Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, August 5, 2013

VIONJO MWEZI MTUKUFU' Mohammad Ali, bondia aliyhesilimu na kutumia ngumi kufikisha ujumbe wa Uisilamu duniani. “Hii ni kazi tu kama nyasi zinavyoota, ndege wanapaa, mawimbi yanagonga mchanga, na mimi napiga watu”.




Akimchakaza mpinzaniwake.
Alizaliwa kama Cassius Marcellus Clay (mdogo) 17 Januari 1942 huko Kentucky. Baada ya kumpiga Sonny Liston na kutawazwa bingwa wa ngumi za uzito wa juu duniani mwaka 1964, clay alitangaza kukubali mafundisho ya dini iliyokuwa ikijulikana kama Nation of Islam, moja ya makundi potofu linalojinasibisha na Uislamu. Alibadili jina lake na kuwa Muhammad Ali. Alisema: “Muhammad Ali ni jina la mtu huru, likimaanisha kipenzi wa Mwenyezi Mungu, nawaomba watu walitumie hili jina popote watakapotaka kuzungumza namimi au kunizungumzia mimi.” Akaamua kubeba lawama kwa uamuzi wake Marekani nzima sanjari na hilo aligoma kujiunga katika jeshi la Marekani katika vita dhidi ya Vietnam. Muhammad Ali hakuitii serikali ya Marekani na alitengwa na jamii za Marekani. Ni muislam mweusi na mpingaji mwenye bidii ambaye atakumbukwa daima kama shujaa wa kupinga vita baada ya kufungiwa kushiriki katika michezo kwa miaka mitatu na nusu kutokana na kukataa kwake kushiriki katika vita. Akielezea kukataa kwake kusimikwa katika jeshi alisema:
“Kwanini nivae gwanda na kusafiri umbali wa zaidi maili 10,000 kutoka nyumbani kwenda kuangusha mabomu na risasi kwa Wavietnam na wakati kwa wale wanaooitwa Wanegro (weusi wa Marekani) kule Lousville wanatendwa kama mbwa na kunyimwa haki zao za kibinadam? Hapana, sitaweza kwenda kokote kusaidia mauaji na kuchoma nyumba za taifa masikini ili kuendeleza ubabe wa hawa mabwana wa watumwa kwa watu weusi dunia nzima. Leo ndio ile siku wa ouvu kama huu kumalizwa. Nimeonywa kwa kufanya hivi naweza poteza mamilioni ya dola lakini ndio nishasema mara ya kwanza na sasa naweza kurudia kwa mara nyengine; maadui wa ukweli wa watu wapo hapa hapa. Sitaiabisha dini yangu, watu wangu na mimi mwenyewe kwa kutumika kutumikisha wale wanaoililia haki yao, uhuru na usawa…Kama ningeona vita hivyo vitaleta uhuru na usawa wa wenzangu milioni 22 hata kusingehitajika shida ya kunitia katika jeshi ningegombea mwenyewe kuungana nao. Sina cha kupoteza kwa kusimama katika imani yangu. Nikipelekwa jela halafu ndio nini?! Tumeshafungwa jela kwa miaka 400.”
Alhamdulillah!
Kwa kweli alipata tabu baada ya hapo kwani alihukumiwa kwenda jela miaka mitano japokuwa alikaa nje kwa dhamana. Pasipoti yake ikafungiwa na Shirika la Ndondi Duniani (World Boxing Association) likamnyang’anya taji la ubingwa na kumsimamisha kupigana kwa muda… na akaweza kutoshiriki katika mapambano yoyote kwa miaka mitatu na nusu kisa ni kuwa na msimamo wa kufata imani yake tu. Maneno ya Ali kwenye gazeti la Sports Illustrated katika wakati huu wa tabu yalikuwa, “Naachia ubingwa wangu, utajiri wangu na hata mustakabali wangu wa maisha ya siku zangu za usoni. Watu wengi mashuhuri walijaribiwa na mitihani kutokana na imani zao za kidini. Naamini nikifaulu mtihani huu nitatoka upya nikiwa mwenye nguvu na jasiri zaidi.” Kukataa kwake kwenda Vietnam kulizagaa katika kurasa za mbele katika magazeti yote duniani. Na mtetezi wakupinga vita mmoja aitwaye, Daniel Berrrigan alisema:
