Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, October 2, 2013

TAZAMA TUKIO ZIMA LA WAFANYA BIASHARA KUGOMA KUNUNUA MASHINE ZA TRA ZENYE THAMANI YA THS 800,000 JIJINI MBEYA, MADUKA YAFUNGWA.




 Polisi wakiwa katika ulinzi mkali 
 Maduka yakiwa yamefungwa 
 Wafanya biashara wakiwa uwanjani kungoja kusikiliza nini  hatma yao
 Baadhi ya watu wakiwa wanakimbia Baada ya Mabomu ya machozi kuanza kurushwa kuepusha vurugu
 Mawe yakiwa yamepangwa kuzuia magari yasiende kokote
 Maduka yote yakiwa yamefungwa eneo la mwanjelwa kupinga ununuzi wa mashine hizo za TRA
 Vijana hawa wakiwa wana nawa uso baada ya Bomu la machozi kuwapitia 
 Jiwe kubwa likiwa limewekwa katika Barabara magari yasipite
 Hali tete Tayari vijana wameanza kuchoma mataili.....


Tuesday, October 1, 2013

WAKAZI WA KIKUYU KUSINI WAANDAMANA KUPINGA BOMOABOMOA ILIYOPANGWA NA CDA MKOANI DODOMA, MKUU WA MKOA AINGILIA KATI




 Maelfu ya Wananchi wa Kata ya kikuyu kusini wakiandamana katika mitaa ya mji wa Dodoma kwa ajili ya kupinga kubomolewa na mamraka ya ustawishaji makao makuu  [CDA] wanaotarajia kubomoa nyumba, mapagale na misingi ya wakazi hao.
  Maelfu ya Wananchi wa Kata ya kikuyu kusini wakiandamana katika mitaa ya mji wa Dodoma kwa ajili ya kupinga kubomolewa na mamraka ya ustawishaji makao makuu  [CDA] wanaotarajia kubomoa nyumba, mapagale na misingi ya wakazi hao.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akipaza sauti ya matumaini kwa wakazi wa Kata ya kikuyu kusini walioandamana kupinga Bomoabomoa ya CDA waliokuwa wamepanga kubomoa nyumba na misingi katika eneo hilo.  Alisema “Naitengua amri hiyo na namwagiza Mkurugenzi akutane na wananchi hawa pamoja na viongozi wao ili kuweza kufikia muafaka kwani kubomoa sio suluhu hamuwezi kubomoa Dodoma nzima na ningependa kuletewa taarifa juu ya sula hili … mnachotakiwa ni kuboresha na kutumia njia sahihi ambazo hazita waumiza wananchi ambao ndiyo wateja wenu.
Diwani wa kata ya Kikiyu kusini Ancelmu Kutaka akifafanua jambo mbele ya Wananchi wa kata hiyo waliondamana kupinga kubomolewa na Mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA] walipanga kuboa wakati wowote kuanzia leo.
Kaimu Mkurugenzi wa CDA Paskas Mulagili Akifafanua jambo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali kuhusu maandamano ya wananchi wa kata ya Kikuyu Kusini walioandamana kupinga ubomoaji unaotarajiwa kufanywa na mamlaka hiyo siku yoyote kuanzia leo. 

Habari na picha na  John Banda, Dodoma
WAKAZI wa Kata za Kikuyu Kusini na Kilimani mkoani Dodoma wameandamana kupinga amri iliyotolewa na Mamlaka ya Ustawishaji ya Makao Makuu (CDA) ambayo inawataka kuhama katika eneo hilo ndani ya siku saba. Wakazi hao walioandamana kutoka Kikuyu hadi Viwanja vya Nyerere Square katikati ya mji wakimtaka mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi kuzungumza nao.

Maandamano hayo yalisindikizwa na ulinzi wa polisi hadi katika viwanja hivyo huku wakazi hao wakiwa wameshikilia mabango yenye jumbe mbalimbali. Wakazi hao wakiwa wanaimba nyimbo huku wakiinua mabango yao juu yenye ujumbe kama Cda ni zaidi ya Alshababi, CCM mnaiona bomoabomoa, Cda ni zaidi ya Nduli Idd Aminini Dada na lingine likisomeka Hata wanyama hupewa hifadhi.

