nyuma ya jukwaa kuu na baadae kukimbilia nyumba zilizo jirani.
DSC07403
Mbowe - SowetoMwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe akiwasili viwanja vya Soweto, Kata ya Kaloleni Jijini Arusha jioni ya leo katika Mkutano wa Chadema kufunga kampeni zake.
DSC07401Mh Mbowe akichangisha pesa mkutanoni hapo sekunde chache kabla ya mlipuko kutokea
DSC07413Hali ilivyokuwa baada ya mlipuko ulioua na kujeruhi vibaya
DSC07407Hali za majeruhi na marehemu wakiwa chini kabla ya kukimbizwa hospitalini
DSC07408
:

Tamasha la Usiku wa Matumaini lanoga hawa kuzichapa Taifa



Ray atakayezipiga na Mhe. Zitto Kabwe
Mhe Zitto Kabwe atakayepigana na Ray

Mhe. Idd Azam atakayepigana na JB
JB Mpinzani wa Mbunge Idd Azan

Mhe Halima Mdee atakayepimana ubavu na Wolper
Wolper atakayechapana na Mhe. Mdee

Mhe Esther Bulaya
Aunty Ezekiel

KATIKA kunogesha Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalofanyika Julai 7 kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano watapanda ulingoni kuzichapa na wasanii wa Bongo Movie.
Kwa mujibu wa Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO) Yasin Abdallah 'Ustaadh' siku hiyo Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe atapanda ulingoni ili kuonyeshana kazi na Vincent Kigosi 'Ray' katika pambano la raundi nne.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azan yeye  ataonyeshana kazi na Jacob Stephen 'JB'. wakati Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Jacklyne Wolper wenyewe watapimana ubavu, kabla ya Ester Bulaya kuchapana na Aunty Ezekiel michezo yote hiyo pia ikiwa ya raundi nne.
Ustaadh, alisema katika kuhakikisha mabondia hao hawaumizani ulingoni watavishwa vifaa maalum vya kukinga vichwa vyao ili wasipate majeraha kichwani.
Rais huyo wa TPBO alisema mara baada ya mapambano hayo ya utangulizi, itashuhudiwa michezo miwili ya kimataifa kati ya mabondia Thomas Mashali na Francis Miyeyusho kuzichapa na Wakenya Patrick Amote na Shadrack Machanje.
Pia maboindia Ramadhani Mkundi atapanda ulingoni pia kupigana na Martin Richard, huku pia ikitarajiwa kuwepo kwa burudani mbalimbali za muziki na mchezo wa soka kati ya wabunge mashabiki wa Simba dhidi ya wale wenzao wa Yanga na Bongo Fleva kuumana na Bongofleva.
Ustaadh alisema michedzo hiyo iliyoandaliwa na Global Publishers ni maalum kwa ajili ya kuchanisha fedha za ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike na kutoa wito wadhamini na watu mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuchangia na pia kuhudhuria tamasha hilo.

Hivi ndivo Jide 'Anaconda' alivyofunika Dar usiku



Mwanadada Judith Mbibo aka Lady Jaydee usiku wa kuamkia Jumamosi ya June 15 amefanikiwa kuweka historia kwenye muziki wa Tanzania kwa kulijaza eneo zima la Nyumbani Lounge alipokuwa akifanya show yake ya kuadhimisha miaka 13 tangu aanze muziki. 
DSC_4275

Katika show hiyo, Lady Jaydee amesindikizwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Juma Nature, Sugu, Profesa Jay, Wakazi, Grace Matata na wengine. Pia Jaydee ameitumia siku hiyo kuzindua albam yake mpya, Nothing But The Truth na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. Hizi ni picha za show hiyo.

Umati wa watu unaoshuhudia show ya Lady J Dee sasa hivi hapa Nyumbani Longe.

Lady J Dee anatoa burudani ya kutosha kwa mashabiki.

Professa Jay akiwa back stage anajiandaa kupanda jukwaani kutoa burudani nzuri kwa mashabiki
 

Miaka 13 ya Lady j Dee#sasa hivi ndiyo Mh.Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu ameingia

Lady J Dee anatoa burudani ya kutosha kwa mashabiki.

Lady J Dee anatoa burudani ya kutosha kwa mashabiki.

Team Times Fm 100.5 (Dj Jors Bless,Ndimbo na Mariam)

Sugu na Mkoloni wanatoa burudani kali kwa mashabiki.

Mama mzazi wa Lady J Dee naye amekuja kushuhudia show ya mwanae.

Juma Nature anatoa burudani kwa mashabiki

Sugu akitoa burudani kali kwa mashabiki
M 2 The P akiongea machache baada ya kukaribishwa kwenye jukwaa na Juma Nature