“Umekuwa msukumo mkubwa kwetu sisi katika harakati zetu za kupinga vita…katika uhamisho wake Ali alisema: “Nategemea kwenda mbali kusaidia kuweka watu huru huko Vietnam na wakati huohuo wenzangu hapa [Wamerika Weusi] wanafanyiwa unyama, inauma kweli. Ni bora niwape habari wote wanaodhani nimepoteza mengi, ukweli ni kuwa nimeingiza vingi zaidi. Nina amani moyoni, na dhamiri iliyowazi. Huwa ninaamka nikiwa na furaha na ninapokiendea kitanda huwa na uso wa bashasha na hata kama wakinifunga, basi nitakwenda gerezani huku nikiwa na furaha pia.”
Katika miaka ya kati  ya 1970, alianza kuisoma Qur’an vizuri na ilipofika mwaka 1975, aliingia kuwa Muislamu wa Kisunni, itikadi sahihi ya kiislamu. Imani yake ya mwanzo kutoka katika mafundisho ya Elijah Muhammad (kama wazungu ni ‘mashetani’ na hakuna pepo wala moto) vyote vikabadilishwa na sasa kweli alijitayarisha kwa ajili ya maisha yake ya akhera. Mwaka 1984, Ali alizungumza hadharani dhidi ya itikadi za kujitenga za Louis Farrakhan, alisema, “Anachofundisha hakiendani kabisa na tunayoamini. Anafundisha njia za kufanya harakati za wakati ule wa kiza, hatutaki kuungana na itikadi hizo hata kidogo.”
Malcolm X alikuwa na mchango mkubwa katika maisha ya huyu bingwa wa uzito wa juu duniani mara tatu katika ndondi. Muhammad Ali aliiambia Young Muslim kuwa Malcolm X alikuwa, “…mzungumzaji mzuri, alikuwa sio muoga. Alinisaidia mimi kuingia katika Uislamu.” Kiufupi Muhammad Ali aliopoa mwongozo na ushauri kutoka Malcolm X ambaye alikuwa akikutana naye mara kwa mara. Kabla ya mechi yake na Liston ambaye alichukuliwa kama mpigananji anayetisha na mwenye nguvu zaidi katika wakati wake,  Malcolm X alimshauri Ali kukumbuka Dawud alivyomshinda jitu kubwa Goliath.
Akiongea na gazeti la Al-Madinah, Jiddah tarehe 15 Julai 1989, alisema:
“Nimepatwa na mambo mazuri mengi katika maisha yangu, lakini hisia zilizonijia siku niliyosimama katika mlima Arafat siku ya Hiija, sema kweli zilikuwa za kipekee. Nilihisi niko katika mazingira yasiyoelezeka, kulikuwa na mahujaji zaidi ya milioni moja na nusu wakimuomba Mwenyezi Mungu awasamehe na kuwabariki. Ilikuwa ni furaha kubwa kuona watu wa rangi zote, mataifa yote, wafalme, viongozi wa nchi, watu wa kawaida kutoka mataifa masikini wote wakiwa ndani ya vazi rahisi jeupe wakimuomba Mwenyezi Mungu bila kujiona wala kudharau  wenzao. Ilikuwa ni zoezi tosha la kuonesha itikadi ya usawa katika Uislamu.”
Mohammad Ali akiwa kwenye ibada ya swala!
Baadhi ya vitu alivyoshinda Ali, ni medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki ya 1960 huko Rome; mshindi wa Taji la Glavu za Dhahabu la Kentucky mara 6; mshindi wa Taji la Glavu za Dhahabu wa Taifa (National Golden Gloves), 1959-60; na mwaka 1996 alichaguliwa kuwasha mwenge wa mashindano ya Olimpiki huko Atlanta; amechaguliwa kuwa miongoni mwa wanandondi wa kukumbukwa wa kimataifa (International Boxing Hall of Fame) mwaka 1990; ameshinda mataji matatu ya uzito wa juu akimshinda Sonny Liston (1964), George Foreman (1974) na Leon Spinks (1978) na hivyo kuwa mwanandondi wa kulipwa pekee kushinda mataji hayo mara tatu. Meneja wake wakati mwnegine huwa anamuita GOAT- linalomaanisha ‘the Greatest of all time’ (Bingwa wa mara zote tangu mchezo huo uanzishwe); 1999 Ali alichaguliwa kuwa mwanamichezo wa karne na kituo cha habari cha Sports Illustrated  na cha BBC; Ali pia amekuwa balozi, akijaribu kuokoa mateka