Wakizunguza na waandishi wa habari katika viwanja hivyo wakati wakimsubiri mkuu wa mkoa baadhi ya wananchi na viongozi wao wa mitaa walidai kuwa lengo la maandamano hayo ni kufikisha kilio chao kwa serikali ya mkoa. Andrew Mdumi mwenyekiti wa mtaa wa Mkalama ambao ni sehemu ya eneo linalotakiwa kuvunjwa alisema kuwa wameamua kufanya maandamano hayo mara baada ya kupewa amri ya kuondoka katika eneo wanaloishi kwa kipindi kirefu.

Mdumi alisema, kuwa Mamlaka ya ustawishi Makao makuu imekuwa ikiwapatia namba kila wakati na kudai kuwa itakuja kuwapimia lakini katika hali ya kushangaza imewapa amri ya kuondoka ndani ya siku saba kwa madai kuwa wamevamia katika eneo hilo ambalo lilikuwewa limetengwa kwajili ya bustani za mbogamboga na matunda. “Wanataka tuondoke ili kupisha kilimo cha mbogamboga na matunda hivi kweli mboga na maisha yetu kipi cha msingi kuna nyumba zaidi ya 1000 ambazo watakakuzibomoa kwajili tuu ya kupisha bustani” alisema

Alisema kuwa wamekuwa wakishirikiana na CDA kwa kipindi kirefu ili kuweza kufanikisha zoezi la upimaji wa viwanja hivyo hata kwa gharama zao wenyewe. Mwekiti wa kamati ya upimaji katika Kata ya Kikuyu kusini Mathew Ndallu, alisema kuwa katika kufuatilia suala hilo la kupimiwa viwanja walikutana na CDA na kukubaliana kuwa waje wafanye utambuzi wa nyumba zilizopo, mapagale na misingi ili waweze kufanya upimaji.
Ndallu alisema kuwa walikubaliana na kuwa kutokana na eneo hilo kuwa halijapimwa wao wako tayari kuchangia gharama za upimaji ili kuwezesha zoezi hilo kufanyika.
“Tulikubaliana nao mara baada ya wao kuja kutambua idadi ya nyumba mapagale na misingi watupimia na sisi tuko tayari kuchangia kiasi cha sh.500,000 kwa kila mwenye eneo” alisema Ndalllu. Aidha alisema kuwa katika hali ya kushangaza pale ambapo walikuwa wanasubiri kupimiwa CDA waliwageuka na kuwataka kwanza wao wapatiwe viwanaja 500 ili waweze kuwapiamia. “Mara baada ya kukubaliana nao kuwa tuko tayari kuchangia lakini Mkurugenzi alituambia kwanza tuwape wao viwanja 500 ili waweze kuja kutupimia na kama hatutakubali basi watakuja kutubomolea” alisema.

Alisema kuwa mara baada ya wao kukataa kumpa mkurugenzi huyo viwanja hivyo aliwaandikia barua hiyo ambayo ilikuwa inawataka wakazi wa maeneo hayo kuondoka kabla ya tarehe 30 ya mwezi Septemba (jana).
“Walituandikia barua ambayo inatutaka kuaondoka ndani ya siku hizo saba ikiwa ni kuanzia tarehe 23 ya mwezi huu ambapo inaishia leo (jana) na kesho (leo )wanakuja kuanza kubomoa” alisema Ndallu.
Alisema kutokana na hali hiyo ambayo imeonyesha kuwa CDA imeshindwa kuwasikiliza kilio chao wameona kuwa hiyo ndiyo njia sahihi ya wao kupata suluhu ya tatizo lao. Alisema kuwa jumla ya mitaa mnne katika kata hizo ndiyo inayotakiwa kubomolewa ambayo ni mitaa ya Mkalama, Chidachi pamoja na Image A na B.

Akizungumza na kundi la wakazi hao mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi, alisema kuwa anatengua amri hiyo iliyotolewa na CDA na kumtaka Mkurunzi wa mamlaka hiyo kukutana na viongozi wa maeneo husika.
“Naitengua amri hiyo na namwagiza Mkurugenzi akutane na wananchi hawa pamoja na viongozi wao ili kuweza kufikia muafaka kwani kubomoa sio suluhu hamuwezi kubomoa Dodoma nzima na ningependa kuletewa taarifa juu ya sula hili … mnachotakiwa ni kuboresha na kutumia njia sahihi ambazo hazita waumiza wananchi ambao ndiyo wateja wenu.