wa Kimarekani wane huko Lebanon mwaka 1985; alikuwa mzungumzaji wa kikosi cha Marekani huko Rwanda mwaka 1996; akaanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii wa Muhammad Ali huko Chicago, Illinois. Tuzo nyengine alizowahi kupokea ni pamoja na Tuzo ya Jim Thorpe (Jim Thorpe Pro Sports Award, Lifetime Achievement) 1992; Tuzo ya the Essence, 1997; Tuzo ya Arthur Ashe kwa Msaada wake kwa Wote, ESPN (Espy), 1997; Tuzo ya msaaada kwa uongozi wa Marekani (Service to America Leadership Achievement), kutoka kwa Baraza la Taifa la Mfuko wa Waaindishi Habari (National Association of Broadcasters Foundation), 2001.
Xxxxxx
Muhammad Ali alinukuliwa akisema: “Naamini Uislamu. Namuamini Allah na napenda amani.” Na pia alishawahi kusema: “Mimi ni Mmarekani. Ni sehemu msiogundua. Naomba mnizoee. Mweusi, naejiamini, nayejigamba; jina langu sio lenu; dini yangu sio yenu; shabaha zangu sio zenu; mnizoee tu.”
Baadhi ya Dondoo Zake Mashuhuri
“Jogoo anawika akishaona mwanga tu. Muweke katika kiza hatawika. Nimeuona mwanga, nawika sasa.”
□ □ □
“Mtu anayeiona dunia akiwa na miaka 50 sawa na alivyoiona alivyokuwa na miaka 20 atakuwa amepoteza miaka 30 ya maisha yake bure”
□ □ □
“Paa (ogelea) kama kipepeo, choma kama nyuki”
□ □ □
“Yule ambaye hajiamini kufanya jambo lenye hatari, hataweza kushinda chochote katika maisha yake.”
□ □ □
“Chuki zisizo na msingi zipo kwa mtu aliye kizani, akipata mwanga anapona ugonjwa huo”
□ □ □
“Nilichukia dakika zote za mazoezi, lakini nikajiambia, “Usiache, pata tabu sasa, na uishi miaka yako yote iliyobaki ukiwa bingwa.”
□ □ □
“Mimi najulikanaa na kupendwa zaidi, kwani hakukuwa na setilaiti wakati wa Musa na Yesu walivyokuwa duniani, hivyo watu wa mbali hawakuwajua.”
□ □ □
“Kama wanaweza kutengeza Penicillin (dawa) kutoka katika mkate uliooza, bila shaka wanaweza wakatengeneza kitu kizuri kutoka kwako.”
□ □ □
“Siiti majivuno (kujigamba) kama utaweza kuonesha”
□ □ □
“Kunyamaa ni dhahabu kama huwezi kufikiria jibu bora”
□ □ □
“Mtu mwenye uwezo kupita kiasi (superman), hahitaji mkanda wa usalama wa kiti (seatbelt)”
“Ni ngumu kuwa mpole ukiwa na nguvu na ushujaa kama mimi.”
□ □ □
“Kuwa bingwa mkubwa inakupasa uamini wewe ni bora. Kama sio jaribu hata kujidhania.”
□ □ □
“Sijawahi kufikiria kushindwa, lakini leo imetokea, kitu bora ni kufanya lililo sahihi. Hilo ni ombi langu kwa wote wanaoniamini. Wote inabidi tukubali kipigo wakati mwengine maishani”
Alisema hayo baada ya kupigwa kwa mara ya kwanza na Ken Norton 31 Machi 1973.
□ □ □
“Mwenyezi Mungu amenipa ugonjwa huu kunikumbusha mimi sio nambari moja; YEYE ndiye.”
(Kwa sasa Muhammad Ali anasumbuliwa na ugonjwa wa kuetemeka [Parkinson’s disease). Ameanza kusumbuliwa na ugonjwa huo tangia 1984.)
□ □ □
“Siulizi eti kwanini mie? Bila sababu yoyote. Kuna jambo zuri hapo kwani nashkuru nimebarikiwa. Mungu anatujaribu. Mengine mazuri na mengine mabaya. Yote ni mitihani kutoka kwake.”
□ □ □
“Usihesabu siku zifanye siku ndio zihesabu.”
□ □ □
“Mimi ni bora, japokuwa sijapigana bado”
□ □ □
Disemba 2004, mhaojaji wa gazeti la Time, alimuuliza Ali kuhusu ratiba zake ambapo alijibu kwa kusema:
“Nasafiri sana. Nafurahia kukutana na mashabiki wangu. Popote niwapo, swala, kusoma na kutafakari vinachukua nafasi kubwa maishani mwangu. Mimi ni yule yule niliyekuwa mwanzo. Ila nafanya vitu siku hizi kwa upole na taratibu tu. Kuna kitu sijabadilika nacho ni bado hodari.”