KESI YA SHEIKH PONDA KUENDELEA KUSIKILIZWA KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI MOROGORO KUANZIA TAREHE 7 NOVEMBER 2013



 Sheikh Issa Ponda akishuka kwenye basi la Magereza tayari Kuingia Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro leo ambapo  Mahakama Ilikuwa inatoa Maamuzi kuhusu Kufutiwa shitaka moja kati ya matatu yanayomkabili Sheikh Ponda katika Mahamama hiyo.Mahakama Imetupilia Mbali Ombi hilo na kesi itaendelea Kusikilizwa katika Mahamama hiyo.Kesi hiyo imeahiriswa Mpaka tarehe 7 November mwaka huu ambapo mahakama itaanza kusikiliza Mashahidi wa kesi hiyo.Sheikh Ponda Amerudiswa Rumande.
 Sheikh Issa Ponda Akiingia katika viwanja vya mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa morogoro..
Sheikh Ponda akiwa mahakamani akimsubiri Hakimu tayari kusikiliza Kesi yake katika Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa morogoro
 Mke wa sheikh Ponda akiwa mahakamani 
 Ulinzi ukiwea umeimarishwa mahakamani hapo leo wakati kesi hiyo ikiendelea katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wsa morogoro
PICHA NA MATUKIO NA MICHAPO BLOG

BALOZI IDDI AKABIDHI HATI ZA UMILIKI WA MASHAMBA YA KILIMO KWA WAKAZI WA KIJIJI CHA NGURUWENI




 Baadhi ya wananchi na wakulima wa Kijiji cha Nguruweni wakiwa katika mkutano maalum  ulioitishwa  na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa kukabidhiwa hati za umiliki wa mashamba ya kilimo katika maeneo yao.
 Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Hati ya umiliki wa shamba Bibi Josephine Yohana kwenye hafla maalum ya kumaliza mgogoro wa mashamba katika kijiji hicho. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