Ingawa habari yake inapaswa kutolewa ushahidi, Ali alikwenda kutembelea mabaki ya WTC New York baada ya mashambulizi ya Septemba 11 na aliulizwa na mwanahabari mmoja anajisikiaje kusikia mtu wa dini moja na yake ndio wanaohusika na mashambulizi hayo. Kwa kebehi akamjibi, “Kwani wewe unajisikiaje kila unavyohisi kuwa Hitler naye anashiriki na wewe katika kufata dini ya Kikristo?
Katika mahojiano na Young Muslim akiwepo Lonnie Ali pia, walimuuliza Muhammad Ali: “Nasikia kabla ya kuwa Muislamu, hukuwa msomaji nilifikiri hujui kusoma vizuri” na Lonnie Ali akajibu badala yake akisema:
“Muhammad alikuwa na ugonjwa wa kutoona herufi vizuri (dyslexia) pale alipokuwa mdogo. Na hakutaka kujishughulisha na kusoma lakini sasa anaweza kutumia masaa kadhaa kwa siku akisoma. Wakati anasoma Qur’an ananakili pembeni aya ambayo imemgusa kwa siku hiyo. Anasoma vitabu vya kiislamu, vitabu vya utafiti, hususani vile vinayoongelea mashaka ya Biblia. Huwa anafatilia vizuri kabisa kuangalia kama kuna upendeleo.”
Na kuna wakati Muhammad Ali alionesha hapo kijitabu kinachoitwa Bible Contradictions (Ukinzani/Makosa ya Biblia). Na swali jengine likafata: “Umeshinda ubingwa wa uzito wa juu wa ndondi mara tatu na umefanikiwa kutetea taji hilo mara 19. Zipi ni shabaha zako kwa sasa?” Muhammad Ali akajibu: “Kutangaza Uislamu, hicho tu.” Na akiwa katika mahojiano mengine na mhariri mkuu wa Beliefnet Deborah Caldwell aliyeongea na Hana Ali kuhusu uhusiano wao na baba yake, alisema:
“…baba yangu sasa yupo kiroho zaidi kukilo kidini tu. Ilikuwa muhimu kwake kuwa na dini na kufata mashiko yake aliyoamini miaka ya mwanzo. Kile kilikuwa kipindi tofauti. Sasa anajaribu kuwaita watu katika Uislamu, japokuwa hawezi kama alivyofanya mwanzoni. Afya na mbinu zake za kiroho zimebadilika; sasa hivi anapenda kwenda kuwafanya watu wawe na furaha, kusaidia watu kwa kutoa sadaka…”
YoungMuslim walimuuliza swali, kipi kilikuwa kikubwa kuliko vyote kukipata, nayeye akasema, “Uislamu”. Wakaendelea kumhoji: “Kama ungekuwa na uwezo wa kurudi nyuma na kubadilisha jambo ungefanya nini?” Akasema kwa kujigamba: “Ningekuwa Muislamu nikiwa na miaka 10.” Katika mahojiano hayo walikosea kumuuliza kipi kitabu akipendacho zaidi? Na kama unavyofikiria alivyojibu: “Hilo ni swali la kitoto! Kipi zaidi ya Qur’an.”
Muhammad Ali kwa sasa anaishi Michigan na mke wake wa nne, Yolanda Williams. Muhammad Ali ana watoto tisa: Rasheedah, Jamilah, Maryam, Miya, Khalilah, Hana, Laila, Muhammad mdogo na Asaad. Wakati alipoamua kustaafu mchezo wa ndondi, kauli yake ilikuwa: “Nastaafu kwani kuna mengi mengine mazuri ya kufanya kuliko kupiga watu.”
Kwa kumalizia, tutatoa jibu alilotoa Muhammad kumpa George Plimpton alipomuuliza swali lililomaliza mahojiano yake naye: “Kipi ungependa watu wakikumbuke kwako pale utapokuwa umekwenda?”
“Ningependa waseme, alichukua vikombe kadhaa vya upendo, alichukua kijiko cha uvumilivu, kijiko kimoja cha ukarimu, painti moja ya huruma (galoni moja ina painti 8). Kwati (quart) moja ya tabasamu (kwati sawa na painti mbili), kiasi kidigo cha kujali, na akakoroga niya na furaha, akaongeza imani nyingi, na akachanganya vizuri mchanganyiko wake, na akagawa kwa watu wake wote katika maisha yake, alimhudumia kila mtu aliyestahili alipokutana naye.”
Subhana rabial aalla wabihamdi!

Saturday, August 3, 2013

WANACHAMA WA HABARI GROUP WAPELEKA MISAADA VITUO VYA WATOTO YATIMA




Diwani wa Viti Maalumu na Mwenyekiti Mtendaji wa Aisha Sururu Fonditioni, Aisha Sururu kulia akiwakabidhi sehemu ya msaada alioutoa kwa ajili ya kuchangia watoto yatima kwa wanachama wa kikundi cha Habari Group  Rabia Bakari kushoto na Asha Bani kwa ajili ya kupeleaka kwa watoto yatima katika vituo mbalimbali  Misaada mingine ilitolewa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, January Makamba,Mmiliki wa Maduka ya Silva Botique, Madam Nora, Katibu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa kiislam Sheikh  Khamisi Mataka, na Mkurugenzi wa Kampuni ya QUALITY Printers And Stationers Amani Sokko PIcha na  BLOG YA SUPER D


Diwani wa Viti Maalumu na Mwenyekiti Mtendaji wa Aisha Sururu Fonditioni, Aisha Sururu kushoto akiwakabidhi sehemu ya msaada alioutoa kwa ajili ya kuchangia watoto yatima kwa wanachama wa kikundi cha Habari Group  Rabia Bakari kushoto na Asha Bani kwa ajili ya kupeleaka kwa watoto yatima katika vituo mbalimbali  Misaada mingine ilitolewa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, January Makamba,Mmiliki wa Maduka ya Silva Botique, Madam Nora, Katibu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa kiislam Sheikh  Khamisi Mataka, na Mkurugenzi wa Kampuni ya QUALITY Printers And Stationers Amani Sokko PIcha na  BLOG YA SUPER D