 Balozi Seif akimpatia Hati Bwana Mohd Ali Pili ya kumiliki eneo la kilimo katika Kijiji cha Nguruweni  ambako kuliibuka mgogoro uliosababishwa na kuinbgizwa watu wasiohusika na maeneo hayo kwa kilimo.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
*****************************************************
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewatahadharisha Wakulima wa Viijiji vya Ndunduke, Nguruweni na Dole  kuhakikisha kwamba maeneo ya kilimo waliyokabidhiwa na Serikali kwa shughuli za Kilimo wanayatumia  kama yalivyopangwa na kukubalika na pande hizo mbili.
Wakulima hao wakaonywa kuwa  ye yote atakaeamua maeneo hayo kuyakata viwanja kwa ajili ya kujenga nyumba au kuyauza kwa mtu mwengine aelewe kwamba Serikali italazimika kumnyang’anya mkulima huyo mara moja.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akikabidhi hati  za umiliki wa mashamba ya kilimo kwa ajili ya wakulima 40 kati ya 181 wa Kijiji cha Nguruweni waliokuwa wakiilalamikia Serikali kwa kipindi kirefu kuidhinishiwa  mashamba wanayoyatumia ili kuendeleza shughuli zao za Kilimo.
Balozi Seif alisema wapo baadhi ya watu wenye tabia ya kuomba mashamba au eka kwa kisingizio cha kuendeleza kilimo lakini badala yake hujenga  tamaa inayowaelekeza kuanza kukata viwanja na kuuzia watu wengine.
“ Nataka nitahadharishe kabisa kwamba Mkulima ye yote atakayediriki kutumia fursa aliyopewa na Serikali ya kuendeleza kilimo kwenye shamba alilokabidhiwa na akaamua kufanya vyengine afahamu kwamba Serikali haitasita kunyang’anya shamba hilo mara moja “. Alitahadharisha Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  aliwapongeza wakulima hao wa Nguruweni kwa ustahamilivu wao mkubwa waliouchukuwa kwa kipindi kirefu kufuatia mgogoro wa maeneo waliyokuwa wakitumia kwa shughuli za kilimo baadhi yake kupewa watu wengine.
Balozi Seif alisema ustahamilivu huo kwa kiasi kikubwa umesaidia kuendeleza amani na utulivu kwenye Vijijini hivyo vya Nguruweni, Ndunduke pamoja  na Dole ambayo imeleta faraja kwa Serikali Kuu kwa vile haikuathiri shughuli za kila siku za kijamii.
Aliwakumbusha wakulima hao kwamba hivi sasa ni muda muwafaka wa kuendeleza shughuli zao za kilimo kwa vile wameshakuwa na uhalali wa kufanya hivyo katika maeneo waliyopewa na Serikali.
Alifahamisha kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikisisitiza na kuhimiza kilimo kwa vile sekta hiyo bado inaendelea kuwa muhimili Mkuu wa uchumi wa Taifa hili.
“ Serikali imekuwa ikihimiza na kusisitiza umuhimu wa kilimo. Lakini Mkulima hawezi kuendeleza kilimo bila ya kuwa eneo la kilimo, sasa kwenu nyinyi hili suala  linaonekana kuondoka “. Alifafanua Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimpongeza Mwenyekiti wa Kamati Maalum aliyoiunda kushughulikia mgogoro huo wa mashamba ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi kwa kushirikiana vyema na watendaji wa Wizara za Kilimo na Ardhi na kuutatua mgogoro huo wa muda mrefu.
Mapema Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali Asili Nd. Ali Juma alisema Taasisi za Kilimo na Ardhi zililazimika kufanya uhakiki wa kina ili kuwatambua wakulima halali waliokuwa wakistahiki kupatiwa hati hizo.
Nd. Ali alisema uhakiki huo ulioshirikisha pia Masheha wa Vijiji vilivyohusika na mgogoro huo vya Nguruweni Ndunduke na Dole umeibua wakulima wapatao 181 ambapo  wakulima 40 kati ya hao wamethibitika kupatiwa hati hizo kwa awamu ya kwanza.
Naibu Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Kilimo na Mali Asili alieleza kwamba kazi ya uhakiki sambamba na uchambuzi kwa wakulima wa Kijiji cha Dole imeshaanza rasmi na inatarajiwa kukamilika katika kipindi kifupi kijacho.
Akitoa shukrani zake Mwenyekiti wa Kamati  Maalum iliyounda  na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozib Seif kushughulikia mgogoro huo wa mashamba ya vijiji vya Nguruweni, Ndunduke na Dole Mh. Abdulla Mwinyi  alisema Wakulima wa Vijiji hivyo  wanapaswa kupongezwa kwa umahiri wao wa ustahamilivu kufuatia mgogoro huo wa mashamba kwenye eneo hilo.
Hata hivyo Mh. Abdulla Mwinyi ambae pia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi amewaomba wale wakulima ambao bado mgogoro wao haujapatiwa ufumbuzi waendelee kuwa na subra kwa vile Serikali kupitia Uongozi wa Kamati hiyo unajitahidi katika kukamilisha mchakato huo.
Akitoa shukrani kwa Niaba ya Wakulima hao Mmoja wa Wazee wa Vijiji hivyo Mzee Kitwana  Mustafa alimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ujasiri na uungwana wake aliouchukuwa wa kutimiza ahadi aliyowapa  mwaka jana wa kumalizika kwa kadia hiyo.
Mzee Kitwana alisema wakulima wa Vijiji hivyo wamefarajika na hatua iliyochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwatatulia kero lililokuwa likiwasumbua kwa miaka mingi iliyopita.
“ Ile furaha yetu tuliyonayo leo kama tumengeruhusiwa basi tunatamani tukubebe na matope yetu Mzee wetu kwa jinsi ulivyotujali na kututhamini  kwa katambua kwamba tulikuwa tukisumbuka kweli kweli “ Alionyesha furaha yake Mzee Kitwana.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwahi kutoa  ahadi kwa wakulima hao wa Nguruweni, Ndunduke na Dole  kwamba Serikali  itayagawa maeneo  yote ambayo kamati aliyoiunda tarehe 14 Disemba Mwaka 2012 Chini ya Mwenyekiti wake Mh. Abdulla Mwinyi  kufanya uhakiki wa mashamba yote yaliyoleta mgogoro.
Wakulima hao waliwahi kutoa shutuma kali kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif dhidi ya watendaji na Maafisa  wanaosimamia Ardhi, Kilimo wakiwemo pia Viongozi wa ngazi ya kati wa Serikali kwa vitendo vyao vya kuingiza wakulima waliokuwa hawahusiki na mashamba hayo.
Watendaji hao walituhumiwa na wakulima hao kuvuruga  jukumu  walilopewa la kusimamia maandalizi ya utolewaji wa nyaraka kwa wakulima 28 wa awamu ya kwanza waliokubalika kupatiwa hati za umiliki huo chini ya aliyekuwa waziri Kiongozi wa mwisho wa SMZ  Mh. Shamsi Vuai Nahodha.
 Serikali ililazimika kuzuia utolewaji wa hati hizo kufuatia hitilafu zilizojichomoza za kupandikizwa baadhi ya watu wasiohusika jambo ambalo lilisababisha mgogoro wa muda mrefu kati ya wakulima hao na watendaji waliopewa jukumu la kusimamia suala hilo.