Wanachama wa kikundi cha Habari Group Rabia Bakari kulia na Asha Bani wakiangalia baadhi ya vyakula na vitu mbalimbali walivyokabidhiwa kwa ajili ya kwenda kugawa kwa watoto yatima PIcha na  BLOG YA SUPER D
Diwani wa Viti Maalumu na Mwenyekiti Mtendaji wa Aisha Sururu Fonditioni, Aisha Sururu kulia akiwakabidhi sehemu ya msaada alioutoa kwa ajili ya kuchangia watoto yatima kwa wanachama wa kikundi cha Habari Group  Rabia Bakari kushoto na Asha Bani kwa ajili ya kupeleaka kwa watoto yatima katika vituo mbalimbali  Misaada mingine ilitolewa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, January Makamba,Mmiliki wa Maduka ya Silva Botique, Madam Nora, Katibu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa kiislam Sheikh  Khamisi Mataka, na Mkurugenzi wa Kampuni ya QUALITY Printers And Stationers Amani Sokko PIcha na  BLOG YA SUPER D

Wanachama wa Habari Group wakia katika picha ya pamoja na na mwenyekiti mtendaji wa Aisha Sururu fondition bi, Aisha Sururu
Moja ya kituo cha kilichopewa misaada na Habari Group Leo

Mwanachama wa Kikundi cha Habari Group Asha Bani kulia akikabidhi sehemu ya msaada  walioutoa kwa  Katibu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Hidaya Orphans Center and Tahfidhil-qur-an cha Buguruni Bw. Abubakari Simba Dar es salaam leo Picha na
www.burudan.blogspot.com

Baadhi ya wanachama wa kikundi cha habari Group wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika Kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Hidaya Orphans Center and Tahfidhil-qur-an cha Buguruni baada ya kutoa misaada mbalimbali leo

Mwanachama wa Kikundi cha Habari Group Asha Bani kulia akikabidhi sehemu ya msaada  walioutoa kwa  Katibu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Hidaya Orphans Center and Tahfidhil-qur-an cha Buguruni Bw. Abubakari Simba Dar es salaam leo Picha na
www.burudan.blogspot.com


Mwanachama wa Kikundi cha Habari Group Asha Bani kulia akikabidhi sehemu ya msaada  walioutoa kwa  Msimamizi Mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al Furqan Islamic Center cha Chanika Bw,Hamisi Omari  Dar es salaam leo Picha na
www.burudan.blogspot.com

Baadhi ya wanachama wa kikundi cha habari Group wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Al Furqan Islamic Center cha Chanika baada ya kutoa misaada mbalimbali leo

TTCL, TSN, TCRA, AICC, YARA WASHIRIKI KIKAMILIFU MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE DODOMA 2013


Kampuni Kongwe ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) nayo ipo katika Viwanja vya Nzuguni, kuelimisha umma juu ya huduma zake. Pichani ni Maofisa wa Kampuni hiyo Thomas Lemunge ambaye ni Afisa Biashara wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (katikati) akitoa elkimu kwa mwananchi huku Afisa Habari, Amanda Luhanga akifuatilia.
 Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakiwa katika picha ya pamoja katika banda lao lililopo ndani ya Viwanja vya Nzuguni Mjini Dodoma yanapofanyika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima Nane Nane. Mwaka huu TCRA wanakuambia 'FUTA-DELETE' ujumbe wowote usio na maana katika simu yako au mtandao wa Barua pepe. Ila Father Kidevu Blog, inaongezea Ujumbe 'PUUZIA-IGNORE' taarifa yeyote isiyo na manufaa kwa jamii katika Mitandao ya Kijamii.
 Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mwasiliano Tanzania (TCRA) anaeshughulika na Uratibu wa Kanda, Victor Nkya akitoa elimu ya FUTA-DELETE kwa vijana waliotembelea banda hilo leo.

 Kikosi kazi cha Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania Standard Newspapers (TSN) Limited ambacho kipo ndani ya viwanja vya Nzuguni katika Banda la Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo katika Maonesho ya siku ya Wakulima Nane Nane yaliyoanza Agosti Mosi na kutaraji kumalizika Agosti 8, 2013 kitaifa Mkoani Dodoma. Kushoto ni Afisa Masoko, Francis Kihinga akiwa na Afisa Mauzo na Masoko, Chikira Mgheni. TSN ndio wachapishaji na wasambazaji wa Magazeti ya Daily News, Sunday News, HABARILEO, HABARILEO Jumapili na SpotiLEO.
 Afisa Masoko wa TSN, Francis Kahinga akigawa majarida ya Elimika na Academy kwa wanafunzi walio tembelea banda la TSN. TSN ndio wachapishaji na wasambazaji wa Magazeti ya Daily News, Sunday News, HABARILEO, HABARILEO Jumapili na SpotiLEO.
 Kampuni Kongwe ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) nayo ipo katika Viwanja vya Nzuguni, kuelimisha umma juu ya huduma zake. Pichani ni Maofisa wa Kampuni hiyo Thomas Lemunge ambaye ni Afisa Biashara wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (katikati) akitoa elkimu kwa mwananchi huku Afisa Habari, Amanda Luhanga akifuatilia.
 Wafanyakazi mbalimbali wa TTCL wakiwa bandani hapo wakitoa elimu ya huduma zao.
Ofisa Masoko na Utafiti wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Linda Nyanda, akiwapa maelezio wanafunzi wa kidato cha tatu wa Sekondari ya Maria de-Mathias ya mjini Dodoma juu ya shughuli mbalimbali za AICC walipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Wakulima nane nane katika Uwanja wa Nzuguni mjini Dodoma.
Ofisa Habari Mwandamizi na Itifaki wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Catherine Kilinda akiwapa maelezio wanafunzi wa kidato cha tatu wa Sekondari ya Maria de-Mathias ya mjini Dodoma juu ya shughuli mbalimbali za AICC walipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Wakulima nane nane katika Uwanja wa Nzuguni mjini Dodoma.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya YARA Tanzania Limited, Catherine Assenga (kushoto) akimsadia mwananchi aliyetembelea banda lao lililopo ndani ya Banda la NMB katika Viwanja vya Maonesho Nane Nane, Nzuguni Mjini Dodoma. YARA ndio wasambazaji wa Mbolea CHAPA MELI.

RAIS KIWETE AFUTURISHA WASANII WA BONGO FLEVA IKULU


Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii wa Bongofleva, Ally Kiba na mdogo wake Abdull Kiba.
 Rais Kikwete akiwa akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa Filamu na  Bongofleva, Hemed Suleiman.
 Rais Kikwete akiwa katika picha ya kumbukumbu na mmoja wa Watangazaji machachari wa Clouds FM,TV, Mbwiga Mbwiguke.
 Rais Kikwete akiwa akiwa katika picha ya pamoja na Msanii Mkongwe wa Bongofleva,Gwamaka Kaihula a.k.a King Crazy G K.
 Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa bongofleva na muigizaji wa Filamu hapa nchini,atambulikae kwa jina la kisanii Zuwena Mohamed a.k.a. Shilole.
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa muziki wa Bongofleva mara baada ya kufturu.Kutoka kushoto,Snura,Keisha,Mwasiti,aliyechuchumaa ni Shilole,Dj Fetty ,Mwanahawa Abdul a.k.a Quee Doreen.
 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya pichani shoto Mwasiti Almas na kulia Zuwena Mohamed a.k.a Shilole wakiwa sambamba na Mtangazaji wa Clouds FM,Dj Fetty wakipakua ftari kufuatia mualiko wa Rais Kikwete kwenye viwanja vya Ikulu,jijini Dar.
 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva wakipata ftari kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar jana kufuatia mualiko wa Rais Kikwete.
 Rais Kikwete akisalimiana na msanii wa bongofleva,Lawrence Malima a.k.a Marlow,kulia kwake ni Ally Kiba pamoja na Abdul Kiba na kushoto ni Mtangazaji wa East Africa Radio, Samisango.
 Rais Kikwete akisalimiana na msanii wamuziki wa kizazi kipya,Chege Chigunda na kulia kwake ni msanii wa bongofleva,Cassim Mganga,wakati wa kupata ftari jana jioni kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar.
 Rais Kikwete akiwasabahi baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya,mara baada ya kupata ftari mapema jana jioni kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar, Rais Kikwete aliwaalika wasanii mbalimbali kupata ftari ya pamoja Ikulu jana jioni.