AIRTEL WAKABIDHI VITABU SHULE ZA SEKONDARI




DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi akiwakabidhi msaada wa Vitabu vilivyotolewa na Kampuni ya simu ya Airtel Wanafunzi Mariamu Hamisi na Theodory Raymond wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari Dodoma wengine katika picha nyuma ni meneja mauzoAirtel Dodoma, Saidimu Ngaleson

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU WAZEE DUNIANI NA WAZEE WA KOROGWE MKOA WA TANGA.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wazee waliohudhuria katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, baada ya kuhutubia katika sherehe hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mazoezi uliopo Kata ya Manundu, Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Mstaafu, Mussa Shekimweli na Mwenyekiti wa sasa CCM mkoa wa Tanga, Henry  Dafa Shekifu, wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mazoezi Kata cha Manundu, baada ya kuhutubia katika sherehe hizo zilizofanyika Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mazoezi Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, leo.
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akivishwa vazi la asili la kabila la Wadigo, na Mwenyekiti wa Umoja wa Wazee wa Wilaya ya Korogwe, Abdallah Semkiwa, wakati wa sherehe za kilele cha Siku ya Wazee Duniani, zilizofanyika mkoani Tanga.
 Sehemu ya wazee waliojitokeza kuhudhuria sherehe hizo.
 Sehemu ya wazee waliojitokeza kuhudhuria sherehe hizo.
 Wasanii wakitoa burudani ya ngoma ya Mdumange, wakati wa sherehe hizo.
 Picha ya pamoja na baadhi ya wazee.

Rais Dk.Shein akutana na Balozi wa Uholanzi na Balozi Mdogo wa China.





 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Uholanzi  Nchini Tanzania Jaap Frederiks,alipofika leo Ikulu Mjini Zanzibar kwa madhumuni ya kusalimiana na Rais.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na  Balozi wa Uholanzi  Nchini Tanzania  Jaap Frederiks, alipofika leo Ikulu Mjini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiagana na Balozi wa  Uholanzi Nchini Tanzania Jaap Frederiks,baada ya mazungumzo yao,alipofika  Ikulu Mjini Zanzibar leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzin Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi Mdogo wa China  Nchini Tanzania ,anayefanyia kazi zake Zanzibar Xie Yunliang,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na  Balozi Mdogo wa China Nchini Tanzania,anayefanyia kazi Zanzibar Xie Yunliang, alipofika jana Ikulu Mjini Zanzibar

mwenge wa uhuru wawasiri jijini mbeya




mkuu wa mkoa wa mbeya Abbas Kandoro akiapa kuwa ameupokea salama mwenge wa uhuru kama alivyokabidhiwa na mkuu wa mkoa wa Njombe leo hii 

 mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akimkabodhi mwenge mkuu wa wilaya ya Mbeya dk Norman Sigala ambaye ataukimbiza mwenge huo kwenye halmashauri yake.
 mkuu wa wilaya ya mbeya Dk Norman Sigala akikiri kuupokea mwenge huo
viongozi mbalimbali wa mkoa wa Njombe na wilaya ya Makete wakielekea kwenda kuukabidhi mwenge huo kwa mkoa wa jirani wa Mbeya(picha zote na Edwin Moshi)

RAHA NA KARAHA YA MVUA DAR



 Dada akiwa amebebwa alipokuwa akivushwa kwa malipo kwenye dimbwi la maji ya mvua eneo la Magomeni Kagera, Dar es Salaam
 Mbebaji akiwa amemwangusha dada huyo kwenye dimbwi
  Dada akimkunja kijana aliyemdondosha kwenye dimbwi.
 Wasamaria wema wakimsaidia dada kumtoa kwenye dimbwi
Dada akilia baada ya kuokolewa.PICHA ZOTE NA KHAMIS MUSSA