MAKUNDI MBALI MBALI MBALI YA VIJANA MKOA WA MWANZA WASHIRIKI MJADALA WA KATIBA MPYA



 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa ufafanuzi wa CCM juu ya Rasimu ya Katiba mpya katika mkutano uliofanyika Mwanza leo na kuwakutanisha vijana wa makundi mbali mbali.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Stephen Wasira akifafanua juu ya mstakabali wa vijana katika mchakato wa Katiba mpya.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dk.Anthony Dialo akichangia mada juu ya umuhimu wa serikali mbili kwa Tanzania.
Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Mkoani Mwanza Sixbert Ruben akielezea umuhimu wa vijana wa Mwanza katika kushiriki kwa kwenye mchakato wa Katiba mpya.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM Martin Shigela akifafanua juu ya umuhimu wa vijana katika suala la  Katiba mpya
Sehemu ya Vijana walioshiriki katika  mjadala wa mchakato wa Katiba mpya uliofanyika leo katika ukumbi wa chuo cha mafunzo Benki Kuu mkoani Mwanza ambapo vijana zaidi ya mia sita walihudhuria.

MAKAMU WA RAIS AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA SHINDANO LA TATU LA KUHIFADHI QUR'AN TUKUFU JIJINI DAR



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza za waumini wa dini ya Kiislamu, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Qur'an Tukufu, iliyofanyika jana usiku Agosti 2, 2013 katika Msikiti wa Istiqaama, jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Sh. milioni 2, mshindi wa kwanza wa kuhifadhi Juzuu 30, Abdulkarim Khamis, wakati wa hafla ya kuwakirimu na kukabidhi zawadi kwa  washindi hao iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam, jana usiku.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Sh. milioni 1.5, mshindi wa kwanza wa kuhifadhi Juzuu 20, Maryam Nassor (8), wakati wa hafla ya kuwakirimu na kukabidhi zawadi kwa washindi hao iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam, jana usiku.
 Mtoto Maryam Nassor (8) akisoma moja ya haya iliyo katika kitabu cha Juzuu kwa kichwa, wakati wa hafla ya kuwakirimu na kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Juzuu iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam, jana usiku.
 Zoezi la utoaji zawadi likiendelea.
 Zoezi la utoaji zawadi likiendelea.
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, kuzungumza na waumini wa dini ya Kiislamu, wakati wa hafla ya Kuwakirimu na kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Juzuu, iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam, jana usiku.
 Sehemu ya waumini wa dini ya Kiislamu, waliohudhuria hafla hiyo.
 Sehemu ya waumini wa dini ya Kiislamu, waliohudhuria hafla hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kukabidhi zawadi za washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Juzuu, wakati wa hafla ya kuwakirimu wasindi hao iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam jana usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kukabidhi zawadi za washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Juzuu, wakati wa hafla ya kuwakirimu wasindi hao iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam jana usiku.